Riwaya : ROHO YA GIZA. SEHEMU YA TATU(3) ****ILIPOISHIA***** Je? mke wangu atanielewa kuishi nae pasipo mtoto! Fundikila akaitikia kwa shingo upande......baada ya kikao kuisha akajitokeza nyumbani.. wakati huo mkewe alikuwa kalala usingizi mzito hakuweza kujua mumewe hakuwemo ndani ya nyumba...kwa sababu alifumbwa kimiujiza na ni mwiko kwa ambaye sio mwanachama kuona jambo hilo! siku zilizidi kusonga,,hatimae mke wake akashika ujauzito! Hilo ni kosa kubwa amelifanya Fundikila! baada ya siku kadhaa kupita mauzauza yakaanza kuiandama nyumba yake.... siku moja nyakati za usiku Fundikila pamoja na mkewe wakiwa wamelala... kiongozi mkuu wa wafuasi wa Lucifer akajitokeza chumbani kwa Fundikila.. *****ENDELEA***** Fundikila akashtuka usingizini,, kumbe alikiwa anaota! akaanza kuingiwa na wasiwasi,,,akajisemea moyoni,, hili ni tatizo.. naamini haikuwa ndoto bali ni kweli....kanitokea usingizini.. hii inaashiria hali ya hatari!! sijui nifanye nini kujiondoa kwenye chama hiki,, hii ni adhabu,, yani mali nilizonazo na heshma kila kona ya mtaa eti nikose mtoto!! haiwezekani..liwalo na liwe,, nipo tayari hata kupoteza uhai wangu lakini si kukosa mtoto.... Fundikila akadamka akazipika hatua kuufuata mlango akatoka nje ya chumba chake.... akazipiga hatua kadhaa akausogelea ukuta unaotenganisha korido katikati.... akasimama kisha akatazama kushoto kulia,,, aakaugusa ukuta huo... akausukuma kwa nguvu.. ukafunguka..... kumbe ukuta huo ni mlango maalumu wa chumba chake chasiri... chumba hicho hakuna anayekijua zaidi yake.... hata fundi aliyetengeneza mlango huo ukafanana na ukuta..... aliuwawa usiku huohuo baada ya kumaliza kutengeneza.... Fundikila aliamua kumuangamiza fundi huyo ili asije akatoa siri.. kwa kuwasimulia mafundi wenzake huko mitaani kuwa nyumba ya Tajiri Fundikila inachumba cha siri ndani yake.... Fundikila akaingia ndani ya chumba hicho.. akaufunga mlango,,kisha akasimama katikati ya chumba hicho.... mara nyingi alikitumia kwa kuomba chochote anachokitaka na kinakuja kimiujiza wakati huohuo..... lakini usiku wa leo Fundikila aliingia ndani ya chumba hicho kwa lengo tofauti!!! akanyoosha mkono wake likajitokeza joho lenye rangi nyeusi na rangi nyekundu.....kisha akanyoosha mkono mwingine ikajitokeza ile fimbo ya dhahabu.. akavua pete yake ya dhahabu... vitu vyote hivyo hajavipata duniani... alilewa huko kuzimu kutoka kwa Lucifer! akavitupa chini kisha akatazama kando kikajitokeza kiberiti.. Fundikila alikuwa na uwezo wa kuomba chochote kile atakacho kwa sababu tayari ni mtumwa/mfuasi wa Lucifer! akaamua kuvichoma moto vitu hivyo kisha akatoka kwenye chumba hicho na kurudi kule chumbani kwa mke wake! akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi! ******************** Asubuhi lalipokucha,, mke wa Fundikila alidamka mapema kama kawaida yake.. akaingia jikoni na kuandaa chai kwa ajili ya mumewe.. alipomaliza akaweka chai na chapati,,maya, matunda,, juisi kwenye meza ya chakula,,kisha akazipiga hatua kuelekea chumbani.... akamkuta Fundikila akitoka bafuni... akamuandalia mavazi,, Fundikila alipomaliza kuvaa akatoka chumbani akaelekea sebuleni kwa ajili ya kupata chai... baada ya dakika kadhaa alimaliza.. kisha akamuaga mkewe kwa kumbusu shavuni! akazioiga hatua kutoka nje.... macho yakamtoka!! hakuliona gari lake.. akajisemea moyoni,, "huyu mwizi kaingiaje humu,,pasipo mimi kusikia! wacha niwahi kutoa taarifa kwenye vyombo vya dora... haiwezekani gari langu la kifahari liibiwe hivi hivi..... akatimua mbio mpaka barabarani.. akakodi taxi.. akaelekea kwenye kituo cha polisi kutoa taarifa.. alipofika.. akaandikisha maelezo.. yule askari akaanza kumuhoji,, akasema,, "nitajie namba ya gari lako! Fumdikila akataja. yue askari akatazama namba ya gari aliyoitaja Fundikila.. lakini haikuwemo katika kitabu cha ofodha. ....askari huyo akasema,, "mbona hakuna namba hiyo... inaonesha kuwa haijawahi kutumika,, yaani kusajiliwa......akaendelea kusema,, "ebu kalete kadi ya gari lako... Fundikila akaomdoka akarudi ndani ya taxi na kuelekea nyumbani kwake.. alipofika akapitiliza mpaka chumbani kwake.. akafungua droo anayoitumia kuweka vitu vyake vya thamani... zikiwemo nyaraka zake muhimu. macho yakamtoka hakuona kitu chochote! droo hiyo ilikuwa tupu! akamuita mkewe.... akamuuliza,, "vitu vilivyokuwa humu kwenye droo umeviweka wapi? mkewe akastaajabu.. akasema,, "tangu umenioa,sijawahi kufungua hiyo droo..wacha nikusaidie kutafuta. huenda uliweka sehemu nyingine... wakaanza kutafuta kila pande ya chumba hicho.. lakini hawakuona chochote.. akazipiga hatua.. akatoka mpaka nje ya geti.. Fundikila alitembea kwa haraka nusu akimbie...akafungua geti kisha akamfuata yule dereva tax.. alipomkaribia akatoa pochi ya mfukoni(warlet) alipoifungua macho yakamtoka!! haikuwa na pesa hata shilingi.. pia kadi yake ya benki haikuwemo.. akazidi kuchanganyikiwa.. akaingia ndani ya taxi,, akasema nipeleke CRDB BANK,, bila kuchelewa dereva akaliwasha gari lake akafuata maelekezo ya mteja wake. bada ya dakika kadhaa walifika.. Fundika akashuka kutoka ndani ya gari hilo.. akazipiga hatua za harakaharaka huku akijikwaa... akahisi tai aliyokuwa kaifunga shingoni mwake inaongeza uzito akaamua kuivua na kuiweka mfukoni..... akaingia ndani ya benki hiyo... akamfuata muhudumu wa benki na kutoa taarifa za upotevu wa kadi yake ya benki... yule muhudumu akatazama kwenye kitabu cha orodha.. lakini halikuonekana jina la Fundikila.. Fundikila akasema, "mimi ni mteja wenu na mara ya mwisho kutoa pesa ni jana mchana.... iweje mniambie sina akaunti kwenye benki yenu... ebu acheni utani... wale wahudumu wakatazamana.... wakahisi huenda Fundikila kapatwa na ugonjwa wa akili!!! kisha wakabaki wakimtazama... Fundikila akaamua kutoka nje ya benkk hiyo.. akaingka ndank ya taxi.. akasema,, "nileleke posta ya zamani.. baada ya nusu saa wakawa wamefika.. Fundikila akashuka kutoka ndani ya gari.. akazipiga hatua kuelekea kwenye kampuni yake angalau akachukue pesa amlilpe yule dereva taxi... alipolikaribia jengo la kampuni hiyo... likatoweka mimiujiza!!! ITAENDELEA............ wingi wa like zenu ndizo zitafanya niilete hadithi hii ya bure kwa wakati.... Lik)

at 3:30 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top