Home → simulizi
→ Riwaya : ROHO YA GIZA
SEHEMU YA KWANZA(01)
Hahahaha huu ni ujinga uliokithiri.. yawezekana vipi kuabudu na kuamini kitu usichokijua... eti Mungu Mungu,, ebu niambie wewe umeshawahi kumuona?
yalisikika maneno akiyaongea kijana mmoja aitwae, FUNDIKILA,,,akiwaambia wenzake,,,Fundikila hakuwa na imani kuwa Mungu yupo,,, badala yake yeye aliamini kuwa kazaliwa tu,, hajaumbwa na Mungu kwa mfano wake! watu walimshangaa sanaa, waengine walimuita Mpagani,, (mtu asiye na dini)
Maisha yalizidi kusonga,,Fumdikila alikuwa na maisha mazuri,, alikuwa anamiliki magari ya kifahari pamoja na majumba ya kifahari.. lakini hakuna hata mmoja aliyefahamu kazi anayoifanya Fundikila!
Kumbe Dundikila alikuwa anamuabudu Shetani(satan) kwa kumtumikia kimatendo na kimwili... kwa kuyafuata yale yasiyompendeza Mungu..
Siku moja Fundikila,, alidamka majira ya saa tisa za usiku.. akatoweka kimiujiza na kwenda kwenye dini yake anayoiamini kuwa ndiyo dini sahihi...dini ya kishetani(satan)
wafuasi wote wa dini hiyo walikuwa wanakutana usiku wa manane kuanzia saa tisa na dakika moja.(Mid night) katika jumba moja kubwa...jumba hilo huwezi kuliona nyakati za mchana,,, linaonekana nyakati za usiku tu.. ambapo Fundikila pamoja na wafuasi wenzake,,nyakati za usiku kwao ni mchana.
walikutana ndani ya jumba hilo kila jumatatu,, jumatano na jumamosi....kwa ajili ya vikao na mikakati ya mioango yao ya kuzimu.
siku ya leo kilikuwa ni kikao maalumu.. akaonekana kiongozi mkuu wa dini hiyo ya kishetani akizipiga hatua na kusimama mbele yao... wakanyanyua mikono yao kwa kufanya ishara ya kumsujudia... kisha akasema,, usiku wa leo ni lazima kila mtu atoe kafara la damu.... pia kwa wale wakongwe wa dini hii waliowahi kutoa kafara zaidi ya mara 29... wao hawatausishwa na kafara tena.....
Kumbe miongoni mwa wafuasi wapya na Fundikila alikuwemo. hivyo kafara linamuhusu!
ilipofika saa tisa na dakika 59 kikao kikafungwa na wafuasi wote wakatoweka kimiujiza kurudi majumbani mwao! isipokuwa wale wafuasi wageni wanahitajika kutoa kafara kabla jua halijachomoza.... hivyo Fundikila akajitokeza nje ya club(kumbi ya starehe) moja ambayo huwa inatumbuiza mziki kuanzia siku ya ijumaa jumamosi na jumapili..
jumamosi ya leo wapenda starehe walikuwa wengi sana ndani ya club hiyo(kumbi ya starehe)
kwa mbali akaonekana mwanaume mmoja akitokea mdani ya club hiyo, akiwa kaongozana na mwanamke mmoja,,watu hao walionekana wamezidiwa na ulevi! walitembea huku wanayumba yumba,, yawezekana wamekunywa pombe kupita kiasi!
wakaingia ndani ya gari,, na kuondoka zao!
Fumdikila alikuwa anawatazama tangu walipotoka ndani ya club mpaka wanavyoingia ndani ya gari.... akajisemea moyoni,, "watu hawa ni halali ya kafara ninalohitajika nilifanye kabla jua halijachomoza.....Fundikila akatoweka kimiujiza,,,
Wale walevi wawili walionekana wamo ndani ya gari,, mwanaume huyo alikuwa analiendesha gari kwa mwendo wa kasi ya ajabu... punde si punde Fundika akajitokeza katikati ya barabara,, yule dereva alipojaribu kukwepa gari likayumbayumba likatoka barabarani,,ikatokea ajali mbaya ya kutisha hakuna aliyepona...
Fundikila akatabasamu kisha akatoweka kimiujiza,,akajitokeza nyumbani kwake... akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi.
siku zilizidi kusonga,, utajiri wa Fundika ukazidi kuongezeka kila kukicha...
Sikumoja nyakati za usiku,, wakiwa katika kikao.... Fundikila akawasilisha ombi.. kuwa anahitaji kuoa.!
kiongozi mkuu akasema,, "ni wazo zuri lakini kunamasharti.... nyakupasa umwage damu ya watu 11 ndani ya siku 11..namaanisha kila siku na usiache hata siku moja mpaka siku 11 zitimie. macho yakamtoka Fundika! akajisemea moyoni ,,"mbona masharti magumu kiasi hiki.. nitaweza kweli?
akajipa imani kuwa ataweza.... kisha akamtazama kiongozi wao na kusema,, "bila shaka nitatekeleza masharti.
kesho yake palipokucha.. Fundikila akatafuta mtu wa kumtoa kafara,,..akafanikiwa akamtoa jirani yake kwa kumuita nyumbani kwake.. kisha akampa chakula chenye sumu inayouwa ndani ya masaa 12.
kesho yake pia akamuuwa jirani yake mwingine aliyekuwa anaishi nyumba ya nyuma kutoka nyumbani kwake!
siku iliyofuata pia akamtoa kafara mmoja kati ya watoto wanaoishi mtaani hapo!
watu wakastaajabu sanana kuona vifo vya mfululizo.... kila siku.....Fundikila aliendelea kutoa kafara kila siku.
hatimae wakatimia watu tisa wakabaki wawili.....
wiku ya leo akiwa kwenyeharakati za kutafuta mtu wa kumi amtoe kafara akakutana na mwanamke mrembo kupita kiasi.. akajikuta amezama kifikra juu ya mwanamke huyo... akamuita,,
mwanamke huyo akaitikia wito,,, bila kuchelewa Fundikila akaanza kumchombeza...
mwanamke huyo akajikuta anakubali pasipokujitambua.. alikubali kila neno aliloliongea Fundikila............ wakabadilishana namba za simu,,,kisha Fundikila akasema nitakutafuta keshokutwa. mwanamke huyo akaondoka zake.
ilipofika majira ya saa moja za usiku.. Fundikila akiwa ndani ya gari lake... akaona watoto wanacheza kando ya barabara..... akajisemea moyoni.. wacha nirahisishe kazi.
mojawapo kati ya watoto hao wawili ni halali ya kafara langu.
Bila huruma Fundikila akaliendesha kwa kasi gari lake na kumgonga mmoja kati ya wale watoto wawili!
mtoto huyo akapoteza maisha papohapo.l!
Fundikila hakupunguza mwendo wa gari lake aliliendesha kwa kasi mpaka nyumbani kwake.......
alipofika akaliegesha gari lake la kifahari ndani ya uzio wa ngumna yake.. akashuka na kuingia ndani ya jumba lake la kifahari... akajisemea moyoni,, "nimebakiza kafara moja.. hii ni kazi ndogo... nimekula ng'ombe mzima nitashindwa mkia?
kesho yake Fundikila alidamka akaingia ndani ya gari lake na kuondoka.... aliwa matembezini.. wazo likamjia akajisemea moyoni,, "leo nitaifanya kazi ya kutoa kafara usiku...
ilipofika majira ya saa moja za jioni... Fundikila akaliendesha gari lake mpaka nje ya mji,, akaliegesha kando ya barabara akisubiri mawindo ya kafara la mwisho.. ili watimie watu 11 aliyoimwaga damu yao kwa ajili ya kafara.
************************************
Upande mwingine alionekana Mchungaji ndani ya gari akiwa na familia yake ...mchungaji huyo alikuwa ametokea kwenye mahuburi ya injili takatifu....
kumbe barabara anayopita ndio ile barabara aliyokuwepo Fundikila kwenye mawindo ya kafara la mwisho... Fundikila akasikia mngurumo wa gari likiendeshwa kwa kasi..
akajisemea moyoni,, wacha nikamilishe kafara...
gari la mchungaji lilipo karibia eneo hilo alilokuwepe Fundikila,,, akajitokeza kimiujiza katikati ya barabara akajibadilisha kuwa jiwe kubwa kiasi,, mchungaji akaona jamba hilo akaanza kusali owa imani pasipo kukwepa akaligonga jiwe hilo likaruka kando.. punde si punde likabadilika na kuwa binadamu! ambaye ni Fundikila
Fundikila aliumia sana akavunjika mguu.. na kupotza fafamu.....Mchungaji akaliegesha gari lake kando akashuka kutoka ndani ya gari na kuelekea pale alipokuwa amedondoka Fundikila.
ITAENDELEA............
wingi wa like zenu ndizo zitafanya niilete hadithi hii ya bure kwa wakati....
Like pia share na marafiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: