Home → simulizi
→ Riwaya : ROHO YA GIZA
SEHEMU YA PILI(2)
Upande mwingine alionekana Mchungaji ndani ya gari akiwa na familia yake ...mchungaji huyo alikuwa ametokea kwenye mahuburi ya injili takatifu....
kumbe barabara anayopita ndio ile barabara aliyokuwepo Fundikila kwenye mawindo ya kafara la mwisho... Fundikila akasikia mngurumo wa gari likiendeshwa kwa kasi..
akajisemea moyoni,, wacha nikamilishe kafara...
gari la mchungaji lilipo karibia eneo hilo alilokuwepe Fundikila,,, akajitokeza kimiujiza katikati ya barabara akajibadilisha kuwa jiwe kubwa kiasi,, mchungaji akaona jamba hilo akaanza kusali owa imani pasipo kukwepa akaligonga jiwe hilo likaruka kando.. punde si punde likabadilika na kuwa binadamu! ambaye ni Fundikila
Fundikila aliumia sana akavunjika mguu.. na kupotza fafamu.....Mchungaji akaliegesha gari lake kando akashuka kutoka ndani ya gari na kuelekea pale alipokuwa amedondoka Fundikila.
******ENDELEA*****
kabla hajamkaribia,, akajitokeza kiongozi mkuu muwakilishi wa shetani hapa duniani... akamchukua Fundikila na kutoweka nae kimiujiza.. pia gari la Fundikila likatoweka kimiujiza! wakajitokeza ndani ya nyumba ya Fundikila...
Mchungaji akashtuka akataja jina la Mungu... huku akisema,, "wewe ndiye muweza wa yote,, naamini haukupanga nipatwe na jambo hili mimi mtumishi wako.. kisha akarudi ndani ya gari na kuliwasha akaondoka zake,, mkewe akamuuliza kunatatizo gani mbona kama haupo sawa? pia watoto wake wakauliza,, "baba nini kimetokea?
kwa imani ndogo ya kiroho,, wenyewe hawakuweza kuona kilichotokea!
mchungaji pekee ndiye aliona jambo hilo,, akasema,, "wacha tufike nyumbani nitawasimulia kilichotokea.
wakati huo huo kule nyumbani kwa Fundikila alionekana akiguswa mguu na kiongozi mkuu wa wafuasi wa shetani hapa duniani....punde si punde mguu wa Fundikila ukajiunga na michubuko ikatoweka mwilini mwake akarudi katika hali yake ya kawaida.
ilipofika majira ya usiku wa manane.. Fundikila akadamka akavaa joho refu lenye Rangi nyekundu na nyeusi....vazi hilo ni maalumu kwa kuomba msamaha kwa Shetani.. kisha akachukua fimbo na kutoweka kimiujiza!! akajitokeza kwenye dunia nyingine tofauti na dunia ya kawaida... sehemu hiyo ilikuwa inatisha kupita kiasi ilizungukwa kwa moto pande zote,,akanyoosha ile fimbo ya dhahabu,, akiwa kaishikilia mkono wa kushoto.. huku mkono wake wa kulia kauweka juu ya kifua chake....ishara ya kuhitaji kuonana ana kwa ana na Shetani(Lucifer) punde si punde akajitokeza Lucifer.
Fundikila akainamisha uso wake chini akasujudu kisha akasema,, "ewe mtukufu naomba unisamehe kwa kushindwa kukamilisha sharti la kafara moja la mwisho.
naomba unipe nafasi nyingine tena,, nakuahidi kesho nitatimiza.
Lucifer akasema,,"ombi lako limekubaliwa lakini kuna shart la mwisho ambalo itabidi ulifuate bila kupinga.... sharti hili utajulishwa baada ya kukamilisha kafara la mwisho na ukishafunga ndoa.
Lucifar akatoweka kimiujiza,, pumde si pende pia Fundikila akajitokeza mdani ya chumba chake... akapanda kitandani na kuutafuta usingizi.
************************************
Asubuhi palipokucha Fundikila alidamka mapema. akaingia bafuni akaoga kisha akatoka nje ya nyumna yake akaingia ndani ya gari na kuondoka zake kwenda kutafuta mtu wa kumtoa kafara....akiwa njiani akamuona fukara(ombaomba)
fukara huyo ni mlemavu wa miguu hajiwezi,,
Fundikila akaliegesha gari lake kando ya barabara akachukua chupa ya juisi akaifungua akaweka sumu maalumu inayouwa ndani ya masaa 12.. kisha akashuka kutoka mdani ya gari akazipiga hatua mpaka pale alipokuwepo mlemavu huyo. ombaomba... alipomkaribia akamkabidhi ile chupa ya juisi kisha akarudi zake ndani ya gari....
mlemavu huyo akaifungua chupa ya juisi hiyo,,kutokana na njaa kali pamoja na kiu,, akainywa kwa pupa...
Fundikila akatabasamu kisha akaliwasha gari lake na kurudi zake nyumbani!
ilipofika majira ya saa tisa za usiku,,, Fundikila akiwa usingizini ikasikika sauti ikimwambia umefanikisha jambo lako... sasa waweza kufunga ndoa. Fundikila akashituka kutoka usingizini.. akaona pete mbili za dhahabu kwa ajili ya ndoa... ni lazima azitumie pete hizo kumvisha mkewe pamoja na yeye mwenyewe.
Siku zilizidi kusonga Fundikila akamptafuta yule mwanamke aliyekutana nae sikuile wakabadilishana namba za simu... wakaanzisha mahusiano ya kimapenzi... hatimae Fundikila akaenda nyumbani kwao mwanamke huyo aitwae DORA...
wazazi wa Dora wakafurahi sana binti yao kuolewa na tajiri...
Dora pia alifurahi kwa sababu kila akipata mchumba na kumpeleka kumtambulisha,, wazazi wake walikataa wakidai kuwa hawawezi kukubali aolewe na masikini fukara.
mipango ya harusi ikafanyika na ndoa ikafungwa.
******BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA*********
Fundikila akapewa masharti kuwa asimpe ujauzito mkewe vinginevyo atapata matatizo makubwa katika maisha yake,, huenda akafa kabisa.. anatakiwa aishi pasipo kupata mtoto!
jambo hilo lilimnyima furaha Fundikila,,akajisemea moyoni,, "sasa huu sio ufahari ni adhabu,, nani atakuwa mrithi wangu..... je mke wangu atanielewa kuishi nae pasipo mtoto!
Fundikila akaitikia kwa shingo upande......baada ya kikao kuisha akajitokeza nyumbani.. wakati huo mkewe alikuwa kalala usingizi mzito hakuweza kujua mumewe hakuwemo ndani ya nyumba...kwa sababu alifumbwa kimiujiza na ni mwiko kwa ambaye sio mwanachama kuona jambo hilo!
siku zilizidi kusonga,,hatimae mke wake akashika ujauzito! Hilo ni kosa kubwa amelifanya Fundikila!
baada ya siku kadhaa kupita mauzauza yakaanza kuiandama nyumba yake....
siku moja nyakati za usiku Fundikila pamoja na mkewe wakiwa wamelala...
kiongozi mkuu wa wafuasi wa Lucifer akajitokeza chumbani kwa Fundikila..
ITAENDELEA............
wingi wa like zenu ndizo zitafanya niilete hadithi hii ya bure kwa wakati....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: