MANUFAA KATIKA NDOA 1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya kiislamu. 2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika hadithi sahihi: “Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu.” [Ahmad] 3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu inayosema kuwa: “Binaadamu anapokufa, basi ‘amali zake nzuri hukatika au humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea du’aa mzee/wazee wake.” [Riyadhus-Swaalihiyn] Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni: 4. Kinga kutokana na Shaytwaan katika mambo yanayopelekea au yanokaribisha tendo la zinaa. 5. Utulivu wa akili na moyo na kuwa na urafiki ambao hupelekea mapenzi na huruma baina ya mume na mke. 6. Kunganisha kwa Familia za pande mbili za ukeni na uumeni. 7. Kusaidiana katika kazi za nyumba (sio kumuachia mke kazi zote za ndani ya nyumba). Hii ni tabia ambayo ingalipo kwa baadhi ya akina baba. Kwa vile tabia hii imekuzwa na utamaduni wetu wa tunakotoka, kinyume kabisa na maamrisho ya dini yetu ya Kiislamu yanavyotuagiza. 8. Kuelimishana majukumu ya kifamilia. Pia kuweka bidii na kuwa tayari kuihami na kuitunza familia. Na vile vile kuishughulikia na kuitimizia mahitaji yake yakiwa ama ya (kimwili, kimavazi, kisiha, kimawazo na kiroho) na kustahamiliana pale panapotokea kutoelewana.

at 12:51 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top