Home → ushauri
→ MATATIZO KATIKA NDOA
Wakati huo huo kuna matatizo yanayopatikana katika ndoa ambayo inabidi tuzingatie na kujichunga ili tuepukane na matatizo hayo. Nayo ni kama yafuatayo:
1. Kushindwa kuchuma pato la halali, ambapo itapelekea kutafuta njia ambazo si za halali za kimapato ili kuweza kutimiza mahitaji ya familia. Haimfalii mke kumlazimisha mumewe ampatie mambo yaliyo nje ya uwezo wa mume. Na tuwaige wanawake wema waliopita, ambao kila waume zao wakitoka kwenda kwenye shughuli zao za kutafuta riziki, wakiwausia kuwa wasirejee na chochote cha haramu. Wakiwanasihi waume zao kuwa ni bora wastahamili kwa njaa ya hapa duniani kwani adhabu ya kesho Aakhirah sio ya kustahamilika.
2. Kushindwa kutimiza majukumu ya ndoa, na hasa kutimiza haki za mke au kutoweza kustahamili kwenye wakati mgumu wa kimaisha. Na tuwe makini katika suala hili kwani kuna ile dhana ya kuwa ndoa ni jambo la kujionyesha tu kuwa fulani kaoa au kaolewa.
“Kila mmoja kati yenu ni mchungaji, na kila mmoja kati yenu atapaswa kuulizwa ya juu ya kile anachokichunga. Mume ni mchungaji wa familia yake, naye atapaswa kuulizwa juu ya anaowachunga. Na mke ni mchungaji wa nyumba ya mumewe, naye pia atapaswa kuulizwa juu ya anachokichunga. Hivyo basi, kila mmoja kati yenu ni mchungaji ambaye atapaswa kuulizwa juu ya anaowachunga” [Al-Bukhaariy na Muslim]
3. Kuacha kushughulikia mambo muhimu ya kidini, kwa mfano kutumia muda mwingi katika mambo ya anasa za kidunia kama vile kuangalia Televisheni, kwenda kwenye shehere za kuzaliwa mtoto au kwa kutimiza umri fulani wa mtoto (birthday party), badala ya kutumia muda huo kwa kutengeneza maisha ya Aakhirah ambayo ndio ya milele. Kama tunavyotanabahishwa kwenye Quraan Tukufu:
“Enyi mlioamini! Yasikusahaulisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Allaah. Na wenye kufanya hayo ndio walio katika khasara.” [Al-Munaafiquun 63: 9]
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: