Home → Love sms
→ ππΊ *MKE NYUMBANI*πΊπ
.
Asalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh. Wapenzi ninaokupendeni kwa ajili ya Allah..Mara nyingi binadamu kwa kutokuelewa tunajikuta tunazidhulumu nafsi zetu kwa kuzitesa na kuzisononesha eti tu kwa sababu huyu mwanamke nimempenda, au huyu mwanamume ninampenda basi lazima tuoane. Na huku huyajui yaliyomo ndani ya moyo wa mwenzako pengine hakupendi na hana malengo ya kuoana nawe. Hebu tujifunze kuyaweka mambo yetu mikononi mwake Allah. Niazimeni macho yenu kwa muda mchache, niwape kisa kidogo mkichukue kwa moyo mkunjufu ili nanyi muwafikishie wengine ambao hatupo nao katika group hili. Sasa tulizeni akili zenu na zitulie tuli, huko Makkah alikuwa Baba mmoja alimpenda Binti fulani kwa mapenzi makubwa hata akatamani awe mke wake! Safari ya Safari ya kutuma Shangazi zake kwenda kwao yule Binti kumhabarisha kuwa, kijana wao anahitaji kumuoa ikawadia. Siku hiyo ilikuwa ni siku nyeusi na chungu mnoo kwa yule kijana kwani hakujua ni majibu gani atayapata toka kwa yule binti. Aliendelea kubaki sebuleni kwake, akazima tv, redio, na hata simu yake ya mkononi hakutamani kuisogelea. Licha ya kwamba jiji la Makkah kwa wakati huo ilikuwa ni msimu wa baridi lakini kijana mwili ulilowa jasho kwa wahka wa kusubiria majibu kutoka kwa mkewe mtarajiwa. Subhana Allah!! Subhana Allah!!..Hivi wapenzi zangu mnaweza mkaamini kwamba hata panya alipogusa mlango kijana aliuendea kuufungua kwa bashasha na huku akisema;"Karibuni Shangazi zangu"..Looh!! maskiniii kumbe ni panya alipita zake
mlangoni, yeye alitarajia ni Shangazi zake wamerejea kuleta majibu. Hatimaye Shangazi zake wakarejea na jibu fupi sana lenye ujumbe uliovunjavunja matumaini, malengo, dhamira, na ndoto zote za kumuoa yule binti mrembo aliyemnyima usingizi na kuukondesha moyo wake, ni kwamba, kijana alikataliwa!!!. Maskini yule kijana usiku ule ulimuwia mchungu na kuamua kumpelekea habari ile Sheikh wa eneo lile na kumuomba akambembeleze yule binti ili tu, apate kumuoa! Jitihada za Sheikh ziligonga mwamba kwani binti alikataa!!.. Wakati yule kijana akiendelea kutafakari kwa nini alikataliwa, akapata habari kuwa yule binti ameolewa, tena ameolewa na rafiki yake yule kijana..Kijana aliumia, akaiona dunia ni chungu mnoo, ukawa ni wakati mgumu saana kwake zaidi ya kumeza jiwe! Sasa tutazame kilichoendelea baina ya yule binti na mume wake,..Ndani ya mwezi mmoja wa ndoa yule binti alianza kuumwa, akapelekwa hospitali kubwa, maana aliyemuoa pia alikuwa na pesa hospital inaitwa King Abdul aziz university hospital inapatikana jeddah kama maili 70 toka mji wa makkah,,maskini binti alikutwa na kansa ya matiti, ikalazimu akatwe titi moja, na hata baada ya hapo mgojwa hakupata nafuu ikabidi madaktari wamshauri kumpeleka Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi..Safari ya Marekani ikaanza, na huko pia madaktari walipofanya uchunguzi, wakakuta kansa imesambaa zaidi hivyo wakakata na lile titi lililobakia!!..Matibabu yalikuwa ghali sana, hivyo mumewe,aliagiza iuzwe nyumba yake ili atumiwe pesa za kugharamia matibabu na kujikimu..Maskini baada ya miezi miwili wakiwa bado hospitali mkewe akafariki dunia, ni kwa sababu vidonda havikupona..Na huku akimwacha mumewe hana nyumba tena na wala hana akiba benki kwa ajili ya matibabu ya mkewe!! Furaha iliyodumu ndani ya ndoa hii ilikuwa ni kwa muda wa siku 30 tu!!! Tizameni jinsi gani Mwenyezi Mungu alimuepusha yule kijana asikutane na haya madhila!! Anasema Mwenyezi Mungu katika (suratul Baqarah, aya:216); "Lakini huenda mkachukia kitu, nacho ni kheri kwenu. Na huenda, mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua,( lakini)nyinyi hamjui."
B
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: