Riwaya: SARAI SEHEMU YA MWISHO. ***ilipoishia*** baba sarai aliamua kwenda kwenye kaburi la mke wake ili akaombe msamaha huenda mambo hayo yanajitokeza kwa makosa aliyoyafanya miaka ya nyuma.....akiwa njiani alisikia sauti ikimuita kutokea upande wa nyuma sauti hiyo iliita jina lake la kizaliwa ambalo lilikuwa halifahamiki.....ni watu wachache waliokuwa wakimuita jina hilo tena ni wa karib....alipogeuka nyuma aliogopa sana akastuka .......akataka kutimua mbio taulo likadondoka........akaliokota haraka alipojifunga kiunoni ghafla sarai alijitokeza....baba sarai alimkumbuka sarai kwa sababu ya kuonekana na sura ya ajabu...... ***Endelea*** Kisha sarai akatoweka kimiujiza...baba sarai akaanza kutimua mbio watu waliokuwa wanamfahamu..walimshangaa kumuona mtu aliyekuwa na majivuno ana dharau kwa ajili ya pesa zake leo hii anakimbia barabarani kifua wazi...yupo peku huku amejifunga taulo tu.... wakati huo baba sarai alikuwa hawajali watu waliokuwa wakimshangaa barabarani...alikimbia umbali mrefu sana alipohisi kachoka akaamua kupunguza mwendo na kusimama chini ya mti uliokuwa kando,..jasho lilikiwa likimtoka alikuwa anapumua kwa pumzi za kutweta...akaketi chini akatafakari sana akajiuliza""inamaana kumbe sarai yupo hai!!! mmh!!!! na kwanini yupo katika hali ya kimiujiza anapotea kama upepo....Eee Mungu....naomba unisamehe nimefanya maovu Mengi naomba unisimamie katika kila jambo kuanzia leo nimebadilisha tabia yangu... baba sarai alinyanyuka akazipiga hatua kuelekea kule kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na mke wake aliyemtelekeza pamoja na mtoto mchanga miaka mingi iliyopita.......alipofika alilifuata kaburi la mama sarai lililokuwa kando ya nyumba....akaanza kuomba msamaha uku machozi yakimtoka...baba sarai alilia kwa uchungu mkubwa.....ghafla alihisi kunamtu kamgusa begani.....alipogeuza shingo yake alimuona sarai.....baba sarai akataka kutimua mbio sarai akasema"""usikimbie baba...napenda kukwambia USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO.....umeishi maisha ya kuhangaika bila kuhua chanzo chake ni nini....sikuzote binadamu wanajikuta wakipata matatizo na maisha yao kuwa magumu pasipo kutegemea.....kwa kutokujua makosa waliyoyafanya...na kubaki kumlaumu Mungu kwa nini amewaumba....ulimtelekeza mama yangu pamoja na mimi nikiwa mtoto mchanga wa siku moja.....kisha sarai akaanza kumsimulia baba yake juu ya kifo cha mama yake.....ilikuwa hivi......sikuile nyumba ya mama saradi ilipokuwa inateketea kwa moto...mama sarai alimchukua sarai na kumtoa nje ili aokoe maisha ya mtoto sarai......mama sarai aliporudi upande wa ndani ili aokoe pesa za mauzo ya wiki ya dukani kwake.....hakufanikiwa kutoka hai..aliteketea kwa moto mdani ya nyumba.....wakati sarai yupo nje alichukuliwa na mzee mmoja aliyekuwa mganga.....kwa lengo la kumtoa kafala sarai kwa sababu mzee huyo alikuwa akitafuta mtoto mdogo kwa ajili ya shughuri zake za kichawi...lakini alipojaribu kutaka kumchinja ....sarai aliongea akasema"" kwa nini unataka kuniuwa????? ninakosa gani??? mzee yule alistahajabu sana alishangaa yawezekana vipi mtoto wa miezi mitano akaongea kama mtu mzima....yule mzee mchawi aliamua kuacha kumuuwa sarai....tangu siku hiyo akaishi nae kama mtoto wake... sarai alipofikisha umri wa miaka kumi na nne...mzee yule alimrisisha uchawi na wiki hiyohiyo yule mzee alifariki...sarai akaamua kutumia uchawi huo kuwaadabisha watu waliokuwa wakiwanyanyasa binadamu wenzao.na hata ule mfupa alioutumia kutengeneza filimbi ulikuwa ni mfupa wa mkono wa mama yake alitengeneza filimbi hiyo ishara ya kumkumbuka mama yake...... akaamua kumuadabisha baba yake kwa kumpa mitihani ya kimaisha ili ajifunze na ajutie kosa alilolifanya miaka mingi iliyopita kwa kuitelekeza familia yake........ wakati sarai akimsimulia baba yake mambo hayo.....baba sarai alilia kwa uchungu huku akimuomba msamaha mtoto wake sarai...... sarai alimsamehe baba yake...akasema"" nimekusamehe baba yangu....baba sarai akamsogelea mwanae wakakumbatiana....kisha sarai akasema ishi kwa furaha na amani...... wapende ndugu jamaa marafiki na majirani zako kama unavyojipenda wewe mwenyewe......nenda nyumbani kwako nitakuja kukutembelea baadae.. kisha sarai akatoweka kimiujiza....baba sarai aliamua kutoa nyasi zilizokuwa zimeota kulizunguka kaburi la mama sarai...alipohakikisha hakuna nyasi hata moja..akasali kumuomba Mungu amlaze mama sarai mahala pema peponi.. kisha akaondoka zake kurudi nyumbani kwake. kesho yake alidamka asubuhi na kwenda kazini alipofika wafanyakazi waliokuwa chini yake walistahajabu kumuona bosi wao anaongea kwa sauti ya taratibu na maneno ya ukarimu..tofauti na siku za nyuma alizokuwa akiwafikea bila sababu wakati mwingine aliwapiga makofi na mitama..yeye kwake ilikuwa ni jambo la kawaida... kisha akaitisha kikao cha dharura akaomba msamaha kwa ubaya wote alio watendea.. walimsamehe....tangu siku hiyo wafanyakazi wa kampuni hiyo waliifurahia kazi yao...walikuwa naamani sana hata utendaji wa kazi ukaongezeka kwa sababu walifanya kazi kwa uhuru sana... kampuni ilipata sifa kwa kuwa kampuni bora inayohusika na usafirishaji hapa nchini......mkurugenzi alimpandisha cheo baba sarai na kumkabidhi kampuni hiyo aisimamie....yeye akafungua kampuni nyingine.. sikumoha sarai alikuja nyumbani kwa baba yake...baba sarai alifirahi sana akasema tafadhali mwanangu naomba tuisha pamoja kwenye nyumba hii....sarai akakubali wakakumbatiana tangu siku hiyo waliishi pamoja mpaka leo hii maisha ya baba sarai yakawa mazuri yenye amani na furaha.. *********MWISHO WA SIMULIZI HII********* ASANTENI.

at 1:20 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top