Story......... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya Nne (4) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp... 0769673145 ilipoishia....... Kwa upande wa kina zaza usiku ule ule walianza kupanga mikakati ya kumteka Frank na kwenda kumtupa mbali kabisa na jiji la dar es salam. Lakini hii ilikuwa kazi ngumu Sana ambayo walihitaji pesa za kutosha na pia wachore ramani ya sehemu watakayoenda kumtupa Frank. .......... Endelea........... Zaza pamoja na wenzake waliumiza kichwa, na hatimaye mmoja wao akapata wazo ambalo moja kwa moja aliliweka hadharani kwa wenzake ili waweze kulifikiria kama ni wazo zuri. " mimi nina watu wangu nawafahamu, ni watu wazuri sana Katika kazi hizi hata kuua kwao ni kitu kidogo tu, hivyo naona tuwape hili dili warusaidie. " aliongea kijana huyo akiwasilisha Wazo Lake. " Wazo zuri Sana mi naungana na wewe moja kwa moja Sasa inabidi utueleze tunawapataje hao watu. " akaongea zaza kumuuga mkono kijana yule. " ninafahamu makao yao kama vip tuongozane mpaka kwao." akaongea kijana yule, na moja kwa moja zaza pamoja na wenzake wakanyanyuka na kuingia kwenye gari Lao na kuanza safari ya kuelekea kwa watu hao. Hapakuwa mbali Sana na sehemu waliyokuwepo, hivyo baada ya dakika chache waliwasili sehemu hiyo. Wakashuka kwenye gari na kubisha hodi kwenye nyumba kubwa iliyokuwa mbele yao. Hakuna mtu aliyewaitikia ndani ya dakika tano wakiwa bado wapo pale mlangoni, lakini ghafla walishtukia wamezungukwa kila sehemu na watu wasiopungua kumi huku wakiwa na bunduki kila mmoja. "mko chini ya ulinzi mikono juu na mjitambulishe nyie ni nani." ikasikika sauti ikiwaamuru wakina zaza. "zaza pamoja na wenzake walitiii na kuweka mikono juu, Kisha zaza akajitambulisha kwa niaba ya wenzake. Zaza pamoja na wenzake walieleweka vizuri Kisha wale watu wakashusha silaha zao chini na kuwakaribisha wakina zaza Katika jumba Lao. " Elezeni shida yenu hatuna muda wa kuangaliana hapa." ikasikika sauti ikiwaambia wakina zaza. Zaza bila kusita alianza kuelezea mipango ya kumteka Frank na kuwataka wao wakawasaidie tu kumtupa mbali na jiji la dar es salam. "hiyo ni kazi ndogo Sana lakini inahitaji pesa kiasi cha shilingi million kumi." ikasikika tena Ile sauti ikiwaambia wakina zaza. "pesa si tatizo pesa Zipo za kutosha." akajibu zaza. "bas vizuri Sana tutawaelekeza namna ya kutupatia hizo pesa alafu mtatuletea huyo kijana mtuachie tumfanyie kazi." ikasema sauti ile. "hamna shida." akajibu zaza. Na muda huo wakapewa maelekezo namna ya kuwaingizia pesa zao, na bila kupoteza muda. Zaza pamoja na wenzake waliondoka usiku ule ule na kuwasiliana mzee Joel na kuwajulisha kias cha pesa wanachohitaji kulitimiza zoezi la kumteka Frank. Mzee Joel wala hakujali kama pesa ile ni nyingi kias gani, yeye alichotaka ni kuwatenganisha Frank na mtoto wake Penina . Usiku ule ule mzee Joel aliweza kuwakabidhi wakina zaza pesa zile na kuwataka wakina zaza wampoteze kabisa Frank lakini wasijaribu kumuua. Zaza pamoja na wenzake nao walizifikisha pesa zile kwa kikosi kile ambacho waliwapa kazi ile ya kumpoteza Frank. Baada ya kuwakabidhi pesa zile, walikubaliana kuwa siku inayofuata wataifanya kazi hiyo kama ipasavyo.* Asubuhi na mapema siku iliyofuata Frank akiwa bado yupo kitandani alishtushwa na mlio wa simu yake ikiita. Frank aliichukua simu yake na alipoangalia mpigaji akakuta ni kipenzi chake Penina. Bila kusita Frank akaipokea simu ile. "my love umeamkaje?" ilisikika sauti nyororo ya Penina ikimuuliza Frank. "nimeamka salama mpenzi wangu sijui wewe?" akajibu Frank na kumuuliza Penina pia. "mimi pia nimeamka salama kabisa mpenzi, na nimekupigia simu asubuhi na mapema kwasababu nataka leo tukanywe Chai wawili." akajibu Penina na kumuambia Frank. "ooh usijali my dear nipo kwa ajili yako kwa lolote lile." akajibu Frank. "ok nakupitia sasa hivi." Penina akamwambia Frank na kukataa simu. Frank muda huo huo alitoka kitandani na kuanza kujiandaa haraka haraka. * Lakini wakati huo huo zaza akiwa na kikos chake walikuwa tayari wameshawasili nyumbani kwa kina Frank kwa ajili ya kutekeleza kazi waliyoagizwa. Frank akiwa tayari ameshajiandaa aliwaaga wazazi wake na kutoka nje ya kwa ajili ya kumsubiri mpenzi wake Penina. Baada ya Frank kutoka nje Bila kutarajia alijikuta anapigwa chuma ya kichwa na kudondoka chini na kuzimia. Na waliofanya kitendo kile hawakuwa wengine bali ni zaza pamoja na wenzake. Haraka haraka Frank alibebwa na kuwekwa kwenye gari yao Kisha gari likaondolewa sehemu ile kwa kasi ya ajabu. Na wakati huo huo Penina ndio alikuwa anawasili na akapishana na gari la kina zaza likiwa Katika mwendo mkali, lakini yeye Penina hakufahamu chochote kinachoendelea. Penina alipaki gari mbele ya nyumba ya kina Frank Kisha akashuka kwa mwendo wa madaha huku tabasumu tamu likiupamba uso wake na kuanza kuelekea ndani kwa kina Frank. "hodi hodi jamani mpaka ndani." ilisikika sauti ya Penina ikibisha hodi lakini muda huo akiwa tayari ameshaingia ndani. "baba na mama shikamooni." akasalimia Penina. "marahaba karibu uketi ." wakaitikia kwa pamoja wazazi wake Frank. "hata sikai jamani nimekuja kumchukua mtoto wenu." akajibu Penina. "yupo nje mbona anakusubiri hujamuona?" akauliza mama yake Frank kwa mshangao huku akitoka nje. "yupo nje mbona sijamuona?" Penina naye akauliza huku akiongozana na mama yake Frank mpaka nje. "mhhh yuko wapi Sasa hebu ngoja nimpigie simu." akasema Penina huku akitoa simu yake na kumpigia Frank. Simu ya Frank iliita bila kupokelewa na alipopiga Mara ya pili akakutana na sauti hii, "simu unayopiga haipatikana kwa sasa tafadhali jaribu tena baadae." Taratibu Penina alianza kunyongonyea na kupoteza tabasumu Lake zuri usoni mwake. "simu haipatikani mama hebu sikiliza." Penina akamwambia mama yake Frank huku akimuwekea simu sikion. "hee mbona makubwa jamani kaenda wapi Sasa huyu Mara hii tu katoka ndani? ." akauliza mama yake Frank huku akiwa ameshika kiuno. Penina naye alizidi kupiga simu bila mafanikio yoyote ya kumpata Frank. Ilibidi mama yake Frank amwite baba yake Frank pamoja na Angel mdogo wake Frank ili wamtafute Frank kwa pamoja. * Gari ya kina zaza ikiwaa Katika mwendo mkali, zaza pamoja na wenzake walimfunga Frank miguu pamoja na mikono Kisha wakachukua kitambaa cheusi na kumfunga Frank usoni ili hata atakapozinduka asiweze kufanya chochote na pia asiweze kugundua sehemu anayopelekwa. Na Kisha simu yake ilipasuliwa kule ndani ya gari pale tu waliposikia ikipigwa na Penina. Moja kwa moja gari ile iliyombeba Frank iliwasili Katika jumba la kikosi kile ambacho wakina zaza walikubaliana nao kwenda kumtupa Frank mbali kabisa na jiji la dar es salam na kamwe asiweze kurudi tena. Baada ya kufikishwa hapo Frank alitolewa kwenye gari la kina zaza na kuwekwa kwenye gari lingine la kikosi kile kingine huku ndani ya gari lile kukiwa na vijana wengine wanne. Na wakati huo huo taratibu Frank alianza kurudiwa na fahamu Zake. Milango ya gari Ile aliyowekwa Frank ilifungwa, na Kisha gari likaanza kuondoka kwenda kumtupa Frank sehemu ambayo kamwe hatoweza kuonana tena na Penina. ........ Itaendelea

at 6:45 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top