Story........ NI WEWE TU PENINA Sehemu ya Tano (5) By GIVAN IVAN PHONE & WHATSAPP_____0769673145 Ilipoishia........... Na wakati huo huo taratibu Frank alianza kurudiwa na fahamu Zake. Milango ya gari Ile aliyowekwa Frank ilifungwa, na Kisha gari likaanza kuondoka kwenda kumtupa Frank sehemu ambayo kamwe hatoweza kuonana tena na Penina. ********Endelea ******* Zaza pamoja na wenzake walipongezana kwa kazi waliyoifanya na kuamini tayari wameshampoteza Frank. Zaza alitoa simu yake na kumpigia mzee Joel na kumpa taarifa Ile. Mzee Joel alifurahi Sana na akaamini sasa tayari anakaribia kutimiza lengo Lake kumtenganisha Penina na Frank. "hahahaaaa ninachokitaka mimi lazima nikitimize mtoto ni wangu lazima aolewe na mtu ninayemtaka mimi." alisikika mzee Joel akijitambaa mwenyewe. * Masaa manne yamepita Sasa bila mafanikio yoyote ya kumpata Frank. Baba yake Frank, mama yake Frank pamoja na Angel wakiwa na Penina walishindwa kuelewa Frank amepatwa na nini ghafla hivyo. Penina ndio alihuzunika Sana hakujua afanye nini kwa wakati ule. "mama ngoja mimi nirudi nyumbani tu maana nahisi kuchanganyikiwa." aliongea Penina kumuambia mama yake Frank. Kisha akaingia kwenye gari yake na kuondoka huku akiwa hana furaha kabisa. Wazazi wake Frank walihisi kuchanganyikiwa kwa mtoto wao kupotea ghafla, lakini walijipa moyo na kuamua kusuburi labda pengine atarejea baada ya Muda. Penina alifika nyumbani na kuanza kupiga honi kwa fujo afunguliwe geti. Hii ilikuwa sio kawaida ya Penina kufanya hivyo, ikabidi Wazazi wake pamoja na Nolan pamoja na Irene watoke nje ili kujua kwa nini Penina amefanya vile. Geti lilifungjliwa Penina akaingiza gari ndani kwa kasi na kulipaki sehemu yake, Kisha akashuka huku akiwa amenuna na kuingia ndani bila kumsemesha mtu yoyote. "kulikoni tena huyu mbona haeleweki?" akauliza mama yake Penina kwa mshangao. "Nenda kamuulize unatuuliza sisi kwani tulikuwa naye." mzee Joel akamjibu mama Penina. Mama yake Penina aliondoka na kumfuata Penina chumbani kwake. Nolan naye akaungana na mama yake kwenda chumbani kwa Penina ili kujua tatizo ni nini. Mzee Joel alibaki akiwa anatabasamu tu kwasababu yeye alijua kila kitu kuhusu Penina. "Penina ni nini tena mwanangu?" akahoji mama yake Penina baada ya kufika chumbani kwa Penina na kumkuta akiwa analia. "Frank mama." akasema Penina huku akizidi kulia, na wakati huo huo Nolan naye aliwasili chumbani kwa Penina. "Frank kafanya nini tena mwanangu hebu nyamaza unieleze vizuri." akaongea mama yake huku akimbebeleza. Penina alimwelezea mama yake pamoja na Nolan mkasa mzima wa jinsi Frank alivyotoweka kimaajabu. Mama yake Penina pamoja na Nolan kaka yake Penina, walipigwa na butwaa kwa maelezo ya Penina. Lakini hata hivyo Nolan akamwambia Penina, "usijali mdogo wangu kwa Sasa wewe tulia mimi nitalifuatilia hili swala hapa nahisi kuna kitu." "kaka mimi naumia Sana sikutegemea kitu hichi tena ghafla hivi." akaongea Penina huku akizidi kulia. "najua unaumia ila nipe Muda nilifuatilie hili swala, naomba uwe mvumilivu." akaongea Nolan kumtuliza Penina. "nyamaza mwanangu usilie tena, mwachie kaka yako hii kazi atakusaidia." akaongea mama yake pia kumtuliza Penina. * Frank taratibu alianza kurudiwa na fahamu akiwa Katika gari Ile aliyowekwa, Frank alianza kujikagua na kugundua kuwa amefungwa miguu mikono pamoja na usoni, hivyo hakuweza kuona chochote zaidi alihisi yupo kwenye gari ambalo lipo kwenye mwendo wa kasi sana. Frank alipiga kelele lakini alitulizwa kwa kupigwa na kitu kizito cha uso na kuzimia tena. Baada ya safari ya masaa ishirini na nne, hatimaye Frank alifikishwa Katika misitu fulani inayopatikana huko tabora. Mida ya usiku usiku Frank alitolewa kwenye gari na kutupwa pembeni ya misitu Ile Kisha wao wakaingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi sehemu ile na moja kwa moja wakaanza safari ya kurudi dar es salam na kumuacha Frank akiwa Katika hali mbaya Katika misitu Ile. Baada ya masaa kadhaa mbele Frank alizinduka na kujihisi yupo sehemu ambayo hakuweza kuilamba. Frank alipojaribu kunyanyuka aligundua kuwa amefungwa miguu, mikono pamoja na usoni hivyo hakuweza kufanya lolote. Frank aliamua kupiga kelele ili aweze kupata msaada lakini hakuweza kufanikiwa kupata msaada. Baada ya kupiga kelele kwa Muda mrefu bila kupata msaada, Frank aliamua kutulia na kusubiri chochote kitakachotokea huku akimuomba Mungu amsaidie.* Wazazi wake Frank walihangaika usiku na mchana bila mafanikio yoyote ya kumpata Frank. Ilifika sehemu Sasa wakaamua kumuachia Mungu kwasababu wao wameshachoka kumtafuta bila mafanikio yoyote. * Kaka yake Penina aitwaye Nolan yeye hakuamini kama Frank amepotea bali aliamini kuna mchezo unafanyika, Nolan alianza kuchunguza juu ya upoteaji wa Frank. Kwanza Nolan alianza kumchunguza baba yake ambaye Muda wote alikuwa pamoja na Irene mdogo wake Penina. "Baba wewe unalichukuliaje hili swala la kupotea kwa Frank mpenzi wake Penina?" akauliza Nolan. "hahahaaaa! wewe nani amekwambia Frank amepotea? Frank hajapotea kashapata mwanamke mwingine akatoroka naye wewe unasema amepotea, acha kujisumbua mwanangu." akaongea mzee Joel baba yake Penina kumuambia Nolan. "Kaka sikia nikuambie, mimi Nina uhakika Frank yupo na mwanamke mwingine nyie mnahangaika tu tena mwambie Penina aache kuhangaika na mwanaume ambaye hajatulia." akaongea Irene mdogo wake Penina kuunga mkono maneno ya baba yake. "Irene mdogo wangu huko unakoelekea unapotea, wewe una uhakika gani na maneno unayoongea?" akauliza Nolan kwa upole. "ana uhakika na anachokiongea wewe unafikiri yupo kwenye ndoto?" akadakia baba yake Penina kumtetea Irene. "Mbona mnateteana kama kuna kitu ndani yenu mbona siwaelewi?" akaongea Nolan kwa mshangao. "huwezi kutuelewa kwasababu upo nyuma Sana kama mkia wa ngombe." akaongea mzee Joel maneno hayo ambayo kidogo yalimfanya Nolan apandwe na hasira, lakini akajitahidi kuzishusha. "ok nashukuru kwa maneno yenu lakini nawaahidi lazima ukweli utajulikana." akaongea Nolan Kisha akanyanyuka na kuondoka. Penina Sasa alikuwa mtu wa kushinda ndani tu huku akiwa hana furaha kabisa kutokana na kutoweka kwa mpenzi wake Frank. Mzee Joel naye Sasa kumbe alikuwa tayari ameshamtafutia Penina mwanaume mwingine wa kutoka Norway na ndio alitaka amuoe mtoto wake Penina. * Hatimaye kulipambazuka Katika misitu ile aliyotupwa Frank. Frank alizidi kuhangaika bila kupata msaada wowote. Njaa pamoja na kiu vilimtesa Sana Frank pale msituni, alipiga kelele mpaka sauti ikaisha bila kupata msaada wowote. "Eeh Mungu Kwanini unaniacha niteseke hivi? Kama huu ndio mwisho wa maisha yangu bas naomba unichukue haraka usiniache nife Katika mateso makali kiasi hiki." akajisemea Frank kwa sauti ya chini akimuomba Mungu wake. Lakini hata hivyo baada ya masaa mawili mbele, aliweza kupita mzee mmoja aliyekuwa akichunga ngombe, karibu na sehemu Ile aliyotupwa Frank na pia akaweza kumuona Frank akiwa amelala pale chini akiwa hajiwezi kwa lolote. ....... Itaendelea Tukutane JUMATATU

at 6:45 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top