Riwaya: SARAI SEHEMU YA KUMI NA TATU(13) ***ilipoishia*** kwa mbali alimuona yule mama muuza mbogamboga akiwa anatembea kando ya barabara huku amembeba mtoto wake mgongoni. baba sarai akaongeza kasi ya kutembea kumfuata mama huyo..alipomkaribia akaanza kufoka ""we mama mchawi rudisha nyumba yangu wewe ndiye uliyekiwa umeketi nje ya geti langu....kipindi naongea na wewe nyumba na gari langu vikatoweka...haya hata kazini jengo silioni...baba sarai akazipiga hatua mbili huku amejiandaa kurusha kofi shavuni kwa mama yule.....alipojaribu kumpiga baba sarahi alistahajabu sana.... ***Endelea*** mama yule alimtazama kwa huruma huku myoto aliyekuwa kabebwa mgongoni akilia kwa sauti kali sana.... baba sarai akasita kurusha kofi huruma ilimuingia alipo ona mtoto yule akilia huku akimtazama..... akaamua kuondoka zake akimuacha mama huyo kasimama.....baba sarai alizipiga hatua bila kujua ni wapi anaelekea...akiwa njiani wazo lilimjia kuwa aende nyumbani kwake huenda akaiona nyumba yake....kwa sababu alikuwa ametembea mpaka akahisi kuchoka...akasimamisha bodaboda akaikodi ili impele nyumbani kwake...bodaboda ya kwanza ilimpitiliza huku dereva akimtazama baba sarai kwa macho ya mshangao....ikapita bodaboda nyingine alipoisimamisha dereva alimtazama tu na kupitiliza bila kusimama...baba sarai aliendelea kushangaa sana...akajiuliza mbona madereva bodaboda hawasimami!!!! kumbe watu wengine walimuina baba sarai kuwa ametapakaa matope mwili mzima....hivyo hata madereva bodaboda hawakutaka kumbeba kwenye pikipiki zao kwa sababu ngui zake zilionekana kutapakaa matope......lakini baba sarai alijiona yupo lawaida kabisa tena akiwa nadhifu... baba sarai aliamua kuelekea kwenye kituo cha daladala alipofika alikuta daladala ikiwa mlango wazi ndani yake walikuemo abiria kiasi...alipotaka kuingia abiria wakashuka wote...wakati huo konda hakuwepo alipofika alistahajabu kumuona baba sarai ameingia ndani ya gari na kukaa kwenye kiti huku akiwa ametapakaa matope....konda akasema""aisee baba angu naomba ushuke utachafua abiria wengine kwa matope yaliyotapakaa kwenye nguo zako....baba sarai alistahajabu sana akasema""we konda yani unanidhalilisha mimi bosi mzima....unasema nguo zangu zinamatope!!!!!! akaamua kushuka akataka kumpiga konda.....watu wakaanza kumshambulia baba sarai kwa maneno...akaamua kuondika zake alitembea kwa miguu kuelekea nyumbani kwake.. **************** upande mwingine alionekana sarai akiwa ndani ya nyumba ya baba yake...alikuwa amekaa juu ya meza huku akipuliza filimbi yake iliyotengenezwa kwa mfupa wa binadamu.... upende mwingine alionekana baba sarai akiwa amekaribia kufika nyumbani kwake kwa mbali aliiona nyumba yake akafurahi akaanza kutimua mbio kuifuata nyumba yake lakini kadri alivyozidi kuisogelea nyumba ilizidi kuonekana kuwa mbali..alikimbia masaa matatu mfululizo bila kuifikia akaamua kusimama akaanza kujiuliza ""hivi mimi naota au hili jambo naliona kwa macho yangu....wakati akijiuliza hivyo akageuza shingo yake alistahajabu kumuona yule mama akitembea kando yake...ghafla mama yule alipotea katika mazingira ya kutatanisha.....baba sarai akaanza kuingiwa na uwoga akaanza kutimua mbio kule alipotoka...ghafla akamuona tena yule mama akiwa mbele yake kwa mbali kidogo..baba sarai alipagawa akaamua kutimua mbio kuelekea upande ambao nyumba yake ilikuwepo..... alipoikaribia aliweza kulifikia geti akafungua na kuingia upande wa ndani.....akapitiliza mpaka kwenye mlango wa kuingilia sebuleni...alipoufungua akaanza kucheka mwenyewe...kisha akasema"""hivi haya mambo uanayotokea ni kweli nayaona au!!!! akazipiga hatua kuingia chimbani kwake..... ghafla simu ua mezani ikaita akaifuata na kuipokea...alikuwa anapiga mkirugenzi akauliza kwa nini leo hajafika kazini bila taarifa??? baba sarai hakuwa na jibu la kimjibu mkurugenzi.. akaikata simu ile...alipogeuka alisikia mtu anapiga hodi akapaza sauti""wewe nani??? yule mti aliyegonga mlango hakujibu kitu alibaki kimya.....baba sarai akazipiga hatua kuufiata mlango ili aone ni nani anaye gonga mlango....alipoufungua mlango alipoufungua mlango hakuona mtu....akaanza kufoka huku akitukana.......akaufunga mlango na kuelekea chumbani kwake.....akapitiliza moja kwa moja mpaka bafuni.....ghafla mlango wa sebuleni uligongwa tena..akajifunga taulo na kutoka kuelekea sebuleni....alipofika alistahajabu kujiona ameketi kwenye sofa...yani mtu aliyekuwa ameketi kwenye sofa alikuwa amefanan nae mpaka mavazi aliyokuwa ameyavaa leo...baba sarai aliogola macho yalimtoka akatimua mbio akafungua mlango ma kutoka nje....akakimbia huku kajifunga taulo..... wakati anakimbia sarai akajitokeza mbele yake lakini yeye hakuwa na uwezo wa kumuona...akajibadilisha na kuwa yule mama ambae alikuwa akimtokea mara kwa mara.baba sarai ikabidi amsimamishe mama huyo na kumuuliza"""hivi ukitazama kule unaiona nyumba yangu?? mama yule alijibu""SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA kisha akazipoga hatua na kuondika zake... baba sarai akabaki anajiuliza ""huyu mama anamaanisha nini?????? baba sarai aliamua kwenda kwenye kaburi la mke wake ili akaombe msamaha huenda mambo hayo yanajitokeza kwa makosa aliyoyafanya miaka ya nyuma.....akiwa njiani alisikia sauti ikimuita kutokea upande wa nyuma sauti hiyo iliita jina lake la kizaliwa ambalo lilikuwa halifahamiki.....ni watu wachache waliokuwa wakimuita jina hilo tena ni wa karib....alipogeuka nyuma aliogopa sana akastuka .......akataka kutimua mbio taulo likadondoka........akaliokota haraka alipojifunga kiunoni ghafla sarai alijitokeza....baba sarai alimkumbuka sarai kwa sababu ya kuonekana na sura ya ajabu...... USIKOSE SEHEMU YA MWISHO JUMATATU. ITAENDELEA....... Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua #kama unataka sehem ya mwisho ni mia tano tu ASANTENI.

at 1:20 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top