Riwaya: SARAI SEHEMU YA KUMI NA MBILI(12) ***ilipoishia*** mama yele alinyanyua uso na kumtazama baba sarai huku machozi yakimlenga machoni...kisha akaondoka zake na kuliacha beseni lililopigwa teke na mboga zote kudondoka kwenye mchanga..wakati huo baba sarai alikuwa akimtazama mama huyo kwa macho ya chuki.. alipogeuza shingo yake ili arudi kwenye gari lake hakuliona gari lake pale alipokuwa amelipaki.. alipogeuza shingo kumtazama mama yule hakumuona hata lile beseni pamoja na zile mboga zilizokuwa zimedondoka chini hakuziona...akiwa anataamaki alistahajabu hata nyumba yake haionekani.... ***Endelea*** baba sarai alichanganyikiwa akahisi hienda anaotoa akaanza kutimua mbio alikimbia bila kujua ni wapi anaelekea.....alipoikaribia barabara kuu akaamua kutembea akakodi taxi impefleke kazini kwake...akampa maelekezo dereva....baada ya muda walifika dereva akasimamisha gari kisha baba sarai akatoa noti ya shilingi elfu kumi akamkabidhi dereva yule akaondoka zake baba sarai alistahajabu hata jengo la kampuni halionekani...akajisemea ""moyoni au nimekosea njia?? lakini kila akitazama mazingira ni yaleyale anayoyaona kila siku....""jamani hivi naota au naona kweli..akazipiga hatua mpaka kwenye duka lililokuwa jirani akauliza ""hivi jengo la kampuni ya usafirishaji lililokuwa maeneo haya ni wapi??? muuza duka alimshangaa baba sarai..kisha akajibu""jengo hilo hapo pembeni yako...baba sarai alipotazama hapakuinesha kama kuna jengo lolote palikuwa wazi kama kiwanja cha mpira..... hakutaka kuendelea kuuliza akazipiga hatia na kuondoka zake......akiwa njiani anatembea alikutana na mfanyakazi aliyekuwa chini yake...akamuita....mfanyakazi yule alimfuata baba sarai... baba sarai akamuuliza""kwani jengo la ofisi liko wapi mbona silioni?? mfanyakazi yule alistahajabu akasema""bosi unatatizo gani mbona jengo la ofisi umeliacha huko nyuma ulipotokea!!!!! baba sarai alizidi kuchanganyikiwa akaamua kusema twende ukanioneshe......yule mfanyakazi akajibu "" nimeagizwa na mkurugenzi tangulia nitakukuta njiani bosi wangu.. baba sarai akasema kwa ukali ""unataka kazi au hutaki kuendelea na kazi???? yule mfanyakazi kutokana na uwoga kwa sababu bosi wake alikuwa mkali wakati mwingine aliwapiga makofi na mitama mbele ya wafanyakazi wenzao...akaamua kuhairisha kwenda kule alipokuwa ameagizwa na mkurugenzi wa kampuni akageuza na kurudi kule ofisini akiongozana na baba sarai... ************** upande mwingine alionekana sarai alijitokeza kwenye nyumba ya baba yake huku akiwa ameshikiria filimbi iliyotengenezwa kwa mfupa wa binadamu...akazipiga hatua akaketijuu yameza akaanza kupuliza filimbi ile. wakati huohuo alionekana baba sarai pamoja na yule mfanyakazi wakizipiga hatua kielekea kwenye jengo la ofisi....baada ya dakika kadhaa walifika baba sarai alikuwa akitefmbea nyuma ya mfanyakazi yule...mfanyakazi yule aliingia kwenye geti kisha akaanza kulifuata jengo la kampuni.. baba sarai alishangaa yeye aliona kama wanaingia kwenye uchochoro...akaendelea kumfuata mfanyakazi huyo...akaingia kwenye mlango mkubawa ili waingie kwenye ngazi ya umeme(lift) baba sarai alikasirika sana yeye aliona wametokezea sokoni....akasimama na kuongea kwa ukali ""hivi wewe mjinga unanitembezatembeza tu haya nani kasema unilete huku sokoni??? yule mfanyakazi alishangazwa na maneno ya bosi wake akajisemea moyoni""yawezekana bosi ameanza kupatwa ugonjwa wa akili..wakati anajiuliza hivyi..baba sarai alimfuata kwa lengo la kumpiga mtama...mfanyakazi huyo aliamua kutimua mbio na kuingia ndani ya lift. baba sarai aliamua kuondoka zake akatoka nje ya geti lakini macho yake yaliona kama ametoka kwenye kichochoro....akazipiga hatua huku akiongea peke yake kwa hasira maneno yasiyoeleka... akiwa njiani.........kwa mbali alimuona yule mama muuza mbogamboga akiwa anatembea kando ya barabara huku amembeba mtoto wake mgongoni. baba sarai akaongeza kasi ya kutembea kumfuata mama huyo..alipomkaribia akaanza kufoka ""we mama mchawi rudisha nyumba yangu wewe ndiye uliyekiwa umeketi nje ya geti langu....kipindi naongea na wewe nyumba na gari langu vikatoweka...haya hata kazini jengo silioni...baba sarai akazipiga hatua mbili huku amejiandaa kurusha kofi shavuni kwa mama yule.....alipojaribu kumpiga baba sarahi alistahajabu sana...... ITAENDELEA....... Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua #Pia samaani kutokuwa hewani jana kutokana na tatizo la umeme kusumbua hila tutaendelea kesho na sehemu ya 13 🙏🏻🙏🏻✔ ASANTENI.

at 1:20 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top