WAKE ZETU HAWAPENDI HII KITU. *Mpo Kwenye Ndoa Kwa Takribani Miaka Mi3 Au Zaid. Bahati Nzuri Mungu Kawajalia Mtoto/Watoto So Ndoa Inafuraha Coz Mmeongeza Familia. KWANZA TUJUE HILI WANANDOA. *Ktk Maisha Ya Ndoa Huwa Inafika Kipindi Wenza Huonana Kama Mbwa Na Paka Kiasi Cha Kutamani Kuachana Na Wakat Mwingine Hata Kudiriki Kusema Bora Nisingeoa Au Kuolewa Na Huyu. *Wanandoa Wanaishi Maisha Yasiyo Na Amani Ndani Ya Ndoa Na Kufanya Hata Maendeleo Kukosekana Ktk Familia. Matatizo Haya Ya Ndoa Huletwa Na Wanandoa Wenyewe Anawezakuwa Mume Au Mke. Leo Ningependa Kuzungumzia Baadhi Ya Matatizo Yale Yanayoletwa Na Wanaume. SHIDA YA WANAUME IKO HAPA. 1. MAJIBU YA KUUDHI. Hili Ni Tatzo Kubwa Sana Tulilonalo Wanaume. Mwanamke Akishazaa Huwa Tunamwona Kama Ameshuka Thamani Kiasi Cha Kudharau Hata Mambo Ya Msingi Akwambiayo. 2. KUTOJALI SAUTI YA MKEO. Utakuta Mwanaume Anasikiliza Shida Za Watu Wa Nje Na Kuzitekeleza Kuliko Hata Za Mkewe Ambaye Ndio Familia Yake. Wanaume Wengi Si Rahisi Kumuona Anaongea Kwa Sauti Ya Mahaba Na Mkewe, Bila Kujali Ni Directi Au Indirect Yani Kwa Njia Ya Simu. Mkeo Anakuuliza Jambo La Msingi Lakn Unavyomjibu Anakosa Kabisa Amani Na Kujiona Kama Vile Sio Mkeo Bali Malaya Mmoja Tu. 3. HESHIMA. Wakezetu Wanahitaji Kuheshimiwa Na Kupendwa Ili Waone Kwamba Wao Ni Wake Hasa Na Si WapitaNjia. 4. MAPENZI & MAJUKUMU. Kunatofauti Kubwa Kati Ya Majukumu Ya Kifamilia Na Majukumu Ya Kimapenz. Waume Wengi Tunafikiri Kutimiza Majukumu Ya Kifamilia Nyumbani Kama Chakula, Malazi, Mavazi, Elimu, Afya Na Mengineyo, Ni Mapenzi Tosha. . . . !! Lah Hasha, Wakezetu Hutazama Zaidi Na Huhitaji Zaidi Ya Hapo. Mke Anahitaji Apate Mapenzi Matamu Kuanzia Sebuleni Hadi Chumbani (Show Kali) Lakn Pia Mkifanya Outing Huwa Anahitaji Uwe Karibu Naye Hata Kama Uko Na Washiji Zako. Sasa Unamkuta Mume Ana Special Outing Zake Bila Mke Lakn Siku Wakitoka Pamoja, Mume Anakuwa Busy Sana Simu Android Yake Au Busy Na Washikaji Hata Story Wanazopiga Nyingi Ziko Nje Ya Himaya Ya Mwanamke. Utakuta Wao Wanazungumzia Mpira Au Ishu Za Kazini Kwao Pekee Kiasi Cha Kumfanya Mkeo Awe Kimya Kabisa. Penda Sana Kufanya Outing Na Mkeo Hata Mara1 Kwa Mwezi Sio Mbaya. Wengi Tunaamini Outing Ni Mpaka Uwe Na Pesa Nyingi, Hii Si Kweli. Dhumuni La Outing Ni Kubadili Mazingira Ili Muweze Ku'Refresh. Mnaweza Kuwa Na Elfu10 Au Zaidi Mkaenda Kiwanja Cha Karibu, Mkanywa Peps Zenu Na Azam Cola Mkamezea Na Clips Za Mihogo Cku Ikaisha, Lakn Outing Hiyo Ikaongeza Afya Ya Mapenzi Na Afya Ya Akili Ktk Ndoa Yenu. UDHAIFU. Udhaifu Wa Mwanamke Ujuu Ya Shetani Lakn udhaifu Wa Mwanaume, Ujuu Ya Mwanamke. HITIMISHO. Wanaume Tuwapende Wake Zetu Na Tuwathamini Lakn Wanawake Watiini Waume Zenu. Wanawake Kuweni Wasafi Muda Wote Sio Kisa Unamtoto Au Watoto Basi Muda Wote Uko Rafu Tu Hata Nyumba Hufagii Au Vitu Fulani Vipo Mahala Ambapo Si Sehemu Yake. Usafi Na Utii Kwa Mumeo Huongeza Thamani Na Utamu Wa Ndoa Maana Hata Mwanaume Mchafu Hupenda Mwanamke Msafi. NB: KUCHEPUKA SIO SULUHU YA NDOA BALI NI KUONGEZA TATIZO. SULUHU NI KUMWOMBA MUNGU AWE KINGA YA NDOA YAKO.

at 9:04 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top