Home → ushauri
→ Wanaume Hii Kitu ni Mbaya Sana...Msiwafanyie Wanawake
👉Mungu anasema si vyema mtu (Mwanaume) awe peke yake. (Mwanzo 2:18), na ni kweli Mwanaume hakuumbwa kuwa peke yake eti jeshi la mtu mmoja hata Mungu anajua, upweke unaleta disorder. Lakini wakati unasubiri au ukiwa kwenye mchakato wa kutafuta mwenzi wa maisha usitumie wanawake kama magazine za waiting room Airport ukiwa unasubiri muda wa kupanda ndege. Usijiingize kwenye mahusiano na mtu eti unavuta-vuta muda kupata mtu sahihi. Ni mbaya sana.
👉Unamtongoza dada wa watu na kumsumbua mpaka anajiaminisha kuwa unampenda kumbe hayuko hata kwenye ndoto zako, unataka tu mtu wa kupotezea mawazo. Yeye (Msichana) anajenga imani kwako na kuanza kukuingiza kwenye mawazo ya hatima (future) yake. Anakubwagia limoyo lake lote, kumbe wewe hata hisia huna. Inaumiza sana.
Bora utumie hiyo nafasi kujikita kwenye michezo au gym au mchakato wa kibiashara, au online courses ili uvute muda ukiwa unajiandaa kupata mtu sahihi wa maisha yako. Kwa nini umwambie mtu unampenda sana na uko tayari kufa kwaajili yake, wakati unajua unamtamani tu na sio kweli kuwa unampenda? Kwanini uumize hisia za mtu kwa makusudi?
Kwa nini ujiingize kwenye maisha ya mtu na kumvurugua utaratibu wake kumpotezea muda wake?
Huenda usingakaba hiyo nafasi angekuwa huru kupata mtu wake wa maisha. Lakini we umekaa kwenye maisha yake kama jiwe kwenye mlango wa kaburi la Lazaro, mbele hasogei nyuma harudi, kila siku unamuumiza tu. Umekuwa kitunguu kwenye maisha ya mtu haishi kulia kwa sababu hisia zako haziko kwake.
👉🏻Hii ni tabia mbaya sana. Kama unasoma post hii na uko kwenye mahusiano na mtu ambaye unampotezea wakati tu huna malengo naye nakusihi umuache mara moja. Kumbuka utapata watoto wa kike najua hautapenda mtu awe kwenye maisha ya mwanao akimpotezea muda.
Haya mambo tunafanya wanaume hata Mungu hapendi. Watu wanafeli masomo, watu wanakunywa sumu, wengine wanafia vitandani mahospitalini wakitoa mimba tulizokataa, wengine wamepata magonjwa ya mioyo kwa sababu ya hayo maumivu tumesababisha. Hayana faida hayo maisha, unajiwekea tu laana na mikosi itakayosakana maisha yako. Na ni utoto na upumbavu kutumia uanaume wako, uongo na ujanja ujanja kuchezea hisia za mtu. Amua kubadilika. Huu sio ujanja ni ufala. TUKUMBUKE MUNGU ANAONA NA UNACHOKIFANYA NI MBEGU UNAPANDA.
#USIJE_KUSEMA_HUKUAMBIWA.
Wanaume Hii Kitu ni Mbaya Sana...Msiwafanyie Wanawake 👉Mungu anasema si vyema mtu (Mwanaume) awe peke yake. (Mwanzo 2:18), na ni kweli Mwanaume hakuumbwa kuwa peke yake eti jeshi la mtu mmoja hata Mungu anajua, upweke unaleta disorder. Lakini wakati unasubiri au ukiwa kwenye mchakato wa kutafuta mwenzi wa maisha usitumie wanawake kama magazine za waiting room Airport ukiwa unasubiri muda wa kupanda ndege. Usijiingize kwenye mahusiano na mtu eti unavuta-vuta muda kupata mtu sahihi. Ni mbaya sana. 👉Unamtongoza dada wa watu na kumsumbua mpaka anajiaminisha kuwa unampenda kumbe hayuko hata kwenye ndoto zako, unataka tu mtu wa kupotezea mawazo. Yeye (Msichana) anajenga imani kwako na kuanza kukuingiza kwenye mawazo ya hatima (future) yake. Anakubwagia limoyo lake lote, kumbe wewe hata hisia huna. Inaumiza sana. Bora utumie hiyo nafasi kujikita kwenye michezo au gym au mchakato wa kibiashara, au online courses ili uvute muda ukiwa unajiandaa kupata mtu sahihi wa maisha yako. Kwa nini umwambie mtu unampenda sana na uko tayari kufa kwaajili yake, wakati unajua unamtamani tu na sio kweli kuwa unampenda? Kwanini uumize hisia za mtu kwa makusudi? Kwa nini ujiingize kwenye maisha ya mtu na kumvurugua utaratibu wake kumpotezea muda wake? Huenda usingakaba hiyo nafasi angekuwa huru kupata mtu wake wa maisha. Lakini we umekaa kwenye maisha yake kama jiwe kwenye mlango wa kaburi la Lazaro, mbele hasogei nyuma harudi, kila siku unamuumiza tu. Umekuwa kitunguu kwenye maisha ya mtu haishi kulia kwa sababu hisia zako haziko kwake. 👉🏻Hii ni tabia mbaya sana. Kama unasoma post hii na uko kwenye mahusiano na mtu ambaye unampotezea wakati tu huna malengo naye nakusihi umuache mara moja. Kumbuka utapata watoto wa kike najua hautapenda mtu awe kwenye maisha ya mwanao akimpotezea muda. Haya mambo tunafanya wanaume hata Mungu hapendi. Watu wanafeli masomo, watu wanakunywa sumu, wengine wanafia vitandani mahospitalini wakitoa mimba tulizokataa, wengine wamepata magonjwa ya mioyo kwa sababu ya hayo maumivu tumesababisha. Hayana faida hayo maisha, unajiwekea tu laana na mikosi itakayosakana maisha yako. Na ni utoto na upumbavu kutumia uanaume wako, uongo na ujanja ujanja kuchezea hisia za mtu. Amua kubadilika. Huu sio ujanja ni ufala. TUKUMBUKE MUNGU ANAONA NA UNACHOKIFANYA NI MBEGU UNAPANDA. #USIJE_KUSEMA_HUKUAMBIWA.
Artikel Terkait
Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi. MSOME SAIKOLOJIA YAKE Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira. MRUHUSU AKUJIBU Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. EPUKA MARUMBANO Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano. MUOMBE MSAMAHA Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.” Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako. ... Read More
VITU VIZURI 60 VYA KUMWAMBIA MSICHANA UMPENDAE:  Ninamaanisha kuwa maneno matamu.Wakati kijana uko kwenye process ya kutafuta na kujaribu kuuteka moyo wa msichana, unatakiwa kujifunza kutumia maneno matamu.Na lazima ujue kuwa sio kila neno unalotumia litagusa moyo wa mwanamke unayemtaka,Lakini maneno matamu yanafanya kazi ya kushangaza . Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. watu wengi pia huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza. sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unaempenda na unahitaji awe wako milele. 1.Macho yako ni mazuri , yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama. 2,Unanifanya niwe mwanaume bora , kwa hio nastahili mapenzi yako. 3.Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu. 4.Wewe ni mzuri na ni mrembo naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua. 5.Unapotabasamu huzuni kwangu hupotea , ghafla nakuwa mtu wa furaha. 6.Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani , lakini umenichagua mimi. 7.Hapana.wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo. 8.Ninapokushika nashisi kulegea kwenye magoti. 9.Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako,ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu. ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu. 10.Siamini , maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi. 11.kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda , natamani niwe na wewe milele. yaani wasife. 12.Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja. 13.Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda,nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia. 14.Kukutana nawe ni kitu ambacho hakijawahi kutokea. 15.Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia , hapo hupotea kabisaaa. 16.Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi. 17.Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama haitatosha kukupenda. 18.Napata furaha nikiwa na wewe. 19. Napenda kutumia muda na wewe. 20.Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa. 21.Natamani maishsa yangu yote nikuone ukiwa na furaha. 22.Usibadilike nakupenda jinsi ulivyo. 23.Nikiwa na wewe nafurahi kama mtoto. 24.Napenda nywele zako. 25.Napenda nikukumbatie ninapokuaga. 26.Natamani kukubusu kila sehemu ya mwili wako. 27.Naanza siku na wewe ndani ya mawazo yangu, na ninamaliza siku na wewe kwenye ndoto zangu. 28. ukiwa na mimi huwa natamani kusimamisha muda, maana muda unakwenda haraka. 29.Nikisikia sauti yako asubuhi , siku nzima ni mtu wa furaha. 30.Tabasamu lako zuri linanifanya niyeyuke. 31.Unaponiaga napata shida kukuruhusu uende. 32. Umenielewa vizuri, ni kama unasoma mawazo yangu. 33.Mungu alikupendelea kukuumba, akili na kila ulichonacho. 34.Najivunia kuwa na wewe na ninafurahia. 35.Napenda unavyosema unanipenda. 36.Mapenzi yetu ni kama mawimbi ya bahari, wakati mwingi hutulia, na wakati mwingine huvuma,lakini yanarudi palepale. 37.mapenzi yetu yawe kama ua rose ambalo halina miiba. 38.Najua kwa nini watu wanatutazama , ni kwa sababu wewe ni mzuri kuliko mwezi. 39.Muda utakuwa hauna thamani endapo sitatumia na wewe. 40.kama siku yangu ingeanza na busu lako, nisingehitaji kahawa. 41.Kama ningeambiwa nielezee rangi, basi ningeenda kwenye rangi za rainbow, kwa sababu wewe ni mzuri.ni wa muujiza. 42.Mimi bila wewe ni mbaya, lakini ni mzuri nikiwa na wewe. 43.Tukishikana mikono na mioyo yetu inashikana,na nafsi zetu zinapatana . 44.Siku ya kwanza tulipokutana, nilijua ipo siku tutakutana tena, na nafurahi imetokea. 45.Nafurahi tumekua pamoja, sina cha kukosa hata kidogo. 46.Moyo wangu unapumua kama ndege, kila unapotabasamu. 47.Kila ninapokuwa nimeshuka moyo, nikikusikia wewe moyo wangu unapata nguvu. 48.Shika mikono yangu nami nitashika moyo wako, tunza kwa maisha yote. 49.Maisha yote , milele yote,isio na mwisho, toka nimekutana na wewe maneno yote yana maana. 50.Siku naona kama mwaka, na siku inapita kama sekunde. 51.Natamani ningekuwa kama pweza mwenye mikono mingi ili nikukumbatie na mikono myote. 52.Siamini katika nafsi mpya, lakini baada ya kukutana na wewe nimeamini, natamani kama ningeweza kurudi nyuma na kutengeneza kitu. 53.Sitaweza kukutoa kwenye mawazo yangu , kwa maana nakuhitaji uwepo. 54.Kuna wakati nahisi upweke, kwa wakati huo, basi huamua kukupigia simu na kusikia sauti yako. 55.Ninapokutizama namuona mungu jinsi alivyokuumba na kukubariki. 56.Unanifanya niwe wa muhimu . 57.Ni siri ambayo inanifanya nikutazame zaidi kwa kila siku. 58.Kuongea na wewe kila siku unanifanya nikufahamu zaidi na zaidi. 59.Moyo wangu nakupa,nipe moyo wako ili tuifungie kwa pamoja, na tutupe ufunguo mbali. 60.Nakuhitaji muda wote, siku , mwaka na hata milele. ... Read More
Majina Ya Watoto Wa Kiume (26)  Katika tamaduni nyingi, majina ya watoto wa kiume hutokana na majira au matukio ya wakati wanapozaliwa. Kwa mfano, wakati mmoja, mwanamke Mwethiopia alijifungua mtoto wa kiume. Shangwe yake ikageuka kuwa majonzi alipoona mtoto wake akiwa amelala bila kusonga. Nyanya yake alipomchukua mtoto huyo ili amwoshe, kwa ghafla mtoto akaanza kusonga, kupumua na hata kulia. Hali hii ikawa chanzo cha jina la mtoto na hiyo wazazi wake wakaunganisha jina muujiza na neno linguine la Kiamhara na kumwita mvulana huyo Muujiza Umefanyika. Nchini Burundi, majina memgin yalitokana na wakati wa vita vilivyokuwemo mwanzo wa miaka ya tisini. Mtoto aliyezaliwa huku mzazi akijifichakutokana na machambulizi angepatiwa jina kama Manirakiza amabalo maana yake ni’Mungu Ndiye Anayeokoa’. Majina mengine ya wakati ule ni kama Twagirimana na Mwana wa Imana ambayo pia humaanisha mwana wa Mungu au mtu aliyeponea vita kwa muujiza wa Mungu. Desturi hii ya majina ya watoto wa kiume imeenea kote ulimwenguni ambapo kuna majina mengi yaliyo na maana ya nyakati kam wakati wa vita, njaa, shjrehe, makumbusho au tukio amabalo watu hupenda kukumbuka kwa kuwapa watoto majina. Kuna majina kadhaa amabyo ni mashuhuri sana ulimwenguni ;Noah, Liam, Mason, Jacob, William, Ethan, Michael, Alexander, James, Daniel na mengine. MAANA MAJINA TUKIZINGATIA HERUFI YA JINA LA KWANZA (KIUME) HERUFI A Watoto wenye jina linaloanza kwa herufi hii hupenda mambo makubwa,hujiamini sana na huwa na uwezo wa kutimiza malengo yao. Ni watoto wenye tahadhari,wachangamfu na hupenda matukio. Kwa kawaida hupenda kuheshimiwa,hupenda mamlaka,na ana kiburi,watoto wapenda hasira.Kidesturi herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI B Mwenye jina linaloanziana na herufi hii ni watoto wakarimu,waaminifu na hupenda kazi sana. Ni wajasiri, shujaa na wakatili katika vita au popote pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.Herufi hii huwakilisha nyota yangombe. HERUFI C Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni motto wa kubadilikana,ni washindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda.Ni watu wabunifu na wanapenda mawasiliano,herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha. HERUFI D Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni anayependa usawa,biashara ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi.Ni wajeuri na wenye msimamo. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa. HERUFI E Mwenye jina linaloanza na herufi ni mtu mwenye roho nzuri,mwenye mapenzi na huruma,mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Ubaya wake ni mtu asiyetegemewa na ni kigeugeu.Herufi hii huwakilishwa na nyota ya samba. HERUFI F Mwenye jina linaloanza na herufi hii n mtu mwenye mapenzi,huruma,roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu,ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke. HERUFI G Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni mtu mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho,ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. Ni mtu mwenye hisia kali,msomi,mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri kutoka kwa watu.Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani. HERUFI H Mwemye jina linaloanzia na herufi hii ni mtoto mwenye ubunifu na nguvu katika biashara,hupata faida kubwa katika anayopenda kutokana na bidii, ni mwenye mawazo mengi,mchoyo na mbinafsi.Herufi hii huwakilisha nge. HERUFI I Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda sharia,ana huruma na utu mzuri.Wakati mwingi ni mtoto mwenye kujiamini sana na mwenye hasira za haraka. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale. HERUFI J Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye matamanio,mkweli,mkarimu na mwerevu.Huwa asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa,wakati mwingine anakuwa ni mtoto mvivu na anayekosa mwelekeo. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi. HERUFI K Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto mjeuri,mwenye msimamo thabiti,mpenda umashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu, ana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana,ni mtoto asiyeridhika. Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo. HERUFI L Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto wa vitendo,mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha,hupatwa na misiba mara kwa mara.Herufi hii huwakilisha nyota ya samaki. HERUFI M Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kujiamini sana,mchapakazi na hupata mafanikio,ni mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI N Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mbunifu, mwenye hisia kali,hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ngombe. HERUFI O Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye subira,mvumilivu,na mwenye bidii ya kusoma.Ni mtoto mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.Herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha. HERUFI P Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye uwezo wa kuamuru na ana hekima kubwa.Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa. HERUFI Q Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtotto mwenye kupenda mambo ya asili,ni watu wasioelezeka,wako na uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya samba. HERUFI R Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mtulivu,mwenye huruma lakini mwenye hasira za haraka.Muda mwingi yeye ni mpenda amani. Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke. HERUFI S Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mvuto kali wa kuleta utajiri,ni mtoto mwenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani. HERUFI T Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda ushauri wa kiroho,anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu, ni watoto wenye hisia kali na wepesi sana kushawishika.Herufi hii huwakilisha nyota ya nge. HERUFI U Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye bahati kwa ujumla,anapenda uhuru katika mapenzi,ni mbinafsi,mwenye tama na anayekosa maamuzi. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale. HERUFI V Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mchapakazi,mwenye bidii asiye choka lakini ni watu wasiotabirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi. HERUFI W Mwemye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mawazo sana,mchangamfu sana,mwenye uwezo wa kutambua watu wabaya na wema, ni wenye tama na hufanya mambo hatari sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo. HERUFI X Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto asiyependa kuwekewa vizuizi hasa katika anasa na ni rahisi kwake kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI Y Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mpenda uhuru na hapendi kupingwa katika jambo lolote,ni watoto wanaokosa uamuzi na husababisha kupoteza bahati katika maisha. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI Z Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda matumaini na amani,ni wenye msimamo mkali japo ni wenye kukubali ushauri . Herufi hii huwakiisha nyota ya ngombe. ... Read More
Hivi unazijua Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda Kwa Dhati??  Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu! ... Read More
MWANAUME ANAPOSEMA HATAKI KUKUOA: MWAMINI  Naandika hii makala kwa sababu nimekutana na maswali mengi ambayo yanaumiza wanawake wengi. Swali linakuwa hivi. Nimekuwa na huyu mwanaume kwa muda mrefu na tumekuwa tukishirikiana mambo mengi. Sijawahi kuwa na hisia kama nilizo nazo kwa mwanaume huyu kwa mtu yeyote. Na nilijua tutakuwa pamoja maisha yetu yote. Tatizo ni kwamba anasema hataki kunioa? Nitafanyaje ili aweze kujua kuwa nampenda na tunaendana vizuri pamoja na tunatakiwa tuoane? Wanaume wengi huwa wanaogopa kuweka ahadi kama hawana uhakika na upendo walio nao kwa mwanamke. Semeni ukweli wanaume. Je ameongelea kuhusu maisha ya baadae? Kuna mpango gani? Ni rahisi kubadilisha mwanaume? Unawezaje kumlazimisha akuoe? Kitu gani cha kufanya kama amesema hawezi kukuoa? Kama amesema hatakuoa, Mwamini . Elewa. Najua tayari jibu umepata kwenye maandiko yangu ya juu, lakini napenda kurudia, huwezi kumlazimisha mwanaume akuoe kama amesema hataki kukuoa. Hataweza. Sasa basi sisemi kama haiwezekani kweli. Kuna wanaume ambao husema hawatakuoa na hubadili mawazo yao na kuamua kuoa mwanamke ambaye alikuwa hapendi kumuoa. Lipo hilo. Mwanaume anayesema hatakuoa na wakati anaishi na wewe, mara nyingi anakupotezea muda na atakwenda kuoa mtu mwingine anayempenda kuliko wewe. Tuangalie kwa nini iko hivyo. Ina maana gani anapokuwa anaongea kuhusu kuchukia ndoa Aina ya mwanaume ambaye atakuambia hatakuoa ni yule ambaye anachukizwa na taasisi ya ndoa au sheria yake. Mwanaume huyo hafikirii kama wazo la kuoa ni zuri kwa kila mtu- anaona hata wanandoa ambao wako pamoja hawaonyeshi kama wana upendo wa kutosha, hawana upendo wa kweli ( anaweza kuwa haamini hata kama kuna upendo) Anafikiria hata kama ataona, mbona ndoa nyingi hazifiki mwisho, au mbona ugomvi ndani ya ndoa hauishi. Vyovyote vile , kwa sababu zozote zile, lakini mwanaume huyu anaonyesha kuchukia taasisi ya ndoa, na hataki kuingia huko, ndio maana hataki kuoa. Kama utasikia akisema hivyo mwamini. Haonyeshi kama atatafuta mwingine ambaye ataweza kubadili mawazo yake kuhusu kuoa.hata kama mnakaa pamoja na mnapendana sana , lakini hatafunga ndoa. Ina Maana Gani Anaposema Muda Wa kuoa Bado. Huyu ni aina nyingine tena.Anasema muda bado, anakuwa na sababu nyingi.Kama hali yake ya maisha haijakaa sawa, hajajenga nyumba, hana gari, na sababu kibao. Mwanaume huyu hana tatizo katika kuoa , Ila wakati bado , hataweza kuoa wakati unaotaka wewe, hata kwa sababu zipi hataweza. Unachotakiwa kufanya ni kumwamini anachokisema. Sababu zake hazina msingi. Kitu cha msingi ni Ukweli anaokuambia.Inaumiza lakini ndio ukweli.Inavunja moyo lakini ndio ukweli, Amini hilo na itaokoa muda wa kwako kusubiri.Na wakati huo huo utakuwa unafanya maamuzi ya kusubiri, kukubali jinsi ilivyo. Lakini kumbuka kuwa ndoa ni kitu cha muhimu sana. Wanaume wanaosema hawataoa huongea ukweli.Kama anakuambia hatakuoa Amini tu. Wanaume wanajua ni mwanamke wa aina gani atakayeishi nae maisha yake yote, uwe makini asije akawa anakutumia huku ana mipango yake .Yapo mambo wanaume huyapenda kwa mwanamke, vile vile yapo mambo ambayo wanawake wanapenda kwa mwanaume. Kama unaona unamlazimisha jambo fulani hataki , kuwa makini. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: