SIRI ZA GIZANI NO 8 Ibra alipo muona ndugu yake anaogeshwa na bibi yake usiku kama ule, kiukweli hakuamini kabisa ikabidi asogeze jicho vizuri ili amuone kama kweli ni Nasra anaogeshwa na wakati kila mtu ameisha msahau akijua ni marehemu tayari. Ibra alipo mtazama vizuri kwa ukaribu akamuona kweli ndugu yake, dahhh alichoka maana Nasra alikuwa amekonda sana, sababu ya chakula kibaya, alafu zile nywere zake alizo kuwa amesuka kipindi anakufa ndo hizo hizo alizo kuwa nazo bado na zimechakaa kweli kweli. Sasa bibi Nasra alihisi kama kuna mtu anamchungulia mlangoni, hapo hapo akamrudisha Nasra kwenye diaba haraka sana. Kumbe Ibra alikimbia kuwa amsha wazazi wake waamke ili waje kumuona Nasra chumbani kwa bibi, Ibra akasema, "baba, baba, babaaa amka njoo umuone Nasra yupo chumbani anaogeshwa na bibi, baba amka nasra wetu hajafa baba", baba yake alitoka akaanza kumchapa Ibra akimwambia, "hivi we mtoto unamatatizo gani kwanini unapenda kutusumbua tukiwa tumelala lakini, mi nina mawazo yangu kibao hapa, mama yako anaumwa kansa naangaika na mawazo bado na wewe unaniletea za kuleta, mshezi kweli, kalaleee" kipindi baba yake anaongea vile, mke wake akasema "mme wangu unaweza kumchapa mtoto bila kujua labda mambo anayo yasema niya ukweli, ebu tumruhusu atwambie alicho kiona usiku wa leo" baba yake akasema, "umeona nini kwani" Ibra akasema, "baba bibi yetu ni mchawi, maana Nasra hajafa bibi ndiye anae chumbani" baba yake akasema, "we mtoto unawazimu gani lakini, hivi hizi laani utaziweka wapi wewe, yaani unamuita bibi yako mchawi una akili kweli" mke wake akasema " mme wangu usikasilike unajua watoto wetu hatukuwazoesha kukaa na bibi zao, labda wakiwaona walivyo zeeka wana hisi ni uchawi au uganga labda tumuelekeze aelewe na sio kumkalipia" Ibra akasema, "baba bibi ni mchawi, kama sio mchawi kwanini anaishi na Nasra peke yake, mwambie amtoe nasra nataka kucheza nae na mimi, kila siku yeye tu anacheza nae" mama Nasra akasema "yaweza kuwa kweli mme wangu" baba nasra akasema "we we we! Naomba msirudie kumuita mama yangu mchawi, yeye amenizaa mimi kama angekuwa mchawi si angeniua nikiwa mdogo, iweje aiteketeze familia yangu, acheni kumsingizia mama yangu bhana, Ibra akasema...ITAENDELEA YA 9

at 12:31 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top