Home → simulizi
→ SIRI ZA GIZANI
NO 7
Nasra aliendelea kulishwa unga wa ugali tu mule kwenye diaba, na kila ilipo fika saa nane za usiku mda alio chukuliwa na bibi yake, Nasra alikuwa anatolewa kwenye diaba kisha anaanza kucheka na kuimba na bibi yake, na mala tu baada ya kuimba na kucheka bibi yake anamrudisha kwenye diaba kama kawaida. Ila kaka yake Nasra yaani Ibra kila alipo kuwa akilala alikuwa anaota ndoto za ajabu sana, na mala nyingi alikuwa anaota kuwa mdogo wake yupo hai hajafa, lakini kila alipo kuwa akimwambia baba na mama yake walikuwa hawamuelewi kabisa maana mtoto walimzika na msiba ulifanyika, mda mwingine Ibra alikuwa anachapwa kwa sababu ya usumbufu wake wa kila siku kwamba "dada Nasra hajafa, dada nasra hajafa uwa namsikia akiimba usiku, yaani namsikia kabisaa, akiimba usiku" hayo maneno alikuwa anayataja sana mpaka mama yake akaanza kumgombeza, lakini ibra kila siku alikuwa anaongea hivyo, maana kumbe bibi yake alivyo kuwa anaimba na kucheza usiku na nasra, ibra alikuwa anasikia maana yeye na nasra wote walizaliwa tumbo moja hivyo damu ilikuwa nzito, siku moja Ibra akiwa amelala aliota sauti ya dada yake imemuijia ikisema, "kaka ibra nenda kwenye kabuli langu" Ibra alikuwa muoga sana kutoka nje usiku, lakini ile ndoto ilimsumbua sana Ibra ikabidi afungue mlango aende nyuma ya nyumba yao kuangalia kabuli la mdogo wake maana ndipo walipo kuwa wamemzika kule kwa nyuma. Ibra alipo fika kwenye kabuli alishangaa sana maana alikuta ile sehemu ipo tambalale kabisa na hakuna kabuli lolote mda ule, ndipo Ibra akakimbia haraka kuingia ndani, akiwa analia huku watu wote wamelala, isipo kuwa bibi yake maana walikuwa ndani na Nasra wanacheza na kuimba ila hakuna alie kuwa anasikia zile sauti zaidi yao wawili.
Siku moja usiku sana bibi yake nasra alikuwa anamuogesha nasra ili asitoe harufu mbaya chumbani maana tangu amfungie hakuwai kuoga ata siku moja. Sasa wakati anamuogesha ibra akawa amesikia sauti za maji kutoka kwenye chumba cha bibi yake huku bibi akisema kwamba "nasra geuka nikusugue na mgongoni kuchafu" ibra alipo chungulia vizuri kwenye kitasa cha mlango akawa amemuona Nasra anaogeshwa kama mtoto mdogo wakati ni dada tu anaeweza kuoga mwenyewe. USIKOSE YA 8...
SIRI ZA GIZANI NO 7 Nasra aliendelea kulishwa unga wa ugali tu mule kwenye diaba, na kila ilipo fika saa nane za usiku mda alio chukuliwa na bibi yake, Nasra alikuwa anatolewa kwenye diaba kisha anaanza kucheka na kuimba na bibi yake, na mala tu baada ya kuimba na kucheka bibi yake anamrudisha kwenye diaba kama kawaida. Ila kaka yake Nasra yaani Ibra kila alipo kuwa akilala alikuwa anaota ndoto za ajabu sana, na mala nyingi alikuwa anaota kuwa mdogo wake yupo hai hajafa, lakini kila alipo kuwa akimwambia baba na mama yake walikuwa hawamuelewi kabisa maana mtoto walimzika na msiba ulifanyika, mda mwingine Ibra alikuwa anachapwa kwa sababu ya usumbufu wake wa kila siku kwamba "dada Nasra hajafa, dada nasra hajafa uwa namsikia akiimba usiku, yaani namsikia kabisaa, akiimba usiku" hayo maneno alikuwa anayataja sana mpaka mama yake akaanza kumgombeza, lakini ibra kila siku alikuwa anaongea hivyo, maana kumbe bibi yake alivyo kuwa anaimba na kucheza usiku na nasra, ibra alikuwa anasikia maana yeye na nasra wote walizaliwa tumbo moja hivyo damu ilikuwa nzito, siku moja Ibra akiwa amelala aliota sauti ya dada yake imemuijia ikisema, "kaka ibra nenda kwenye kabuli langu" Ibra alikuwa muoga sana kutoka nje usiku, lakini ile ndoto ilimsumbua sana Ibra ikabidi afungue mlango aende nyuma ya nyumba yao kuangalia kabuli la mdogo wake maana ndipo walipo kuwa wamemzika kule kwa nyuma. Ibra alipo fika kwenye kabuli alishangaa sana maana alikuta ile sehemu ipo tambalale kabisa na hakuna kabuli lolote mda ule, ndipo Ibra akakimbia haraka kuingia ndani, akiwa analia huku watu wote wamelala, isipo kuwa bibi yake maana walikuwa ndani na Nasra wanacheza na kuimba ila hakuna alie kuwa anasikia zile sauti zaidi yao wawili. Siku moja usiku sana bibi yake nasra alikuwa anamuogesha nasra ili asitoe harufu mbaya chumbani maana tangu amfungie hakuwai kuoga ata siku moja. Sasa wakati anamuogesha ibra akawa amesikia sauti za maji kutoka kwenye chumba cha bibi yake huku bibi akisema kwamba "nasra geuka nikusugue na mgongoni kuchafu" ibra alipo chungulia vizuri kwenye kitasa cha mlango akawa amemuona Nasra anaogeshwa kama mtoto mdogo wakati ni dada tu anaeweza kuoga mwenyewe. USIKOSE YA 8...
Artikel Terkait
Story - - - - - NI WEWE TU PENINA. BY GIVAN IVAN PHONE & WHATSAPP____0769673145 Karibuni tuianze story yetu hii mpya yenye kusisimua iliyojaa visa mbali mbali kuhusu mapenzi. Sehemu ya kwanza (1) Mapenzi ya vijana wawili walionza kupendana toka wakiwa wadogo mpaka Sasa wakiwa na umri wa miaka 25 kila mmoja, yalikuwa yakizidi kukolea kila siku na kuwa matamu zaidi na zaidi. Vijana Hawa ni Frank pamoja na Penina. "nahisi kuvurugwa nahisi kufa kufa yaani najiona kama napepea juu juu kwa jinsi navyompenda mpenzi wangu Penina." alikuwa frank akiongea maneno hayo mbele ya wazazi wake pamoja na mdogo wake Wa kike aitwaye Angel. "na siku si nyingi utakuwa chizi wewe sio kwa kupenda huko kaka yangu." akaongea Angel kumuambia Frank. "acha niwe chizi tu mdogo wangu, lakini sio chizi wa kutembea uchi barabarani bali chizi wa kupenda." akaongea Frank maneno hayo na kuwafanya wazazi wake wacheke sana. "lakini mwanangu Sasa inabidi mfanye taratibu mfunge ndoa Sasa." aliongea baba yake Frank. "Hamna shida baba usijali yote hayo yatafanyika muda mfupi ujao. " Akaongea Frank ambaye muda wote furaha ilijaa usoni mwake. *wakati huo huo Penina mpenzi wake Frank naye alikuwa katika moja saloon akitengeneza nywele zake ikiwa ni maandalizi ya kwenda kukutana na mpenzi wake Frank. " Dada nitengeneze vizuri tafadhali maana napenda muda wote niwe navutia mbele ya mpenzi wangu." aliongea Penina kumwambia mwanadada aliyekuwa akimtengeneza nywele. "usijali dada nitakutengeneza vizuri mpaka mwenyewe ufurahi." Dada yule akamjibu Penina na kumfanya atabasamu. Baada ya dakika kadhaa Penina alimaliza kutengenezwa nywele zake na moja kwa moja akazama kwenye pochi yake na kutoa simu yake, kisha akatafuta Jina lililoandikwa my love Frank na moja kwa moja akazipiga namba hizo. * Frank akiwa bado anaongea na wazazi wake ghafla simu yake ilianza kuita, akatoa na kuangalia mpigaji ni Nani. Frank alianza kutabasamu baada ya kukuta mpigaji ni Penina kipenzi cha moyo wake. "haloo mke wangu mtarajiwa mambo vip?" akaongea Frank baada ya kupokea simu. "poa tu mpenzi wangu nimekumiss hadi nahisi kizunguzungu." akajibu Penina. "Asante mpenzi wangu yaani kuachana Jana tu ndio kunimiss hivyo?" " yeah nimekumis sana hebu jiandae nakupitia Sasa hivi tukale bata kidogo. " akaongea Penina kumwambia Frank. " waoow ok najiandaa Sasa hivi utanikuta tayari my love." akajibu Frank na simu ikakatwa. Frank aliwaacha wazazi wake pale sebuleni kisha yeye akaenda kujiandaa kwa ajili ya kutoka na mpenzi wake. Penina naye baada ya kukataa simu aliingia kwenye gari yake nyeupe aina ya rava4 na kuanza kuelekea nyumbani kwa Frank. Tumfahamu Penina vizuri. Penina ni mwanamke mrembo sana aliyebarikiwa na Mungu kuwa na kila kitu kizuri katika mwili wake. Popote pale Penina alipopita aliacha gumzo kwa wanaume ambao walikuwa wakimmezea mate. Penina ametoka katika familia ya kitajiri yenye watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume ambao ni Nolan, Penina na Irene. Penina amefanikiwa kusoma mpaka elimu ya juu kabisa na kufanikiwa kuwa mfanyabiashara mdogo anayechipukia kwa kasi sana. Penina alianza uhusiano wa kimapenzi akiwa kidato cha tatu, na alianza uhusiano na kijana aliyeitwa Frank ambao mpaka Sasa wapo pamoja. Lakini kitu kimoja ambacho kanalitia dosari penzi tamu kabisa la Penina na Frank, ni baba yake Penina kutopenda mwanawe aolewe na Frank. Baba yake Penina hakutaka kabisa mtoto wake aolewe na Frank, yeye alitaka mtoto wake aolewe na mzungu kutokana na uwezo wao wa kipesa. Mama yake Penina pamoja na Nolan kaka yake Penina ndio Watu pekee waliokuwa wanayaunga mkono mapenzi ya Penina na Frank katika familia yao. Lakini Irene mdogo wake Penina pamoja na baba yake Penina ndio watu pekee ambao walikuwa hawataki kabisa kuyaona mapenzi ya Penina na Frank yakiendelea. * Frank yeye anatoka katika familia yeye hali ngumu kimaisha, hawakuwa na uwezo hata wa kuwa na nyumba nzuri kama wenzao. Frank aliishia kidato cha pili kutokana na wazazi wake kutokuwa na uwezo wa kumuendeleza zaidi. Kadhalika pia Angel mdogo wake Frank naye aliishia darasa La saba kutokana na Wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza zaidi. * Baada ya dakika kadhaa Penina aliwasili nyumbani kwa kina Frank, akapaki gari yake pembeni na kushuka Kisha akaingia katika nyumba ya kina Frank ambayo ilikuwa imechoka Sana. "waoow mkwe wetu karibu Sana." mama yake Frank ndio alimpokea Penina kwa furaha Sana. "Asante Sana mama yangu nimekaribia." akajibu Penina huku akiketi pembeni ya mama yake Frank. "eeh mwanetu lete habari." akaongea mama yake Frank. "Sina hata mpya nimekuja kumchukua mtoto wenu." akajibu Penina. Na Muda huo huo Frank akajitokeza akiwa tayari ameshajiandaa. Licha ya umaskini uliopo katika familia Yao, bado Frank alijitahidi Sana katika kuupendezesha mwili wake ili aweze kuendana na mpenzi wake Penina ambae Muda wote alikuwa mtu wa kupendeza tu. "waoow my love mwaaa." Penina ndio alinyanyuka na kumkumbatia Frank na kumuachia busu Zito la shavu. Frank naye hakuwa nyuma alimpokea mpenzi wake kwa furaha pia. Penina pamoja Na Frank waliaga na kutoka nje, wakaingia kwenye gari na kuondoka. "tunaelekea wapi Sasa mpenzi wangu?" akahoji Frank. "surprise my love sikuambii tunaelekea wapi." Penina akamjibu Frank huku akitabasamu. "haya bhana bas nafunga macho mpaka tufike." akaongea Frank na kumfanya Penina azidi kutabasamu.* Katika bar moja iliyopo maeneo ya sinza kikao kimoja kilikuwa kikiendelea, na huku kilichokuwa kikipangwa Katika kikao kile ni namna ya kulivunja na kuliharibu penzi la Penina na Frank. Mzee Joel ambaye ni baba yake Penina, pamoja na Angel ambaye ni mdogo wake Penina pamoja na vijana wengine watatu wa kiume na mmoja wa kike, ndio waliokuwa wahusika wakuu wa kikao kile. .... Itaendelea ... Read More
Story........ NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na tano (15) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp..... 0769673145 Ilipoishia...... Nolan alishtuka vibaya mno na kuona hapa shughuli ni nzito tena nzito Sana. Lakini mzee Joel ndio alikuwa na furaha Sana kwa kushuhudia kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na buffalo. Nolan alinyanyuka na kujitikisa na kujiweka Sawa kwa ajili ya kuendelea na mpambano. ***********Endelea *********** Baada ya Nolan kusimama tu buffalo hakumpa hata nafasi ya kumeza mate alimfuata kwa kasi na kumrushia mateke manne mfululizo na yote yakampata Nolan na kumuweka chini kwa Mara ya pili. Shughuli ilikuwa nzito Sana kwa Nolan kwani hajawahi kukutana na mtu mwenye spidi ya kupigana kama buffalo. Kwa Mara nyingine Nolan alinyanyuka tena huku akiwa tayari ameshawekwa alama usoni. Buffalo kama kawaida yake hakutaka kumpa nafasi ya kupumua, akamfuata kwa kasi na kurusha ngumi nyingine nzito lakini hii Nolan akaiona na kuikwepa ikaenda kugonga dirisha na kuvunja lile lote. Nolan naye this time round akasema hata mimi sicheki na wewe, Nolan aliruka na kumtandika buffalo teke la mgongo na kumtupa nje kwa kupitia pale dirishani. Nolan hakutaka kupoteza Muda akaruka na kumfuata buffalo huko huko nje. Dick pamoja na vijana wake wakiwa pamoja na mzee Joel nao wakatoka nje kushuhudia vita ile kali. Nolan baada ya kufika nje akakuta tayari buffalo ameshanyanyuka. Nolan akarusha ngumi nzito lakini buffalo akaikwepa na kurusha teke ambalo Nolan pia alilikwepa. Ngumi nzito ikarushwa na Nolan kwa Mara nyingine na kumkuta buffalo ya kichwa, lakini pia Nolan naye akapatwa teke Zito la tumbo kutoka kwa buffalo. Vita ile ilikuwa kali Sana kati ya buffalo na Nolan. Lakini mwisho wa siku ilikuwa ni lazima mshindi apatikane. Nolan alijikuta akiishiwa nguvu baada ya kupigana muda mrefu na buffalo na kujikuta akishindiliwa ngumi nzito mfululizo kwenye tumbo zisizopungua kumi Kisha akatandikwa moja nzito ya uso na kutupwa mbali na kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa. Lakini wakina Dick pamoja na vijana wake waliona huyu jamaa kwa Jina la buffalo hafanyi poa, wakaamua kumsaidia Nolan. Kwa pamoja walianza tena kumshambulia buffalo. Lakini kwa bahati mbaya hawakuwa na uwezo wa kumpiga buffalo wakajikuta wakitandikwa tena kama watoto na buffalo. Mzee Joel alifurahi Sana na kuona Sasa hakuna panya yoyote wa kunisumbua. Lakini kidogo hivi akanyanyuka Nolan akiwa ametokwa na wazimu. "suti ya harusi nimeshaandaa pamoja na taratibu zingine zote inawezekanaje wewe kimtu mmoja uje na kuharibu mipango yangu inawezekanaje??" akajisemea Nolan akiwa tayari amekwisha nyanyuka. Buffalo alimwaangalia Nolan na kucheka kwa dharau, lakini Nolan awamu hii hataki kucheka na mtu anachotaka Sasa ni kuua mtu bila huruma. Nolan akatoka mbio na kuanza kumfuata buffalo kwa kasi nyingine ambayo haielezeki Kisha akaruka na kukunja miguu na kumgonga buffalo kwa magoti na kumtupa chini. Nolan hakutaka kumpiga buffalo akiwa chini akamsubiri anyanyuka. Buffalo aliponyanyuka Nolan akaruka tiktak na kumpata buffalo mateke ya uso na kumuweka buffalo chini kwa Mara nyingine. Nolan akamsubiri tena buffalo anyanyuke kwa Mara nyingine, na buffalo aliponyanyuka Nolan akateleza kwa magoti mpaka kwenye miguu ya buffalo na kuanza kumshindilia buffalo ngumi nzito nzito za tumbo zisizopungua ishirini, Kisha akanyanyuka haraka na kabla buffalo hajaenda chini Nolan akaamua kummaliza kabisa. Nolan aliruka na kutua shingoni mwa buffalo na kumshindilia ngumi zingine za kichwa na kumpasua kichwa hadharani huku mzee Joel pamoja na wakina Dick wakiwa wanashuhudia. Habari ya buffalo ikaishia pale pale. Mzee Joel aliamua kutoroka baada ya kuona mtu aliyekuwa akimtegemea ameshauwawa hivyo akajua kwa vyo vyote vile yeye pia atakuwa Katika wakati mgumu hivyo akaona njia rahisi ni kutoroka tu. Lakini kwenda kutoroka mzee Joel alidakwa na wakina Dick na kuanza kupewa kichapo cha maana. Mzee Joel alitandikwa akatandikwa mpaka Sasa Nolan akamwonea tena huruma baba yake, akawaamuru wakina Dick wamuache. "tumemuacha muheshimiwa Ila tunachotaka atupe pesa zetu au atupe Penina tuondoke nae." akaongea Dick kumwambia Nolan. "mnachoweza kupata ni pesa zenu lakini sio Penina, kwasababu siku chache zijazo Penina anafunga Harusi na kijana mmoja wanaependana kwa dhati." akaongea Nolan maneno hayo ambayo yalikuwa machungu masikioni mwa Dick. "ok nipeni pesa zangu niondoke maana tumepoteza Muda wetu bila faida yoyote." akaongea Dick kinyonge. Lakini hata hivyo mzee akadai hana pesa yoyote, pesa zote amekwishazitumia na zingine akadai walimuibia na hajui nani alimwibia. Nolan alicheka Sana kimoyo moyo kwasababu alijua yeye ndio alikuwa akimwibia baba yake pesa zile. Nolan akaamua kumtetea baba yake, akawaambia wakina Dick hakuna pesa yoyote watapata kwasababu walifanya ujinga kutoa pesa hizo wakati wakijua hawana uhakika wa kumpata Penina. Nolan aliwataka wakina Dick watoweke sehemu ile haraka iwezekanavyo kabla hajawaangamiza na wao. Dick pamoja na vijana wake walijikuta wakiondoka kinyonge huku wakiamini kabisa walifanya makosa makubwa Sana na hivyo wakaamua kuondoka na kurudi nchini mwao bila kinyongo chochote. Huku mzee Joel alipiga magoti na kutubu makosa yake kwa mtoto wake Nolan na kumuomba amsamehe. Yenyewe hata hivyo damu ni nzito kuliko maji, Nolan aliamua kumsamehe baba yake lakini kwa jinsi baba yake alivyompa mateso Nolan akaamua lazima amtandike ngumi moja ya maana kama njia ya kumsamehe. Nolan alimsogelea baba yake na kumuwekelea ngumi moja nzito ya uso na kumuweka baba yake chini, Kisha akaenda akamnyanyua na kumkumbatia na kumsamehe. Baada ya siku kadhaa ya Nolan kuweka mambo Sawa hatimaye Penina na Frank walirejea Tanzania na Kisha harusi yao ikafanyika bila tatizo Lolote huku ikihudhuriwa na watu wengi kupita maelezo. Mzee Joel pia alikuwepo kwenye harusi ile pamoja na mkewe huku wakifurahia harusi ya mtoto wao licha ya kwamba moyo ulikuwa ukimsuta mzee Joel. Kadhalika pia baba yake Frank pamoja na mama yake Frank pia walikuwepo kwenye harusi ile huku wakiwa wameketi kwenye Meza ya heshima kabisa. Nolan pia alikuwepo kwenye harusi ile na yeye ndio alikuwa msimamizi wa kila kitu kilichokuwa kikiendelea Katika harusi ile. Harusi ilikuwa nzuri na yenye kuvutia na kila mtu alifurahishwa nayo. Hatimaye harusi ilimalizika salama na maisha yakaanza rasmi Sasa kati ya Frank na Penina wakawa Sasa ni baba na mama. Lakini pia Frank na Penina waligeuka kuwa matajiri wakubwa kutokana na zawadi mbali mbali walizokabidhiwa Katika harusi yao. Hivyo pia waliweza kuwafanya Wazazi wao waishi maisha mazuri na kusahau ya nyuma yaliyopita. Lakini heshima kubwa ilienda kwa Nolan kwasababu bila yeye wasingefika hapo walipo. Na hata walipofanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume wakaamua kumuita Nolan kumpa heshima kaka yake Penina na shemeji yake Frank. Frank na Penina walifanikiwa kupata mtoto wa pili naye pia alikuwa ni wa kiume wakaamua eti kumuita VAN B na maisha yakaendelea. **************MWISHO ************** mkumbuke nilisema hii story ni zawadi ya xmas na mwaka mpya haikuwa Katika mipango yangu. Hivyo nawashukuru wote mliokuwa pamoja Nami kwa kulike kucoment pamoja na kushare. Mwisho niwaambie tu kuna story nyingine iko jikoni Mungu akijaalia itaanza kuruka mwezi wa pili. Who killed my father "nani alimuua baba yangu" ndio Jina la story mpya inayokuja. Ukiniita VAN BOY utakuwa hujakosea hata kidogo. Nawapenda Sana. ... Read More
*MUUZA MAZIW EP 08* “nzuri tu kaka, shikamoo!” Aliitikia Penina na kasha kumwamkia kaka yake “marhaba mdogo wangu>“ Aliitikia salamu. “Penine kanenepa kweli safari hii, shule imempenda kweli.” Aliongea Lisa. “hapana wifi!?” Penina aliongea na kasha kucheka, ukweli ni kwamba kweli alikuwa amenenepa na kujengeka shepu kwa mahipsi na makalio yaliyo fungashika kiinye plus gwedegwede. Waliongea mengi wakiwa na furaha ya kuwa pamoja tena. Upande wa Lisa moyoni hakuwa na furaha hata kidogo, muda wote alifikiria jinsi ya kumtoa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo. Alifahamu fika jinsi swala hilo lilivyokuwa gumu kwani chumba alichomficha ndicho chumba atakacholala penina , hakuelewa angeweza vipi kumtoa muuza maziwa katika chumba hicho bila ya Penina kugundua. “sijui nitafanya nini mungu wangu?” Aliwaza bila kupata jawabu, hakuona aibu kumshikilikisha Mungu katika uovu wake. “atalala tu lakini , na hivi alivyochoka, na huo ndio utakuwa muda muafaka” Alizidi kuwaza, Hiyo ndio ilikuwa njia pekee aliyoitegemea alitumaini Penina atakapolala ndio uwe muda muafaka. “wifi vipi mbona utafikiri uko mbali sana!?” Penina aliuliza baada ya kugundua kwamba Lisa hayupo pamoja nao katika maongezi. “hapana nipo , mbona tupo pamoja!.“ Aliitikia Lisa haraka haraka baada ya kuzinduka toka kwenye mawazo mazito aliyokuwa nayo. “kweli Lisa upo tofauti sana leo” Jerry nae alikazi “hapana jamani mbona nipo sawa!” Lisa alizidi kujitetea kwa nguvu zake zote kwani hakutaka mtu yoyote ahisi chochote kuhusiana na swala hilo la muuza maziwa, alichokifanya baada ya hapo ni kujaribu kujichekesha na kuonyesha kuwa ana furaha ili kupoteza kabisa hisia za mumewe pamoja na wifi yake. Waliongea kutwa nzima mpaka usiku ukaingia , baada ya chakula cha usiku kila mmoja alielekea chumbani kulala Jerry na mkewe chumbani kwao na Penina pia alielekea chumbani kwake. Wakiwa kitandani kwao si Jerry wala mkewe aliyeonekana kumjali mwenzake, kila mmoja aligeukia upande wake , kila mmoja alirizika na usaliti alioufanya mchana wa siku hiyo. Jerry alipotembea na Sekritari wake wakati Lisa alipotembea na muuza maziwa. Hakuna aliyejua maovu ya mwenzie kila mmoja alimuona mwenzake karanga bao na kumlalia mzungu wa nne. xxxxx- – – – xxxxxx—- – — xxxxxxxx Saa sita na nusu usiku Penina alishtuka toka usingizini , hii ni baada ya kusikia mlio wa kabati likifunguliwa , haraka alisogeza mkono wake kwenye swich ya taa na kuiwasha. Mwanga ulitanda chumba kizima . Penina hakuamini alipomuona mtu akiwa amesimama karibu kabisa na kabati huku kabati likiwa wazi. “kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1” Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri. Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa. “mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!” Aliongea Lisa kwa mshituko CHANZO: /“utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?” Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa. Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati. “da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi” Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi. ITAENDELEAMUUZA MAZIW EP 09 ILIPOISHIA….. “kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1” Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri. Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa. “mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!” Aliongea Lisa kwa mshituko “utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?” Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa. Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati. “da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi” Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi. MUENDELEZO WAKE : “kumbe wewe nan……….?” Penina alijikuta anakatisha kauli yake baada ya kumuangalia vizuri muuza maziwa, hakuamini alichokiona alihisi kama vile yuko ndotoni. “Karani!!!!” Aliita Penina kwa mshangao huku akiwa ameduwaaa. “Penina!!!” Muuza maziwa nae aliita mara baada ya kumuangalia vizuri penina. Wote walibaki wakishangaa huku wakiangaliana usoni, kumbukumbu zao zilirudi nyuma miaka miwili iliyopita. Suji sekondari katika bweni la wasichana chumba namba ishirini na moja. Penina akiwa amelala kwenye kitanda cha dabodeka, ikiwa ni mara yake ya kwanza kulala ndani ya chumba hicho. Sababu hiyo ilikuwa ni siku yake ya kwanza toka ahamie bwenini , mwanzo alikuwa akikaa kwenye nyumba ya mkuu wa shule. Akiwa kitandani hapo alisikia mlio wa mluzi ukisikika kwa mbali karibu kabisa na dirishani sehemu ambapo alikuwa amelala. “it ndizi time!” [ni muda wa ndizi] Mwanafunzi mmoja aliongea kwa sauti ya kunon’gona kasha wenzake walicheka kwa sauti za chinichini. Penina hakuelewa chochote kilichoendelea. Mwanafunzi mmoja aliamka na kwenda kufungua mlango. Watu wane wakiwa wamejitanda khanga waliingia ndani, Penina alizani watu hao ni wasichana. Aliduwaa pale walipotoa Khanga zao. Wote walikuwa ni wanaume. Kila mmoja alienda kwenye kitanda chake waliongea lakini sauti zao zilikuwa za kunon’gona. Penina alibaki ameduwaa tu asijue nini cha kufanya , katika chumba hicho ni yeye peke yake ndio alikuwa amelala peke yake. Alijaribu kuutafuta usingizi lakini alishindwa , vilio vya mahaba alivyokuwa akivisikia usiku huo vilimtesa kupita kiasi, alitamani na yeye lakini hakukuwa na mwanaume kwa ajili yake. Alibaki akijigaragazagaragaza tu kitandani kwake. Mpaka kufikia saa kumi na nusu alfajiri wanaume walipoondoka bado yeye alikuwa hoi. Mchna alimfuata maria na kumweleza shida yake. “na wewe unataka ndizi?” “mmh, mwenzangu manaake hali mbaya!” “usihofu , nitamwelza Bakari akufanyie mpango”. “nitafurahi kweli maanake we acha tu!” Ahadi ya maria ilikuwa kweli , Penina aliteseka kwa siku moja tu , siku iliyofuata nae aliletewa ndizi yake. Ni hapo ndipo alipokutana naKarani mchunga n’gombe wa akina Bakari, ambae sas ndio muuza maziwa. Karani alikuwa akimfikisha Penina mpaka basi jambo lililomfanya Penina ampende kupita kiasi, alimuahidi kwamba atakuwa nae milele lakini ajabu ghafla alitoweka. Alipomuuliza Bakari kuhusu swala hilo alimwambia hajui alikoelekea. “nyumbani katoroka alafu ameiba baadhi ya nguo zangu , hafai kabisa yule jamaa.” BakaRi aliongea kauli hiyo iliyomaliza kabisa nguvu za Penina. Alimpenda sana Karani na alitaka kuwa nae siku zote za maisha yake. Hakuelewa ataishi vipi bila kuwa nae. “lakini usihofu Penina nimekuletea mwingine” Bakari aliongea akiwa ametabasamu huku akishika bega la kijana mpya aliyekuja nae siku hiyo. Penina alimwangalia kijana huyo kuanzia chini mpaka juu lakini hakuona hakuona cha kumlinganisha na Karani. “Siitaji tena kama Karani hayupo basi “ Penina alijibu kwa dharau. “Penina hata huyu yuko bomba tena mkali kuliko hata Kara….” “Nimesema sitaki husikii” Penina alifoka tena kwa sauti kubwa jambo ambalo liliwaogopesha wote, sababu lilikuwa ni jambo la hatari, hawakutaka kuendelea kumsemesha waliogopa angewasababishia msala kwa mlinzi endapo ataisikia sauti yake. Siku iliyofuata Penina aliamua kuhama chumba hicho kwani hakuona raha tena ya kuwa ndani ya chumba hicho wakati Karani hayupo. Rafiki zake walimbembeleza asahau habari ya Karani na akubali kuwa na yule kijana mpya ili arudi kwenye kile chumba lakini yeye aliwakatalia katakata , hakuona mwanaume wa kumfananisha na Karani wake. Wiki moja baada ya Penina kuhama ndani ya chumba hicho mlinzi alishtukia mlinzi alishtukia kila kitu . Aliwakamata wanaume wote wakiwa ndani ya kile chumba cha kina Maria na kasha wanafunzi wote waliokutwa ndani ya chumba hicho walifukuzwa shule. Penina alikuwa ameponea chupuchupu, kama isingekuwa Karani kutoroka nyumbani kwa kina Bakari basi leo hata yeye angelikuwa miongoni mwao na Karani wake. Wiki moja baada ya Penina kuhama ndani ya chumba hicho mlinzi alishtukia mlinzi alishtukia kila kitu . Aliwakamata wanaume wote wakiwa ndani ya kile chumba cha kina Maria na kasha wanafunzi wote waliokutwa ndani ya chumba hicho walifukuzwa shule. Penina alikuwa ameponea chupuchupu, kama isingekuwa Karani kutoroka nyumbani kwa kina Bakari basi leo hata yeye angelikuw miongoni mwao na Karani wake. Jambo hilo lilimfanya azidi kumpenda Karani na kujipa ahadi kwamba lazima siku moja atamtafute mahali popote duniani.. Ajabu leo anamkuta ndani ya chumba chake cha kulala. Hakutaka kumuuliza amefikaje , iwe kweli amekuja kuiba au vyovyote alichofikiria sasa ni kumuokoa ili kaka yake asijue kwamba yumo humo. “Ngo, ngo ngo” Mlango uligongwa , Penina pamoja na Muuza maziwa walichanganyikiwa. “Penina!, Penina! Fungua mlango usihofu nina Bastora!” Kauli hiyo toka kwa Jerry ndio ilizidi kuwachanganya akili. “Tafadhari niokoe Penina sitaki kufa leo!” “Usihofu Karani nitafanya kila njia!” Penina aliongea. ITAENDELEA..*MUUZ MAZIW EP 10* MWISHOOOOOOOOO Wazo la kuingia kabatini lilikuja tena kichwani kwa muuza maziwa, na Penina bila kuchelewa akaufunga mlango wakabati hilo. “Penina fungua mlango” alijua labda mwizi huyo amemteka mdogo wake. Upande wa lisa alizidi kuchanganyikiwa. Sauti ya Jerry ilisikika tena huku akizidi kuugonga gonga mlango kwa nguvu, akilini mwake “Fungua Penin…..” Jerry alikatiza kauli hiyo baada ya Penina kufungua mlango. “yuko wapi, yuko wapi huyo mwizi?’” Jerry aliuliza huku akiwa ameishika Bastora yake sawia , tayari kwa kufyatua risasi. “hapana kaka!” “hapana nini kakimbia eeh au kaificha?” “sio mwizi kaka!’ “sio mwizi!? ,nani? Na yuko wapi?” Aliuliza kwa mshangao. “Ni ndoto nilikuwa naota “ “Ndoto!!?” “ndio kaka!” “ooh! Jamani penina umetushtua wenzako , uuh!” Aliongea Lisa na kuvuta pumzi , kwani wasi wasi ulimtoka baada ya kusikia kama ni ndoto. “Penina unauhakika kama ni ndoto!” Jerry aliuliza huku akiliangalia kabati, kasha akaanza kulisogelea taratibu. “ndio ! Ndio! Kaka” Penina aliitikia kwa hofu , alihisi kwamba pengine Jerry amegundua kitu, hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Lisa ambae alichanganyikiwa kabisa. “hapana siwezi kurihusu jambo hili hata kidogo” Aliwaza Lisa pale Jerry aliponyoosha mkono ili kushika kitasa cha kabati hilo., alimkimbilia haraka. “Honey umekwisha elezwa kwamba ni ndoto kwanini unapoteza muda , twende tukalale mpenzi mwenzako nimechoka>“ Lisa aliongea kwa sauti laini. “Hapana nataka kufunga vizuri hili kabati”. Aliongea Jerry huku akilisukumiza kabati, hakujua kwamba halijajifunga vizuri kwa sababu kuna mtu ndani. Alilisukumiza huku muuza maziwa akisikilizia maumivu ya kuminywa na kabati hilo, alijuzuia kupiga kelele huku mwili mzima akitetemeka kwa woga. “Achana nalo hilo Dear kwanza kabati lenyewe hilo bovu.” “bovu!!!” “eeh bovu hata mimi wifi alinieleza’ Penina alidakia “sasa kwanini hamjamuita Fundi?” “usijali mpenzi nitamuita kesho, twende basi tukalale.” Lisa aliongea kwa sauti nyororor ambayo ilimshawishi Jerry moja kwa moja. “Lala salama Penina “ Aliaga “sawa kaka “ Walitoka na kwenda chumbani kwao wakiwa wamekumbatiana.. Penina aliufunga mlango kwa furaha na kisha kwenda kulifungua kabati. Alikuwa na hamu kweli ya kuwa na Karani wake. Karani ambae hadi wakati huo alikuwa akitetemeka kwa hofu, hakuamini kabisa kwamba ndani ya chumba hicho yumo yeye na Penina pekeyeo. “kabla ya yote nikumbatie mpenzi!.“ Penina aliongea akiwa na tabasamu zito usoni kwake . Muuza maziwa hakusita kumkumbatia. “siamini kabisa mpenzi!” “hata mimi penina!” “hivi umejuaje kwamba ninaishi hapa?” Aliuliza penina akiamini kwamba kilichomleta muuza maziwa humo ni yeye. “Nilikuona ulipokuwa unaingia” Muuza maziwa alijibu, hakutaka kumweleza kwamba aliyemleta humo ni wifi yake. “ndio maana nakupenda Karani!” “hata mimi nakupenda!” Karani nae akaitikia Alimsogelea zaidi na kumbusu ‘mwaaaa!!!’ ‘Mwaaa!!!’ Penina nae aliitikia busu hilo. Muuza maziwa kama kawaida yake akaanza manjonjo yake, Penina alikwisha jua nini kinachofuata akaanza kujichekesha kwa kicheko cha kugunaguna. “unajua nafanya kazi gani sasa?” Muuza maziwa aliuliza “sijui!” Penina aliitikia “Nauza maziwa!” “aah kwa hiyo nikuite Muuza maziwa sio.” “sawa sawa watu wote wananiita hivyohivyo.” “haya basi muuza maziwa nataka unipe mambo” “hapa ndio mahala pake, utapata ondoa hofu!” Muuza maziwa aliitikia na kuanza kumtekenya Penina kwa ulimi wake. Penina alicheka kwa kicheko cha chinichini, mambo ya muuza maziwa yalimfanya akumbuke kipindi walipokuwa wote kule shule kipindi Karani ni mchunga ng’ombe lakini sasa yuko mjini na ni MUUZA MAZIWA. END OF SEASON ONE. ... Read More
CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA NANE (08) ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA: Basi alijikuta mpweke sana na alijikuta anatamani, kuongea na vicent,ili apate kampani na kupoteza muda kidogo. Hata sijui ni kwanini alimuwaza vicent kuwa ndio mtu pekee wa kumtoa upweke. Hata mimi sijui,ila tutajua hivi karibuni. Basi aliingalia simu kwa muda nakujifikiria ampigie au atulie asimpigie. Basi nafsi ya niram ikawa inashindana,moja inamwambia piga nyengine, inamwambia usipige ila akiwa katika mgongano wa kutoa maamuzi nini afanye, gafla akaona kitu moyo ukapiga paaaaah!!! .alishindwa kuamini alichokiita. endelea........ Niram alishindwa kuamini alichokionaa, kwa muda ule kiukweli alitoa macho kama ndubwi, spidi ya moyo kwenda mbio vilizidi kuongezea. Hakuamini kuona mtu aliyekuwa anamuhitaji kwa muda huo ndo alikuwa anampigia.basi alichukua simu yake na kuipokea. "hellow vicent".ilikuwa ni sauti tamu yenye kusisimua mwili.hakika hata vicent alipata kigugumizi cha gafla na wakati yeye ndie aliepiga. "aaaghahg!! Niambie niram umeshindaje kipenzi? ".aliongea vicent kwa sauti ya upole na ya kiume,kiasi niram alijisikia raha sana kuisikiliza. "nipo poa kulikuwa na wageni leo basi kulikuwa na kazi kweli".aliongea niram kwa sauti yake ile nzuri na ya upole, kama ya Madeko hivi. "oooh pole mamy si ungeniita nije nikusaidie".aliongea vicent, kwa utani huku akisubiri jibu. "ahhhhah! Uongo tu ungekuwa kweli wewe".alijichekesha ki kikekike niram huku anabadili mikao ya kukaa pale alipokuwa. "yaap ningekuja kwanini nisije kwa rafiki yangu kumsaidia jamani?".alijiongelesha kama anauliza hivi huku ikiwa sauti fulani inayoonyesha hali ya kujali. Niram alifurahi sanaa kusikia vile. "mmh! Basi nashukuru kwakunijali kipenzi".aliongea niram kwa madeko. "usiliongelee hilo ni wajibu wangu kama rafiki".aliongea vicent. "basi wifi anapata raha sana".aliongea niram huku akitia kijineno cha mtego. "sina mama yangu, bado sijabahatika".aliongea vicent kwa utulivu wa hali ya juu, kwa hakika ungesema kweli mwanaume ndiyo huyu. Alijua sana kuongea na mwanamke na akaelewa. "ooh usijali Mungu atakupa my"aliongea niram. "sawa nashukuru sana na mimi ntajiona ni mwenye bahati".alijibu vicent,basi waliongea mengi sana mpaka walipoagana, kwa maana kesho ilikuwa ni siku ya shule. **** Ilikuwa ni siku ya pili, watu walikuwa na pilikapilika zao kama kawaida. Huku kila mmoja akiwa katika harakati za utafutaji. Magari yakikuwa yanapishana kila wakati. Basi muda huo shuleni niram, alikuwa ni mtu wa tabasamu muda wote,alikuwa kachangamka sana hata marafiki zake wakimshangaa, ila aliyejua tofauti ya niram ni hajra peke yake. Alimtazama kwa muda kisha akamuuliza "vipi dada mbona huko happy hivyo?".aliuliza kwa sauti ya chini hajra, huku wengine wakiwa bize kufanya yao. "mmh kwani nikoje jamani!?".akiuliza niram,huku akiachia tabasamu pana sana usoni mwake. "we mwenyewe ujioni kama upo tofauti leo?".aliongea hajra huku akapachika na swali. "hamna bwana mama jana alinifurahisha sana ".aliongea niram, huku akionyesha kuwa hakuwa akiongopa. "oooh!! Sawa".alijibu hajra, huku anageuka kujumuika na wengine. Niram yeye muda wote alikuwa ni kutabasamu alijishangaa hata kwanini, anajiona ni mwenye amani sana. Basi akachukua kitabu na kuanza kujisomea kwa umakini wa hali ya juu. **** Na huku shuleni kwa akina vicent mambo yalikuwa hatari. Maana suma alikuwa ana mchecheto wa hali ya juu halikuwa kwenye stori za kufa mtu. "basi jana niwaambie si somoe akanipigia bwana unajua nilichokifanya nikamchunia mi nilikuwa na miadi na hadija ye ananiletea kiwingu".akanyamaza kidogo kisha akaendelea. "basi jana nikakutana na hadija weeeeeh!!mtoto fundi mtoto anakata uno kama feniii we acha, yule mtoto balaaa".aliongea suma huku richard na vicent wakiwa wanamuangalia.ila rachard mbavu alikuwa hana kwa kicheko, huku vicent akiwa kutabasamu tu. "umemaliza? ".aliuliza vicent. "daah!huyu kashaanza ulokole wake".aliongea suma. "siyo ulokole uwo ni ushamba, we mwenyewe unaona sifa alafu ukigongewa dada yako unawaka kama pilipili ".aliongea vicent akionyeshwa kuchukizwa na rafiki yake huyo. "yani kwakuwa wewe upendo kwahiyo sisi tusiongee? "alihoji suma, huku kama alishaanza kupaniki hivi maana sura ilichenji. "yani hakuna kusema chochote hapo tabia zako azituvutiii unawazalilisha dada zetu tusikuambie".aliongeara Richard huku amemkazia macho bila chembe ya uoga. "mwambie huyoo huo ni ujinga broo".aliongea tena vicent huku anamtazama. "eeh basi yaishe ,tuongee mengine vipi yule mtoto wa Kihindi nipe stori basi".aliongea tena suma. "aisee suma ukoje mbona hupendeza kuwa mmbea".aliongea richard. "aaah! Kausha mi si nishabadili mada, nauliza mambo mengine".alijitetea suma huku akikaa vizuri kuambiwa yaliyojiri. "hivi unajua kwanini jana nilikukatia simu? Coz lisilokuhusu usilikingie kifua, kila mtu apambane na hali yake mambo ya mahusiano yangu hayakusu"aliongea vicent huku akinyanyuka,na kuanza kutoka nje, richard akamfuata, maana vicent alionyesha kuchukia. Suma akabaki katulia kanywea vibayaaaa, kama kamwagiwa maji.*** Mama vicent alikuwa sebuleni, alikuwa amekaa na mama wa makamo kama yeye kwakweli walionekana ,kama wapo kwenye maongezi mazito, maana vilisikika vicheko vya hali ya juu. Ila gafla wakaacha kucheka macho yote yakageuka kutazama........ Itaendelea. ... Read More
NILIPOTEZA WATOTO WANGU WANNE (Mkasa wa maisha ya ndoa ya Naomi) Sehemu ya kwanza(01) Naitwa Naomi Charles,katika maisha yangu sikuwahi kuamini haswa mambo yanayohusiana na nguvu za giza,kitu pekee nilichojua ni kwamba hivi vitu huwa vipo midomoni mwa watu tu,lakini kadri nilivyozidi kukua na kuingia katika maisha ya ndoa hapo ndipo nilipokuja kushuhudia kwa macho yangu kwamba haya mambo si ya kwenye midomo ya watu,bali yanafanyika na kuishi katika jamii mwa watu. Ndugu yangu amini nakuambia,kama kuna mwanga basi elewa hata giza lipo,na siku zote lengo la kuwepo mwanga ni kwasababu ya kukimbiza giza,kusingekuwa kuna ulinzi wa Mungu endapo kama mambo ya giza yasingekuwepo,nilichokuja kuamini ni kwamba siku zote uwepo wa mwanga wa Mungu wa wanadamu ni kwasababu ya kukimbiza giza linalowanyemelea wanadamu. Niliwahi kusoma vitabu na kama vile "Dollo,Mama yangu anakula nyama za watu" na kitabu cha "Jini lilivyonilelea mwanangu kimiujiza",waliandika na kusema hiyo ni mikasa ya ukweli lakini bado nilisema kwamba huu ni utashi tu wa utunzi wa watu. Ni miaka takribani 15 imepita tangu niamue kuachana na safari ya ndoa na John mume ambae nilipenda kumuita J...Alinioa ndoa ya halali kabisa,nakumbuka kipindi naonana nae alikuwa na miaka 40 wakati huo mimi nilikuwa na miaka 28,alikuwa ameniacha mbali ki umri lakini haikuwa sababu ya penzi letu kufa. Lakini kuna mambo mawili ambayo yalinishangaza kwake,alikuwa na umri mkubwa sana na majukumu ya kumuingizia pesa lakini cha ajabu bado alikuwa anaishi na Mama yake mzazi,cha pili ni kwamba aliniambia kwamba alipokuwa na umri wa miaka 30 alipataga mke ambae walipanga kuoana lakini aliamua tu kuishi nae nyumbani kwao kama mke wake,baada ya miaka mitano kupita John aliniambia mwanamke yule aliamua kukatish safari ya mahusiano na yeye,alibahatika kuzaa nae watoto wawili lakini wote walifariki. John hakuniambia ni sababu ipi iliyomfanya hasa aachane na yule mwanamke. Nakumbuka baada ya ndoa yangu mimi na John nilimshawishi na kumwambia kwamba mimi staki tuendelee kukaa pale na mama yake,tuondoke tukaanzishe maisha yetu na kama Mama tutaendelea kumjali maana si kwamba amezeeka kufikia kipimo cha kuweza kukaa nae na kumlea. John alinikubalia na kusema tutahama lakini tukae kae kwanza pale kwao wakati anajipanga. Miezi miwili ilipita tangu ndoa,hatimae nilishika ujauzito tukiwa bado tunakaa na palepale kwa Mama yake,ambae ni mama mkwe wangu,wote walifurahi baada ya kuona mimi nimekamata ujauzito. Wanasema kulea Mimba sio kazi bali kulea mtoto,miezi tisa si mingi kama ukiwa na subira,hatimae nilishusha mtoto wa kiume,furaha kubwa ilitawala baina ya familia zetu pamoja na mimi na mume wangu,ilikuwa ni furaha isiyo na kifani,wajirani na marafiki wa kutembelea hawakukosekana,taratibu kazi ya kulea mtoto ilianza. Hatimae miezi sita ilipita,mtoto alizidi kuchangamka,kilichobaki kinaniumiza ni kwamba kila nikimuambia mume wangu tuhame kwa mama yake tukaanzishe maisha yetu alikuwa ananijibu bado hajajipanga,likikuwa linaniumiza sana kichwa swala hili na nilijikuta nakata tamaa ya kuwa namuuliza mara kwa mara. Katika safari yangu ya ndoa sintakuja kuusahau usiku,usiku ambao vindumbwe ndumbwe na maajabu vilianza katika maisha yangu,nakumbuka nilikuwa nimelala mimi na mume wangu pamoja na mtoto wangu huyo wa miezi sita,ambae tulimpa jina la Grey,niliota tumezunguukwa na wanawake wanne mimi na mume wangu kwenye kitanda ambacho tulikuwa tumelala,wanawake hao walikuwa wamevalia shuka nyeupe ambazo wamejifunga rubega,nilitaka kupiga kelele lakini moja ya wanawake wale aliniziba mdomo kisha mmoja wao akanyoosha mikono yake na kumchukua mwanangu,nilikodoa macho na kutamani kupiga kelele lakini nilishindwa kwasababu nilishikwa,nilimkazia macho yule mwanamke aliemchukua mwanangu na ndipo niliposhikwa na bumbuwazi baada ya kugundua kwamba ni mama mkwe wangu.Alianza kuondoka na mwanangu huku akifuatiwa na wale wanawake watatu waliobaki,nilianza kupiga kelele za kumlilia mwanangu mpaka nalia huku nikiinuka kitandani kuwafuata,ghafla nilishtushwa na mume wangu huku akiniambia"we Naomi unaenda wapi huko na kupiga kelele na wakati mtoto huyu hapa,umepatwa na nini".Nilianza kuhema huku nikimwangalia mwanangu kama yuko salama,wakati huo nikawa namwaga jasho. Hazikupita sekunde nyingi,mwanangu alianza kulia huku akitoa povu jeupe mdomoni.Nilijikuta naanza kuchanganyikiwa akili.... JE NINI KITAENDELEA Je Grey atapona...? Je ndoto aliyoota Naomi inauhalisia wowote katika maisha yao..? tukutane sehemu ya pili kesho jioni panapo majaaliwa. Ruksa kushare,pia toa maoni yako ili watu wajifunze zaidi. NILIPOTEZA WATOTO WANGU WANNE-(02) (Mkasa wa maisha ya ndoa ya Naomi) Ilipoishia. Hazikupita sekunde nyingi,mwanangu alianza kulia huku akitoa povu jeupe mdomoni.Nilijikuta naanza kuchanganyikiwa akili.... Sasa endelea... Nilijikuta nalia tu huku nikiita"Greeeey....Greeey",wakati huo sasa mume wangu nae ndipo alipomtazama mtoto wetu na kugundua kwamba mdomoni anatoka povu,nilimuona ameshtuka ghafla na kuinuka kutoka kitandani huku akiuliza"Naomi,mtoto amekuwa na nini,inamaana alikuwa anaumwa harafu hukuniambia mpaka amezidiwa hivi..?". Moja kwa moja Mume wangu alijua labda huenda nimemficha sikumwambia kama Grey alikuwa anaumwa kitu ambacho hapana. Grey alizidi kulia zaidi na wakati huo povu jeupe liliendelea kumtoka,wote tulikuwa tumechanganyikiwa hatujui tufanye nini,ndipo Mume wangu alienda sebureni na kuchukua maji haraka haraka kisha kumnywesha Grey,wakati anakunywa maji alitulia kwanza kulia lakini baada ya kumaliza tu kunywa maji kilio kiliendelea tena,nilimchukua na kuanza kumnyonyesha lakini alikataa ziwa,mara muda haukupita Bibi yake ambae ni mama yake na Mume wangu akawa ametugongea mlango"nyie kuna nini tena humu?,mbona mtoto analia hivi".Mume wangu alimfungulia mlango kisha akaingia ndani,alifika na kuanza kumtazama mtoto ambae alikuwa bado analia,mimi nilijikuta naacha kumtazama mwanangu badala yake nilianza kumtazama huyu mkwe wangu huku nikikumbuka nilichoota,nilitamani nijue zaidi hivi nilichoota kina uhalisia au ilikuwa ndoto tu. Ghafla nilimuona Mama mkwe wangu akimuweka mwanangu kitandani na kusema"huyu mtoto mbona ameumwa ghafla hivi kulikoni,au alianza toka mchana lakini hukutuambia,hebu mwangalieni na mwili wake ulivyobadilika na kuwa mwekundu"aliposema hivyo moyo ulinilipuka na kuacha kumtazama yeye kisha kumtazama mwanangu,sikuamini kuona mwili wa mwanangu aliekuwa mweupe umekuwa mwekundu rangi ya damu kabisa,kulia nako kukazidi,nilimchukua na kuanza kumbembeleza lakini haikusaidia kitu,matokeo yake na mimi nilijikuta naanza kulia huku nikisema"Baba Grey mwanangu anakufa,Mwanangu anakufaaa"Nililia sana wakati huo Baba Grey nae anawaza afanye nini. Mama mkwe alitoka ghafla kisha kuelekea sebureni,alikaa huko kwa dakika kadhaa kisha akarudi na maji kwenye kikombe akasema"Hebu mnyweshe haya maji nimeyachanganyia chumvi na sukari huenda yakamsaidia",kweli niliyachukua haraka haraka kisha nikamnywesha,kweli duniani kuna maajabu,kwani baada tu ya kumnywesha yale maji Grey aliacha kulia na kukubali kunyonya lakini mwili wake uliendelea kuwa mwekundu. Ilikuwa mida ya saa kumi usiku na ndipo Baba Grey alisema sasa tumpeleke Grey hospitali,kweli juhudi za kujiandaa kwenda hosipitali zilianza na hatimae safari ilitimia,tulifika kwenye Zahanati moja hivi iliyokuwa jirani na sisi na kumkuta daktari wa zamu,walitupokea kisha wakamuangalia mtoto kitendo kilichofanya daktari ashtuke baada ya kumuona ni jinsi gani Grey alivyokuwa mwekundu,harakati za vipimo na matibabu vilianza,juhudi zilifanyika na wapimaji wakati sisi tukiendelea kusubiri,majibu yalikuja ya kushangaza kwani tuliambiwa kwamba Grey hana ugonjwa wowote,hapo ndipo nilipoanza kuona kwamba huenda kweli kuna mauza uza. Tulipewa kitanda ili mwanangu alale kwa ajiri ya kukicha aendelee na matibabu zaidi,nilikaa na mwanangu pale kitandani wakati huo Baba Grey aliniacha huku akisema kwamba anaenda kutoa taarifa na kufanya mchakato wa chakula asubuhi ili aniletee.Nilibaki na mwanangu mle wodi ya watoto akiwa amelazwa,nilipomnyonyesha alikuwa akinyonya kama kawaida.lakini ghafla alianza kukataa ziwa,hali ya kulia ilizidi,alianza kulia toka saa kumi na moja na nusu ya alfajiri,wauguzi walikuja tena kwa ajiri ya vipimo lakini majibu ni yale yale kwamb hamna ugonjwa,walimpa dawa za kutuliza maumivu lakini hazikuzaa matunda.Hatimae ilipofika mida ya saa moja mwanangu Grey aliaga dunia...... JE NINI KITAENDELEA Je ni nini kipo nyuma ya pazia katika kifo hicho cha Grey. Usikose sehemu inayofuata kesho muda na wakati kama huu. NILIPOTEZA WATOTO WANGU WANNE-(03) (Mkasa wa maisha ya ndoa ya Naomi) Tulipoishia .... Hatimae ilipofika mida ya saa moja mwanangu Grey aliaga dunia...... Sasa endelea... Kilio changu kizito kilitawala ndani ya chumba kile katika wodi ya watoto,uchungu mzito wa uzazi na kuondokewa na mtoto ulitawala ndani ya moyo wangu,mawazo yangu yote nilijua na kufahamu kwamba mwanangu hajafa katika kifo salama,bali ameondolewa Duniani kwa kulazimishwa.Wauguzi na akina mama wengine ambao walikuwa wanauguza watoto zao walijitahidi sana kunituliza lakini ndio kama walikuwa wanazidisha maumivu moyoni mwangu. Mwisho mume wangu alikuja akiwa ameleta chai,alipofika kwenye chumba ambacho ndicho tulikuwa tumelazwa na mwanangu moja kwa moja alijua tayari mtoto wetu hayupo duniani,kwani alinikuta bado nalia lia japo sio kama mwanzo kwasababu Wamama wenzangu walikuwa wakijitahidi sana kunipoza na kunituliza,hapakuwa na kingine zaidi ya mchukua mtoto wetu Grey ambae alikuwa tayari ni marehemu kwa ajiri ya kuanza safari ya kurudi nyumbani kuweka msiba,tulichukua gari huku mimi njia nzima nikienda nalia. Grey alikuwa bado mdogo,alikuwa na miezi sita hivyo hata mazishi yake yalipangwa yafanyike siku hiyo hiyo,kila mara nilikuwa nauchungulia mwili wa mwanangu,sikuamini kama kweli amenitoka,nilikuwa nimemzoea,alikuwa na afya nzuri na mwenye kuchangamka,lakini kilichokuja kunitisha zaidi Grey baada ya kufariki mwili wake uliirudia hali yake kwa maana ya kwamba ile hali ya mwili kuwa mwekundu utafikiri kalowekwa kwenye damu ilitoweka.Nilibaki najiuliza huu ni ushirikina wa namna gani,sikutaka kumtuhumu mama mkwe moja kwa moja kwasababu sikuwa na ushahidi wowote,ndoto pekee huwezi ukaitumia kumuhukumu mtu,japo ilikuwa ni ndoto ya mashaka. Hatimae saa kumi ya jioni ilifika muda ambao ulipangwa kwa ajiri ya mwanangu Grey kuzikwa,watu mbalimbali,majirani ndugu na marafiki walikusanyika kwa ajiri ya kutoa heshima zao za mwisho kwa kichanga changu kile,pale nilijifunza kitu kimoja kwamba siku zote ukiishi na watu vizuri basi utakuwa mtu wa watu,mwanangu alikuwa ni mdogo na asiejulikana sana mbele za watu,lakini watu waliohudhuria walikuwa ni wengi kiasi kwamba ni msiba wa mtu mzima na umaarufu wake. Basi jioni iliisha kwa kumpumzisha mwanangu katika nyumba yake ya milele. Hatimae maisha ya upweke bila kulea bila kunyonyesha yalirudi,tulikaa wiki moja na baada ya hapo ndugu jamaa na marafiki waliokuwa wamekuja kututembelea nao waliondoka na hatimae tulibaki tukiishi watu wanne kama mwanzo yaani mimi,mume wangu,mama mkwe wangu pamoja na mdada wa kazi aliekuwa akiitwa Rhoda. Sikujiskia tena kuendelea kukaa na pale pamoja na mama mkwe wangu,hatimae niliamua kuanza kumsumbua mume wangu kwamba inatupasa tuhame pale tukaanzishe maisha yetu,lakini bado juhudi za mume wangu kujaribu kukataa ziliendelea,na mimi pia neno kuhama nililigeuza wimbo wa taifa mdomoni mwangu kila mara nilipokaa nae.Hatimae siku moja aliniambia kwamba amenielewa na atakaa kuongea na mama yake ili tuweze kuondoka na kwenda kuanzisha maisha yetu. Moja kati ya siku nyingine ambayo sintakuja kuisahau katika maisha yangu ni siku ambayo nilikuwa natokea chumbani naelekea sebureni,nilichungulia kidogo nikaona mtu na mama yake wamekaa wanaongea,yaani mume wangu na mama yake,kwakweli nilinyata taratibu taratibu mpaka karibu na ukuta wa kukatizia kuingia sebureni ili niweze kusikia wanazungumza nini,nilitamani sana kusikia wanazungumzia swala la mimi na mume wangu kuhama,nilikuwakuta wameshaanza mazungumzo ambayo sikujua wanaanzia wapi lakini tumbo lilikuja kushtuka baada ya kumsikia mama mkwe wangu akitoa kauli kwa mume wangu na kumwambia"Sawa kama mnataka kuhama hapa nyinyi hameni lakini ukumbuke kwamba bado una deni kubwa sana kwangu,bado hujakamilisha kile kinachohitajika kwahiyo wewe hama lakini ukae unajua kwamba deni langu ni lazma ulipe"Tumbo lilinikata na kuanza kujiuliza ni aina gani ya deni ambalo mime wangu anadaiwa na mama yake,nilitamani niendelee kusikia mazungumzo zaidi lakini nilimuona mama mkwe wangu akinyanyuka na kushika njia ya mlango kuelekea nje. JE NINI KITAENDELEA Je ni aina gani ya deni ambalo anadaiwa John na mama yake..? Usikose sehemu inayofuata hapa hapa kesho panapo majaaliwa. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: