Home → simulizi
→ MREMBO HIMANA
(Full story )
Jana usiku niliamka mida ya saa nane, na kama kawaida yangu, nikalia sana. Ni ajabu kwa mwanaume kulia, lakini kwangu imekuwa kitu cha kawaida sana. Nadhani ninapolia huwa najihisi nafuu kiasi, na kwa namna fulani napunguza uchungu ulio ndani yangu. Nimekuwa nikifanya hivyo kwa muda wa mwaka mzima sasa, lakini usiku wa jana ulikuwa tofauti kidogo. Baada ya kulia sana, niliamua kwamba huu ndio utakuwa mwisho.
Mwaka 2007 tarehe kama ya jana nilikutana na binti mmoja nikiwa masomoni Arusha. Huyu binti ni mmang’ati kwa kabila, ana urefu wa wastani, rangi ya ngozi nyeupe inayofanana mwili mzima, yaani si kama rangi za mabinti wa siku hizi za kuchanganya na kutafutiza. Ni mzuri mno kwa sura, kama unavyojua wadada wengi wa mkoa huo. Ngozi yake ni laini na nyororo kama ya mtoto mdogo, na ni mwenye macho mazuri. Yaani kwa kifupi hana kasoro ya kuonekana kwa macho.
Tulikutana kituo kimoja cha daladala wilayani Monduli, mimi nikiwa naelekea Arusha mjini. Nilimkuta amekaa, kama ana huzuni, japo hilo halikuficha uzuri wake. Nilimsogelea na kumuuliza kwa kuonesha kujali, “Mrembo, nini tatizo? Unaonekana una huzuni”. Alinitazama na kujibu kwa upole sana,”Hapana, niko sawa”. Niliamua nitatumia fursa hiyo kuongea naye, na kweli alinionesha ushirikiano mzuri tuu. Tulizungumza kwa kifupi, nikimuuliza maswali ya hapa na pale, kasha likaja gari tukapanda. Uelekeo wetu ulikuwa mmoja, na kwa nasibu tulikaa siti moja. Tuliendelea na mazungumzo na huyo binti, aliyejitambulisha kwa jina la Himana, na kiukweli niliifurahia safari yangu.
Kufika mjini, mahala ambapo sote tulishuka, tayari tulishajenga urafiki kiasi cha kukubaliana kuonana tena na hata kupanga siku ya kuonana. Sidanganyi, wakati huo nilikuwa tayari kwenye mahusiano, na binti ambaye tulipendana sana. Huyo mpenzi wangu naweza sema hatukuwahi kukosana kwa miaka mitatu yote tuliyokuwa pamoja, ukiacha mikwaruzo kidogo sana ya mara chache. Nilimpenda sana mpenzi niliyekuwa naye, Hilda, na nilimuahidi tungeoana mara tuu baada ya kumaliza masomo yangu ya muda mfupi huko Arusha. Tayari nilishajitambulisha kwao, na kwa uwezo wa wastani niliokuwa nao, nilijitoa kwake kwa kiwango kikubwa kiasi cha kumuaminisha kwamba mimi ndiye mume wake. Sikuwahi kuvutiwa na msichana mwingine yeyote zaidi ya Hilda, mpaka nilipokutana na Himana.
Tulianza mawasiliano ya kasi sana na Himana, kiasi cha kunifanya nianze kumpuuza Hilda. Nilijihisi kuvutiwa na Himana, na kila mara mawazo yaliponijia kuwa nina mpenzi anayeniamini na kunithamini, akili yangu haikunipa hiyo fursa kwa muda mrefu bali ilinielekeza kwa Himana ambaye wakati huo penzi kubwa lilianza kushamiri kati yetu. Binti huyu, aliyepata umri wa miaka 21 tu wakati huo, alinionesha mapenzi nisiyowahi kuona kabla. Hapa niwe muwazi zaidi, kwa miaka mitatu niliyokuwa kwenye mahusiano na Hilda, hatukuwahi kukutana kimwili, isipokuwa mwezi mmoja kabla ya safari yangu ya kwenda Arusha. Hilda alikuwa na misimamo binafsi ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa, na niliweza kumvumilia kwa miaka mitatu huku nikiwa muaminifu kwa asilimia 100. Baada ya kujitambulisha kwao rasmi, na kuanza hatua za kuoana, ndipo alikubali tukutane kimwili, na alifanya hivyo kunihakikishia kuwa hata ninapokwenda kusoma, nijue kwamba mimi ndiye mwanaume wake pekee, na alinipenda kwa dhati, hivyo nisimpe msichana mwingine moyo wangu.
Kwa bahati mbaya sana, Himana alinisahaulisha hayo yote. Tuliingia kwenye mahusiano kwa kasi sana, alinifuata popote, aliniletea vyakula, alizungumza nami maneno ya mahaba na hakutaka kujua kama nina uhusiano au la. Alinipa raha kiasi cha kupuuza ahadi zote tulizowekeana na Hilda, na sikukumbuka tena gharama nilizoingia kwa ajili yake wala heshima niliyokuwa nayo kwa familia yake. Hilda alianza kulalamika kuwa nimepunguza mapenzi kwake, lakini nilimpuuza. Sikujali tena hisia zake, nilidharau hata bikira yake ambayo mimi ndiye niliitoa, na sikuona tena uthamani wake kama hapo awali.
Mapenzi na Himana yalishamiri sana, nikamaliza shule yangu lakini sikutamani kurudi Dar es Salaam nilipoishi. Niliamua kufatilia uhamisho kazini kwangu, na kwa vigezo ambavyo nilitoa, haikuwa ngumu kupata. Nilijaribu kutoa vigezo vya msingi kuhusu uhutaji wa mtu wa taaluma yangu katika ofisi zetu za Arusha. Sikumjulisha Hilda juu ya uamuzi wangu wa kuhama, isipokuwa nilipopata uhamisho nilimwambia kuwa ofisi imeamua kunihamisha. Mara kadhaa nikiwa nasoma na hata baada ya kumaliza masomo alinitaka tuonane, kwa kuniomba niende Dar es Salaam walau mara moja, au hata yeye aje Arusha, lakini nilimpa sababu kadhaa na kumkatalia. Mawasiliano kati yetu yalizidi kuwa hafifu na muda nilioahidi tungeoana ulipita. Hilda alikuwa na asili ya ukimya, lakini nilimfanya awe mtu wa kulalamika. Hata hivyo, malalamiko yake hayakuisumbua akili yangu ngaa kidogo. Nilimpuuza, na kuendeleza mahusiano yangu motomoto na Himana.
Siku zilipita, miezi ikasogea, nikaona nahitaji kuwa na huyu binti Himana, kwenye maisha yangu yote. Nilimueleza kuhusu suala la kumuoa, akakubali, lakini akawa kana kwamba ananipiga chenga kunipeleka kwao. Baada ya kulazimisha kwa muda mrefu, alinipeleka kwa familia aliyoitambulisha kama ya wazazi wake, familia inayojiweza kiasi. Alinitambulisha kwa binti mwingine mkubwa ambaye alisema ni dada yake wa pekee. Wakati huo tayari tuliishi pamoja, na pamenzi yalizidi kushamiri kati yetu. Hilda aliendelea kunitafuta, na mara hii ni yeye ndiye alisababisha tuwasiliane kwani bila kunipigia basi nisingethubutu kumtafuta. Tulipanga harusi ndogo na Himana, tukaamua tuifanyie huko huko Arusha, nikaenda kwao kutoa mahari, lakini nilishangaa kwamba hakukuwa na shamrashamra za mahari au za kuolewa kwake tofauti na familia nyingi za kitanzania.
Tulioana, nikafanya kuwaalika wazazi ambao mwanzo walipingana namimi sana juu ya suala hilo, lakini hawakuwa na namna zaidi ya kumkubali yule niliyemchagua. Taarifa zilimfikia Hilda kuwa nimeoa, na naumia sana ninapoandika hii habari kuwa mpenzi wangu aliamua kujiua kwa kunywa sumu. Moyo wake mdogo haukuweza kustahimili kusalitiwa na mwanaume aliyemuamini sana. Labda kwa miaka mitatu yote nilimuonesha mimi ni malaika, hivyo ikawa vigumu kwa akili yake kuamini kuwa malaika amekuwa shetani. Habari ya kifo chake ilinifanya nimwambie Himana ukweli kuhusu mimi na Hilda, lakini cha kunishangaza, hakujali bali alinipa pole na kunifariji sana.
Baada ya harusi, mapenzi yalizidi kushamiri, tukapata mtoto mmoja wa kike. Tumekaa kwenye ndoa miaka sita, lakini sikuwahi kujua ndugu zaidi wa Himana mpaka mwaka huo wa sita ambapo alikuja nyumbani kwetu mzee, aliyedai kuwa ni baba yake. Huyu ni tofauti kabisa na mzazi wake niliyemfahamu kabla. Mzee yule alikuja akilia na kumuomba binti yake arudi kwao japo akamuone mama yake mzazi aliye kwenye hali mbaya ya afya. Hata hivyo Himana hakukubali na aliishia kumfukuza kama mbwa. Miezi michache baadaye walikuja wanaume wawili, mmoja alijitambulisha kama kaka yake na mwingine kama mume wake. Niliogopa sana, nikaanza kuhisi kuna mengi yamejificha, japokuwa baada ya tukio la yule mzee, Himana alikataa katakata kuwa ni baba yake. Mara hii tena aliwakana hawa wanaume, akidai hawajui wala hajawahi kuwaona, jambo ambalo nililitilia mashaka sana.
Nilianza kufanya uchunguzi wa chini kwa chini, bila mke wangu kujua. Kuna mengi nilianza kugundua mabayo singependa kuyaeleza, lakini kikubwa niligundua kuwa ile familia aliyonipeleka Himana haikuwa yake bali ya rafiki yake. Niligundua pia kuwa aliolewa, kijijini alipoishi, akiwa na miaka 18 tena kwa hiari yake mwenyewe, kwani kabla ya kuolewa alijiingiza kwenye mahusiano kadhaa pale kijijini. Mwanaume aliyemuoa hakuwa wa kijijini, hivyo alimleta mjini, lakini mwaka mmoja tuu baada ya ndoa yake hakuwa anashikika tena. Alichukuliwa na mwanaume mwingine mtu mzima na kuishi naye, na mpaka tunaonana alikuwa kwenye mahusiano na huyo mtu mzima.
Nilijitahidi kutomuonesha kuwa nimejua ukweli huo. Ilinigharimu kufanya utafiti wa kina, kusingizia safari kadhaa, kuonana na rafiki zake na hata kwenda nyumbani kwao pasipo yeye kujua. Nakumbuka siku moja, baada ya uchunguzi wangu kukamilika, nilikusudia kuwa ningemwambia ukweli. Moyo wangu uliuma mno, nilimpenda sana huyu mwanamke na nilitamani kuwa yale yote niliyoyajua juu yake yawe ni uongo. Nilitumai kuwa huenda angekana na kunipa uhakika kuwa yote ni uongo, lakini haikuwa hivyo. Alinisikiliza nikiongea naye, na kasha kunijibu kwa kujiamini kuwa ni kweli yote ninayosema. Niliumia, kupita kiasi, nikatamani ajitetee lakini hakufanya hivyo. Nilitamani hata aniombe msamaha lakini pia hakufanya hivyo na badala yake aliendelea kuishi kana kwamba hakuna kilichotokea.
Nikiwa bado naugulia maumivu, na wakati huohuo najaribu kumsamehe ili tuendelee kuishi kwa amani, siku moja usiku aligonga hodi mwanaume mmoja pale nyumbani. Tulimkaribisha ndani, lakini mke wangu alionekana mwenye kustuka sana. Yule mwanaume alimsalimia Himana kama watu wanaofahamiana, kisha alianza kumlaumu na kumuhukumu mbele yangu. nilibaki nashangaa, sijui nini cha kufanya, na mke wangu akabaki kimya kabisa, asiyeweza kujitetea. Baada ya muda yule mzee alitoa pisto ndogo kiunoni na kwa hasira alimpiga mtoto wangu aliyekuwa amejilaza miguuni mwa mama yake, akampiga na Himana mwenyewe kichwani.
Nikiwa nimechanganyikiwa, nilipiga nilikaa chini na kuanza kulia. Yule mtu alinipiga mimi pia risasi maeneo ya shingoni ambapo nilipoteza fahamu na kuja kujikuta niko hospitali. Hapa ninapoongea nina mwaka mzima, siwezi kutembea, mwili umepooza kuanzia miguuni kwani inasemekana nilijeruhiwa mishipa inayohusika na uwezo wa kutembea, ya uti wa mgongo. Nimeshatibiwa sana bila mafanikio. Mbaya zaidi nilikuja kupata fahamu na kupewa taarifa kuwa mke wangu na binti yangu walifariki na kuzikwa nikiwa sijitambui. Yule muuaji alijisalimisha polisi na sasa anatumikia kifungo cha maisha, lakini haiondoi uchungu niliopitia na ambao ninao mpaka sasa.
Najilaumu, najuta, naumia lakini sina cha kufanya. Inavyoonekana jamaa alifiwa na mkewe, na aliamua kumuoa Himana ambaye alikuja kumtoroka baada ya kukutana namimi.
Himana, binti mwenye kila sifa ya kuitwa mrembo, ameujeruhi moyo wangu. Sasa namkumbuka Hilda, aliyenipenda kwa dhati, aliyejitoa kwa ajili yangu. najutia kumfupishia maisha yake, naona Mungu amenilipa mara mia. Nimepoteza binti yangu kipenzi na wa pekee, nimepoteza familia na mbaya zaidi nimepoteza thamani ya maisha yangu. nimelia kwa muda wa mwaka sasa lakini imefika mahala nimefika mwisho wa kulia, na hapo nikaamua niandike hadithi hii fupi kunihusu iwe fundisho kwa wengine. Si kuwa ni kosa kubwa kuachana na mpenzi wako na kuwa na mtu mwingine, lakini Je, unamuachaje? Alikuamini kiasi gani? Na sababu hasa ya kumuacha ni ipi? Ulimpa ahadi zipi? Machozi tunayowaliza wapendwa wetu ipo siku nasi tutayalia. Namuomba Mungu anisamehe, na ninaamini kuna siku nitainuka tena.
……………………….MWISHO………………………..
MREMBO HIMANA (Full story ) Jana usiku niliamka mida ya saa nane, na kama kawaida yangu, nikalia sana. Ni ajabu kwa mwanaume kulia, lakini kwangu imekuwa kitu cha kawaida sana. Nadhani ninapolia huwa najihisi nafuu kiasi, na kwa namna fulani napunguza uchungu ulio ndani yangu. Nimekuwa nikifanya hivyo kwa muda wa mwaka mzima sasa, lakini usiku wa jana ulikuwa tofauti kidogo. Baada ya kulia sana, niliamua kwamba huu ndio utakuwa mwisho. Mwaka 2007 tarehe kama ya jana nilikutana na binti mmoja nikiwa masomoni Arusha. Huyu binti ni mmang’ati kwa kabila, ana urefu wa wastani, rangi ya ngozi nyeupe inayofanana mwili mzima, yaani si kama rangi za mabinti wa siku hizi za kuchanganya na kutafutiza. Ni mzuri mno kwa sura, kama unavyojua wadada wengi wa mkoa huo. Ngozi yake ni laini na nyororo kama ya mtoto mdogo, na ni mwenye macho mazuri. Yaani kwa kifupi hana kasoro ya kuonekana kwa macho. Tulikutana kituo kimoja cha daladala wilayani Monduli, mimi nikiwa naelekea Arusha mjini. Nilimkuta amekaa, kama ana huzuni, japo hilo halikuficha uzuri wake. Nilimsogelea na kumuuliza kwa kuonesha kujali, “Mrembo, nini tatizo? Unaonekana una huzuni”. Alinitazama na kujibu kwa upole sana,”Hapana, niko sawa”. Niliamua nitatumia fursa hiyo kuongea naye, na kweli alinionesha ushirikiano mzuri tuu. Tulizungumza kwa kifupi, nikimuuliza maswali ya hapa na pale, kasha likaja gari tukapanda. Uelekeo wetu ulikuwa mmoja, na kwa nasibu tulikaa siti moja. Tuliendelea na mazungumzo na huyo binti, aliyejitambulisha kwa jina la Himana, na kiukweli niliifurahia safari yangu. Kufika mjini, mahala ambapo sote tulishuka, tayari tulishajenga urafiki kiasi cha kukubaliana kuonana tena na hata kupanga siku ya kuonana. Sidanganyi, wakati huo nilikuwa tayari kwenye mahusiano, na binti ambaye tulipendana sana. Huyo mpenzi wangu naweza sema hatukuwahi kukosana kwa miaka mitatu yote tuliyokuwa pamoja, ukiacha mikwaruzo kidogo sana ya mara chache. Nilimpenda sana mpenzi niliyekuwa naye, Hilda, na nilimuahidi tungeoana mara tuu baada ya kumaliza masomo yangu ya muda mfupi huko Arusha. Tayari nilishajitambulisha kwao, na kwa uwezo wa wastani niliokuwa nao, nilijitoa kwake kwa kiwango kikubwa kiasi cha kumuaminisha kwamba mimi ndiye mume wake. Sikuwahi kuvutiwa na msichana mwingine yeyote zaidi ya Hilda, mpaka nilipokutana na Himana. Tulianza mawasiliano ya kasi sana na Himana, kiasi cha kunifanya nianze kumpuuza Hilda. Nilijihisi kuvutiwa na Himana, na kila mara mawazo yaliponijia kuwa nina mpenzi anayeniamini na kunithamini, akili yangu haikunipa hiyo fursa kwa muda mrefu bali ilinielekeza kwa Himana ambaye wakati huo penzi kubwa lilianza kushamiri kati yetu. Binti huyu, aliyepata umri wa miaka 21 tu wakati huo, alinionesha mapenzi nisiyowahi kuona kabla. Hapa niwe muwazi zaidi, kwa miaka mitatu niliyokuwa kwenye mahusiano na Hilda, hatukuwahi kukutana kimwili, isipokuwa mwezi mmoja kabla ya safari yangu ya kwenda Arusha. Hilda alikuwa na misimamo binafsi ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa, na niliweza kumvumilia kwa miaka mitatu huku nikiwa muaminifu kwa asilimia 100. Baada ya kujitambulisha kwao rasmi, na kuanza hatua za kuoana, ndipo alikubali tukutane kimwili, na alifanya hivyo kunihakikishia kuwa hata ninapokwenda kusoma, nijue kwamba mimi ndiye mwanaume wake pekee, na alinipenda kwa dhati, hivyo nisimpe msichana mwingine moyo wangu. Kwa bahati mbaya sana, Himana alinisahaulisha hayo yote. Tuliingia kwenye mahusiano kwa kasi sana, alinifuata popote, aliniletea vyakula, alizungumza nami maneno ya mahaba na hakutaka kujua kama nina uhusiano au la. Alinipa raha kiasi cha kupuuza ahadi zote tulizowekeana na Hilda, na sikukumbuka tena gharama nilizoingia kwa ajili yake wala heshima niliyokuwa nayo kwa familia yake. Hilda alianza kulalamika kuwa nimepunguza mapenzi kwake, lakini nilimpuuza. Sikujali tena hisia zake, nilidharau hata bikira yake ambayo mimi ndiye niliitoa, na sikuona tena uthamani wake kama hapo awali. Mapenzi na Himana yalishamiri sana, nikamaliza shule yangu lakini sikutamani kurudi Dar es Salaam nilipoishi. Niliamua kufatilia uhamisho kazini kwangu, na kwa vigezo ambavyo nilitoa, haikuwa ngumu kupata. Nilijaribu kutoa vigezo vya msingi kuhusu uhutaji wa mtu wa taaluma yangu katika ofisi zetu za Arusha. Sikumjulisha Hilda juu ya uamuzi wangu wa kuhama, isipokuwa nilipopata uhamisho nilimwambia kuwa ofisi imeamua kunihamisha. Mara kadhaa nikiwa nasoma na hata baada ya kumaliza masomo alinitaka tuonane, kwa kuniomba niende Dar es Salaam walau mara moja, au hata yeye aje Arusha, lakini nilimpa sababu kadhaa na kumkatalia. Mawasiliano kati yetu yalizidi kuwa hafifu na muda nilioahidi tungeoana ulipita. Hilda alikuwa na asili ya ukimya, lakini nilimfanya awe mtu wa kulalamika. Hata hivyo, malalamiko yake hayakuisumbua akili yangu ngaa kidogo. Nilimpuuza, na kuendeleza mahusiano yangu motomoto na Himana. Siku zilipita, miezi ikasogea, nikaona nahitaji kuwa na huyu binti Himana, kwenye maisha yangu yote. Nilimueleza kuhusu suala la kumuoa, akakubali, lakini akawa kana kwamba ananipiga chenga kunipeleka kwao. Baada ya kulazimisha kwa muda mrefu, alinipeleka kwa familia aliyoitambulisha kama ya wazazi wake, familia inayojiweza kiasi. Alinitambulisha kwa binti mwingine mkubwa ambaye alisema ni dada yake wa pekee. Wakati huo tayari tuliishi pamoja, na pamenzi yalizidi kushamiri kati yetu. Hilda aliendelea kunitafuta, na mara hii ni yeye ndiye alisababisha tuwasiliane kwani bila kunipigia basi nisingethubutu kumtafuta. Tulipanga harusi ndogo na Himana, tukaamua tuifanyie huko huko Arusha, nikaenda kwao kutoa mahari, lakini nilishangaa kwamba hakukuwa na shamrashamra za mahari au za kuolewa kwake tofauti na familia nyingi za kitanzania. Tulioana, nikafanya kuwaalika wazazi ambao mwanzo walipingana namimi sana juu ya suala hilo, lakini hawakuwa na namna zaidi ya kumkubali yule niliyemchagua. Taarifa zilimfikia Hilda kuwa nimeoa, na naumia sana ninapoandika hii habari kuwa mpenzi wangu aliamua kujiua kwa kunywa sumu. Moyo wake mdogo haukuweza kustahimili kusalitiwa na mwanaume aliyemuamini sana. Labda kwa miaka mitatu yote nilimuonesha mimi ni malaika, hivyo ikawa vigumu kwa akili yake kuamini kuwa malaika amekuwa shetani. Habari ya kifo chake ilinifanya nimwambie Himana ukweli kuhusu mimi na Hilda, lakini cha kunishangaza, hakujali bali alinipa pole na kunifariji sana. Baada ya harusi, mapenzi yalizidi kushamiri, tukapata mtoto mmoja wa kike. Tumekaa kwenye ndoa miaka sita, lakini sikuwahi kujua ndugu zaidi wa Himana mpaka mwaka huo wa sita ambapo alikuja nyumbani kwetu mzee, aliyedai kuwa ni baba yake. Huyu ni tofauti kabisa na mzazi wake niliyemfahamu kabla. Mzee yule alikuja akilia na kumuomba binti yake arudi kwao japo akamuone mama yake mzazi aliye kwenye hali mbaya ya afya. Hata hivyo Himana hakukubali na aliishia kumfukuza kama mbwa. Miezi michache baadaye walikuja wanaume wawili, mmoja alijitambulisha kama kaka yake na mwingine kama mume wake. Niliogopa sana, nikaanza kuhisi kuna mengi yamejificha, japokuwa baada ya tukio la yule mzee, Himana alikataa katakata kuwa ni baba yake. Mara hii tena aliwakana hawa wanaume, akidai hawajui wala hajawahi kuwaona, jambo ambalo nililitilia mashaka sana. Nilianza kufanya uchunguzi wa chini kwa chini, bila mke wangu kujua. Kuna mengi nilianza kugundua mabayo singependa kuyaeleza, lakini kikubwa niligundua kuwa ile familia aliyonipeleka Himana haikuwa yake bali ya rafiki yake. Niligundua pia kuwa aliolewa, kijijini alipoishi, akiwa na miaka 18 tena kwa hiari yake mwenyewe, kwani kabla ya kuolewa alijiingiza kwenye mahusiano kadhaa pale kijijini. Mwanaume aliyemuoa hakuwa wa kijijini, hivyo alimleta mjini, lakini mwaka mmoja tuu baada ya ndoa yake hakuwa anashikika tena. Alichukuliwa na mwanaume mwingine mtu mzima na kuishi naye, na mpaka tunaonana alikuwa kwenye mahusiano na huyo mtu mzima. Nilijitahidi kutomuonesha kuwa nimejua ukweli huo. Ilinigharimu kufanya utafiti wa kina, kusingizia safari kadhaa, kuonana na rafiki zake na hata kwenda nyumbani kwao pasipo yeye kujua. Nakumbuka siku moja, baada ya uchunguzi wangu kukamilika, nilikusudia kuwa ningemwambia ukweli. Moyo wangu uliuma mno, nilimpenda sana huyu mwanamke na nilitamani kuwa yale yote niliyoyajua juu yake yawe ni uongo. Nilitumai kuwa huenda angekana na kunipa uhakika kuwa yote ni uongo, lakini haikuwa hivyo. Alinisikiliza nikiongea naye, na kasha kunijibu kwa kujiamini kuwa ni kweli yote ninayosema. Niliumia, kupita kiasi, nikatamani ajitetee lakini hakufanya hivyo. Nilitamani hata aniombe msamaha lakini pia hakufanya hivyo na badala yake aliendelea kuishi kana kwamba hakuna kilichotokea. Nikiwa bado naugulia maumivu, na wakati huohuo najaribu kumsamehe ili tuendelee kuishi kwa amani, siku moja usiku aligonga hodi mwanaume mmoja pale nyumbani. Tulimkaribisha ndani, lakini mke wangu alionekana mwenye kustuka sana. Yule mwanaume alimsalimia Himana kama watu wanaofahamiana, kisha alianza kumlaumu na kumuhukumu mbele yangu. nilibaki nashangaa, sijui nini cha kufanya, na mke wangu akabaki kimya kabisa, asiyeweza kujitetea. Baada ya muda yule mzee alitoa pisto ndogo kiunoni na kwa hasira alimpiga mtoto wangu aliyekuwa amejilaza miguuni mwa mama yake, akampiga na Himana mwenyewe kichwani. Nikiwa nimechanganyikiwa, nilipiga nilikaa chini na kuanza kulia. Yule mtu alinipiga mimi pia risasi maeneo ya shingoni ambapo nilipoteza fahamu na kuja kujikuta niko hospitali. Hapa ninapoongea nina mwaka mzima, siwezi kutembea, mwili umepooza kuanzia miguuni kwani inasemekana nilijeruhiwa mishipa inayohusika na uwezo wa kutembea, ya uti wa mgongo. Nimeshatibiwa sana bila mafanikio. Mbaya zaidi nilikuja kupata fahamu na kupewa taarifa kuwa mke wangu na binti yangu walifariki na kuzikwa nikiwa sijitambui. Yule muuaji alijisalimisha polisi na sasa anatumikia kifungo cha maisha, lakini haiondoi uchungu niliopitia na ambao ninao mpaka sasa. Najilaumu, najuta, naumia lakini sina cha kufanya. Inavyoonekana jamaa alifiwa na mkewe, na aliamua kumuoa Himana ambaye alikuja kumtoroka baada ya kukutana namimi. Himana, binti mwenye kila sifa ya kuitwa mrembo, ameujeruhi moyo wangu. Sasa namkumbuka Hilda, aliyenipenda kwa dhati, aliyejitoa kwa ajili yangu. najutia kumfupishia maisha yake, naona Mungu amenilipa mara mia. Nimepoteza binti yangu kipenzi na wa pekee, nimepoteza familia na mbaya zaidi nimepoteza thamani ya maisha yangu. nimelia kwa muda wa mwaka sasa lakini imefika mahala nimefika mwisho wa kulia, na hapo nikaamua niandike hadithi hii fupi kunihusu iwe fundisho kwa wengine. Si kuwa ni kosa kubwa kuachana na mpenzi wako na kuwa na mtu mwingine, lakini Je, unamuachaje? Alikuamini kiasi gani? Na sababu hasa ya kumuacha ni ipi? Ulimpa ahadi zipi? Machozi tunayowaliza wapendwa wetu ipo siku nasi tutayalia. Namuomba Mungu anisamehe, na ninaamini kuna siku nitainuka tena. ……………………….MWISHO………………………..
Artikel Terkait
Story - - - - - NI WEWE TU PENINA Sehemu ya pili (2) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp___0769673145 Ilipoishia........ Katika bar moja iliyopo maeneo ya sinza kikao kimoja kilikuwa kikiendelea, na huku kilichokuwa kikipangwa Katika kikao kile ni namna ya kulivunja na kuliharibu penzi la Penina na Frank. Mzee Joel ambaye ni baba yake Penina, pamoja na Angel ambaye ni mdogo wake Penina pamoja na vijana wengine watatu wa kiume na mmoja wa kike, ndio waliokuwa wahusika wakuu wa kikao kile. *********ENDELEA ******** "sitaki mwanangu aolewe na yule mlala hoi kwa namna yoyote Ile naomba muyakatishe mpenzi yao, nitawapa pesa yoyote mnayotaka." alisikika mzee Joel akiwaambia vijana wake. "hamna shinda mzee wetu kuanzia Sasa tupo Katika mipango ya kuliharibu penzi hilo usijali mzee wetu." kijana mmoja aliyeitwa zaza ndio alisikika akiwaambia mzee Joel maneno hayo. "nitafurahi Sana kama hili likifanikiwa siwezi kukubali mwanangu aolewe na yule mnuka jasho." mzee Joel bado alizidi kuongea kwa jazba. "baba hata mimi nakuunga mkono Dada hawezi kuolewa na yule mnuka shombo." aliongea Angel naye kumuunga mkono baba yake. "hamna shida mzee Joel tutafanya mnayotaka." akaongea Zaza. "bas Sawa ngoja niwape pesa ya maji ili muweze kuianza kazi Mara moja." akaongea mzee Joel na kutoa pesa kias cha shilingi laki mbili na kumkabidhi Zaza agawane na wenzake. "Asante Sana mzee wetu na kuanzia Sasa sisi tunaianza Kaz." akaongea Zaza huku akipokea pesa zile, na Kisha wakaagana na mzee Joel na kuondoka.* Katika ukumbi mmoja wa starehe mziki wa taratibu ulikuwa ukipigwa kwa utaratibu wa hali juu kabisa, huku watu wawili wanaopendana kupita maelezo wakiwa ndani ya ukumbi huo huku wakiburudika na mziki mwororo uliokuwa ukipigwa Katika ukumbi ule, watu hao ni Penina pamoja na Frank. "Frank nakupenda Sana mpenzi wangu sijui nifanye nini ili ujue ni kwa kiasi gani, nafahamu jinsi baba yangu anavyokuchukia Ila yeye hawezi kuwa chanzo cha mimi kutokukupenda wewe, hakika nakupenda Sana." aliongea Penina maneno hayo akimuambia Frank na kujilaza kifuani mwake. "nafahamu Penina ni kwa kiasi gani unanipenda na pia unatambua ni kwa kias gani mimi nakupenda, napenda nikuahidi tu kuwa NI WEWE TU PENINA hakuna mwingine zaidi yako." Frank naye alimwambia Penina maneno hayo ambayo yalimfanya Penina azidi kutoa tabasamu tamu usoni mwake na kuzidi kumvuruga Frank, ambaye alijiona ni mwanaume mwenye bahati Sana kuwa na msichana mrembo kama Penina. Kama Kuna zile sifa wanaume huzitafuta kwa wanawake bas Penina alikuwa nazo na zingine za ziada. "yaani mpenzi wangu kila nikikuangalia nakuwa na maswali mengi ya kijinga ya kukuuliza kwa jinsi tu ulivyo mzuri." aliongea Frank akimwambia Penina. "hahahaaaa maswali gani hayo mpenzi wangu hebu niulize moja." akaongea Penina na kumtaka Frank amuulize moja. "swali moja ambalo huwa najiuliza kila ninapokuona huwa najiuliza hivi wewe ulizaliwa na mwanadamu au Mungu ndio alikutengeneza mwenyewe alafu akakuleta duniani?" akauliza Frank huku akiwa anamtazama Penina. "hahahaaaa Frank mpenzi wangu mi nimezaliwa na mwanadamu kama wewe." akajibu Penina huku akicheka kwa maneno ya Frank. "najua wewe umezaliwa na mwanadamu kama mimi Ila wewe ni mrembo Sana Sana sanaaa." akaongea Frank huku akizidi kumsifia Penina. Penina naye alifurahi Sana na kuzidi kuwa na furaha zaidi kwa sifa alizokuwa akipewa na Frank. "Asante Sana mpenzi wangu kwa sifa zote ulizonipa ila Kuna kitu nataka nikuambie." akaongea Penina na kumtizama Frank. "kitu gani tena mpenzi wangu?" akahoji Frank huku akiwa ametumbua macho. "mbona umeshtuka hivyo Sasa?" Penina akamuuliza Frank baada ya kumuona ametumbua macho. "lazima nishtuke si unajua tena namna navyokupenda isije ikawa ni kitu kibaya." Frank akamjibu Penina. "usijali mpenzi sio kitu kibaya na nina Imani utafurahia." Penina akamwambia Frank kumtoa hofu. "ok niambie bas ni kitu gani?" akahoji Frank huku akionekana kuwa na haraka ya kutaka kujua. "nataka siku chache zijazo tufunge ndoa alafu tufanye harusi kubwa ili tuwakomeshe maadui zetu ambao hawataki kutuona tukiwa pamoja.." Penina ndio alimwambia Frank ambaye alikuwa kimya kumsikiliza. "kweli mpenzi wangu hata mimi nimeshaliwaza hilo tatizo lipo kwangu, bila Shaka unatambua hali iliyopo Katika familia yetu, hatuna uwezo kipesa hivyo nahitaji muda zaidi kulitimiza hilo Penina." Frank akamwambia Penina huku akiwa amepoteza tabasamu usoni mwake. "Frank mpenzi wangu ondoa Shaka kuhusu hilo mimi nina uwezo wa kulisimamia hilo mwanzo mpaka mwisho, na kuthibitisha hilo hapa nimekuja na funguo nne, moja ni ya duka kubwa la kuuza bidhaa za jumla na moja, mwingine ni wa gari kubwa la kubebea mizigo, mwingine ni wa nyumba mpya niliyowanunulia wazazi wako kama zawadi ya kunizalia mwanaume anayenipenda kwa dhati na mwingine ni wa gari ndogo nililokununulia wewe mpenzi wangu. " alimaliza Penina kumwambia Frank maneno hayo na kumuacha akiwa mdomo wazi. " waooow ni ngumu Sana kuamini ila acha niamini tu, Asante Sana mpenzi wangu." alisema Frank huku akimkumbatia Penina na kumshushia mabusu mfululizo. "usijali mpenzi wangu ila nataka utambue nayafanya yote haya kwasababu nakupenda Sana, lakini pia ni moja wapo ya maandalizi ya harusi yetu." Penina akamwambia Frank huku akiwa amejilaza kifuani mwake. "nashukuru Sana Penina mpenzi wangu kusikia hivyo na mimi nikuahidi kuwa na wewe mpaka mwisho wa uhai wangu hakika ni wewe tu Penina." Frank akamwambia Penina huku akiwa amemkumbatia kwa nguvu. Wakati huo tayari Muda ulikuwa umeenda Sana na tayari ilikuwa ni saa moja usiku, hivyo Frank na Penina waliondoka kurudi nyumbani huku Penina akimuahidi Frank kumkambidhi vitu vyote alivyomwambia siku inayofuata. Penina alimfikisha Frank nyumbani kwake, Frank akashuka kwenye gari na kumuuga mpenzi wake Penina. Kisha Penina akageuza gari na kuondoka. Baada ya Penina kuondoka tu, Frank kabla hajapiga hata hatua moja kuondoka pale, ghafla alishtukia amezungukwa na vijana watatu wa kiume waliokuwa wamevalia miwani nyeusi kila mmoja. Na hata Frank alipowaangalia hakuweza kuwafahamu. ....... Itaendelea. ... Read More
Story......... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya Nne (4) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp... 0769673145 ilipoishia....... Kwa upande wa kina zaza usiku ule ule walianza kupanga mikakati ya kumteka Frank na kwenda kumtupa mbali kabisa na jiji la dar es salam. Lakini hii ilikuwa kazi ngumu Sana ambayo walihitaji pesa za kutosha na pia wachore ramani ya sehemu watakayoenda kumtupa Frank. .......... Endelea........... Zaza pamoja na wenzake waliumiza kichwa, na hatimaye mmoja wao akapata wazo ambalo moja kwa moja aliliweka hadharani kwa wenzake ili waweze kulifikiria kama ni wazo zuri. " mimi nina watu wangu nawafahamu, ni watu wazuri sana Katika kazi hizi hata kuua kwao ni kitu kidogo tu, hivyo naona tuwape hili dili warusaidie. " aliongea kijana huyo akiwasilisha Wazo Lake. " Wazo zuri Sana mi naungana na wewe moja kwa moja Sasa inabidi utueleze tunawapataje hao watu. " akaongea zaza kumuuga mkono kijana yule. " ninafahamu makao yao kama vip tuongozane mpaka kwao." akaongea kijana yule, na moja kwa moja zaza pamoja na wenzake wakanyanyuka na kuingia kwenye gari Lao na kuanza safari ya kuelekea kwa watu hao. Hapakuwa mbali Sana na sehemu waliyokuwepo, hivyo baada ya dakika chache waliwasili sehemu hiyo. Wakashuka kwenye gari na kubisha hodi kwenye nyumba kubwa iliyokuwa mbele yao. Hakuna mtu aliyewaitikia ndani ya dakika tano wakiwa bado wapo pale mlangoni, lakini ghafla walishtukia wamezungukwa kila sehemu na watu wasiopungua kumi huku wakiwa na bunduki kila mmoja. "mko chini ya ulinzi mikono juu na mjitambulishe nyie ni nani." ikasikika sauti ikiwaamuru wakina zaza. "zaza pamoja na wenzake walitiii na kuweka mikono juu, Kisha zaza akajitambulisha kwa niaba ya wenzake. Zaza pamoja na wenzake walieleweka vizuri Kisha wale watu wakashusha silaha zao chini na kuwakaribisha wakina zaza Katika jumba Lao. " Elezeni shida yenu hatuna muda wa kuangaliana hapa." ikasikika sauti ikiwaambia wakina zaza. Zaza bila kusita alianza kuelezea mipango ya kumteka Frank na kuwataka wao wakawasaidie tu kumtupa mbali na jiji la dar es salam. "hiyo ni kazi ndogo Sana lakini inahitaji pesa kiasi cha shilingi million kumi." ikasikika tena Ile sauti ikiwaambia wakina zaza. "pesa si tatizo pesa Zipo za kutosha." akajibu zaza. "bas vizuri Sana tutawaelekeza namna ya kutupatia hizo pesa alafu mtatuletea huyo kijana mtuachie tumfanyie kazi." ikasema sauti ile. "hamna shida." akajibu zaza. Na muda huo wakapewa maelekezo namna ya kuwaingizia pesa zao, na bila kupoteza muda. Zaza pamoja na wenzake waliondoka usiku ule ule na kuwasiliana mzee Joel na kuwajulisha kias cha pesa wanachohitaji kulitimiza zoezi la kumteka Frank. Mzee Joel wala hakujali kama pesa ile ni nyingi kias gani, yeye alichotaka ni kuwatenganisha Frank na mtoto wake Penina . Usiku ule ule mzee Joel aliweza kuwakabidhi wakina zaza pesa zile na kuwataka wakina zaza wampoteze kabisa Frank lakini wasijaribu kumuua. Zaza pamoja na wenzake nao walizifikisha pesa zile kwa kikosi kile ambacho waliwapa kazi ile ya kumpoteza Frank. Baada ya kuwakabidhi pesa zile, walikubaliana kuwa siku inayofuata wataifanya kazi hiyo kama ipasavyo.* Asubuhi na mapema siku iliyofuata Frank akiwa bado yupo kitandani alishtushwa na mlio wa simu yake ikiita. Frank aliichukua simu yake na alipoangalia mpigaji akakuta ni kipenzi chake Penina. Bila kusita Frank akaipokea simu ile. "my love umeamkaje?" ilisikika sauti nyororo ya Penina ikimuuliza Frank. "nimeamka salama mpenzi wangu sijui wewe?" akajibu Frank na kumuuliza Penina pia. "mimi pia nimeamka salama kabisa mpenzi, na nimekupigia simu asubuhi na mapema kwasababu nataka leo tukanywe Chai wawili." akajibu Penina na kumuambia Frank. "ooh usijali my dear nipo kwa ajili yako kwa lolote lile." akajibu Frank. "ok nakupitia sasa hivi." Penina akamwambia Frank na kukataa simu. Frank muda huo huo alitoka kitandani na kuanza kujiandaa haraka haraka. * Lakini wakati huo huo zaza akiwa na kikos chake walikuwa tayari wameshawasili nyumbani kwa kina Frank kwa ajili ya kutekeleza kazi waliyoagizwa. Frank akiwa tayari ameshajiandaa aliwaaga wazazi wake na kutoka nje ya kwa ajili ya kumsubiri mpenzi wake Penina. Baada ya Frank kutoka nje Bila kutarajia alijikuta anapigwa chuma ya kichwa na kudondoka chini na kuzimia. Na waliofanya kitendo kile hawakuwa wengine bali ni zaza pamoja na wenzake. Haraka haraka Frank alibebwa na kuwekwa kwenye gari yao Kisha gari likaondolewa sehemu ile kwa kasi ya ajabu. Na wakati huo huo Penina ndio alikuwa anawasili na akapishana na gari la kina zaza likiwa Katika mwendo mkali, lakini yeye Penina hakufahamu chochote kinachoendelea. Penina alipaki gari mbele ya nyumba ya kina Frank Kisha akashuka kwa mwendo wa madaha huku tabasumu tamu likiupamba uso wake na kuanza kuelekea ndani kwa kina Frank. "hodi hodi jamani mpaka ndani." ilisikika sauti ya Penina ikibisha hodi lakini muda huo akiwa tayari ameshaingia ndani. "baba na mama shikamooni." akasalimia Penina. "marahaba karibu uketi ." wakaitikia kwa pamoja wazazi wake Frank. "hata sikai jamani nimekuja kumchukua mtoto wenu." akajibu Penina. "yupo nje mbona anakusubiri hujamuona?" akauliza mama yake Frank kwa mshangao huku akitoka nje. "yupo nje mbona sijamuona?" Penina naye akauliza huku akiongozana na mama yake Frank mpaka nje. "mhhh yuko wapi Sasa hebu ngoja nimpigie simu." akasema Penina huku akitoa simu yake na kumpigia Frank. Simu ya Frank iliita bila kupokelewa na alipopiga Mara ya pili akakutana na sauti hii, "simu unayopiga haipatikana kwa sasa tafadhali jaribu tena baadae." Taratibu Penina alianza kunyongonyea na kupoteza tabasumu Lake zuri usoni mwake. "simu haipatikani mama hebu sikiliza." Penina akamwambia mama yake Frank huku akimuwekea simu sikion. "hee mbona makubwa jamani kaenda wapi Sasa huyu Mara hii tu katoka ndani? ." akauliza mama yake Frank huku akiwa ameshika kiuno. Penina naye alizidi kupiga simu bila mafanikio yoyote ya kumpata Frank. Ilibidi mama yake Frank amwite baba yake Frank pamoja na Angel mdogo wake Frank ili wamtafute Frank kwa pamoja. * Gari ya kina zaza ikiwaa Katika mwendo mkali, zaza pamoja na wenzake walimfunga Frank miguu pamoja na mikono Kisha wakachukua kitambaa cheusi na kumfunga Frank usoni ili hata atakapozinduka asiweze kufanya chochote na pia asiweze kugundua sehemu anayopelekwa. Na Kisha simu yake ilipasuliwa kule ndani ya gari pale tu waliposikia ikipigwa na Penina. Moja kwa moja gari ile iliyombeba Frank iliwasili Katika jumba la kikosi kile ambacho wakina zaza walikubaliana nao kwenda kumtupa Frank mbali kabisa na jiji la dar es salam na kamwe asiweze kurudi tena. Baada ya kufikishwa hapo Frank alitolewa kwenye gari la kina zaza na kuwekwa kwenye gari lingine la kikosi kile kingine huku ndani ya gari lile kukiwa na vijana wengine wanne. Na wakati huo huo taratibu Frank alianza kurudiwa na fahamu Zake. Milango ya gari Ile aliyowekwa Frank ilifungwa, na Kisha gari likaanza kuondoka kwenda kumtupa Frank sehemu ambayo kamwe hatoweza kuonana tena na Penina. ........ Itaendelea ... Read More
Story........ NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na tano (15) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp..... 0769673145 Ilipoishia...... Nolan alishtuka vibaya mno na kuona hapa shughuli ni nzito tena nzito Sana. Lakini mzee Joel ndio alikuwa na furaha Sana kwa kushuhudia kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na buffalo. Nolan alinyanyuka na kujitikisa na kujiweka Sawa kwa ajili ya kuendelea na mpambano. ***********Endelea *********** Baada ya Nolan kusimama tu buffalo hakumpa hata nafasi ya kumeza mate alimfuata kwa kasi na kumrushia mateke manne mfululizo na yote yakampata Nolan na kumuweka chini kwa Mara ya pili. Shughuli ilikuwa nzito Sana kwa Nolan kwani hajawahi kukutana na mtu mwenye spidi ya kupigana kama buffalo. Kwa Mara nyingine Nolan alinyanyuka tena huku akiwa tayari ameshawekwa alama usoni. Buffalo kama kawaida yake hakutaka kumpa nafasi ya kupumua, akamfuata kwa kasi na kurusha ngumi nyingine nzito lakini hii Nolan akaiona na kuikwepa ikaenda kugonga dirisha na kuvunja lile lote. Nolan naye this time round akasema hata mimi sicheki na wewe, Nolan aliruka na kumtandika buffalo teke la mgongo na kumtupa nje kwa kupitia pale dirishani. Nolan hakutaka kupoteza Muda akaruka na kumfuata buffalo huko huko nje. Dick pamoja na vijana wake wakiwa pamoja na mzee Joel nao wakatoka nje kushuhudia vita ile kali. Nolan baada ya kufika nje akakuta tayari buffalo ameshanyanyuka. Nolan akarusha ngumi nzito lakini buffalo akaikwepa na kurusha teke ambalo Nolan pia alilikwepa. Ngumi nzito ikarushwa na Nolan kwa Mara nyingine na kumkuta buffalo ya kichwa, lakini pia Nolan naye akapatwa teke Zito la tumbo kutoka kwa buffalo. Vita ile ilikuwa kali Sana kati ya buffalo na Nolan. Lakini mwisho wa siku ilikuwa ni lazima mshindi apatikane. Nolan alijikuta akiishiwa nguvu baada ya kupigana muda mrefu na buffalo na kujikuta akishindiliwa ngumi nzito mfululizo kwenye tumbo zisizopungua kumi Kisha akatandikwa moja nzito ya uso na kutupwa mbali na kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa. Lakini wakina Dick pamoja na vijana wake waliona huyu jamaa kwa Jina la buffalo hafanyi poa, wakaamua kumsaidia Nolan. Kwa pamoja walianza tena kumshambulia buffalo. Lakini kwa bahati mbaya hawakuwa na uwezo wa kumpiga buffalo wakajikuta wakitandikwa tena kama watoto na buffalo. Mzee Joel alifurahi Sana na kuona Sasa hakuna panya yoyote wa kunisumbua. Lakini kidogo hivi akanyanyuka Nolan akiwa ametokwa na wazimu. "suti ya harusi nimeshaandaa pamoja na taratibu zingine zote inawezekanaje wewe kimtu mmoja uje na kuharibu mipango yangu inawezekanaje??" akajisemea Nolan akiwa tayari amekwisha nyanyuka. Buffalo alimwaangalia Nolan na kucheka kwa dharau, lakini Nolan awamu hii hataki kucheka na mtu anachotaka Sasa ni kuua mtu bila huruma. Nolan akatoka mbio na kuanza kumfuata buffalo kwa kasi nyingine ambayo haielezeki Kisha akaruka na kukunja miguu na kumgonga buffalo kwa magoti na kumtupa chini. Nolan hakutaka kumpiga buffalo akiwa chini akamsubiri anyanyuka. Buffalo aliponyanyuka Nolan akaruka tiktak na kumpata buffalo mateke ya uso na kumuweka buffalo chini kwa Mara nyingine. Nolan akamsubiri tena buffalo anyanyuke kwa Mara nyingine, na buffalo aliponyanyuka Nolan akateleza kwa magoti mpaka kwenye miguu ya buffalo na kuanza kumshindilia buffalo ngumi nzito nzito za tumbo zisizopungua ishirini, Kisha akanyanyuka haraka na kabla buffalo hajaenda chini Nolan akaamua kummaliza kabisa. Nolan aliruka na kutua shingoni mwa buffalo na kumshindilia ngumi zingine za kichwa na kumpasua kichwa hadharani huku mzee Joel pamoja na wakina Dick wakiwa wanashuhudia. Habari ya buffalo ikaishia pale pale. Mzee Joel aliamua kutoroka baada ya kuona mtu aliyekuwa akimtegemea ameshauwawa hivyo akajua kwa vyo vyote vile yeye pia atakuwa Katika wakati mgumu hivyo akaona njia rahisi ni kutoroka tu. Lakini kwenda kutoroka mzee Joel alidakwa na wakina Dick na kuanza kupewa kichapo cha maana. Mzee Joel alitandikwa akatandikwa mpaka Sasa Nolan akamwonea tena huruma baba yake, akawaamuru wakina Dick wamuache. "tumemuacha muheshimiwa Ila tunachotaka atupe pesa zetu au atupe Penina tuondoke nae." akaongea Dick kumwambia Nolan. "mnachoweza kupata ni pesa zenu lakini sio Penina, kwasababu siku chache zijazo Penina anafunga Harusi na kijana mmoja wanaependana kwa dhati." akaongea Nolan maneno hayo ambayo yalikuwa machungu masikioni mwa Dick. "ok nipeni pesa zangu niondoke maana tumepoteza Muda wetu bila faida yoyote." akaongea Dick kinyonge. Lakini hata hivyo mzee akadai hana pesa yoyote, pesa zote amekwishazitumia na zingine akadai walimuibia na hajui nani alimwibia. Nolan alicheka Sana kimoyo moyo kwasababu alijua yeye ndio alikuwa akimwibia baba yake pesa zile. Nolan akaamua kumtetea baba yake, akawaambia wakina Dick hakuna pesa yoyote watapata kwasababu walifanya ujinga kutoa pesa hizo wakati wakijua hawana uhakika wa kumpata Penina. Nolan aliwataka wakina Dick watoweke sehemu ile haraka iwezekanavyo kabla hajawaangamiza na wao. Dick pamoja na vijana wake walijikuta wakiondoka kinyonge huku wakiamini kabisa walifanya makosa makubwa Sana na hivyo wakaamua kuondoka na kurudi nchini mwao bila kinyongo chochote. Huku mzee Joel alipiga magoti na kutubu makosa yake kwa mtoto wake Nolan na kumuomba amsamehe. Yenyewe hata hivyo damu ni nzito kuliko maji, Nolan aliamua kumsamehe baba yake lakini kwa jinsi baba yake alivyompa mateso Nolan akaamua lazima amtandike ngumi moja ya maana kama njia ya kumsamehe. Nolan alimsogelea baba yake na kumuwekelea ngumi moja nzito ya uso na kumuweka baba yake chini, Kisha akaenda akamnyanyua na kumkumbatia na kumsamehe. Baada ya siku kadhaa ya Nolan kuweka mambo Sawa hatimaye Penina na Frank walirejea Tanzania na Kisha harusi yao ikafanyika bila tatizo Lolote huku ikihudhuriwa na watu wengi kupita maelezo. Mzee Joel pia alikuwepo kwenye harusi ile pamoja na mkewe huku wakifurahia harusi ya mtoto wao licha ya kwamba moyo ulikuwa ukimsuta mzee Joel. Kadhalika pia baba yake Frank pamoja na mama yake Frank pia walikuwepo kwenye harusi ile huku wakiwa wameketi kwenye Meza ya heshima kabisa. Nolan pia alikuwepo kwenye harusi ile na yeye ndio alikuwa msimamizi wa kila kitu kilichokuwa kikiendelea Katika harusi ile. Harusi ilikuwa nzuri na yenye kuvutia na kila mtu alifurahishwa nayo. Hatimaye harusi ilimalizika salama na maisha yakaanza rasmi Sasa kati ya Frank na Penina wakawa Sasa ni baba na mama. Lakini pia Frank na Penina waligeuka kuwa matajiri wakubwa kutokana na zawadi mbali mbali walizokabidhiwa Katika harusi yao. Hivyo pia waliweza kuwafanya Wazazi wao waishi maisha mazuri na kusahau ya nyuma yaliyopita. Lakini heshima kubwa ilienda kwa Nolan kwasababu bila yeye wasingefika hapo walipo. Na hata walipofanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume wakaamua kumuita Nolan kumpa heshima kaka yake Penina na shemeji yake Frank. Frank na Penina walifanikiwa kupata mtoto wa pili naye pia alikuwa ni wa kiume wakaamua eti kumuita VAN B na maisha yakaendelea. **************MWISHO ************** mkumbuke nilisema hii story ni zawadi ya xmas na mwaka mpya haikuwa Katika mipango yangu. Hivyo nawashukuru wote mliokuwa pamoja Nami kwa kulike kucoment pamoja na kushare. Mwisho niwaambie tu kuna story nyingine iko jikoni Mungu akijaalia itaanza kuruka mwezi wa pili. Who killed my father "nani alimuua baba yangu" ndio Jina la story mpya inayokuja. Ukiniita VAN BOY utakuwa hujakosea hata kidogo. Nawapenda Sana. ... Read More
MUUZA MAZIW EP 07 “aaaaahh!! Jamani wifi wao!!” Aliongea kwa furaha baada ya kumuona mgeni aliyekuwa akigonga ni penina. “asante wifi , shikamoo!” Penina aliongea na kisha kumkumbatia wifi yake kwa furaha. “ marhaba wifi ,vipi masomo?” Aliongea huku akiipokea mizigo aliyo ibeba “naendelea vizuri tu wifi” “haya mungu akusaidie” Aliongea lisa na kuelakea sebuleni , aliiiweka mizigo pembeni ya kochi na kasha kuelekea sehemuk ilipo friji. Penina, penina akaamua kuichukua mizigo ili aipeleke chumbani. “hapana wifi, hapana , hiyo iache hapo hapo nitaiingiza mwenyewe,, wewe kwanza kunywa juisi upumzike.“ Aliongea lisa huku akiwa ameshikilia jagi lenye juisi pamoja na glasi, alifanya hivyo kwa sababu chumba anachotakiwa kulala penina ndicho chumba ambacho amemficha muuza maziwa. “usipate tabu wifi wangu kunywa juisi upumzike, nipo kwa ajili yako “ Aliongea lisa huku akiibeba mizigo na kuelekea chumbani na kumuacha penina akinywa juisi taratibu. Alipoingia chumbani alimshutua muuza maziwa na kumweleza hali halisi. “kwahiyo nitatoka saa ngapi humu?” “ itabidi uvumilie mpaka usiku wifi akilala , mlango wa nje nitauacha wazi leo” Aliongea lisa “Sawa lakini vipi kuhusu chakula manaake niana njaa” “ usijali nitakuletea utakula humu humu , jitahidi usitoke nitajaribu kufanya mpango hata kamakabla ya usiku ikiwezekana” “poa” Muuza maziwa aliitikia “alafu nitaa……” Lisa alikatiza kauli yakebaada ya kusikia mlio wa kitasa kikifunguliwa. Haraka haraka muuuza maziwa aliingia kabatini na kisha lisa aliufunga mlango wa kabati hiyo kabla hata hajauachia mlango huo alisikia sauti nyuma yake. “wifi mbona unagombana na hilo kabati!?” Swali hilotoka kwa penina lilimfanya lisa ashikwe na kigugumizi cha ghafla huku akitoa maelezo ya kujikanyagakanyaga. “ah, mh, a-, u-n-a-j-u-a hi-li ka-ba-ti ni bo-vu” “limeharibika , ooh, mungu wangu!” Penina aliongea huku akilisogelea kabati hiloili kuiangalia sehemu ilipoaribika. “ah, hapana wifi usiiguse hapa nimeitegesha , iache hivyo hivyo mpaka atakapokuja fundi kulirekebisha” Aliongea Lisa haraka haraka. “okey”[sawa] Aliongea Penina huku akitikisa kichwa kuonyesha kwamba ameelewa. “nataka kuoga wifi” “na kweli manaake umechoka kweli kweli wifi yangu” Aliitikia Lisa haraka haraka kwani alijua huo ndio upenyo wa kumtoa muuza maziwa. Na kweli penina alipoingia bafuni lisa aliufungua mlango wa kabati haraka na kumtoa muuza maziwa , akala chakula haraka na kuanza safari ya kutoka nje ya nyumba hiyo , walipofika kwenye mlango wa kutokea muuza maziwa alimbusu lisa kwa mara ya mwisho , alipomaliza kufanya hivyo alitoka ndani ya chumba hicho na kutokeza koridoni ili atoke nje kabisa ya nyumba hiyo lakini kabla ya kufanya hivyo alisikia muungurumo wa gari, halikuwa gari lingine bali gari la Jerry mume wa Lisa. Hofu iliwaingia kwa ghafla na haraka haraaka walirudi tena chumbani kwa penina , ambapo kama kawaida alimfungia muuza maziwa kabatini, hawakuwa na njia nyingine tena bali hile waliyoipanga awali, muuza maziwa asubiri mpaka usiku wa manane Penina atakapo lala ndipo atoke kwani Lisa atauacha mlango wa kutokea wazi. Lisa alipomaliza kumfungia muuza maziwa katika kabati alitoka nje ya chumba hicho,akiwa koridoni aligongana ana kwa ana macho na mumewe. Wote wawili waliinamisha vichwa vyao chini. Kwani kila mmoja aliona aibu kwa kumsaliti mwenzake. Lisa kwa muuza maziwa na Jerry kwa sekritari wake. “Ah, mmh, wifi amekuja , kakaribu!” Aliongea Lisa kwa kujiumauma huku akiwa na wasi wasi. “ asante amekuja saa ngapi?” “sio muda mrefu” “aah yuko wapi sasa nimsalimie?” “yuko bafuni anaoga” “Okey” [sawa] Aliitikia na kisha kuelekea chumbani kwake. Lisa nae alimfuata mumewe nyuma hukubado akiwa na hofu juu ya kugundulika kwa uwepo wa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo. “Pole na kazi dear” Aliongea Lisa huku akijibaraguza kwa kumvua tai mume wake, macho yake bado yalikuwa na aibu sababu bado alikuwa na wasi wasi kwamba labda mumewe amegundua chochote. “ah, asante mpenzi” Aliitikia Jerry huku akitabasamu, lakina nae pia tabasamu lake liliishia mdomoni tu moyoni nafsi ilimsuta . Maovu aliyoyafanya na sikritari wake ofisini kwake yalikuwa bado yakionekana katika kichwa chake. Akavua nguo na kuingia bafuni kuoga lisa nae alimfuata na kujumuika nae kuoga . Alifanya hivyo ili Jerry hasihisi chochote. Walioga huku kila mmoja akiwa hana habari na mwenzake. Kwani wote wawili walikuwa wamechoka, walipomaliza kuoga wakavaa na kasha kwenda sebuleni. Huko wakamkuta Penina akianga lia tv. “mdogo wangu huyo!” Jerry aliongea kwa furaha huku wakicheka. “kaka!” Penina aliitikia na kisha kumkimbilia kaka yake. “waoo!!!” Waliongea kwa pamoja na kisha kukumbatiana kwa furaha. “habari za masomo!?” ITAENDELEA.. ... Read More
*Love bite* Sehemu Ya Kwanza (1) Ni siku ya jumapili iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa watu kutoka sehemu mbali mbali walionekana kwenye kumbi za starehe. Wengi ambao walikua wanapenda taarab basi walijazana travertine hotel kuwaangalia jahazi. Kwa wengine wanaopenda bongo flavour basi walikutana bills,maisha,masai..Dar live na kumbi zingine zilikuwa na wasanii pendwa waliokuwa wanaburudisha week end hiyo. JOTHAN alikua anapendelea sana mixing za ma dj mbali mbali. Hivyo jumapili hiyo aliamua kwenda coco beach usiku huo. Upepo mwanana uliokuwa ukipuliza huko coco beach na ukichanganya na big screen iliyokuwa inaenda sambamba na mixing za maana alizokuwa anazipiga dj huyo aliyezikonga roho za watu wengi waliokuwa pale, iilikuwa burudani tosha kwa waliohudhuria usiku ule. Jotham alipaki gari yake pembeni, alichagua kiti kilichukokuwa karibu na meza ya mwisho na kuagiza kinywaji alichokipendelea na kuendelea kufurahia mziki uliokuwa unaonyeshwa kwenye screen hiyo. Mara kwa mara madada poa walikuwa wanajipitisha pale alipo, lakini aliwachora tu na hakuwa na mpango nao. Baada ya dakika kadhaa, walitokea madada watatu waliokuwa wameingia pale coco beach na kuanza kutafuta mahali pa kukaa. Waliangaza meza nyingi zilikua na nafasi ya mtu mmoja au wawili tu na wao walikuwa na lengo la kukaa wote watatu kwenye meza moja. Baada ya kuangaza kwa muda, waliiona meza aliyokaa Jothan ikiwa na nafasi tatu za kukaa. Waliisogelea ile meza na walipokaribia tu kuifikia ile meza. Walishuhudia jamaa mmoja akiwa ameenda kukaa pale. “wewe kaka sogea sehemu yetu.” Aliongea mmoja kati ya wale wadada watatu baada tu ya kuifikia ile meza. “mbona hakuna alama yoyote kuwa mlikaa hapa. Hakuna vinywaji wala kitu chochote.” Aliongea yule jamaa huku akionyesha wazi kuvutiwa na ile sehemu iliyokuwa chemba lakini ikiwa inaonyesha vizuri ile tv. “ni vyema uwapishe kwa sababu waongeacho sio uongo.” Aliongea Jotham kumwambia yule jamaa. Hakuwa anapenda makelele ambayo alijua yatatokea baada ya mvutano huo wa kugombania ile sehemu. Yule jamaa akaamua kunyanyuka na kuwapisha wale warembo na yeye kwenda kukaa meza nyingine. “ahsante sana kaka, maana yule jamaa alitaka atubanie wakati sisi tumehangaika kutafuta meza tutakayokaa wote watatu”. Aliongea yule dada aliyeonekana kama kiongozi wao. Mavazi waliyovaa yalitosha kumshawishi mvulana yeyote rijali na kufanya iwe lazima macho ya matamanio kumtoka. Uzuri wa mabinti hao likuwa unashinda lakini huyo aliyekuwa kiongozi wao aliwazidi wenzake kwa kila kitu. Macho ya Jotham yaliona kila kitu kutoka kwa binti huyo mbichi. Chuchu zilitokeza kwa kujichora kwenye gauni ile nyepesi ambayo haikuwa na nguo nyingine ndani. “sikiliza oda zao, ziingize kwenye bili yangu” aliongea Jotham baada ya kumuita muhudumu aliyekuwa anamuhudumia toka afike pale. “ahsante.” Waliitikia wale madada baada ya kupewa ofa hiyo. Waliagiza vyakula na vinyaji walivyopendelea. Walipiga story za kawaida huku wakigongeana glass za vinywaji na kucheka. Jotham alikuwa kimya wakati wote huku akiwa bize kuangalia na kusikiliza mixing ambazo ndizo zilizomleta pale. Baada ya masaa kadhaa, alimuita muhudumu na kulipia bili yake. “ahsante kwa ofa yako.” Aliongea yule kiongozi wao baada ya Jotham kuwaaga. Jotham aliingia kwenye gari yake aina ya opah na kuondoka eneo hilo. Njiani alimkumbuka yule dada lakini aliishia kucheka tu kwakua hakuwa na hisia zozote za mapenzi juu yake. Zaidi alimtamani kuwa nae japo kwa usiku mmoja kwa jinsi alivyotoka. Hakika alikuwa na kila aina ya uchochezi wa kufanya ngono. Alifika kwake usiku mnene na kwenda kulala fofofo kutokana na usingizi uliojaa wakati huo. Asubuhi aliamka na uchovu tele na kwenda kuoga ili kujaribu kuupunguza uchovu aliokuwa nao. Alipomaliza kuoga. Alijiandaa tayari kwa kwenda kazini. Alisumbuka sana kuwasha gari lake lakini halikuwaka. Alipoangalia mafuta, aligundua kuwa wese lilikuwa limekata. Kwa kuhofia kuchelewa zaidi kazini, aliamua kwenda kituoni na kupanda daladala. Alifika kazini huku macho yake yakiwa mekundu yaliyoashiria kuwa bado alikuwa na usingizi. “mshikaji bora ukapate supu, maana hiyo harufu ya pombe uliyamka nayo ni noma. Utaongea vipi na bosi?” alishauri mmoja wa wafanyakazi wenzake aliyekuwa karibu naye. “poa, ngoja nielekee canteen basi.” Aliongea Jothan na kwenda canteen kupata supu ya mbuzi na chapati. Baada ya kunywa chai, alirudi na kuendelea na kazi. Saa nane ndio muda waliokuwa wanatoka kazini. Alienda kupata chakula cha mchana canteen na kuondoka zake kuelekea kituo cha daladala ambacho hakikuwa mbali na ofisini kwao. Alisubiri daladala kwa muda na kupanda gari iliyokuwa inaelekea mwenge kwa malengo ya kushuka kinondoni anapoishi. Usingizi ulichukua nafasi yake baada ya kupanda tu lile gari lililokuwa likisubiri abiria kwa dakika kadhaa pale kituoni Baada ya muda mrefu kidogo kupita, aliamka na kuangalia gari lilikuwa limefika wapi. Wakati akiwa anaanga angaza, macho yake yaligongana na yule mrembo aliyekuwa naye kwenye meza moja siku ya jana yake. Wote walikumbukana na kila mmoja akamuachia mwenzake tabasamu. Hapo alifanikiwa kumuona vizuri huyo msichana mwenye kila sifa ya uzuri. Usingizi uliendelea kumzonga Jotham na kujikuta anapitiwa na usingizi bila kuongea chochote na yule msichana. Gari lilifika mpaka mwenge na kupitiliza kituo alichokua anashuka Jothan. Aliamshwa na konda baada gari kushusha abiria wote. “tuko wapi hapa.” Aliuliza Jothan baada ya kuamka na kuangalia nje ambapo kulikua tofauti na mazingira anayoishi. “tumeshafika mwenge kaka.” Alijibu yule konda. Jothan aliangalia huku na kule na hakuona abiria yeyote aliyekuwa kwenye lile gari zaidi yake. Hakusikitika kupitishwa kituo, bali alisikitika sana kutochukua namba wala kujua jina la yule msichana aliyevutika naye zaidi baada ya kuonana nae kwa mara ya pili. Hakua na budi Jotham, zaidi ya kubaki ndani ya daladala na kugeuza nalo. Alipofika kinondoni kwa manyanya alishuka na kufuata njia ilyoelekea shule ya kambangwa secondary school na kupita chuo cha tumaini na kuingia nyumbani kwake ambapo hapakuwa mbali na pale. Hakuwa na hela nyingi sana, ila uwezo wa kula anachokitaka na kubadilisha nguo alikuwa nao. Alifika nyumbani na kujilaza kitandani kwake. Aliamka sa tatu usiku na kutoka kwenda sheli kununua mafuta kwenye kidumu kisha akaenda bar ya jirani na kupata chipsi kuku kisha akarudi nyumbani na kufungua tv na kuangalia yaliyomo. Saa tano usiku alianza kunyemelewa na usingizi,. Alizima tv yake na kwenda kulala. Alijikuta yupo na msichana yule mzuri kwenye fukwe za bahari wakipanga maswala yao ya kuoana. Alitoa pete na kumvisha mwanamke huyo mwenye kila aina ya sifa zilizompeleka Jotham kudata juu yake. Alikurupuka asubuhi na kugundua kuwa hali ile haikuwa halisi, bali alikua anaota.. aliangalia Alarm yake ambayo ilikuwa inalia wakati huo na kuizima. Alijiandaa na kupanda gari yake ambayo alishainunulia mafuta na kwenda nayo kazini kama kawaida. Baada ya mwezi mmoja kupita, Jothan alipata uamisho kikazi kwa miezi sita huko Morogoro. Alilaani ila hakua na jinsi kukubaliana na matakwa ya kazi. Ile ndoto ya kukutana tena na yule msichana iliyeyuka kwakua alijua kabisa kuwa kukaa kwake huko marogoro utakuwa mwisho wa kukutana tena na yule msichana kwa miezi mingi. Siku ya safari ilipofika. Alijiandaa na kupitiwa na gari la ofini kwao na kusafiri pamoja na wenzake waliopata uhamisho huo wa muda huko morogoro. Alifanya kazi huko kwa miezi mitatu na kupelekwa Arusha kwa ajili ya kumalizia miezi hiyo mitatu iliyobakia. Nia na madhumuni ni kuwafundisha kazi wafanyakazi wa mikoa hiyo kwakua ofisi yao ilikua imefungua matawi mapya katika mikoa hiyo. Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kurudi Dar, Jothan alipita barabara moja na kumkuta msichana mzuri akiwa ameshika tenga anauza maua. Moyo ulimlipuka ghafla na kujikuta anamsogelea yule dada bila kujitambua. “unauzaje maua” aliuliza Jothan huku akimuangalia binti yule mzuri ambaye alikua anatabasamu baada ya kumuona yeye pale. “shilingi elfu moja kwa kila moja.” Aliongea yule dada bila kumuangalia Jothan usoni. “nikitaka yote utaniuzia shilingi ngapi?” aliuliza Jothan huku akizidi kumtathmini binti yule huku akionyesha kufurahi na muonekano mzuri aliokuwa nao msichana huyo. “nisaidie kuhesabu, kisha nitajie idadi ili nikuuzie kwa bei ya jumla.” Aliongea yule dada na kumfanya Jothan kushangaa. Alijiuliza maswli ya haraka . labda hyule msichana hajui kusoma au alikua anamtega. “kwanini usiniambi tu, maana siyo mengi yaliyobaki.” Aliongea Jothan kwa sauti ya upole. “mi sioni kaka yangu.” Aliongea yule dada na kumfanya Jothan kupigwa na butwaa. “kweli???” aliuliza Jothan huku akiwa haamini alichoambiwa na yule dada. Kwa kumuonyeshea kuwa haoni, yule dada alivua miwani na kumuonyesha macho yake ambayo yalikuwa na watoto ndani. Aliingiwa na roho ya imani Jothan na kukiri moyoni kuwa yule dada alikua nahitaji msaada kwakua tatizo lake linatibika ila matibabu yake yalikuwa ghali sana. “unaishi mbali na hapa?” aliuliza Jothan baada ya kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kuyachukua maua sita yaliyobakia. “si mbali na hapa, ni mtaa watatu hapo mbele.” Aliongea yule dada mwenye asili ya kichaga lakini asiyekuwa na lafudhi hiyo wala meno yake kuharibika. Ngozi yake ilikubali baridi na kuwa nyeupe yenye mvuto. “unaonaje kama nikikusindikiza?” aliuliza Jothan. “sawa” Alijibu yule dada na safari ya kuelekea kwao ilianza. Mwendo wa kuupapasa kwa fimbo ndio uliomfanya Jothan kuamini kuwa ni kweli huyo dada alikua kipofu. Alikaribishwa mpaka ndani na kukutana na mama yake huyo binti. “karibu baba,”alikaribisha mama yake yule dada na kuwapisha. “huyo ndio mama yangu wa peke, sina msaada mwengine zaidi yake.” Aliongea yule dada huku anatabasamu. Hakua anamuona Jothan ambaye wakati huo alikua anaumia juu ya msichana huyu ambaye alionyesha hali aliyokuwa nayo ameizoea. Aliaga baada ya kuongea na kupiga stori mbili tati ikiwemo maisha yao kwa ujumla. Alirudi kwenye nyumba waliyopangiwa na kumpa story rafiki yake anayekaa naye kwenye nyumba hiyo. “kwa hiyo unataka ufanyaje ndugu yangu,” aliuliza rafiki yake huyo baada ya kumpa mkanda mzima. “nitajitahidi kwa uwezo wangu wote ili BAHATI apone kabisa.” Aliongea Jothan na kumuonyesha rafiki yake ni jinsi gani ameguswa na mdada huyo. “kwa hiyo unampango wa kumchukua na kwenda naye Dar?” aliuliza rafiki yake huyo huku wakiendelea kula bisi zilizokuwa kwenye meza yao. “exactly” alijibu Jothan kiingereza kuonyesha msisitizo. Asubuhi ya siku ya pili, Jothan aliamka na kwenda tena kwa kina Bahati. Kabla hajafika, tayari alishamuana dada huyo mwenye juhudi na kazi yake akiwa barabarani kama kawaida yake akiuza maua. “mambo Bahati.” Alisalimia Jothan Kwakua sauti ya Jotham alikua ameshaijua, alimng`amua na kuachia tabasamu mwanana lililomuacha hoi Jotham. “safi” alijibu Bahati. Waliongea mengi na kubwa zaidi ni juu ya Jothan kumsaidia Bahati swala lake la macho. Bahati alifuraha sana na wote wakaenda kwa mama yake na kumpa taarifa zile njema. “nitashukuru sana mwanangu..mungu akuzidishie.” Aliongea mama yake Bahati na zoezi la kujiandaa kwa ajili ya safari ya Dar-es-salaam lilianza mara moja kwa kufua nguo zake chafu na kupanga zingine kwenye mabegi. “tutakupitia kesho saa kumi na mbili asubuhi.” Aliongea Jothan na kuaga. Bahati alipanga kila kitu chake akisaidiwa na mama yake tayari kwa safari ya kesho yake ambayo ilikuwa na matumaini makubwa kwake. Alisali na kumuomba mungu afike Dar salama na lengo la kufanyiwa upasuaji lifanikiwe kwa nguvu zake mungu wa viumbe vyote. Asubuhi na mapema gari ya kina Jothan ilimpitia Bahati na safari ya kuitafuta Dar-es-salaam ilianza. Njiani walipiga story na kucheka kama vile walikuwa wamezoeana muda mrefu au walikuwa wameshakutana kabla. Uchangamfu wa Bahati uliwapendeza watu wote waliokuwemo kwenye lile basi. Bahati alipendelea kukaa dirishani kwa ajili ya upepo. Lakini Jothan aliamini kuwa Bahati alikua anatamani pia kuona vilivyokuwa nje. Saa nane mchana walifika mombo na kupaki gari lao kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Waliokwenda haja walienda ilimradi safari ikiendelea pasiwe na usumbufu kati yao. “unapendelea chakula gani?” aliongea Jothan baada ya kuingia naye Bahati kwenye mgahawa huo. “kama kuna wali huwa napenda hata ikiwa na mboga yoyote.” Aliongea Bahati. Jothan alimuagizia wali na nyama ya kuku. “ahsante kwa chakula.” Aliongea Bahati baada ya kumaliza kula kile chakula. Baada ya hapo safari iliendelea na kufika ubungo saa kumi na mbili jioni. Safari ya kuwapeleka makwao ilianza na Jothan na Bahati walishuka kinodoni na kuingia ndani. Kutokana na uchovu wa safari, Jothan alimpeleka Bahati chumba atakachokuwa analala na kutoka nje kununua chakula watakachokula usiku huo. Baada ya kiza kutawla, Jothan alimpelekea chakula Bahati na kumuonyesha choo na bafu ambavyo vyote vilikua mule ndani kwenye kile chumba. Baada ya mapumziko ya siku mbili, Jothan alimpeleka Bahati kwenye hospitali kubwa ya macho CCBRT kwa ajili ya upasuaji. Vipimo vilileta majibu mazuri kuwa kulikowa na uwezekano mkubwa wa kutolewa hivyo vitoto vya jicho na Bahati kona tena. Tarehe ya upasuaji ilipangwa kwa ajili ya upasuaji huo na Jothan alimpeleka Bahati ili apate huduma hiyo ambayo kama itafanikiwa itakuwa imempa maisha mengine kabisa mrembo huyo ambaye alikuwa haoni toka alipozaliwa.. Muenendo mbaya wa utendaji kazi huko marogoro ndio uliomfanya Jothan kurudishwa tena mkoani humo. Alisikitika kumuacha mgeni wake katika hospitali kabla hajashuhudia matokeo ya upasuaji huo, lakini hakuwa na jinsi kwakua aliuachia uongozi jukumu la kumuangalia mgonjwa wake huyo. Miezi sita ilikatika akiwa huko Morogoro huku mawasiliano yakikosekana kati yake na Bahati. Hata alipouuliza uongozi wa kampuni yao walimwambia kuwa walikuwa wamempa kiasi cha hela baada ya kupona na tokea wamkabidhi hawakupata mawasiliano naye. Mawazo yalimsonga Jothan na hakujua kwanini Bahati aliamua kufanya vile. Baada ya uchumi wa kampuni hiyo kutengamaa na kupata uongozi uliokuwa ukipiga kazi kama ipasavyo, Jothan alirudi Dar kuendelea na majukumu yake ya kila siku. Alipofika nyumbani kwake palikuwa pamefungwa kama alivyo paacha. Aliingia ndani na kuikagua nyumba yake kwa macho kisha akaenda kulala kutokana na uchovu aliokuwa nao. Usiku wa jumamosi, aliamua kwenda club kwakua ni muda mwingi alikosa kwenda. Hivyo aliamua kwenda kupata mixing za ma dj wakubwa ambao wanajua kubadilisha nyimbo na kumfanya mtu aburudike na mpangilio wa nyimbo wanazoziweka kulingana na wakati. Wakati akiwa anaburudika na kinywaji chake huku akipata burudani nyingine akiwa kwenye kiti, mzuka alkampanda na kujikuta anaingia kati na kuucheza wimbo ulimvutia zaidi. Style alizocheza ziliwavutia wengi hadi baadhi ya wasichana walimfuata na kucheza nae. Aliifurahia sana hiyo siku na kurudi nyumbani akiwa na hamu ya kwenda tena siku ya jumapili. Kwakua alikua na likizo ya mwezi mzima kazini, hakuona tabu kulala mchana ili usiku akeshe tena kutokana na kuwa mziki ni starehe kubwa anayoipenda japokuwa siyo muimbaji. Siku hiyo alifika mapema na kutulia kwenye meza kwanza za nyuma na kuendelea kupata kinywaji na nyama choma kwa wingi. Wasichana wengi walimshobokea na kuomba ofa za bia. Kwakua Jothan alikuwa akiingia sehemu yoyote ya starehe huwa anakua amependeza mfukoni, basi hakuona shida kumwaga ofa mbali mbali kwa wanaomuomba bila kujali jinsia. Wakati disco likizidi kuchanganya. Kwa mbali kwenye mwanga hafifu Jothan alimuona msichana aliyemfananisha. Hakujiuliza mara mbili, alinyanyuka na kumfuata pale pale kwenye meza yao. Kadri alivyozidi kumsogelea, ndipo sura ya yule binti iliyozidi kumjia kichwani. Alimsogelea na kumuangalia kwa ukaribu zaidi. “kaka,tukusaidie nini?” aliuliza yule dada baada ya kumuona Jothan akiwa mbele ya meza yao amesimama na kumuangalia kupita kiasi. “sijui ndio wewe au nakufananisha?” aliongea Jothan huku akiwa haamini baada ya kumuona yule binti aliyekuwa kapendeza kupita kiasi. “kaka hizo swaga za kizamani kweli, za kuaza kufananishana mara sijui nilikuona wapi, achana na sisi bro” aliongea yule dada na kuwafanya wenzake kucheka. Kutokana na hadhi aliyokuwa nayo Jothan, alifedheheka kiasi na kumfanya akubali matokeo. Aliwaacha wale mabinti huku wakiwa wanamjadili na yeye kurudi kwenye siti yake. Ladha ya club ilipotea na kuamua kurudi nyumbani kwake. Alijitupa kitandani na kuwaza sana. Kwa jinsi alivyotekoa kufurahi kumuona tena yule msichana na majibu aliyopewa hata kabla hajajitambulisha yalimtia simanzi. “naweza kusema kuwa hawezi kunifahahamu, lakini hata sauti kashindwa kuitambua?… au kwa sababu sauti yangu ilikuwa ya kilevi?” Alijiuliza Jothan maswali mengi bila ya kuwa na majibu. Asubuhi ya siku ya pili alienda kupata supu maeneo ya karibu na kwao. Aliporudi alijitupa kitandani na usingizi ukamchukua mpaka saa kumi jioni. Njaa ilikuwa ina muuma sana. Aliamua kutoka na gari lake na kwenda kwenye Bar kubwa iliyokuwa msasani kwa ajili ya kupata chakula ambacho siku hiyo kilikuwa kinapikwa kwa ustadi mkubwa. Aliagiza oda yake na kuletewa baada ya muda kama wa dakika tano. Kabla hajaanza kula, kwa mbali aliisikia sauti ya yule mmsichana aliyekutana naye Club usiku wa jana yake. Alinyanyuka na kwenda kwenye ile meza ambayo alimkuta akiwa na rifiki yake mmoja wa kike. “samahani, wewe sio BAHATI!!!?” Aliuliza Jothan huku akiwa na uhakika asilimia zote kwakua alikua anafahamu fika kuwa yule ndiye mwenyewe kutokana na sauti yake na muanekano wake ingawaje kwa sasa alikuwa anavutia zaidi. “ndio mimi, umenijuaje?” aliuliza yule dada na Jothan aliachia tabasamu huku akitikisa kichwa chake. “ina maana Bahati hata sauti yangu huikumbuki?” aliuliza Jothan huku akiwa haamini kumuona Bahati akiwa na macho mazuri tena yaliyoongezewa uzuri na kope za bandia alizo bandika. “ningekuwa nakujua nisingekuuliza umenijuaje?” alijibu yule dada na kuendelea kuifyonza juice yake iliyosindikizwa na chpsi pamoja na nyama choma waliyokuwa wanakula yeye na rafiki yake. “nitakushangaa sana ukisema kuwa sauti ya Jothan hauikumbuki.” Aliongea Jothan na kubaki kumuangalia Bahati aliyepigilia mapigo ya ki sister duu. “WHO A JOTHAN BY THE WAY????” Aliuliza yule dada na kumfanya Jothan aondoke bila kuaga. Alienda counter na kulipia oda yake bila kuigusa na kuondoka zake. Hakuamini kuwa Bahati angewaza kuongea yale maneno mbele yake tena kwa nyodo wakati ni yeye ndie aliyemleta mjini na kumpa msaada wa kuyatibu macho yake baada ya yeye kuikubali hali ya ukipofu kutokana na kuwa kulikuwa na uhaba wa pesa nyumbani kwao. Jothan ilibaki kidogo tu agonge wakate anaendesha kutokana na mawazo yaliyochanganyikana na hasira kwa kile alichofanyiwa na Bahati.. Alijilaumu sana kwenda kula chakula pale na kuambulia maumivu. Alijuta kukutana tena na Bahati ingawaje mwanzoni alikuwa na hamu ya kuonana nae. Alifika nyumbani na kujilaza. ”who a Jonathan by the way??” Aliirudia ile kauli ya Bahati na kujikuta anashindwa kuamini kuwa yule ndie bahati halisi aliyemtamkia maneno yale. ITAENDELEA ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: