MUUZA MAZIW EP 07 “aaaaahh!! Jamani wifi wao!!” Aliongea kwa furaha baada ya kumuona mgeni aliyekuwa akigonga ni penina. “asante wifi , shikamoo!” Penina aliongea na kisha kumkumbatia wifi yake kwa furaha. “ marhaba wifi ,vipi masomo?” Aliongea huku akiipokea mizigo aliyo ibeba “naendelea vizuri tu wifi” “haya mungu akusaidie” Aliongea lisa na kuelakea sebuleni , aliiiweka mizigo pembeni ya kochi na kasha kuelekea sehemuk ilipo friji. Penina, penina akaamua kuichukua mizigo ili aipeleke chumbani. “hapana wifi, hapana , hiyo iache hapo hapo nitaiingiza mwenyewe,, wewe kwanza kunywa juisi upumzike.“ Aliongea lisa huku akiwa ameshikilia jagi lenye juisi pamoja na glasi, alifanya hivyo kwa sababu chumba anachotakiwa kulala penina ndicho chumba ambacho amemficha muuza maziwa. “usipate tabu wifi wangu kunywa juisi upumzike, nipo kwa ajili yako “ Aliongea lisa huku akiibeba mizigo na kuelekea chumbani na kumuacha penina akinywa juisi taratibu. Alipoingia chumbani alimshutua muuza maziwa na kumweleza hali halisi. “kwahiyo nitatoka saa ngapi humu?” “ itabidi uvumilie mpaka usiku wifi akilala , mlango wa nje nitauacha wazi leo” Aliongea lisa “Sawa lakini vipi kuhusu chakula manaake niana njaa” “ usijali nitakuletea utakula humu humu , jitahidi usitoke nitajaribu kufanya mpango hata kamakabla ya usiku ikiwezekana” “poa” Muuza maziwa aliitikia “alafu nitaa……” Lisa alikatiza kauli yakebaada ya kusikia mlio wa kitasa kikifunguliwa. Haraka haraka muuuza maziwa aliingia kabatini na kisha lisa aliufunga mlango wa kabati hiyo kabla hata hajauachia mlango huo alisikia sauti nyuma yake. “wifi mbona unagombana na hilo kabati!?” Swali hilotoka kwa penina lilimfanya lisa ashikwe na kigugumizi cha ghafla huku akitoa maelezo ya kujikanyagakanyaga. “ah, mh, a-, u-n-a-j-u-a hi-li ka-ba-ti ni bo-vu” “limeharibika , ooh, mungu wangu!” Penina aliongea huku akilisogelea kabati hiloili kuiangalia sehemu ilipoaribika. “ah, hapana wifi usiiguse hapa nimeitegesha , iache hivyo hivyo mpaka atakapokuja fundi kulirekebisha” Aliongea Lisa haraka haraka. “okey”[sawa] Aliongea Penina huku akitikisa kichwa kuonyesha kwamba ameelewa. “nataka kuoga wifi” “na kweli manaake umechoka kweli kweli wifi yangu” Aliitikia Lisa haraka haraka kwani alijua huo ndio upenyo wa kumtoa muuza maziwa. Na kweli penina alipoingia bafuni lisa aliufungua mlango wa kabati haraka na kumtoa muuza maziwa , akala chakula haraka na kuanza safari ya kutoka nje ya nyumba hiyo , walipofika kwenye mlango wa kutokea muuza maziwa alimbusu lisa kwa mara ya mwisho , alipomaliza kufanya hivyo alitoka ndani ya chumba hicho na kutokeza koridoni ili atoke nje kabisa ya nyumba hiyo lakini kabla ya kufanya hivyo alisikia muungurumo wa gari, halikuwa gari lingine bali gari la Jerry mume wa Lisa. Hofu iliwaingia kwa ghafla na haraka haraaka walirudi tena chumbani kwa penina , ambapo kama kawaida alimfungia muuza maziwa kabatini, hawakuwa na njia nyingine tena bali hile waliyoipanga awali, muuza maziwa asubiri mpaka usiku wa manane Penina atakapo lala ndipo atoke kwani Lisa atauacha mlango wa kutokea wazi. Lisa alipomaliza kumfungia muuza maziwa katika kabati alitoka nje ya chumba hicho,akiwa koridoni aligongana ana kwa ana macho na mumewe. Wote wawili waliinamisha vichwa vyao chini. Kwani kila mmoja aliona aibu kwa kumsaliti mwenzake. Lisa kwa muuza maziwa na Jerry kwa sekritari wake. “Ah, mmh, wifi amekuja , kakaribu!” Aliongea Lisa kwa kujiumauma huku akiwa na wasi wasi. “ asante amekuja saa ngapi?” “sio muda mrefu” “aah yuko wapi sasa nimsalimie?” “yuko bafuni anaoga” “Okey” [sawa] Aliitikia na kisha kuelekea chumbani kwake. Lisa nae alimfuata mumewe nyuma hukubado akiwa na hofu juu ya kugundulika kwa uwepo wa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo. “Pole na kazi dear” Aliongea Lisa huku akijibaraguza kwa kumvua tai mume wake, macho yake bado yalikuwa na aibu sababu bado alikuwa na wasi wasi kwamba labda mumewe amegundua chochote. “ah, asante mpenzi” Aliitikia Jerry huku akitabasamu, lakina nae pia tabasamu lake liliishia mdomoni tu moyoni nafsi ilimsuta . Maovu aliyoyafanya na sikritari wake ofisini kwake yalikuwa bado yakionekana katika kichwa chake. Akavua nguo na kuingia bafuni kuoga lisa nae alimfuata na kujumuika nae kuoga . Alifanya hivyo ili Jerry hasihisi chochote. Walioga huku kila mmoja akiwa hana habari na mwenzake. Kwani wote wawili walikuwa wamechoka, walipomaliza kuoga wakavaa na kasha kwenda sebuleni. Huko wakamkuta Penina akianga lia tv. “mdogo wangu huyo!” Jerry aliongea kwa furaha huku wakicheka. “kaka!” Penina aliitikia na kisha kumkimbilia kaka yake. “waoo!!!” Waliongea kwa pamoja na kisha kukumbatiana kwa furaha. “habari za masomo!?” ITAENDELEA..

at 11:55 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top