MKE WANGU AMEBADILIKA. Akapokea sms kwenye simu yake. Sms kutoka kwa mkewe. Sms ilisomeka hivi; "Hi my love, niko katika mood ya maombi. Kuna jambo lolote unataka niliombee?" Mume akaisoma sms mara mbili mbili kwa mshangao. Mkewe hajamuita kwa jina la "my love" kwa kipindi kirefu sana. Na zaidi mkewe hajawahi kumuuliza jambo la kuombea. Ughafla huu ukamshangaza! Mume akaona amjibu tu hivyo hivyo..akamrudishia sms kwa kuandika; "Fanya maombi ya shukrani, mshukuru Mungu kwa ajili ya promotion niliyopata kazini". "Umepanda cheo? Lini?" Mkewe akamtumia sms ya kumuuliza. Mume akakukumbuka kuwa hakumwambia mkewe kwamba amepanda cheo. Kwa sababu mkewe ni jeuri huwa hawezi ku-appreciate jitihada zake na kazi ngumu anazofanya. Yeye hua ni kulalamika tu. Hivyo alivyopanda cheo aliona akimwambia mkewe ataishia kulalamika. "Ni mwezi, niko na ofisi mpya hivi sasa. Samahani, sikukwambia mapema". Mume akajibu. Dakika nne zikapita bila mkewe kumjibu sms ya mwisho. Mume akajua mkewe ameshakasirika kama kawaida yake. Simu yake ikaita. Mkewe alikuwa anapiga. Mume akaguna. Hiki ni kimbembe, anahofia drama za mkewe. "Hello" mume akapokea simu. "Hi my love" mke akaongea upande wa pili. "Mmh" Mume akaguna baada ya kuitwa 'my love'. Sio kawaida hii. Mke akaendelea kuongea kwenye simu.. "Samahani mume wangu, nilikua na-drive nimetoka shule kwa binti yetu Monalisa kwenye siku yao ya vipaji shuleni. Oh, tumebarikiwa na Mungu kuwa na huyu binti wa ajabu. Anakipaji kikubwa cha kuimba. Ameshinda tuzo shuleni. Shule imemtunuku nishani". Mke akamwambia mumewe kwenye simu kwa furaha. Mume akashikwa na mshangao. Hakutarajia mke ataongea na yeye kwa ustarabu na kwa furaha kiasi kile. "Ameshinda tuzo ya uimbaji? Oh my God. Hongera sana kwa binti yetu Mona." Mume nae akajibu kwa furaha. "Ndio ameshinda tuzo, amekuwa wa kwanza. Inabidi tuanze kumpeleka kwenye darasa la muziki pia. Natamani na wewe ungekuwepo. Ila usijali nimerekodi video alivyokua akiimba" Mke akaongea. Mume akawa bado amechangamyikiwa. Kwa kawaida mkewe angeanza kumlaumu kwa namna gani alivyo baba mbaya kwa vile hashiriki kwenye shughuri za shuleni kwa watoto wao wawili. Mfano siku za wazazi na siku za vipaji vya watoto shuleni. Ingawa mkewe anafahamu kabisa kazi zinambana na kazi ya mkewe kidogo inao unafuu hivyo mke anaweza kwenda. Mume angependa kweli kuhudhuria lakini kazi sio rafiki kwake. Licha ya hayo mkewe alikua akimlalamikia. "Anyway my love, nilikupigia simu kukupongeza kwa kupanda cheo. Ninajivunia sana kuwa na wewe. Najua uko busy na kazi, je naweza kuomba na wewe kwenye simu?" Mke akaongea. Mume akakohoa kidogo kwa mshangao. "Ndio, ndio tuombe tu haina shida" mume akaongea. Kwa mara ya kwanza kama wanandoa wakasali pamoja kupitia simu. Ilikuwa ni sala fupi lakini yenye faraja. "Amen" mke akamaliza. "Amen" mume nae akaitikia. "Ok my love. Nikuache uendelee na kazi. Tutaonana baadae nyumbani. Nakupenda eeh!". Akakata simu. Mume akaangalia kwenye screen ya simu yake. Akaona picha ya kwake, mkewe na watoto wao wawili. Picha ya muda kama mwaka mmoja hivi uliopita na akai-save kama wallpaper na screensaver. Akajikuta akitabasamu huku akiangalia screen. "Mambo mazuri" akawaza kichwani mwake. Akajikuta akiwa na mood nzuri na akafanya kazi vizuri zaidi. Akawa na furaha pamoja kujiamini fulani hivi baada ya kuongea na ile simu ya mkewe. Akawa akicheka na kufurahi zaidi na wafanyakazi wenzake pale ofisini. Akapokea sms kutoka WhatsApp. Alikuwa ni mkewe. Amemtumia ile video ya binti yake Mona akiimba shuleni kwenye siku ya vipaji. "Muangalie binti yetu. Awww..inafurahisha na inatia moyo" ilikuwa ni caption ya hiyo video aliyotuma. Mume akaidownload video na kuangalia binti yake akiimba kwenye stage. "Nimemiss vingi mke wangu" mume akamjibu mkewe baada ya kuiangalia video. "Oh ndio. Ila nimemwambia Mona kwamba baba hajaweza kuja kukuona ukiimba kwa sababu amebanwa na kazi. Na kwamba wewe ni baba bora" Mke akamjibu mumewe. Mume akajihisi kusisimka mwili. Akaweka simu yake mezani. Akatafakari. Mkewe ambae mara kwa mara amekuwa akimtuhumu kuwa hawajibiki kama baba bora, leo amemsifia na kusema yeye ni baba bora?? "Asante sana mke wangu. Hayo maneno yamenipa faraja na kuniongezea nguvu". Mume akamjibu sms baada ya kuichukua mezani tena. "Mona ana macho kama yako" mke akamjibu mumewe. "Hahaa hahaa. Asante mama. Mona analips na nywele kama zako" Mume nae akamjibu. "Kweli? Natamani niwe na nywele kama za Mona. Hata hivyo leo wakati naoga niliona unywele mweupe. Naanza kuota mvi sasa hivi" Mke akamtumia sms mumewe. "Karibu kwenye ulimwengu wa mvi. Mimi nimeshaona mvi tatu mpaka saa hizi" mume nae akamjibu. "Ukirudi kazini utaungana na mimi kuoga leo usiku? Then uniangalie huenda nina mvi nyingi tu huku nyuma ya kichwa..wink wink.." mke akatuma tena sms. Mume akajawa na furaha. Hakumbuki ni lini yeye na mkewe kwa mara ya mwisho wame-chat kwa furaha hivi kwenye simu. Wakawa wana-chat huku mume akifanya kazi. Mpaka muda wa kuondoka ulipofika. Mume Akajipiga selfie akiwa katika ofisi yake mpya na akamtumia mkewe aione ofisi. Hajawahi kufanya hivi. Kupiga picha sehemu alipo na kumtumia mkewe. Ila muda huu kutokana na sms nzuri za mkewe, amejikuta akifanya yale aloshindwa kufanya hapo kabla. Akaendesha gari kuelekea nyumbani. Huku akitabasamu na kusikiliza muziki mzuri. Mume akafika nyumbani. Akafungua mlango na kukuta watoto wake wawili wakifanya homework. "Hello love" mke akamuita mumewe na kumbusu kwenye shavu. Nini kinaendelea? Mke wake hajawahi kumsalimia kwa style hiyo ya kimahaba. Mara nyingi hata hua hamjali...hua wanasalimiana utafikiri masela wa Kigogo sambusa. "Habari za kazi Mume wangu" mke akauliza. "Nzuri tu love. Unaonekana mzuri" mume automatically akajikuta akisukumwa kueleza ukweli wa jinsi anavyomuona mkewe. Hajawahi kumsifia kwa kipindi kirefu sasa. Mke na mume wakaangaliana kwa muda kidogo kwa macho ya kutamaniana. Mke akaelekea jikoni, alikuwa anapika. Mume akaenda mezani kwa watoto wake. Mona akamsimulia baba yake kuhusu tuzo aliyoipata shuleni kwa kipaji cha kuimba na mwanae mdogo wa kiume Piere akamsimulia kuhusu kuwika katika kikosi cha soka cha shule yao na kuwa nyota wa mchezo (man of the match). Mume akagundua watoto wake wanafuraha kubwa sana tofauti na siki zingine huko nyuma. Ni kama wamechukua mood ya mama yao leo. "Babe, umekumbuka kununua chumvi niliyokwambia?" Mkewe akamuuliza mumewe huku akipika jikoni. Mumewe alisahau. Hapa matatizo yataanza sasa. Siku zote mkewe hulalamika na kuropoka mbele ya watoto kama mumewe akisahau jambo aliloombwa na mkewe. Mume akasimama na kuelekea jikoni. "Samahani mama. Nilisahau kupitia supermarket" mume akaongea. "Honey, usijali" mke akaongea kwa upole. "Nimejisahau Mama Mona. I'm sorry" Mume akaomba samahani. Mke akampapasa mkono na kumwambia, "Usijali nitajua nini cha kufanya" "Kuna duka la Mangi kule chini, ngoja niende nikanunue pale" mume akaongea huku akielekea mlangoni. "Hapana usijali" mke akamjibu mumewe. Lakini kwa sababu ya jinsi mkewe anavyom-treat leo mume akataka kufanya lolote kwa ajili ya mkewe. "Baba, tununulie na lollipops" Mona na Piere wakamueleza baba yao. Baba akaondoka nyumbani. Akipiga mluzi huku akiwa na furaha. Akarudi nyumbani na kukuta suprise. Mkewe na wanawe wawili wakampa keki ndogo. "Hongera baba" yalikuwa maneno ya Mona na Piere yakiwa yameandikwa kwenye kadi mbili walizompa baba yao. "Hongera kwa kupandishwa cheo baba" yalikuwa maneno ya mkewe huku akimbusu kwenye shavu. Mume akajihisi kupendwa na watu wa nyumbani mwake. Na akajivunia utendaji kazi wake. Mke akamaliza kupika, then yeye na watoto wake wawili wakaandaa chakula mezani; kitu kingine ambacho si cha kawaida pale nyumbani kwao. Chakula kikaandaliwa. Kwa pamoja wakala kwa furaha. Ni muda wa watoto kulala. "Ngoja tupige selfie ya familia" mume akatoa ombi. Wakaja kwa pamoja, wakakumbatiana na kupiga selfie kadhaa huku wakiwa na furaha. Mke akaomba wanawe waongoze sala. Watoto wakasali na kwenda kulala. Mke akaanza kufuta meza. Mume akajikuta nae akisaidia. Akaenda hatua zaidi na kusaidia kuosha vyombo huku wakiongea kuhusu watoto wao na mambo mengine. Mume akambusu mkewe katika lips. "Nakupenda" mume akamwambia mkewe huku akiwa ameshika kiuno. Mke akamtiza mumewe kwa macho ya mahaba. Ni muda mrefu toka mumewe amemueleza kwamba anampenda. Nae akambusu kwenye lips za mumewe. "Mke wangu, leo umenikimbusha mwanamke niliyemuoa. Umenikumbusha ile sababu ya kukuoa wewe na kuwaacha wengine. Umenionesha kwamba mke ndiye anaebeba furaha ya nyumba na familia kiujumla. ...Unapokuwa mwanga, nami natoa mwanga, nyumba yetu inamulikwa na mwanga. Umenikumbusha zile siku tulipikuwa tuna-date" Mume akamwambia hayo mkewe na kumbusu. Mke akamtizama mumewe machoni, akaweka mikono yake kwenye mabega ya mumewe. Na akamueleza haya; "Nimesoma katika kitabu kwamba mwanamke hata atakapoolewa, abaki kuwa yule yule wa kipindi alipokuwa kwenye uchumba au mahusiano. Natakiwa nikitunze na kujipenda na kuwapenda walio wangu..... ..kuna vitu ambavyo vilikuvutia mpaka ukaonelea niwe girlfriend wako na mwishoe kuwa mkeo. Qualities zangu ulizoziona namna navyoongea na wewe na jinsi ninavyokujali. Sikutakiwa nipoteze hizo qualities baada ya kunioa. Nimerudi mume wangu...nipokee tena. "Na kama hivyo mke wangu, umenifanya nikupende tena...natamani nikutongoze upya" mume akamwambia mkewe. Mke akamvuta mkono mumewe, wakaelekea chumbani na kumwambia, "Honey, tulikubaliana leo tunaoga wote" Wakaingia bafuni...kilichofanyika humo mimi na wewe hakituhusu...ni cha wanandoa tu! Ila walitoka wakiwa na furaha tele na ndio mwanzo wa ndoa yao kuanza upya tena! Busara yangu; "A successful marriage requires falling in love many times, always with the same person". Share

at 12:11 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top