Home → ushauri
→ MKASA WA KUSISIMUA: HAKUNA LAANA MBAYA KAMA KUMKANA MAMA YAKO MZAZI
#inasikitisha pole sana binti
*🌹Binti mmoja ambaye alitokea katika familia masikini alifanikiwa kusoma kwa shida mpaka kufanikiwa kuwa mwanasheria. Alipata kazi nzuri, akiishi katika nyumba nzuri ya kifahari.*
*🌹Pamoja na maisha mazuri lakini binti aliwasahau kijijini kwao, alikua akituma pesa kidogo lakini hakutaka kwenda. Alitaka kuyasahau maisha yake yote ya mateso ya kijijini.*
*🌹Hata kwa marafiki zake alijitambulisha kama kazaliwa Dar huku akidanganya kuwa wazazi wake wamefariki nayeye alikua ndiyo mtoto pekee, hii ni kwasababu marafiki zake wote walikua wakitoka katika familia za kitajiri.*
*🌹Baada ya kukaa muda mrefu bila kufika kijijini kwao wazazi wake walipata wasiwasi, huku wakiwa na wasiwasi kuwa kuna kitu kimempata, walichangisha nauli na Mama yake ambaye alikua mzee sana alipanda gari na kwenda kumuona mjini.*
*🌹Alipelekwa na jirani yao mmoja ambaye alikua akifahamu alipokua akiishi yule binti. Mama alifika na kukuta binti akiwa na afya nzuri, hana tatizo lolote. Binti alikasirika sana kumuona Mama yake kwani alikuja bila taarifa.*
*🌹Hakumsalimia vizuri na kila saa alikua akimlaumu kwanini hakupiga simu kwanza na kama ni hela si angesema amtumie. Mama huku akitokwa na machozi ya furaha alisema shida yake haikuwa hela bali kumuona mtoto wake baada ya muda mrefu.*
*🌹Binti alimdanganya Mama yake kua ile nyumba ni nyumba ya kampuni hivyo haruhusiwi kuishi na mtu yoyote kutokana na kazi aliokuwa anaifanya hivyo yeye asingeweza kuishi pale.*
*🌹Mama hakuwa na maneno, alimuambia hamna shida yeye kwakua ashamuona mwanae roho yake imetulia kwani hakuenda kukaa pale alienda tu kumuona.*
*🌹Binti alimuacha Mama yake apumzike siku ile na kesho yake ili siku inayofuata apande gari kurudi kijijini. Siku iliyofuata baada ya kutoka kazini rafiki zake walikuja, kulikua na sehemu ambayo walishapanga kwenda.*
*🌹Walimkuta Mama yake akiwa nnje akipunga upepo. Walimsalimia vizuri na binti alipowaona aliwakimbilia kuwawahi ili Mama asijitambulishe kwao, alifika na kuwaharakisha rafiki zake ili waondoke.*
*🌹Walipotaka kujua ni nani, alijikuta anadanganya “ Huyo Mama amepotea njia, alipita hapa alikua anamtafuta mtoto wake akakosea nyumba, sasa ndiyo namsaidia, aligonga kwangu kuomba simu, kwani alikua na namba ya mwanae kwenye kikaratasi.*
*🌹Nimeshampigia mwane atakuja kumchukua. Binti alionge akiamini kuwa kesho yake anamuondoa Mama yake mule ndani hivyo rafiki zake hawatamuona tena.*
*🌹Wakati akiongea yale maneno hakujua kuwa Mama yake anasikiliza, alistuka baadaye alipogeuka wakati anafungua mlango wa gari ili aingie. Mama yke alikua anatokwa na machozi, binti alijikaza kama vile hakumuona akaingia kwenye gari na kuondoka.*
_____________________
*🌹Baada ya mizinguko yake binti alirudi nyumbani, hakumkuta Mama yake, alimuuliza mfanyakazi wa ndani akasema hajui, alijua wameondoka wote kwani alimuacha nnje wakati yeye anatoka na gari.*
*🌹Binti alianza kupaniki, alisubiria mpaka usiku wa mamnane lakini Mama yake hakurejea. Hapo alianza kuchanganyikiwa, kichwa kikikumbuka maisha ya shida waliyopitia, namna ambavyo Mama yake alivyoteseka kwaajili yake.*
*🌹Machozi yalinza kumtoka akijutia mambo aliyomfanyia Mama yake. Alimtafuta yule Kaka ambaye alimleta Mama yake pale lakini hakuwa akijua chochote. Usiku ulipita akiwa macho, asubuhi alilazimika kwenda kazini kwani alikua na kikao.*
*🌹Lakini mchana alishindwa kuvumilia, ilibidi kwenda Polisi na kuanza kumtafuta Mama yake lakini hakupatikana. Siku moja ilipita na hatimaye yapili ilipita bila kumuona Mama yake, alianza kuwa na wasiwasi.*
*🌹Akiwa ofisini hajui hili wala lile rafiki yake mmoja alikuja, walianza kuongea akiwa hana raha kabisa. Rafiki yake alimuuliza tatizo lilikua nini akaamua kumuambia, lakini kabla hajaanza kuonge arafiki yake alisema.*
*🌹“Halafu shogaa nilitaka kusahau, unamkumbuka yule Bibi ambaye tulimkuta kwako jana?”*
*``Ndiyo namkumbuka! Amefanya nini? Umemuona wapi?” Alijikuta anadakia kwa haraka kutaka kujua.*
*Basi jana wakati natoka kazini nikapita sehemu, nimekuta watu wamezunguka, kumbe kagongwa na bodaboda kaumia kichwani, watu wakawa wanakimbia kukwepa ushahidi.*
*🌹Namimi nikapita, sasa baadaye narudi kumbe watu walimuacha pale Bibi wawatu mpaka Polisi wanakuja lisaa lizima baadaye basi Bibi wawatu kashafariki. Kusema kweli roho iliniuma sana kwa kumpita bila kumsaidia…”*
*🌹Rafiki yake aliongea kwa masikitiko, lakini kabla hajamalizia yule binti alidondoka na kupoteza fahamu. Alizinduka yuko hospitali kazungukwa na marafiki zake na mchumba wake.*
*🌹Walimuuliza sababu ndipo alipoamua kuwaelezea, kila mtu alimshangaa kwa kumficha Mama yake, walihangaika kumtafuta wakakuta maiti yake, wakamsaidia kusafirisha maiti mpaka Kijijini.*
*🌹Walizika salama lakini baada ya kurudi mchumba wake alimuacha, marafiki zake wote aliokuwa akiwaona wa maana walimtenga kutokana na tabia zake. Binti alishikwa na msongo wa mawazo.*
*🌹Kila siku ilikua mtu wa kulia tu, alishindwa kufanya kazi vizuri, jambo lililopelekea *afukuzwe kazi*.
*Kafukuzwa nyumba ya kifahari aliyokua akiishi na sasa yuko mtaani akitafuta ajira huku akiona hata aibu kurudi nyumbani kuwaona ndugu zake.*
Kama kisa hiki kimekugusa na unampenda sana Mama yako, unakumbuka asili yako #SHARE na marafiki zako, kuna mtu atajifunza kitu hapo😑
Nakutakia Siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
Usisahau ku LIKE
MKASA WA KUSISIMUA: HAKUNA LAANA MBAYA KAMA KUMKANA MAMA YAKO MZAZI #inasikitisha pole sana binti *🌹Binti mmoja ambaye alitokea katika familia masikini alifanikiwa kusoma kwa shida mpaka kufanikiwa kuwa mwanasheria. Alipata kazi nzuri, akiishi katika nyumba nzuri ya kifahari.* *🌹Pamoja na maisha mazuri lakini binti aliwasahau kijijini kwao, alikua akituma pesa kidogo lakini hakutaka kwenda. Alitaka kuyasahau maisha yake yote ya mateso ya kijijini.* *🌹Hata kwa marafiki zake alijitambulisha kama kazaliwa Dar huku akidanganya kuwa wazazi wake wamefariki nayeye alikua ndiyo mtoto pekee, hii ni kwasababu marafiki zake wote walikua wakitoka katika familia za kitajiri.* *🌹Baada ya kukaa muda mrefu bila kufika kijijini kwao wazazi wake walipata wasiwasi, huku wakiwa na wasiwasi kuwa kuna kitu kimempata, walichangisha nauli na Mama yake ambaye alikua mzee sana alipanda gari na kwenda kumuona mjini.* *🌹Alipelekwa na jirani yao mmoja ambaye alikua akifahamu alipokua akiishi yule binti. Mama alifika na kukuta binti akiwa na afya nzuri, hana tatizo lolote. Binti alikasirika sana kumuona Mama yake kwani alikuja bila taarifa.* *🌹Hakumsalimia vizuri na kila saa alikua akimlaumu kwanini hakupiga simu kwanza na kama ni hela si angesema amtumie. Mama huku akitokwa na machozi ya furaha alisema shida yake haikuwa hela bali kumuona mtoto wake baada ya muda mrefu.* *🌹Binti alimdanganya Mama yake kua ile nyumba ni nyumba ya kampuni hivyo haruhusiwi kuishi na mtu yoyote kutokana na kazi aliokuwa anaifanya hivyo yeye asingeweza kuishi pale.* *🌹Mama hakuwa na maneno, alimuambia hamna shida yeye kwakua ashamuona mwanae roho yake imetulia kwani hakuenda kukaa pale alienda tu kumuona.* *🌹Binti alimuacha Mama yake apumzike siku ile na kesho yake ili siku inayofuata apande gari kurudi kijijini. Siku iliyofuata baada ya kutoka kazini rafiki zake walikuja, kulikua na sehemu ambayo walishapanga kwenda.* *🌹Walimkuta Mama yake akiwa nnje akipunga upepo. Walimsalimia vizuri na binti alipowaona aliwakimbilia kuwawahi ili Mama asijitambulishe kwao, alifika na kuwaharakisha rafiki zake ili waondoke.* *🌹Walipotaka kujua ni nani, alijikuta anadanganya “ Huyo Mama amepotea njia, alipita hapa alikua anamtafuta mtoto wake akakosea nyumba, sasa ndiyo namsaidia, aligonga kwangu kuomba simu, kwani alikua na namba ya mwanae kwenye kikaratasi.* *🌹Nimeshampigia mwane atakuja kumchukua. Binti alionge akiamini kuwa kesho yake anamuondoa Mama yake mule ndani hivyo rafiki zake hawatamuona tena.* *🌹Wakati akiongea yale maneno hakujua kuwa Mama yake anasikiliza, alistuka baadaye alipogeuka wakati anafungua mlango wa gari ili aingie. Mama yke alikua anatokwa na machozi, binti alijikaza kama vile hakumuona akaingia kwenye gari na kuondoka.* _____________________ *🌹Baada ya mizinguko yake binti alirudi nyumbani, hakumkuta Mama yake, alimuuliza mfanyakazi wa ndani akasema hajui, alijua wameondoka wote kwani alimuacha nnje wakati yeye anatoka na gari.* *🌹Binti alianza kupaniki, alisubiria mpaka usiku wa mamnane lakini Mama yake hakurejea. Hapo alianza kuchanganyikiwa, kichwa kikikumbuka maisha ya shida waliyopitia, namna ambavyo Mama yake alivyoteseka kwaajili yake.* *🌹Machozi yalinza kumtoka akijutia mambo aliyomfanyia Mama yake. Alimtafuta yule Kaka ambaye alimleta Mama yake pale lakini hakuwa akijua chochote. Usiku ulipita akiwa macho, asubuhi alilazimika kwenda kazini kwani alikua na kikao.* *🌹Lakini mchana alishindwa kuvumilia, ilibidi kwenda Polisi na kuanza kumtafuta Mama yake lakini hakupatikana. Siku moja ilipita na hatimaye yapili ilipita bila kumuona Mama yake, alianza kuwa na wasiwasi.* *🌹Akiwa ofisini hajui hili wala lile rafiki yake mmoja alikuja, walianza kuongea akiwa hana raha kabisa. Rafiki yake alimuuliza tatizo lilikua nini akaamua kumuambia, lakini kabla hajaanza kuonge arafiki yake alisema.* *🌹“Halafu shogaa nilitaka kusahau, unamkumbuka yule Bibi ambaye tulimkuta kwako jana?”* *``Ndiyo namkumbuka! Amefanya nini? Umemuona wapi?” Alijikuta anadakia kwa haraka kutaka kujua.* *Basi jana wakati natoka kazini nikapita sehemu, nimekuta watu wamezunguka, kumbe kagongwa na bodaboda kaumia kichwani, watu wakawa wanakimbia kukwepa ushahidi.* *🌹Namimi nikapita, sasa baadaye narudi kumbe watu walimuacha pale Bibi wawatu mpaka Polisi wanakuja lisaa lizima baadaye basi Bibi wawatu kashafariki. Kusema kweli roho iliniuma sana kwa kumpita bila kumsaidia…”* *🌹Rafiki yake aliongea kwa masikitiko, lakini kabla hajamalizia yule binti alidondoka na kupoteza fahamu. Alizinduka yuko hospitali kazungukwa na marafiki zake na mchumba wake.* *🌹Walimuuliza sababu ndipo alipoamua kuwaelezea, kila mtu alimshangaa kwa kumficha Mama yake, walihangaika kumtafuta wakakuta maiti yake, wakamsaidia kusafirisha maiti mpaka Kijijini.* *🌹Walizika salama lakini baada ya kurudi mchumba wake alimuacha, marafiki zake wote aliokuwa akiwaona wa maana walimtenga kutokana na tabia zake. Binti alishikwa na msongo wa mawazo.* *🌹Kila siku ilikua mtu wa kulia tu, alishindwa kufanya kazi vizuri, jambo lililopelekea *afukuzwe kazi*. *Kafukuzwa nyumba ya kifahari aliyokua akiishi na sasa yuko mtaani akitafuta ajira huku akiona hata aibu kurudi nyumbani kuwaona ndugu zake.* Kama kisa hiki kimekugusa na unampenda sana Mama yako, unakumbuka asili yako #SHARE na marafiki zako, kuna mtu atajifunza kitu hapo😑 Nakutakia Siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda Usisahau ku LIKE
Artikel Terkait
HIVI UNAIJUA MAANA YA MAPENZI VIZURI AMA.......???  Jina mapenzi limeweza kupewa maana nyingi kulingana na maongezi yanayozunguka jina hilo. Mapenzi yaweza kusemwa kwamba ni jina linaloonyesha hisia za mtu iwe mahaba, pendo kwa mtu ama upendo wa Mungu. Mara nyingi watu wengi hukosea kwa kuchambua mapenzi katika mahaba pekee. Watu wengi hudhania mapenzi huwa yanahusisha moyo wa binadamu, lakini hakika ni kwamba huhusisha ubongo wa mwanadamu. Kuna aina nyingi za mapenzi ambazo binadamu huonyesha katika maisha yao wanapoendelea na shughuli zao za kila siku. Kama binadamu sisi husahau aina nyingine za mapenzi kwani wengi wetu hawajui neno mapenzi lina maana nyingi. Kwa kufafanua mapenzi yapo na aina zifuatazo Mapenzi ya kimwili (Eros) Aina hii ya mapenzi ni ya kimahaba. Kwa mfano mwanamume kumtamani mwanamke ama vile vile mwanamke kumtamani mwanamume kwa hamu ya ngono. Hapa mapenzi huwa yanayoendelezwa na hisia za kumtaka yule mwingine kimapenzi. Hii ndio aina ambayo watu wengi duniani hudhani ndio maelezo kamili ya mapenzi ill hali hii ni moja yapo ya zingine nyingi. Aina hii ya mapenzi ni muhimu kwa watu wanaoanza kutongozana ama watu wanaofikiri kuwa katika uhusiano. Mapenzi ya Urafiki (Philia) Aina hii ni ambayo inavutiwa na mtu kukufanyia kitendo kizuri ama kukusaidia ama ni mtu mzuri kwa ujumla. Mapenzi hapa yaweza kuwa kwa ndugu ama rafiki yako mzuri. Mapenzi haya huwa sana ambapo mtu wanashiriki maadili sawa na mwenzake na kwamba hisia zao sinaambatana ama mmoja anapokea matendo sawia na yale anamwelekezea yule mwenzake. Mapenzi ya aina hii yanaenziwa sana duniani. Wataaluma huamini kwamba mapenzi ya urafiki husaidia kutoa tamaa ya mwili na kuzingatia kufahamiana zaidi kwa marafiki na dunia kwa jumla. Mapenzi ya Familia(Storge) Aina hii ya mapenzi ni inayoonekana na wazazi kwa watoto wao na pia kutoka kwa watoto kwa wazazi. Aina hii hutofautiana na ya urafiki kwani haizingatii kile mtu anachokutendea bali uhusiano wa kidamu na vile wazazi na watoto wao wanavyotegemeana. Sifa za binafsi hazizingatiwi hapa ili wazazi waonyeshe wanao hisia hizi. Uhusiano wao huchangia kwa mapenzi haya. Mapenzi haya huhusishwa na mtu kujiskia yuko huru na salama. Mapenzi ya Kujitolea(Agape) Aina hii ya mapenzi inazingatia asili, mapenzi kwa Mungu au miungu na mapenzi kwa usiowajua. Hii ni mapenzi ya kujitolea kwa ubinafsi ama mapenzi ya ubinadamu. Aina hii inahusishwa na kuto tarajia malipo au kitu chochote kwa matendo unayoyafanya. Yaani ni mapenzi yakujitolea mhanga. Aina hii ya mapenzi hutusaidia kuwapenda watu tusiowajua na kusaidiana kibinadamu kwa hali yoyote ile. Dunia yastahili kuwa na aina hii kwa wingi ili tukaweza kukaa kwa amani na furaha. Mapenzi kwa Mungu ama niungu pia huwa katika aina hii. Kumwabudu Mungu aliye binguni ni mfano mmoja wa kueleza aina hii. Mapenzi Changamfu (Ludus) Aina hii ya mapenzi ni mapenzi yasio na dhamira yoyote na ma mzaha tu. Mapenzi haya hayana masharti hata kidogo. Mfano wa aina hii ya mapenzi ni kama mtu anovyomtongoza mwingine, kupinga densi na kucheza. Aina hii ya mapenzi haina mambo mengi kwani huwa ni kawaida tu. Aina hii huwa sawa kwa watu wanaojitosheleza kimaisha. Aina hii ya mapenzi huwa gumu wakati mtu mmoja hufasiri kwamba mwingine ana hamu ya kimwili. Inafaa watu waweze kuelewa kama wanahamu zaidi na raha na kufurahi tu. Mapenzi Madhubuti(Pragma) Aina hii ni mapenzi ambayo yako na msingi wa wajibu wako kwa mwingine na wa kuzingatia maslahi ya mwingine ya siku za usoni. Mfano mwema ni kwa wapenzi ambao wako katika ndoa. Aina hii inahusishwa na uvumulivu na maelewano kati ya walio katika ndoa. Aina hii ya mapenzi hukuzwa kwa muda wa miaka kadha na ndio maana yaitwa madhubuti ya ka kudumu. Mvuto wa kimwili sana hauzingatiwi katika aina hii ya mapenzi bali kujengana kimawazo na kufanya maisha yao kuwa bora zaidi. Kinyume na aina zingine za mapenzi mapenzi madhubuti huzingatia pande zote mbili za wapenzi wawili. Lazima wewe wanapendana ama kuwa na mafikira na dhamira sawia. Mapenzi ya Kibinafsi (Philautia) Mapenzi haya ni ya mtu binafsi. Aina hii ya mapenzi huwa ina matokeo mawili, yaweza kuwa nzuri ama ya kudhuru. Upande mbaya wa aina hii huwa kwa ile hali ya ubinafi, kutafuta umaarufu na kutafuta utajiri na hufanya mtu kujiona ana dhamana kuliko mtu mwingine yeyote. Upande huu hufanya mtu akajiona yuko mkubwa kuliko mungu. Pia kuna upande mzuri wa aina hii ya mapenzi ambao inahusiana na mtu kujijua, kwa kufahamu uwezo wako na kujidhamini kwa uzuri wako na unachoweza kufanya. Kwa uhusiano wowote, huwezi kumpenda mwingine kama wewe mwenyewe hauna mapezi ya kibinafsi. Kwa kujipenda kwanza ndio tunaweza kupenda wengine na kuwatunza vizuri maishani. Aina hii ni muhimu sana kwa maisha ya kila mwanadamu. Mapenzi ya kibinafi humsaidia mtu kujua mazuri na mabaya na kupanga maisha yake kwa nji inayostahili. Mapenzi ya kibinafsi humwongezea mtu hali ya kujiamini na kujidhamini. Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi huweza kuelewana sana na watu wengi kwa vile kwa kujidhamini watu pia hukudhamini. Hii husaidia kwa vile mnaelewana na watu kazini, nyumbani na mahali pengine ambapo mnapatana. Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi hawahitaji kujigamba ili watu wawajue ama kujionyesha kwa watu. Uzuriwao hujionyesha kwa wanayofanya na wanavyoongea. Watu wanaojipenda kibinafsi huwa wako huru kwa mambo mapya na uwazi. Uchambuzi na ufahamu wa mapenzi ni nini husaidia kila mwanadamu kutambua aina gani anafaa kuwapa watu kwa kila wakati na aina gani ya mapenzi kutupilia mbali. Mwanadamu anaweza penda ila kwa hiari yake. Haina maana lazima mtu akupende ndio umpende nawe. Kila mwanadamu anauwezo wa kumpenda mwingine ama kitu anachotaka hata kama yeye mwenyewe hajapatiwa mapenzi hayo. Lazima kama mwanadamu kufanya mapenzi kama kitu cha kawaida kwa kila tunachofanya maishani. Iweke iwe sehemu ya maisha yako na utu wako. Pia ni muhimu kuwa na aina hizi zote za mapenzi kwa uhusiano kwa kila siku na watu wengine ilituweze kuishi maisha marefu. Kama binadamu, mapenzi ya muhimu sana ni yale ya kujitolea na yale ya kibinafsi. Unapokuwa na mapenzi yasiyo tarajia kitu chochote na mapenzi yako mwenyewe ndio utaweza kuwapa watu mapenzi hayo mengine. Tukiweza kushikilia aina zote zingine za mapenzi kwa mahusiano yetu basi tutakuwa na maisha marefu na yenye kufana. Mapenzi ni kitu muhimu maishani na ni sharti yaenziwe na kila mwanadamu. ... Read More
NJIA RAHISI 13 ZA KUWA NA FURAHA KILA SIKU  Mabadiliko yalio mepesi kwenye tabia zako za kila siku yatakuweka kwenye mstari wa furaha unayoitaka Umejikuta uko kwenye siku tofauti, story hizo hizo, imekuwa ni kawaida yako? Basi muda huu , sio kesho , sio wiki ijayo, ni wakati wa kubadilisha historia yako. ni za haraka, rahisi na hazina gharama unapofanya hivyo na matokeo yatakupa furaha unayoitaka. 1.Pata masaa 7 mpaka 8 ya kulala usiku. Kulala usingizi wa kutosha unapata furaha, utaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi zako , na utakuwa na mahusiano mazuri. weka simu yako mbali unapoenda kulala, usitumie chakula kingi wakati wa jioni. 2.Amka mapema , dakika 30 kabla . Kama wewe ni mfanya kazi wa kuajiriwa na una tabia ya kuchelewa kazini, jaribu kuamka mapema dakika 15 au 30 kila siku kwa ajili ya kujiandaa vizuri na kukumbuka vitu vyote vya kufanya, kuchukua siku hio. utaona tofauti ya tabia yako. 3.Meditate. Hii ni kubwa. meditate kwa muda wa dakika 10 au 20, utapata faida nyingi zaidi ya furaha, pamoja na kuwa muwazi, kuwa na malengo ya siku nzima. Anza siku yako na meditation. utajiepusha na tress na wasiwasi na hutachanganyikiwa na kazi zako. 4.Jipe nafasi wengi wetu huwa tunajaza vitu nyumbani, ofisini hata vile ambavyo havina kazi, hatuvitumii. inaharibu mfumo mzima wa akili yako, hisia zako, na mwili wako. Ondoa vitu ambavyo huvitumii, tupa nje au gawia watu ambao wanahitaji kuwa navyo, hali yako ya furaha itaboreka. Na hutalemewa na kazi nyingi. 5.Jifunze kitu kipya Jitahidi kujifunza kitu kipya kila siku, kwa sababu hio ndio changamoto itakayokupa furaha, kujifunza kitu kipya inaboresha afya yako ya mwili na akili, kujifunza utajenga ujasiri pia na utakuwa sharp. 6.Tembea mara kwa mara Kutembea kwa dakika 30 kwa siku moyo wako utakuwa unafanya kazi vizuri, utapunguza hasira, hutakuwa na chuki. Kama unaona ni ngumu kwako kutembea , hasa kama una gari , jifunze kupaki gari yako mahali mbali na ofisi , tembea . anza kutumia maji ya kutosha. utapata faida nyingi . 7.Usijihusishe na mambo ya mitandao. Ni rahisi kuingia instagram, facebook na zingine, lakini wachunguzi wanasema kwamba ukizidisha kujihusisha na mitandao unaweza kuharibu afya yako ya akili. badala ya kutumia nusu saa kwenye mitandao, unaweza kufanya kitu kingine unachokipenda, au kusoma kitabu, kujifunza mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiboresha mwenyewe kuwa mwenye afya. 8.Kuwa mwema. Ukarimu unakuongoza kwenye furaha yako mwenyewe na utakuwa mwenye afya bora. vitu ambavyo vinavyo chochea furaha ni kutoa , na kuwa mkweli , utapata faida , na utajisikia vizuri kuwa sehemu ya baraka kwa mtu fulani. kujitolea kufanya kitu, au kumwachia mtu kiti kwenye daladala. Sehemu ngumu? lakini nzuri. 9.Kaa na watu wenye furaha. Angalia watu unaoshinda nao, unaofanya nao kazi, ni watu wa aina gani. kwa sababu kuna msemo unasema kuwa ukikaa na ua rose utanukia hata kama ulikuwa hunukii. Fanya hivyo na utaweza kufungua mlango mpya kwa ajili yako maishani. utaiona furaha ikitiririka kama mto. 10.Don’t gossip. Kuseng’enya, umbeya, itakusababishia maradhi ya misongo na kukosa furaha. mtu mmbeya hawezi kusaidia kitu. wakati mwingine jitenge na watu kama hawa, au unapoona kuna kutoelewana na wafanya kazi wenzako, jaribu kutulia kwanza , badilisha negative to positive. Sema kitu kizuri kuhusu mtu. ni vizuri. kwa sababu utajiwekea alama nzuri kwako. 11.Tumia muda wako na watu unaowapenda Unapoongea na familia au marafiki kwenye simu , inatia moyo. mawasiliano hayo yanakupa afya na furaha.Fikiri ilivyo vizuri kama utaenda kula na rafiki yako mahali fulani, au kuamua kupika nyumbani , au kucheza na watoto wako kitu kama game, mpira, inafurahisha. 12.Journal Kuandika vitu vya kufanya kwa siku, au kuandika vitu unavyotaka kuvipata, Lengo hili dogo litaongeza IQ yako na kuleta utulivu wa kuboresha ujasiri wako, ukiwa na tabia hii kila siku , furaha haitakosekana kwako na utapata faida ya akili na hisia zako zitakuwa bora. 13.Jizoeze kujijali. Unapojijali ,Utaona faida zake, pamoja na kuondoa stress na wasiwasi, utakuwa mtu wa kuwaza mazuri na utaboresha immunity.pata muda kila siku kufanya kitu kwa ajili ya furaha, kama vile mazoezi, kupika chakula kizuri, kusoma . utaanza kushangaa jinsi ilivyo rahisi kuwa na furaha unapojijali na utaboresha akili yako na mwili wako, na roho yako. Kama unavyojua , kuna njia nyingi zinazotushambulia kwa siku, Ondoka mahali ambapo panaharibu ratiba yako. sasa, kama kitu kingine chochote,mafanikio ni kufanyia kazi. kwa hio pick one, and let the fun begin! ... Read More
Je Wajua Kwanini Wanawake Hula Vyakula vya Ajabu Ajabu Wakiwa Wajawazito?  Tabia hii inayojulikana kwa Kiingereza kama “Pica” inatokana na mtu kutamani kula vitu vyenye virutubisho kidogo sana au visivyo na virutubisho vya aina yoyote kwa mwili. Tamaa hizi huwa zinawapata watoto au mama mjamzito kutafuna vitu ambavyo kimsingi si chakula – kama udongo au chaki. Jina hili la pica ni aina ya ndege ambaye anajulikana kwakuwa anakula kitu chochote, hana anachochagua. Ni kweli kwamba wajawazito wengi hupata hamu ya kula vitu ambavyo si vyakula walivyozoea kula mara kwa mara wakiwa si wajawazito; wengi wao ni rahisi kuwaelewa kwa sababu hukimbilia mchele, barafu na vinginevyo ambavyo si vitu vibaya kula. Kwa watoto, hii ni tabia iliyozoelekakwakuwa inawatokea watoto wengi ambao ni kati ya asilimia 25 na 30% ya watoto wote; lakini kwa wanawake wajawazito, inatakiwa iwe kwa kiwango cha chini zaidi. Nini kinasababisha tabia hii kwa wajawazito? Sababu ya baadhi ya wanawake kuwa na tabia hii wakati wa ujauzito haijulikani hasa. Kwa sasa hakuna sababu maalumu, lakini kwa mujibu wa Jarida la Chama cha Watu Wanaoishi na Ugonjwa wa Kisukari nchini Marekani, tabia hii yawezekana ikasababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Baadhi wanadai kwamba hali hii inaashiria kwamba mwili unajaribu kupata vitamini na madini mengine yanayokosekana kwenye chakula cha kawaida ambacho mtu anakula. Muda wingine tabia hii yawezaikatokana na kuumwa viungo au akili kwa muda mrefu. Baadhi ya vitu vya ajabu ambavyo wajawazito hupenda kula Vitu vinavyopendwa zaidi na wajawazito wengi ni udongo, uchafu. Vitu vingine ni njiti za kiberiti zilizochomwa, mawe, mkaa, barafu, dawa ya meno, sabuni na mchanga. Mjamzito anapokula vitu hivi hujisikii raha kana kwamba amekula chakula chenye faida kubwa kwake na kwa mtoto aliye tumboni. Kuna hatari yoyote kwa mtoto aliye tumboni? Kula vitu ambavyo si vyakula kimsingi ni jambo linaloweza kusababisha madhara kwa mjamzito mwenyewe na mtoto aliye tumboni. Kula vitu hivi kunaweza kuharibu mfumo wa kawaida wa kunyonya virutubisho kutoka kwenye vyakula na kusababisha mwili wako upungukiwe na madini muhimu unayoyahitaji kwa afya yako na ya ukuaji wa mtoto vilevile. Tabia hii ni hatarishi sana kwakuwa vitu ambavyo si vyakula vinaweza kuwa na viambata ambavyo ni sumu au vyenye vijidudu vinavyoathiri mwili. Kudhibiti tabia hii Usihamaki unapojikuta unatamani vitu vya ajabu ajabu wakati wa ujauzito: inatokea sana na si jambo la kushangaza kwako pia. Jambo la muhimu ni kumjulisha muuguzi wako au wahudumu wa kliniki unayohudhuria kujua maendeleo yako ya mtoto tumboni ili akuelimishe na ahakikishe kwamba una uelewa kuhusu hatari zinazoambatana na tabia hiyo. Baadhi ya mbinu za kutumia kushinda tamaa hizo Mtaarifu mhudumu wako wa afya kwenye kliniki unayohudhuria na muangalie kumbukumbu za ukuaji wa mtoto tumboni pamoja na hali yako ya kiafyaFatilia kiwango chako cha madini ya chuma mwilini pamoja na kiwango cha vitamini na madini mengine unayotakiwa kulaOmba ushauri kuhusu kitu gani uwe unakula ili kubadili ili kuepuka vitu vya ajabu (waweza kumung’unya/ kutafuna vitu kama pipi au ‘big g’ isiyo na sukariMwambie hata rafiki yako mmoja kuhusu hamu hizi na umtake awe anakukataza unapokula vitu vya ajabu ... Read More
Zoezi lenye kuufanya uume usimame kwa muda mrefu na kuchelewa kukojoa wakati wa kufanya mapenzi  Misuli inayohusika na nguvu za kiume na kuwahi kumaliza wakati wa tendo la kufanya mapenzi huitwa ”puboccugeous Muscle” maarufu inajulikana kama Pelvic Muscle. Misuli hii inapokuwa dhaifu,uwezo wa kusimamisha uume kwa muda mrefu na kuchelewa kukojoa wakati wa kufanya mapenzi huwa mdogo. Zoezi lenye uwezo wa kuongeza nguvu ya misuli ya uume ,linaloweza kuufanya uume kusimama kwa muda mrefu,bila kusinyaa wala kuchoka,hili ni zoezi kama mfano wa zoezi lolote la kunyanyua vyuma vizito ambalo husaidia misuli kuinuka ,kukua na kuongezeka ukubwa na nguvu. ZOEZI LA KWANZA Wataalam wa mambo ya mapenzi wamethibitisha zoezi la misuli ya uume liitwalo ”physiotherapy”ndiyo hurudisha uwezo wa nguvu za kiume za asili,zoezi hili halina madahara yoyote kiafya na linaweza kufanyika wakati wowote. JINSI YA KUFANYA ZOEZI HILI Ukiwa umekaa popote fanya zoezi hili asubuhi na jioni na hali ya kuwa hauna mkojo kabisa(yaani kojoa kwanza) Ukiwa umekaa anza kujibinya kama mtu aliyebanwa na mkojo halafu choo kipo mbali,bana ili mkojo usikutoke kwa kukaza misuli hiyo ya sehemu nyeti,fanya mara 20>25 asubuhi na jioni kila unavyobana hesabu 3 mpaka 5 kisha unaachia,unabana tena hivyo hivyo. Endelea na zoezi hilo kiasi cha wiki,baada ya wiki mbili ongeza ubanaji zaidi kutoka mara 20 mpaka 70. Endelea kufanya zoezi hili kwa wiki 6 na matokeo mazuri huanza kuonekana wiki ya 4 mpaka 6 FAIDA YA ZOEZI HILI 1.Husaidia mzunguko wa damu kuingia kwenye uume na kuufanya uume utanuke na kuwa mgumu zaidi 2. Misuli ya uume itakuwa imara na kuweza kuzuia shahawa na hivyo kukuwezesha kumridhisha mwenza wako kila mara 3. Litakuwezesha kujibana kila unapotaka kukojoa huwapo kwenye tendo la ndoa(usingoje mpaka utamu umezidi utashindwa)jibane kama unajizuia kukojoa mkojo wa kawaida lakini usikate kiuno wakati mwenzio anaendelea kutingisha nyonga. Ikiwezekana hata fikra za utamu huo zihamishe kwa sekunde kadhaa mpaka hali hiyo ya kutaka kukojoa ikiondoka zirudishe fikra ili kuendelea na mwenzio kwa pamoja katika game hilo la kiutu uzima. Kasi iendelee na utaendelea hivyo mpaka uhakikishe mwenzio amekojoa ,na anaweza kukojoa hata mara 3,yaani ukiridhika kuwa mwenzio ameridhika au ukiskia ile sauti “”inatoosha” ndyo sasa nawe ukojoe hapo mwenzio atapata raha zaidi. ZOEZI LA PILI Uinue juu na kuushusha uume wako,uchezeshe juu chini,chini juu mara 5 mpaka 10,fanya mara mbili tatu huku unapumzika kidogo,uwe unaminyaminya kidogo wakati huohuo unavuta hewa kwa pua na kuitoa kwa mdomo. fanya zoezi hili mara kwa mara japo mara 3 kwa wiki linaweza kukusaidia kuimarisha misuli yako ya uume. ZOEZI LA TATU Ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara huimarisha moyo,ubongo na misuli ya uume ,wanasayansi wamelithibitisha hili kuwa ufanyaji wa mara kwa mara husaidia uume kupata nguvu(zipo tofauti kati ya uwezo wa mwanamme mwenye mke mmoja na mwenye wake wengi) Mwenye wake wengi anaongeza nguvu zaidi, Mwenyez Mungu anataka wanaume wa kiislam waimarishe misuli hii kwa kutoa fursa ya kufanya tendo la ndoa mara kwa mara pale alipowaamrisha waoe kuanzia wake wawili mpaka wanne wakiweza. Kadri unavyoongeza mke ndivyo unavyojiongezea uwezo kwa aliyeoa wake wawili na zaidi,pima uwezo uliokuwa nao ulipokuwa na mke mmoja kisha zitazame nguvu hizo baada ya kuongeza mke wa pili watatu na wanne Ndiyo maana utakuta mtu mwenye wake wawili akifiwa na mmoja huongeza mke ili kuziba pengo hilo. ... Read More
Mbinu Tata Za Kumfanya Mwanamke Ajigonge Kwako Kirahisi  #1 Mfanye mwanamke ajieleze kwako Unaweza kumuuliza swali kama “Ni kitu gani ambacho kinakufanya unique/tofauti na wengine?” Ama kumwambia, “Wewe unakaa mdogo sana kiumri kwangu. Ni kitu gani ambacho uko nacho ambacho kitaziba pengo hilo?” Ataanza kukupatia sababu ambazo anajiona kuwa yeye ni unique – kiufupi atakuwa akijaribu kujieleza zaidi ili ajipendekeze kwako/ umpende zaidi. Yaani atakuwa anajaribu kuhakikisha kuwa unaridhika na kila kitu ambacho atakwambia. Na uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa kadri mwanamke anavyokuwa mrembo ndivyo zaidi utakavyohitajika kumfanya ajihitimishe kwako, usiogope kumuuliza maswali ambayo yatamlazimu ajihitimize kwako. Muulize maswali mazito. Muulize maswali ambayo itakuwa ngumu kwake kujihitimu kwako. Na kitu cha kufurahisha kuhusu wanawake warembo, ni kuwa wamezoea kufukuziwa na wanaume kiasi cha kuwa ukianza kuuliza maswali na kujihitimu kwako, atafall na wewe zaidi. Hii ni kwa sababu hawajazoea kuulizwa maswali kama hayo. Hawajazoea kuambiwa, “Wewe si mwanamke type yangu.” ama, “Ningekutongoza lakini unanikumbusha ndugu yangu wa kike mdogo.” Pia unapaswa kuhitimisha wanawake kulingana na ladha yako. Labda kwa mfano hupendi wanawake wanaovuta sigara, kunywa pombe nk, basi mhitimishe kwa kutumia mambo haya. Usimfiche. Mwambie ukweli. Kumwambia mambo kama haya kutamfanya ajue vigezo vyako. Unampa challenge na yeye kutaka kutimiza vigezo vyako. Mbinu hii ni rahisi ya kumuwin kirahisi na kumfanya akufukuzie. #2 Tumia Mwili wako Mara ya kwanza unapoongea na mwanamke huwa anaangalia kando. Wewe ndie uko wazi, unaongea na yeye, unamwangalia, lakini yeye ameangalia kando kabisa. Hapo kuna ile hisia ambayo inakuja ndani yako kuwa huyu mwanamke hamakiniki na wewe kabisa. Well, hapa ndipo unatumia mbinu funge ya kuiga vile ambavyo anafanya yeye. Wakati umemuapproach, si lazima umuangalie mzima mzima kwanza, unaweza kuangalia kiupande. Na akiongea kitu ambacho umependezwa nacho, unaweza kutumia mwondoko wazi kwa kuangalia upande wake. Na akisema kitu ambacho hujapenda basi tumia mwondoko funge kwa kuangalia kando. Mbinu hii hufanya kazi kwa kuchukua atenshen na umakinifu wa mwanamke. Atamakinika kwa kila neno ambalo atakwambia. Mwishowe itajeuka kuwa ni yeye ndiye anayekufukuzia na wala si wewe. Mbinu hii pia inampa confidence ya kutamka mambo ambayo si rahisi kutamkwa na mwanamke hivihivi. #3 Ongea Kwa Kujiamini na Amri Ndani yake Katu mwanamke hawezi kukufukuzia kama utatumia toni saidizi kama, “Mambo waendeleaje?” ambapo sentensi kama hii toni ya sauti inapanda mwishoni. Kama vile unauliza swali. Matumizi ya sentensi hizi zitakufanya uonekane mtu mdhaifu, mhitaji, na utafanya wanawake wakukimbie. Lakini ukitumia toni saidizi zilizovunjwa kwa mwanamke kama, “Hey! Njoo hapa! Waendeleaje!” unatoa sauti ya kuamrisha na ya kutoa maelekezo. Na kwa kuwa uasili wa mwanamke ni kufuata amri, atakujibu kwa kutafuta toni saidizi ili aweze kujihitimisha kwako. Atakwambia, “Mmh, jina langu ni Mamito?” huku akitaka umthibitishe. So, ukimwambia, “Sasa, mpangilio wako ni upi!? kwa toni saidizi iliyovunjwa, atakujibu... “Mmh, mimi mwanafunzi nasomea...huu ni mwaka wangu wa...” Kiufupi hapa anajaribu kujieleza zaidi kwako kulingana na vile sauti yako ilivyotoka. [Soma: Jinsi ya kuwa mwanaume bora ya wote] #4 Weka nafasi na Pozi Katika Maongezi yako Unapoongea na mwanamke, hutaki kuona umepalilia maongezi bila mpangilio, badala yake huwa unataka nafasi angalau kurudi nyuma kiasi kuyapa maongezi yenu nafasi ya kupumua. Unaruhusu kuwe na angalau kimya ndani yake. Kimya ambacho kinaenda polepole. Na nafasi ambayo utampa mwanamke nafasi ya kujileta kwako ili kuteka atenshen yako. So mpe mwanamke nafasi ya kujiekeza kwako, na utagundua kuwa mwanamke huyu anakusaidia pakubwa kuyafanya maongezi yenu yanawiri. Atafurahi kukupa namba yake ya simu kwa kuwa anakufukuzia. Atafurahi kukutana na wewe katika deti ya pili. Na hatakutatiza zile nyakati za mwisho mwisho za kumuomba penzi. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: