CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SITA (06) ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO: Siku ya pili, vicent alitoka mapema nyumbani, aliwahi shule kabla hata ya rafiki zake. Hii yote ni kutokana hata usingizi haukupatikana,kutokana na mawazo aliyo nayo. Alikuta baadhi ya wanafunzi wapo darasani, Alifika akakaa kwenye kiti na kufungua begi,kuchukua kitabu na kuanza kusoma. Ila hata sijui nini kilimtuma kutazama mbele maaana alijikuta anatoa macho. ENDELEA....... Alijikuta Anatoa macho, baada ya kuona,marafiki zake nao wamewahi shule. Aiseeee vicent alichekaaaa sana, mpka akajishika tumbo. "hadi nyinyi mmewahi leo aaah kweli mtihani siyo poa".aliongea vicent huku anawatazama kwa zamu. "mimi mwenyewe sijaamini nilivyo kuona ndo maana nikasimama mlangoni nihakikishe ni wewe au hahhhhhah".aliongea Richard huku anaelekea kule alipo vicent.ila cha kushangaza suma akuchangia neno zaidi ya kuachia tabasamu na kutembea kwenda walipokuwa wenzake. "aiseeee kama tuliambizana yani"aliongea tena vicent. Hapo suma ndo na yeye akanyanyua,mdomo wake na kuongea. " hivi unajua kwanini nimeshindwa kuongea chochote?,nikwasababu naona uchuro hapo nje nimekutana na rich, hapa nakuona wewe, nikawa najiuliza hivi hawa waliambizana nini mimi wamenichunia ila nimewabamba".aliongea suma,huvu anavuta kiti anakaa. "hii ili iweje sasa imetokea tu"alijibu richard. "sisi hatuwezi kukufanyia hivyo kwasababu sote ni wamoja". Alisema vicent, suma hakuwa na neno. " oyaa tusomeni basi kabla muda wa kwenda mstalini aujafika"aliongea tena vicent. "poa mwanangu umeongea point" alijibu suma.basi kikapita kimyaa,kila mtu alifanya yakeee kwa muda huo. ******* Mwezi ulipita,hatimae miezi, na si vicent, wala niram aliye kumbuka kama walishawahi kuonana. Basi ilikuwa weekend, moja walionekana marafiki, watatu wakiwa wamesimama stendi ya mabasi,si wengine bali ni vicent, richard na suma wakiwa wamevalia nguo za nyumbani.ilibaki kama wiki mbili wafanye mtihani. Ilionyesha kuwa walikuwa wamelewa kwenye maongezi sasa sijui vicent, walikuwa wanasubiri usafiri maana vicent hakuwa na gari siku hiyo. Mara gaflaa walishtushwa na sauti, nyororo iliotokea,barabarani. "vicentiiiiiiiiiiiii" ilikuwa sauti ya niramu, aliekuwa ndani ya range nyekundu, huku akiwa amependa,kupindukia wanasemaga kadamshi, ile mbayaaaa. Wote macho yalikuwa mbele,ila hakuna mtu alieshtuka kama vicent, maana akutegemea kuonana na binti yule ana muwaza siku zote. Na ilikuwa muda Awajaonana. Kiukweli vicent, moyo ulikuwa unampenda mbio vibaya.ila alijikaza, huku nyuma suma pamoja na richard, aisee!! Macho yaliwatoka maana walishindwa kuelewa, wanae muona machoni mwao, ni jini au malaika. Vicent alijikongoja mpaka kwenye dirisha la gari, na kumsababishia niram. " mambo niram siamini kama ni wewe, kumbe unani nakumbuka? ".alijikuta anaongea mfululizo vicent huku akiuliza, swali humohumo. "poa vicent, nakukumbuka sana vp leo huna usafiri? Maana naona kama mpo wenyewe mnasubiri usafiri? ".aliuliza niram,huku macho akiwaelekezea wakina rich. "aaah ndiyo tunamsubiri dereva tax mmoja hivi,katuambia hayupo mbali".alijibu vicent huko akiangalia huku na kule kama anaetafuta kitu. "haah kwani mnaelekea wapili niwape lifti?maana mimi naelekea mbezi"aliuliza niram. Vicent akapiga mahesabu ya haraka,alafu akaongea. "aaah! Wale wanarudi nyuma ila mimi naenda kunduchi" alijibu vicent. Ila wadau ngoja niwaambie kitu, vicent ameongopa, kwasababu wenzie wanaenda kawe sawa yeye anaenda kunduchi, ila njia ni ileile wameachwa wakina suma, yeye angeendelea mbele, ila aliamua kusema vile ili aweze, kutupa ndoano Kiulaini. Tuendelee, basi niram akamwambia "basi twende nikupe lifti waage wenzio".vicent akachomoka na kuwafata, wenzie alimkuta suma anashauku si mchezo. " vipi yule ndo yule demu uliesema? Na anaelekea wapi ili atupe lift basi kama vipi" alijikuta anaongea maneno,mfululizo na swali juu. "hamna aendi huko kaniambia nimsindikize kariakoo".aliongea vicent huku anageuka nyuma, akagongana macho na niram,wote wakatabasamu. "duuuh mwana kwahiyo umetuacha? ".aliongea richard huku anakazia macho kwenye gari. "aaah aina jinsi ila chukueni hii mpande tax".alisema vicent huku anazamisha mkono mfukoni na kutoa noti tatu za elfu kumi akamkabidhi suma. Suma alizichukua na kuzitia mfukoni. "oyaaa Usikose kutupigia ukifika home"alisema rich. Na suma akadakia. "ndiyo utupe data zote maana duuuh! Mpaka nakuonea wivu".vicent hakutia neno aliishia kutabasamu huku Anaendelea kutembea, basi aliingia ndani ya gari, huku ukimya mwingi ulitawala.vicent akaona avunje ukimya, "basi nilijua utanisahau kabisa".aliongea Vicent Huku ametoa tabasamu hafifu usoni mwake, Huku macho yanatazama mbele. "Ooooh!!Hapana siwezi kukusahau,mtu muhimu Kama wewe Kwa ule Msaada wako ".aliongea Niram,huku anamwangalia Vicent, macho yakakutana, wote wakatabasamu, Niram akageuka mbele na kuendelea, kuushika usukani akizidi kukanyaga mafuta. "hahhhhah!! Ni kweli niram lakini Siyo wote wanao kumbuka fadhila".aliongea Vicent ,Huku kimoyomoyo akiomba wasifike haraka. "haaahhh sawa bwana Wala ujaongopa, ".aliongea niram,huku akizidi kuuchapa mwendo, na bahati nzuri hakukuwa na foleni. "niram nikuombe kitu Kama hutojali? ".aliuliza Vicent Huku amemgeukia kabisa, aliongea Kwa sauti nzito, tens yakubembeleza. "usijali Kama kipo Ndani ya uwezo wangu ntakupa".alijibu niram. Vicent hakaona asizubae Sana, akasema alilokusudia."nilikuwa naomba unisaidie namba yako ya simu ili niwe nawasiliana nawe hata kukujulia Hali,maana tushakuwa marafiki".aliongea Vicent,kwa umakini wa hali ya juu ili asije kukosea step,akamkwaza Niram. " Ooooh!! Wala usijali Kwa hilo".alisema niram, huku anamtajia namba zake. Vicent aliziandika kwenye simu yake. " asante sana".alishukuru vicent. "asante nawe kwa kushukuru".alijibu niram, mara ikawa kama vituo viwili vicent ashuke. "sasa niram mie nashuka hapo kituo kinachofuata utaniacha hapo" aliongea vicent, lakini kama ungemuona moyoni mwake, alichukia kupita kiasi, alitamani wazunguke mpaka alfajiri. Duuuuh kweli mapenzi siyo poa wadau. "haaah ni hapo oky sawa"alijibu niram, na alipofika, akakanyaga break, na kusimamamisha gari. "oooh!!asante sana umenifaa mungu akufikishe salama".aliongea vicent huku anafungua mlango wa gari na kushuka. "haya asante ufike salama pia".alijibu niram, akawasha gari na kuishia, vicent alibaki anampungia mkono, mpaka alipo ishia. Kiukweli ile siku aliiona ya bahati sana kwake, hakika alikuwa na furaha mno. Alifika kwao. Akagonga geti likafunguliwa, alikuta mlinzi akamsalimu, na kuingia ndani hakumkuta yeyote ndani zaidi ya house girl. Alimsalimia akajitupa kitandaniii , pwaaaaaaah!! Aliangalia sana juu vicent, hakika kuwa na namba ya niram,kwake ilikuwa ni furaha tupu. ********* Vanessa alikuwa mezani wakipata chakula cha usiku, maana leo ilikuwa weekend kwahiyooo alikuwa mwenyewe jikoni, ila leo mawazo yalipungua kwani mawasiliano yalikuwa kama zamani na hadi asubuhi ya siku hiyo, vicent alimuaga kuwa atatoka na wakina richard. Mara ghafla alishtukia, akizibwa macho. "mmmh juliana nini bwana,ebu acha mzaha njoo ule"aliongea vanessa. " mmmh dada kwahiyo wewe mtu wako wa karibu ni Vanessa tu? ".aliuliza kwa manung'uniko Clara. Mdogo wake wa nne akitoka huyo ndo juliana, kumbuka wakiume ni wawili kwenye familia yao na ndio wakwanza na wapili. "hamna mamy wote nawapenda ila nilijua yeye, kaa chini ule mdogo wangu".aliongea Vanessa kwa sauti ya kubembeleza,huku akimvuta akae. Basi mambo yakaisha,walikula kwa furaha, wazazi na kaka zao hawakuwepo, walibaki wenyewe. ********* Niram alikuwa chumbani kwake akijisomea, wakati huo alikuwa ameshakula, alikuwa kitandani miguu kuegemeza ukutani, muda wote alikuwa mtu mwenye tabasamu usoni, kilicho mfurahisha akijulikani Mara ghafla simu ikaanza kuita...... Itaendelea CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SABA (07) ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: Niram alikuwa chumbani kwake akijisomea, wakati huo alikuwa ameshakula, alikuwa kitandani miguu kuegemeza ukutani, muda wote alikuwa mtu mwenye tabasamu usoni, kilicho mfurahisha akijulikani Mara ghafla simu ikaanza kuita. endelea........ Mara gafla akaona simu inaanza kuita. Niram akaangalia mpigaji, akaona namba ngeni. " mmh! Atakuwa Nani huyu?".alijiuliza niram, alitafakari Sana maana sikawaida kupigiwa na namba ngeni, baada ya kutafakari kwa muda.akaamua kupokea. "hellow".aliitika niram. "hallow Niram huko poa?, Vicent hapa". Ilisikika sauti upande wa pili."oooh! Vicent nashukuru mungu niko poa sijui wewe ulifika salama? ".alijibu niram nakupachika swali. "nilifika salama niram hofu ilikuwa kwako".alisema vicent. "namimi nashukuru mungu nimefika salama".alijibu niram kwa sauti nyororo kabisa. ****** Vanessa alikuwa ndani kwake akaona mbona muda unaenda sana,na ajaona msg wala simu kupigwa kutoka kwa vicent. Alikaa akasubiri na kusubiri weeeeh lakini ikawa kimya. "mmmh!! Ina maana itakuwa ajarudi bado huko alipoenda"alijisemea mwenyewe, akaona muda unaenda lakini simu aipigwi. "mmh ngoja nipige"aliamua apige yeye, akachukua simu yake na kuipiga. Jibu alilokutana nalo ni NAMBA UNAYOPIGA INATUMIKA KWA SASA.. "mmmh saa tano hii au ndo amerudi hivyo anaongea na wenzie kuwa julisha kuwa amerudi?".alijiuliza jibu akakubaliana kuwa anawasiliana na rafiki zake. ****** Huku vicent akiwa anaongea, akaona kama kuna mlio wa simu nyengine kuingia akaiangalia , alipoona mpigaji kuwa ni Vanessa akaendelea kuongea. Simu iliita mpka ikakata. Waliongea mengi na baadae niram akaaga kuwa anahitaji kupumzika. Basi waliagana na simu ikakatwa. Baada ya hapo alipiga simu kwa Vanessa,huku Akiwa ameshaupanga uongo wa kumwambia. "hellow baby mbona kimya, na napiga unatumika?".aliongea vanessa mara baada ya kupokea simu. "aaah amna nilikuwa naongea na mzee maana mchana,hakuwa na nafasi ndo kunitafuta sasahivi".alijibu vicent kwa ujasiri wa hali ya juu,bila kubabaisha maneno. "oooh kumbe haya niambie mizunguko ilikuwaje? ".Aliuliza Vanessa huku alibadili mikao ya kila aina Hapo kitandani. "ilikuwa poa sema nimechoka sana".alijibu vicent huku akijifanya anapiga mihayo. "oooh basi pumnzika baba angu tutaongea kesho".aliongea Vanessa kwasauti fulani hivi ya madeko. "sawa mama ntakuchek kesho ulale salama"alimaliza kuongea vicent akakata simu. Alienda moja kwa moja bafuni akaoga, maana choo kilikuwa ndani kwake humohumo. Alipomaliza alitoka sebleni muda ulikuwa umeenea sana ila alikuwa bado ajala, alikuta msichana ameshaenda kulala,aliwasha taa ya sebuleni akachukua sahani jikoni nakuenda kula chakula. Mara ghafla akasikia mlango unafunguliwa alikuwa mama yake, "yani wewe Bwana mi nilivyorudi nikaambiwa upo ndani nikajua ushakula".aliongea mama yake vicent,huku anavuta kiti pale sehemu ya kulia chakula akakaa. "hapana mama uwezi amini yani nilipitiwa na usingizi nikalala ndo nimeshtuka sasa hivi".aliongopa vicent, aisee huyu jamaa hatari."ooooh pole baba ni uchovu tu huo"aliongea kwa huruma mama yake. "asante mama".alijibu vicent huku anafakamia wali kwa maini. Basi waliongea mengi mama mtu alinyanyuka, na kuenda kulala. "ukimaliza usisahau kuzima taa baba".aliongea mama yake. "sawa mama ntaizima".vicent alikula akashushia juisi, akaelekea kwenye swichi akazima taa na kuenda kulala. ******* Pilikapilika zilikuwa zinaendelea, katika nyumba ya kina niram.ilikuwa Jumapili kulikuwa na ugeni mkubwa kwao, kuna ndugu zao walikuja.basi yalipikwa masontojoo siyo ya kawaida. Zilisagwa juisi za matunda basi ilikuwa tafrani. Niram akutulia alikuwa bize vibaya. "niram ebu kuongezeae chumvi kwenye biriani kule".ilikuwa sauti ya mama yake. "sawa mama".alijibu huku anaacha alichokuwa anafanya na kwenda kuweka chumvi kwenye chakula. Kila kitu kilikuwa sawa sasa niram alikuwa chumbani anajiandaa akaoge. ******** Suma alipoona ajapigiwa jana, akaona isiwe kesi ngoja amchek yeye maana umbea ulikuwa unamuwasha mtoto wa kiume huyu. Akukubali kitu kimpite hivihivi,yani alikuwa tofauti na richard mwenzie hakuwa mpenda kufuatilia yasiyo muhusu. Basi aliweka vocha akampigia "oyaaa mwanangu unayumba"haliongea suma ."hamna nilichoka sana yani uwezi amini ".alijibu vicent. "eeeh ilikuwaje jana na yule mtoto mzuri?".aliongea suma huku akitegesha masikio vizuri kupata udaku "hahhhhah suma eeh nna kazi kama unataka kuhusu hiyo stori ntakupigia baadae " "ok poa basi usisahau ".alijibu suma huku anakata simu. Ila suma akakumbuka kitu ayaaaaaah!! Daaah!!.Nimesahau kumuuliza Kitu, yeye na haraka zake mpaka nimesahau".aliongea suma huku anamlaumu vicent,kwa uamuzi wa kukata simu haraka. "anyway nitamchek baadae".aliongea suma, mara kisimu chake kikaanza kuita."duuuh huyu somoe ana mpya gani nae mi leo nnampango wa kuonana na hadijaa".alijiseme suma kimoyomoyo ,huku anaangalia ile simu bila kuipokea. Labda niwafafanulie vijitabia vya huyu ismail au kwa ufupi ndo unaweza kumuita suma. Yani suma yupo tofauti na wenzake, suma kwanza ni mwingi wa habari,anapenda kujua mambo ya watu ni mwongeaji mno kuliko wenzake.ajatulia hata kidogo isimpitie sketi mbele yake lazima amfate tu, ila richard na vicent wapo tofauti sana na yeye, richard ana mahusiano na binti mmoja anasoma, shule tofauti na yao. Na ni huyohuyo tu ndo yupo nae. Lakini suma weeeeeeh!! Mwiko mkubwa tena uchuro, kutulia na mwanamke mmoja. Basi baada ya simu kukata akaizima na kuendelea na mambo mengine. ******* Ilikuwa ni mida ya jioni. Wageni wameshaondoka, nyumbani kwa kina niram. Na mama yake kama unavyomjua mtu wa pilikapilika usiseme, alikuwa ameshaenda kuzurura muda mrefu. Aaaaah ahhh!!,sijui muhindi gani huyu mwenye tabia za Kiswahili.ok tuachane nae tuendelee. Basi niram alikuwa amekaa sebuleni peke yake, maana mdada wa kazi hupendelea kukaa ndani kwake kama kazi ameshazimaliza. Basi alijikuta mpweke sana na alijikuta anatamani, kuongea na vicent,ili apate kampani na kupoteza muda kidogo. Hata sijui ni kwanini alimuwaza vicent kuwa ndio mtu pekee wa kumtoa upweke. Hata mimi sijui,ila tutajua hivi karibuni. Basi aliingalia simu kwa muda nakujifikiria ampigie au atulie asimpigie. Basi nafsi ya niram ikawa inashindana,moja inamwambia piga nyengine, inamwambia usipige ila akiwa katika mgongano wa kutoa maamuzi nini afanye, gafla akaona kitu moyo ukapiga paaaaah!!! .alishindwa kuamini alichokiita. Itaendelea....

at 10:36 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top