Story...... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na tatu (13) Ilipoishia....... Mzee Joel ndio hakuamini baada ya kuingia ndani na kukuta vijana wote wamelazwa chini alafu kidogo hivi akatokeza Nolan akiwa amepigilia suti nyeusi Kisha akamwambia baba yake ambaye ni mzee Joel, "naenda kwenye kikao cha harusi ya Penina na Frank na kama utahitaji kadi unijulishe nikuletee ya kwako." ***********Endelea ********* Nolan baada ya kumuambia baba yake maneno hayo aliingia kwenye gari na kuondoka. Nolan alifikia sehemu ambayo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kutengeneza kadi za harusi. Nolan alitengeneza kadi za harusi zisizopungua Mia moja hamsini kwa ajili ya harusi ya Penina na Frank. Kadi hizo hazikuwa za kuchangia harusi ya Frank na Penina bali kadi za mualiko. Nolan alijipanga kusimamia kila kitu Katika harusi ya Penina na Frank hivyo yeye alitengeneza kadi ambazo ni kama kiingilio cha kuhudhuria harusi hiyo bila kuchangia chochote. Nolan baada ya kukamilisha zoezi la kutengeneza kadi zile akaanza kutafuta ukumbi Mkubwa wenye hadhi ya kufanyia sherehe ya harusi ya Frank na Penina. Nolan alifanikiwa kuupata ukumbii ambao aliuhitaji na baada ya hapo Nolan akaanza kuzigawa kadi zile kwa watu mbali mbali ikiwemo na marafiki pia. Nolan moja kwa moja aliwasili nyumbani kwa kina Frank na kuwakuta Wazazi wake Frank ambao walimpokea kwa furaha Sana. "kikubwa kilichonileta hapa ni kuhusu harusi ya mtoto wenu Frank pamoja na mdogo wangu Penina, napenda kuwaafahamisha kuwa taratibu za harusi ya ndugu zetu hawa inaendelea vizuri na hapa nimewaletea kadi za mualiko." alianza kuongea Nolan baada ya kukaribishwa ndani na Wazazi wake Frank huku akiwakabidhi kadi zile Wazazi wake Frank. "Asante Sana kijana wetu na hongera Sana kwa hapa ulipofikia Mungu azidi kukusimamia zaidi na zaidi." wakaongea Wazazi wake Frank huku wakimshukuru Sana Nolan. "msijali Sana hii kazi ilikuwa lazima niifanye na lazima nitaitimiza, na kingine ninachotaka kukifanya kwa Sasa nataka niwahamishe hapa nyumbani kwenu niwapelekee sehemu mkakae hapo kwa siku kadhaa mpaka pale harusi ya mtoto wenu itakapokamilika, nafanya hivi kwa sababu ya usalama wenu kwasababu kuna vita kubwa inaendelea. " akaongea Nolan na kutoa maelezo hayo ambayo Wazazi wake Frank walikubaliana nayo bila wasi wasi wowote. Wazazi wake Frank pamoja na Mdogo wake Frank walijiandaa na kuondoka na Nolan ambaye aliwapeleka Katika hotel moja iliyopo nje kidogo ya jiji la dar es salam na kuwataka wakae hapo kwa wiki tatu kabla ya harusi ya Frank na Penina na gharama zote atazisimamia yeye Nolan. Nolan baada ya hapo alishika njia ya kurudi nyumbani kwa ajili ya kwenda kupumzika kidogo. * Dickson aliwasili Tanzania kwa Mara nyingine tena Ila awamu hii alikuwa na vijana wake wanne alioongozana nao. Baada ya kuwasili uwanja wa ndege moja kwa moja Dickson pamoja na vijana wake walichukua gari ndogo na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mzee Joel.* Mzee Joel alizidi kuchanganyikiwa baada ya kumaliza siku ya pili Sasa bila kumuona Penina na wala hajui ni wapi Penina alipo. Jambo hilo lilimvuruga Sana mzee Joel na kumfanya ashindwe hata kula chakula anachopikiwa na mkewe. Mzee Joel pia aliweza kuwasiliana na mkuu wa kikosi cha the killer na kumueleza jinsi vijana wake walivyoshindwa kuifanya kazi waliyoagizwa na kujikuta wakipokea kichapo kikali kutoka kwa Nolan. Mkuu yule wa kikosi cha the killer aliyejulikana kwa Jina la buffalo alipigwa na butwaa baada ya kupewa taarifa zile na mzee Joel. buffalo hajawahi kuamini kama kuna mtu yoyote anayeweza kupambana na vijana wake na akawaweza, hivyo taarifa zile zilimshangaza Sana. Buffalo akaamua ni lazima amjue huyo kijana ni nani aliyeweza kuwatandika vijana wake. "mzee hiyo kazi niachie mimi nitapambana nae mwanzo mwisho." akaongea buffalo kumwambia mzee Joel. Mzee Joel aliweza kumuelewa buffalo na kukataa simu na kumsubiri buffalo aingie kazini mwenyewe kwasababu yeye ndio mtu pekee Sasa aliyebaki wa kumtegemea. Dakika chache baada ya mzee Joel kuongea na buffalo, mzee Joel alipata taarifa kuwa kuna wageni nje wanahitaji kuonana na yeye. Mzee Joel alitoa ruhusa wageni hao wakaribishwe ndani. Kitendo bila kuchelewa wageni wale walifunguliwa geti na kukaribishwa mpaka ndani. Mzee Joel alishtuka baada ya kuona ugeni wenyewe ni wa Dickson pamoja na vijana wake wanne. "karibuni karibuni Sana." akaongea mzee Joel huku akijaribu kujichekesha japo hakuwa na amani hata kidogo. "hatuna haja ya kukaa mzee Joel, tumekuja kumchukua Penina nataka kujua kama inawezekana au haiwezekani?" akauliza Dick huku akionesha dhahiri kupandwa na hasira. "inawezekana kijana wangu tafadhali kaeni kidogo bas." akaongea mzee Joel kwa upole. "nimeshakuambia hatuna haja ya kukaa sisi tumekuja kumchukia Penina tu." akaongea Dick kwa msisitizo. "kijana wangu Dick naomba nipe muda wa siku mbili tu nitakuwa tayari nimeshakamilisha hili swala." akaongea mzee Joel kuwaambia wakina Dick. "Mzee umenipotezea Muda na umekula pesa zangu nyingi Sana, Sasa naondoka na kesho nitarudi unikabidhi Penina la sivyo pesa zangu utarudisha na utalipa Muda wangu nilioupoteza kwa ajili yako." akaongea Dick kwa jazba na kuondoka pamoja na vijana wake na kumuacha mzee Joel akitokwa na jasho jembamba. Baada ya dakika chache wakina Dick kuondoka Nolan naye aliwasili nyumbani na kumkuta baba yake akiwa na mawazo tele huku pembeni akiwa chupa ya pombe kali. "Baba shikamoo" akasilimia Nolan lakini alijua baba yake hataitikia salamu yake. Mzee Joel kweli hakuitikia salamu ya Nolan alibaki akimtizama tu kwa hasira. Nolan naye hakujali alitoa kadi tano za harusi ya Penina na Frank na kumwekea baba yake kwenye Meza iliyokuwa mbele yake. "karibu Sana Katika harusi ya Penina na mpenzi wake wa Muda mrefu Frank, wewe pamoja na rafiki Zako mnakaribishwa. " Nolan ndio alimwambia baba yake mzee Joel baada ya kumuwekea kadi zile kwenye Meza iliyokuwa mbele yake, Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake. ............ Itaendelea

at 6:48 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top