Story - - - - - NI WEWE TU PENINA. BY GIVAN IVAN PHONE & WHATSAPP____0769673145 Karibuni tuianze story yetu hii mpya yenye kusisimua iliyojaa visa mbali mbali kuhusu mapenzi. Sehemu ya kwanza (1) Mapenzi ya vijana wawili walionza kupendana toka wakiwa wadogo mpaka Sasa wakiwa na umri wa miaka 25 kila mmoja, yalikuwa yakizidi kukolea kila siku na kuwa matamu zaidi na zaidi. Vijana Hawa ni Frank pamoja na Penina. "nahisi kuvurugwa nahisi kufa kufa yaani najiona kama napepea juu juu kwa jinsi navyompenda mpenzi wangu Penina." alikuwa frank akiongea maneno hayo mbele ya wazazi wake pamoja na mdogo wake Wa kike aitwaye Angel. "na siku si nyingi utakuwa chizi wewe sio kwa kupenda huko kaka yangu." akaongea Angel kumuambia Frank. "acha niwe chizi tu mdogo wangu, lakini sio chizi wa kutembea uchi barabarani bali chizi wa kupenda." akaongea Frank maneno hayo na kuwafanya wazazi wake wacheke sana. "lakini mwanangu Sasa inabidi mfanye taratibu mfunge ndoa Sasa." aliongea baba yake Frank. "Hamna shida baba usijali yote hayo yatafanyika muda mfupi ujao. " Akaongea Frank ambaye muda wote furaha ilijaa usoni mwake. *wakati huo huo Penina mpenzi wake Frank naye alikuwa katika moja saloon akitengeneza nywele zake ikiwa ni maandalizi ya kwenda kukutana na mpenzi wake Frank. " Dada nitengeneze vizuri tafadhali maana napenda muda wote niwe navutia mbele ya mpenzi wangu." aliongea Penina kumwambia mwanadada aliyekuwa akimtengeneza nywele. "usijali dada nitakutengeneza vizuri mpaka mwenyewe ufurahi." Dada yule akamjibu Penina na kumfanya atabasamu. Baada ya dakika kadhaa Penina alimaliza kutengenezwa nywele zake na moja kwa moja akazama kwenye pochi yake na kutoa simu yake, kisha akatafuta Jina lililoandikwa my love Frank na moja kwa moja akazipiga namba hizo. * Frank akiwa bado anaongea na wazazi wake ghafla simu yake ilianza kuita, akatoa na kuangalia mpigaji ni Nani. Frank alianza kutabasamu baada ya kukuta mpigaji ni Penina kipenzi cha moyo wake. "haloo mke wangu mtarajiwa mambo vip?" akaongea Frank baada ya kupokea simu. "poa tu mpenzi wangu nimekumiss hadi nahisi kizunguzungu." akajibu Penina. "Asante mpenzi wangu yaani kuachana Jana tu ndio kunimiss hivyo?" " yeah nimekumis sana hebu jiandae nakupitia Sasa hivi tukale bata kidogo. " akaongea Penina kumwambia Frank. " waoow ok najiandaa Sasa hivi utanikuta tayari my love." akajibu Frank na simu ikakatwa. Frank aliwaacha wazazi wake pale sebuleni kisha yeye akaenda kujiandaa kwa ajili ya kutoka na mpenzi wake. Penina naye baada ya kukataa simu aliingia kwenye gari yake nyeupe aina ya rava4 na kuanza kuelekea nyumbani kwa Frank. Tumfahamu Penina vizuri. Penina ni mwanamke mrembo sana aliyebarikiwa na Mungu kuwa na kila kitu kizuri katika mwili wake. Popote pale Penina alipopita aliacha gumzo kwa wanaume ambao walikuwa wakimmezea mate. Penina ametoka katika familia ya kitajiri yenye watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume ambao ni Nolan, Penina na Irene. Penina amefanikiwa kusoma mpaka elimu ya juu kabisa na kufanikiwa kuwa mfanyabiashara mdogo anayechipukia kwa kasi sana. Penina alianza uhusiano wa kimapenzi akiwa kidato cha tatu, na alianza uhusiano na kijana aliyeitwa Frank ambao mpaka Sasa wapo pamoja. Lakini kitu kimoja ambacho kanalitia dosari penzi tamu kabisa la Penina na Frank, ni baba yake Penina kutopenda mwanawe aolewe na Frank. Baba yake Penina hakutaka kabisa mtoto wake aolewe na Frank, yeye alitaka mtoto wake aolewe na mzungu kutokana na uwezo wao wa kipesa. Mama yake Penina pamoja na Nolan kaka yake Penina ndio Watu pekee waliokuwa wanayaunga mkono mapenzi ya Penina na Frank katika familia yao. Lakini Irene mdogo wake Penina pamoja na baba yake Penina ndio watu pekee ambao walikuwa hawataki kabisa kuyaona mapenzi ya Penina na Frank yakiendelea. * Frank yeye anatoka katika familia yeye hali ngumu kimaisha, hawakuwa na uwezo hata wa kuwa na nyumba nzuri kama wenzao. Frank aliishia kidato cha pili kutokana na wazazi wake kutokuwa na uwezo wa kumuendeleza zaidi. Kadhalika pia Angel mdogo wake Frank naye aliishia darasa La saba kutokana na Wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza zaidi. * Baada ya dakika kadhaa Penina aliwasili nyumbani kwa kina Frank, akapaki gari yake pembeni na kushuka Kisha akaingia katika nyumba ya kina Frank ambayo ilikuwa imechoka Sana. "waoow mkwe wetu karibu Sana." mama yake Frank ndio alimpokea Penina kwa furaha Sana. "Asante Sana mama yangu nimekaribia." akajibu Penina huku akiketi pembeni ya mama yake Frank. "eeh mwanetu lete habari." akaongea mama yake Frank. "Sina hata mpya nimekuja kumchukua mtoto wenu." akajibu Penina. Na Muda huo huo Frank akajitokeza akiwa tayari ameshajiandaa. Licha ya umaskini uliopo katika familia Yao, bado Frank alijitahidi Sana katika kuupendezesha mwili wake ili aweze kuendana na mpenzi wake Penina ambae Muda wote alikuwa mtu wa kupendeza tu. "waoow my love mwaaa." Penina ndio alinyanyuka na kumkumbatia Frank na kumuachia busu Zito la shavu. Frank naye hakuwa nyuma alimpokea mpenzi wake kwa furaha pia. Penina pamoja Na Frank waliaga na kutoka nje, wakaingia kwenye gari na kuondoka. "tunaelekea wapi Sasa mpenzi wangu?" akahoji Frank. "surprise my love sikuambii tunaelekea wapi." Penina akamjibu Frank huku akitabasamu. "haya bhana bas nafunga macho mpaka tufike." akaongea Frank na kumfanya Penina azidi kutabasamu.* Katika bar moja iliyopo maeneo ya sinza kikao kimoja kilikuwa kikiendelea, na huku kilichokuwa kikipangwa Katika kikao kile ni namna ya kulivunja na kuliharibu penzi la Penina na Frank. Mzee Joel ambaye ni baba yake Penina, pamoja na Angel ambaye ni mdogo wake Penina pamoja na vijana wengine watatu wa kiume na mmoja wa kike, ndio waliokuwa wahusika wakuu wa kikao kile. .... Itaendelea

at 6:44 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top