Home → simulizi
→ KIJIJI CHA SHETANI
Sehemu Ya Tatu
Ilipoishia
...... Wazee wa kichawi walikasirika sana na amri ilitolewa alieharibu kazi ile atafutwe na auwawe na pia kabla wiki haijaisha pia Mama Zuma nae anatakiwa Auwawe na sasa zilikuwa zimebakia siku sita.Bi Hindu akawa amenunua kesi na mara moja wakawa tayari wamemtambua kupitia Mitambo yao ya kichawi.Mzee Shomary alikasirika sana Kuona mkewe kaingilia kazi.
Sasa Endelea
......Wakiwa bado mle chumbani yaani Bi Hindu,Mwanae ambae ni Mama Zuma pamoja na Zuma na wadogo zake ambao ni Miriamu na Amos hali ya hewa ilianza kubadilika mle chumbani.
* * * * *
Kule porini alipo mzee shomary,Mzee Kagusa pamoja na wale Bibi vizee wanee,Waliitana katika pango moja ambalo walipenda sana kulitumia katika vikao vyao,pango hilo lilikuwa la kutisha sana kwani kila mara walionekana bundi mbalimbali wakiruka na kutua huku na kule,Pia sauti na milio ya paka ilikuwa haikatiki eneo lile,Ki ufupi eneo lile lilikuwa la kutisha sana,Mwanga wake ulikuwa hafifu zaidi ya giza kuwa limetawala.Waliingia mle ndani na Bibi mmoja kati ya wale bibi vizee wanne aliliza vidole vyake viwili vya mkononi kwa kuvisugulisha na vikalia "Taaaap"...Pale pale mienge miwili ya moto iliwaka ukutani ndani ya pango lile na kutoa mwanga japo ulidhibitiwa bado na giza,Lakini ilikuwa ni nafuu kuliko lile giza lililokuwepo mwanzo.Palikuwa na meza moja kubwa sana lakini viti havikuwepo,Wakiwa wamesogea kwenye zile meza mara alitokea fisi mmoja mkubwa sana na kwenda mbele kabisa ya meza kisha alisimama fisi yule na kujiweka vizuri hapo ndipo Mzee wao kiongozi mchawi wa wachawi alienda kukaa yaani si mwingine ni Mzee Kagusa,Mara baada ya kukaa mgongoni kwa fisi yule kisha na kuweka mikono mezani ndipo fisi mwingine alijitokeza alikuwa mkubwa japo sio kama yule wa mara ya kwanza na hapo ndipo msaidizi wa kundi zima la uchawi katika anga la Ujiji alikaa nae alikuwa si mwingine bali ni Mzee shomary ambae Babu yake Zuma.Na mwisho viti vingine Vinne vilikuja vyenye kimo sawa navyo si vingine ni fisi wanne kwa ajiri ya wale Bibi wazee wanne nao waweze kuketi.
Kiongozi wa kikao hicho alikuwa si mwingine bali ni mzee Kagusa.Mzee kagusa ndie aliekuwa kiongozi wa kikao kile na kundi lile,Si kwamba Mzee Shomary pamoja na kuuwa watu wengi hajawahi kuwa kuongozi,Hapana alishawahi kuwa kiongozi kipindi anakaa Kibondo alipokulia ila kutokana na kuua watu wengi pia na kujulikana kwake mbele ya watu wengi wa kibondo kuwa yeye ni mchawi kulimfanya ahame na kuja hapo ujiji,Ni kawaida kwamba mara unapohama katika eneo lako hata kama ulikuwa kiongozi mkubwa kule basi ukifika ugenini ni lazima ukubali yule uliemkuta awe kiongozi wako.
Licha ya kufika pale baada ya kumuoa Bi Hindu Mzee Kagusa alimchagua Mzee shomary na kuwa msaidizi wake mahali pale.
Kikao kilianza na maada nzima iliyokuwa pale mezani ni kuhusu Bi Hindu kwanini amesaliti kundi,Walikuja mezani ili kusikiliza uamuzi wa mumewe ambae ni mzee Shomary kuhusu mke wake na sasa Mzee Kagusa alitupia swali kwa Mzee Shomary"Mzee mwenzangu na kiongozi mwenzangu,Mkeo na mpendwa wetu amesaliti taratibu,sheria na Mamlaka za kundi letu ,Nadhani wewe mwenyewe unajua kuwa sheria inasemaje kwa mtu anaezuia kazi zetu zisisonge mbele na pia ni adhabu gani ataipata kutoka kwa mungu wetu,tupo hapa kusikiliza uamuzi wako wa mwisho juu ya mkeo."Alisema kiongozi mkuu Mzee Kagusa.
Mzee Shomary kabla ya kujibu alishusha pumzi kidogo kisha akasema"Mimi sina cha kusema zaidi ya kusema nimeshaua watu wengi,ndugu zangu wengi,watoto wangu wengi mpaka hivi sasa kwa hiyo sioni shida kabisa kusimamia sheria yetu kuwa yoyote anaesaliti ni lazma AUWAWE,kwa hiyo mimi ninachosema kwasababu amevunja sheria na taratibu zetu basi ni lazima auwawe,sioni shida kumpoteza yeye,Nilishaapa mbele ya mungu wangu huyu kuwa tangu siku niliyokunywa na kula nyama na damu za wazazi wangu basi sintaogopa kuua yoyote atakaekatiza mbele yangu na kuzuia mpango wangu.Nasema hivi mke wangu Bi hindu achukuliwe aletwe hapa na shughuri ya kuutoa mwili wake sadaka kwa mungu wetu ianze"Alisema Mzee Shomary na kupitisha Hukumu ya kifo kwa mke wake bila huruma.
* * * * *
Wakiwa bado mle chumbani taratiibu upepo ulinza kuvuma nje ya nyumba ya Mama Zuma,Moja kwa moja Bi Hindu alijua nini kinaendelea hivyo aliaga mapema na kumuaga Mama Zuma aliekuwa tayari ameshakuwa na afya njema.Mama Zuma katika maisha yake yote hakuwahi kujua kama wazazi wake ni wachawi kweli zaidi ya kusikia tu uvumi kwa watu.
Bi Hindu aliondoka haraka mpaka nyumbani kwake na kufika kuanza kupekuwa mkoba wake.Alikuwa akitafuta dawa kwa ajiri ya kupambana na ajikinge mwenyewe lakini alikuwa tayari kachelewa,Akiwa chumbani upepo mkali wa kishetani ulivuma ndani ya chumba kile na kuanza kupeperusha vitu mle ndani kitendo kilichosababisha Bi Hindu ashindwe afanye kipi,Upepo ule ulianza kumzunguuka na mara kupitia kingo ya ukuta yaliingia majini mawili yenye kutisha sanaa yakiwa na mkia mlefu nyuma,Nywele nyingi na chafu sana zilizolala,Kucha ndefu mno pia yalikuwa yametoa ulimi zao zilizokuwa ndefu zinazoburuza kifuani na zenye kudondosha matone ya damu kama mnyama alietoka kula nyama,Hawakuwa na meno ya binaadamu bali ya wanyama aina ya dubu meno ambayo yamechongoka sana,macho yao yalikuwa mekundu yenye kama kuwaka moto kwa ndani,Yalianza kusogea yakimfuata Bi Hindu.
Bi Hindu pamoja na kuishi kwake maisha ya kichawi hakuwahi kuonana na shetani wa namna ile wenye kutisha vile,Hakuwa na chakufanya zaidi ya kutetemeka.
Akiwa anatetemeka na vitu ndani kuvurugika mara nje hodi iligongwa"Bibi hodiiii"Ilikuwa si sauti nyingine bali ni sauti ya ZUMA.
JE NINI KITAENDELEA
Je Zuma alikuja kutafuta nini kwa bibi yake tena ikiwa mama kule aliachwa hali imetengamaa
Je Bi Hindu ataokoka kweli mikononi mwa majitu yale
SIku zinaenda zinakatika je nini hatima ya Zuma na Mama yake kuchukuliwa na kundi la kichawi
ASANTENI SANA
KIJIJI CHA SHETANI
Sehemu ya Nne
Ilipoishia
... Bi Hindu pamoja na kuishi kwake maisha ya kichawi hakuwahi kuonana na shetani wa namna ile wenye kutisha vile,Hakuwa na chakufanya zaidi ya kutetemeka.
Akiwa anatetemeka na vitu ndani kuvurugika mara nje hodi iligongwa"Bibi hodiiii"Ilikuwa si sauti nyingine bali ni sauti ya ZUMA.
Sasa Endelea.
....ZUMA akiwa pale nje alihisi mambo yanayoendelea mle ndani mwa bibi yake hayakuwa ya kawaida.alianza kusikia kama upepo wa ajabu ajabu ukipuliza na kupepelusha vitu mle ndani,alipiga tena hodi na hali ilikuwa ile ile ya ukimya.
Mle ndani yale mashetani mawili yaliyotumwa yalizidi kumsogelea Bi Hindu hatimae yakamfikia karibu yake,wakati huo Bi hindu alikuwa hana sehemu ya kukimbilia alikuwa ameshafika kwenye ukuta,Bi Hindu alisikia vema sana hodi zilizobishwa na mjukuu wake kule nje lakini kila alikuwa akijalibu kutoa sauti ilikuwa haitoki,alijalibu kupiga kelele lakini pia nayo haikutoa sauti hivyo alishindwa kufanya chochote kile.
Zuma nje alisubiri na hatimae uvumilivu wa zile fujo mle ndani ulimshindwa alianza kuhisi tayari bibi yake atakuwa kwenye matatizo,Jukumu aliloamua kulichukua ni kuingia ndani bila hodi ili kuona nini kinajiri.Zuma alisukuma mlango na kuingia ndani kwa Bibi yake,pia moja kwa moja alipitiliza mpaka chumbani kwa bibi yake,Kitu alichokutana nacho kilimfanya Zuma atoke nje mbio na kuanza kukimbia kuelekea kwao.
Aliona zile nyuso za mashetani wale zikiwa kwenye pembe ya ukuta wa chumba zikiwa zimemshikilia Bibi yake ambae wakati huo alionekana kama mtu ambae tayari amekufa au amezimia.Na Zuma alipoingia tu chumbani sehemu ile ya ukuta ilifunguka kama mlango na wale mashetani mawili walipotea kama upepo kupitia ule mlango.Zuma alikuwa amekuja kwa Bibi yake kumshukuru na pia kumuelezea yale yote aliyoyaona ndotoni lakini kwa bahati mbaya ndio alikutana na bibi yake anatoweka.
Kitendo kile kilimfanya Zuma akimbie kwenda nyumbani huku analia kwa ajiri ya kwenda kutoa taarifa kwa mama yake kwa kile alichokiona."Mamaaa..nyumbani kwa bibi....nyumbani kwa bibi'Zuma alifika nyumbani ambapo alimkuta mama yake tayari yuko vizuri na mwenye afya nzuri akiwa kakaa nje,Zuma alishindwa kutoa taarifa lasmi na badala yake kuishia kusema tu hilo neno la Mama nyumbani kwa bibi,Aliwa analia alimshika mkono mama yake na kuanza kuelekea nyumbani kwa bibi yake akiwa na Mama yake,Mama Zuma nae tumbo lilianza kumkata akitaka kujua je nyumbani kwa mama yake kuna nini hivyo walijikuta wakitembea haraka kwenda kuwahi kujua kuna nini,Wakati wote huo Zuma haongei zaidi ya kulia.
Walifika nyumbani kwa Bi Hindu na moja kwa moja waliingia hadi ndani,Zuma hakuamini macho yake baada ya kuingia mle ndani ambapo alipaacha pamevulugika kila kitu kikiwa hovyo hovyo kutokana na upepo mkali wa yale mapepo alikuta pamepangika vizuri na mpaka kitanda kimetandikwa vizuri,Palikuwa hamna hata karatasi wala nguo iliyokuwa imekaa vibaya au kudondoka chini,Zuma aliishiwa la kusema na hata kulia kukaisha.Mama yake alimuuliza"Ulikuwa usema nyumbani kwa bibi kwani kuna nini?,Na mbona bibi yako alisema akifika nyumbani anaondoka kwenda kutafuta kuni sasa kwani amepatwa na nini?,Na mbona sasa hayupo,?"Kwa maswali yale Zuma aliishiwa la kusema,Alitamani amsimulie mama yake mkasa mzima wa kuanzia kwenye ndoto lakini alishindwa.
Taratiibu bila hata kuongea Zuma alianza kuondoka kuelekea nyumbani,Kijasho chembamba kilimtoka hakika akaamini kweli kazi anayo,Na walidhamiria kweli kumtoa mama yake kafara kwa ajili yake,Akiwa njiani huku akilejea nyumbani Zuma alijikuta analia kilio cha kwikwi hasa akifikilia kumpoteza mama yake na hakuna msaada mwingine zaidi ya Bibi.
* * * * * *
Katika Falme na tawala ya kishetani,Ndani ya msitu mnene wa hifadhi ya Gombe katika mti mkubwa aina ya mbuyu,Paliandaliwa eneo maalumu la kutolea sadaka kwa ajili ya Shetani mkuu wa eneo lile,Palitengenezwa kichanja maalumu cha kutolea sadaka kwa ajiki ya Shetani wao,Ikiwa ni katikati ya msitu ule wa Gombe uliosongamana na miti mingi na kutengeneza kiza totolo eneo lile,palikuwepo pia na wachawi wadogo wadogo wakike na wakiume ambao walikuwa uchi wa mnyama huku wamejipaka aina flani ya unga mweupe mwili mzima,Mikononi mwao walikuwa wameshika pembe za ng'ombe wakipuliza na kuimba huku wameshikilia mioto inayowaka kuashilia zoezi la sadaka limekalibia,Japo ilikuwa ni mda wa kama mchana mchana hivi lakini walitengeneza mazingira ya uchawi na eleo lile likawa giza la usiku,Waliokuwa wanaimba na kuuzunguuka mbuyu ni wafuasi wa kichawi wa eneo la Ujiji zima,Haijalishi ulifuatana na mama yako au baba yako lakini sharti la zoezi hilo ni kuwa uchi wa mnyama kuimba nyimbo za ajabu huku mkizunguuka ule mbuyu mkubwa na mnene ulioonekana kuishi miaka mingi sana.
Walikuwa wakisubiri kafara ambae ni Bi Hindu aletwe kwa ajili ya Zoezi zima la utoaji kafara na sasa hatimae zile Shetani mbili zilizotumwa kumfuata Bi Hindu zilitia timu.Wazee na wakuu wa uchawi katika ule mji walikuwa wakiangalia ngoma zilivyokuwa zikiendelea pale huku wakifurahi sasa walisimama kwa ajili ya kuanzisha zoezi zima.Na wazee hao si wengine bali ni Mzee Kagusa kama kiongozi akifuatiwa na Mzee Shomary pia na wale Bibi vizee Wanne.
Pia uimbaji wa ngoma ulibadilika eneo lile na hatimae zikaanza ngoma za kutoa mwili wa mtu kafara,Mashetani yale mawili yalifika na kuulaza mwili wa Bi Hindu ambae tayari alikuwa kaishanyang'anywa uchawi na nguvu za giza alizokuwanazo pia pamoja na kuzimishwa wala asiweze kujitambua au kufanya kitu chochote.Chini ya Uchanja ule paliwekwa mabakuli mengi na makubwa kwa ajili ya kazi maalumu ya kudaka damu,Mzee Shomary kama Muhusika na pia kama ndie mwenye mke alikabidhiwa kisu kwa ajili ya kwenda kutoa Moyo wa mkewe ambae ni Bi Hindu ili mungu wao ashuke kupitia mbuyu aweze kupewa kama sadaka na sasa Mzee Shomary alinyanyuka na kukipokea kisu.Wakati huo shangwe ziliendelea ngoma zilipigwa na furaha iliongezeka.Mzee Shomary alikishika kisu kwanza kabla ya kuendelea na zoezi la utoaji moyo,Alimuangalia mkewe aliekuwa kalala pale kwenye uchanja,ni kama tayari ameshakufa,Alikumbuka siku ya kwanza katika maisha yake kukutana nae na kumpenda angali akiwa bado kijana,Alikumbuka maisha yao yalivyokuwa na walivyofanya mengi wakiwa pamoja,Alimwangalia usoni mkewe na kusogeza mwanga wa moto karibu na kugundua ni kama mkewe alikuwa amelala huku akionyesha tabasamu la kilio.
Kwa mara ya kwanza Mzee Shomary alidondosha chozi jingine kama siku ile aliyodondosha akiwa mdogo alipowauwa wazazi wake.
JE NINI KITAENDELEA
...Je Mzee Shomary atamuua mkewe?
...Je nani atamsaidia tena Mama Zuma?
.....Watafanikiwa kumuunganisha Zuma uchawini?
Usikose Sehemu ya Tano ya simulizi hii kesho saa 5 Asubuhi.Pia Samahani kwa kuwacheleweshea kama siku mbili hivi.
ASANTE SANA.
KIJIJI CHA SHETANI
Sehemu ya Tano
Ilipoishia
....Kwa mara ya kwanza Mzee Shomary alidondosha chozi jingine kama siku ile aliyodondosha akiwa mdogo alipowauwa wazazi wake.
Sasa Endelea
...Kitendo cha kukumbuka siku aliouwa wazazi wake kiliingiza roho ya ukatili ndani yake,Alijisemea moyoni"Nilipoteza wazazi wangu ambao niliwapenda kuliko kitu chochote duniani,Na siku hiyo niliapa mbele ya Mungu wangu kuwa sintarudi nyuma katika maamuzi ya mauwaji....Nisamehe sana mpenzi wangu thamani ya kukupoteza wewe bado haijafikia thamani ya wazazi wngu,nitakukumbuka daima kama mke wangu kwaheri".Mzee Shomary alisema maneno hayo kisha akamtazama Bi Hindu ambae wakati ule alikuwa kama amelala kutokana na kupewa uchawi mzito ndani yake,Mzee Shomary alionyesha tabasamu la mwisho kwa mkewe kisha akanyanyua kisu juu,baada ya kukinyanyua juu huku akiwa ameshika kwa mikono miwili alikirudisha kwa kasi zaidi moja kwa moja mpaka kifuani kwa Bi Hindu sehemu ya moyo,Maskini Bi Hindu alifumbua macho na kutaka kunyanyua kichwa lakini ilishindikana,Radi na ngurumo kali zilianza kupiga eneo lile wakati huo Bi Hindu alishika mikono ya Mzee Shomary iliyokuwa imeshikilia kisu pale kwenye kifua eneo la upande wa moyo,Alitamani kunyanyua kichwa na kusema neno kwa mumewe lakini haikuwezekana kutokana na uchawi aliokuwa tayari kamezeshwa,damu nzito ilitililika kutoka sehemu ile ya moyo na kumwagika kwa chini ya kichanja ambapo tayari kulikuwa na bakuri kubwa la kuipokea damu ile.
Hatimae baada ya kutapatapa sana Bi Hindu aliaga Dunia na mwili wake ukawa wa baridi,Mzee Shomary aliuchimbua moyo kutoka kifuani kwa Bi Hindu na kuutoa wote kisha kuuweka kwenye bakuri,Wakati huo radi ziliendelea kupiga huku shangwe za nyimbo nazo zikipamba moto zaidi.
Baada ya Mzee Shomary kumaliza ile shughuri aliondoka eneo lile na kuuacha mwili wa mke wake ukiwa na shimo kubwa sehemu ambapo moyo umetolewa,Habari za Bi Hindu zikawa zimefika mwisho wake.Na sasa alinyanyuka kiongozi mkuu ambae ni Mzee Kagusa kwa ajiri ya kwenda kuukabidhi moyo kwa shetani wao mkuu wa anga lile,alifika eneo lile la ule mbuyu ambapo kuna mwili wa Bi Hindu na lile bakuri la moyo,aliita watu wanne waje waushughurikie mwili wa Bi Hindu kuuondoa pale na kwenda kuuandaa kwa ajiri ya sherehe nzima inayofuata,Baada ya Mwili wa Bi Hindu kuondolewa pale na sasa alikamata Bakuri lililokuwa na moyo na kulinyanyua juu huku kapiga magoti,alianza kuongea maneno na lugha isiyojulikana huku bakuri kalielekeza juu,ngurumo na radi viliongezeka kwa kasi sana eneo lile na hatimae tetemeko likaanza kutikisa ardhi ya eneo lile,wachawi wale waliokuwa wakiimba na kucheza walilala chini kifudifudi kusujudu huku wameziba masikio yao kutokana na kelele nyingi zilizokuwepo eneo lile,wakati huo mzee Shomary macho yake yalibadilika na kuwa mekundu huku pia akendelea kuongeza kasi ya kuingea lugha ile isiyojulikana.
GHAFLA eneo lile radi kali zenye miale ya moto zilianza kushuka katika lile bakuli lililokuwa na moyo,zilipiga radi kama tatu kali na nzito na hatimae hali ya pale ilitulia,tukio lile halikuwa la kimchezo maana kila mtu alibaki hoi sana kutokana na balaa lile,Mzee Shomary aliookuja kushusha chombo hapakuwepo mle hata tone la damu,pia moyo nao haukuwepo,tayari sadaka ila ilikuwa imeshachukuliwa na shetani wao wa eneo lile na kafara ilikuwa tayari imekamilika.Sasa sherehe ziliendelea pia ngoma na shangwe kuwa jambo limefanikiwa
NI ukweli usiopingika na wazi kuwa unaposikia mtu ametolewa kafara ni kwamba mwili wake na damu yake vimeenda kutumika katika eneo la uchawi kama chakula,hivyo kafara huwa ni kama sadaka juu ya jambo fulani.Mwili wa Bi Hindu siku hiyo ulikuwa kafara mbele ya wachawi wale,Wakati sherehe zinaendelea bakuri lile la damu liliwekwa meza kuu ambapo walikuwa wamekaa Mzee Shomary,Mzee kagusa pamoja na wale Bibi Vizee wanne,Walikuwa kama wanasubiria kitu flani ili waendelee na jambo.Na kitu hicho walichokuwa wanasubiri si kingine bali ni nyama ya mwili wa Bi Hindu uliochukuliwa pale kwenye uchanja na kwenda kukatwa katwa vipande vipande kwa ajili ya chakula.Kwao chakula yaani nyama ya binaadamu na damu huwasaidia kuwatia nguvu katika mambo yao ya uchawi.
Hatimae Sinia kubwa lililetwa mezani lililokuwa limesheheni vipande vya myama vilivyokatwa katwa,hapo ndipo sherehe ilizidi kunoga zaidi na amri ilitolewa kuwa sasa zamu ya kupata chakula imefika."Kama ilivyokawaida yetu tutoapo kafara,kila mmoja atapita hapa kupata kipande kimoja cha nyama na damu hii kidogo ili tuendelee kuwa na nguvu na tudumu zaidi na zaidi.Tawala yetu ni lazima itadumu milele,na eneo hili lazima tutatawala milele na wala hakuna mtu yeyote atakaetuzuia"Maneno haya aliyasema Mzee Kagusa na kusababisha furaha kubwa kwa wafuasi wa uchawi waliokuwepo eneo lile.Walianza kupita mmoja mmoja eneo la meza kuu na kulishwa kipande cha nyama pamoja na damu,Nyama ile ilikuwa mbichi kabisa ambayo bado inadamu,cha ajabu ni kuwa kila mmoja aliifurahia sana huku sherehe ya ngoma iliendelea na hatimae wafuasi wote waliisha na wakaendelea kucheza huku wakiunzunguuka mbuyu wakiwa wameshika mienge ya moto na pembe za ng'ombe wakipuliza.
Sasa ilikuwa zamu ya meza kuu kupata chakula huku wakiendelea kushehereka kwa kutazama ngoma zinavyoendelea.Sherehe ile iliisha majira ya saa 10 jioni siku hiyo.Mzee Shomary pamoja na wachawi wenzake walikuwa hawajarejea majumbani kwao toka usiku ule kwenye tukio la Zuma na sasa ilikuwa saa 10 jioni ambapo sherehe ilifungwa.
* * * * * *
ZUMA siku hiyo alijikuta ameipoteza kwa kutokwenda shule toka asubuhi yake baada ya mama yake kuamka akiwa na hali ile,Jalibio la mtihani ule lilimpita siku hiyo japo kuwa alikuwa kidato cha nne akielekea kumaliza,bado alikuwa akitamani kumwabia mama yake yote anayoyajua lakini alishindwa,Alikuwa amekaa peke yake kwenye msingi wa nyumba yao jioni ile akiendelea kuwaza hapa na pale yale yote yaliyotokea.Mama yake alikuwa na wadogo zake eneo la jikoni muda huo wakiandaa andaa maswala ya chakula cha usiku maana ilikuwa yapata majira ya jioni saa kumi na moja hivi.
ZUMA akiwa amekaa kwenye msingi akitafakari yaliyotokea pia na aliyoyaona kwa bibi yake ghafla Mmama mmoja ambae ni jirani yao na Bibi na Babu yake Zuma alikuja akiwa analia nyumbani kwa akina Zuma,Alifika hata bila ya salamu moja kwa moja alitoa ujumbe kwa Mama Zuma"Mama Zuma Bi Hindu mama yako amefariki....Jamani Bi Hindu jilani yangu mweee nilikuzoea sana kwanini umeondoka wakati ulikuwa bado na nguvu za kutosha"Mama yule aliendelea kulia huku akiongea maneno yale.Pale pale Mama Zuma bila hata kusema kitu alianza kudondosha kilio huku akikimbia kuelekea nyumbani kwa mama yake kuhakikisha kama kweli amefariki.Mama Zuma alikimbia kama mwehu huku khanga alizokuwa amejifunga zikiwa zinadondoka,Hakujali hilo bali aliendelea kukimbia huku akilia sana.
ZUMA alisikia taarifa hizo akiwa amekaa pale nyuma ya nyumba kwenye msingi,hakuchelewa na yeye aliunga msafara moja kwa moja kwenda kushuhudia kama kweli,Wakati anakimbia alikuwa akiwaza kichwani mwake kuwa huyo ni babu yake ndio amefanya yote hayo kwa sababu bibi yake amehusika kumsaidia mama yake ambae alitakiwa afe.
Moja kwa Moja bila hata hodi Mama Zuma na Zuma walitua chumbani kwa Mzee Shomary kuona kama kweli,Walifunua shuka na kukuta ni kweli mwili wa Bi Hindu ukiwa umelala.Zuma aliendelea kuukagua zaidi ajabu ni kwamba hapakuwa na hata jeraha moja katika mwili,kubwa zaidi hata ile sehemu ambayo moyo ulichomolewa napo palikuwa pako kama kawaida hapakuonekana na shimo lolote.
Zuma akiwa mle chumbani alisikia babu yake akiongea na majirani akiwaadithia ilikuwaje mpaka Bi Hindu amefariki,Alisema"Mimi niliamka asubuhi sana nikamwambia kuwa naenda porini kwenye ukataji wangu wa nyasi na kamba nae akasema baadae kidogo kwenye mida ya saa nne nae ataelekea porini akatafuta angalau kuni za kupikia sasa nimeludi hapa jioni hii nakuta yeye bado hajarudi nimekaa kaa kidogo nashangaa hawa hapa vijana wawili wanamleta wakisema wamemkuta kando kando ya barabara porini akiwa amelala kumtikisa wakagundua tayari amefariki hivyo jukumu walilofanya ni kumleta hapa"Alisema mzee Shomary.
Zuma alitoka mle chumbani ili kuwashuhudia hao vijana ni akina nani walioleta mwili wa Bibi yake.Alipowatazama tu moja kwa moja akakumbuka ni kama hizo sura aliziona siku ile usiku kwenye lile tukio la yeye kutaka kukabidhiwa uchawi.Hivyo babu yake alidanganya.Ukweli ni kwamba aliekuwa kalala mle ndani kwa macho ya nyama alionekana Bi Hindu lakini kwa Macho ya kishetani na kiroho ulikuwa ni mgomba wa ndizi uliovaa sura ya Bi Hindu.Maana Bi Hindu habari zake zilikuwa tayari zimeisha na tayari walikuwa wameshamtafuna.
Zuma moja kwa moja akiwa amejaa hasira alimuangalia babu yake,na hapo ndipo walipogonganisha macho yao wote wawili.Balaaaa....
JE NINI KITAENDELEA
Usikose sehemu ya Sita ya simulizi hii ya kusisimua
ASANTENI SANA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: