Home → simulizi
→ RIWAYA JINI HUSNAT
MTUNZI: ZUBERI MAVUGO
SEHEMU YA KWANZA.
Ulikuwa ni ukumbi mkubwa ulojaa watu wenye hela zao,kila starehe iliyopo katika dunia hii ilikwepo hapo kasino ilo lilijaa wadachi,waindi,walokuwa wakijiuza mziki mkubwa ulikuwa ukiendelea kuwaburudisha wateja wa club hiyo kulikuwa kuna walinzi wa kutosha,walokuwa tayari kupambana na kiumbe chochote kitakachotaka kuleta shida gari aina mbali mbali za kitajiri ziliingia na kutoka na wasichana warembo ni ukumbi ulosifika kwa matanuzi yote uyatakayo
JOHN VERGAN kama mwenyewe alivyopenda kujiita alikuwa counter akitupia pombe yake taratibu! machangudoa wachache walijipitisha mbele yake lakini ilo wala akulijali wengine awakuishia kujipitisha tu kwani walimfata na kutaka kutoa company lakin VERGAN hakuwa tayari,mawazo yalitawala kichwa chake aligubia bia kwa fujo aikujulikana kipi kilichomtesa kijana huyo mwenye umbo la wastani si mrefu sana wala si mfupi sana,maji ya kunde mwenye body sex mwili wa mazoezi alikuwa na kila mvuto wa kimapenzi kwa mwanamke amwangaliaye! wanawake wengi sana walimmezea mate lakin moyoni mwake alikwepo mwanamke mmoja tu MOURINE huyu ndo alomfanya VERGAN Agubie ile bia kwa hasira na hisia tele MAPENZI yalimtesa alimpenda mtu asiyempenda tena secretary wake macho yake makubwa yaliyozungukwa na nyuzi nyembamba nyeusi yalitua mkononi mwake alivaa saa ya dhahabu iliyosomeka ni saa sita na nusu usiku akashusha pumzi taratibu ni wazi alishachoka na usingizi ulishaanza kuyanyemelea macho yake kilevi kilishaanza kumlevya akajinyanyua pale huku akipepesuka na kuanza kuondo
*****
"simu unayopiga aipatikani tafadhali jaribu tena badae" ndiyo kauli ilojibu upande wa pili JOHN VERGAN alizidi kunywa bia yake taratibu mpaka alipotosheka kwa vyovyote muda ule MOURINE asingeweza kuja akiwa anapepesuka taratibu alinyanyuka na kuelekea nje kwa hatua fupi aliiendea gari yake ilokuwa nje na kujipakia ndani toka jioni alikwepo katika hoteli ile mpaka muda ule aliiwasha gari na kuiondoa kwa kasi.
-.....-.....-.....-
MOURINE msichana mrembo kiumbo na secretary wake VERGAN akiwa ndani ya gari yake jioni hii moyoni mwake alikuwa na raha sana! kitendo cha BOSI wake kumuitaji hotelini kilimpa faraja,ni kweli alimpenda bosi wake yule.na bosi wake alishamwonesha ishara zote za kumpenda,akutaka kumkubali kwa kutopenda kuonekana mrahisi ila siku hii ya leo alijihisi hali flan si ya kawaida alijihisi KUMPENDA na kuitaji kuwa pamoja naye kimapenzi hisia zile zikamfanya aongeze mwendo wa gari lake kumuwai mwanaume yule ghafla akiwa katika mwendo mkali akakatisha mwanamke mrembo mbele ya gari.MOURINE akajaribu kupiga break ila gari likamvaa dada yule MOURINE akiwa kachanganyikiwa baada ya kujiisi kumgonga mdada akashuka kwa speed mpaka mbele ya gari lake AKUKUWA NA MAITI WALA MDADA MOURINE akashtuka,kwa haraka akarudi garini na kujaribu kuwasha gari GARI LIKAGOMA,akazidi kuchanganyikiwa
.akashika simu yake nayo kwa ajabu ikawa imezima charg.safari ya MOURINE ikawa imefia hapo.
BADO JOHN VERGAN moyo wake ulijaa simanzi ghafla akiwa kwenye mwendo wa wastani mbele yake akamuona msichana mrembo,msichana alozivuta na kuziamisha HISIA zake akazidi kupunguza mwendo wa gari na alipo mfikia dada yule kabla ajamsemesha dada yule akamuwahi
"kaka naomba lifti" VERGAN akujibu swali lile kwani akili yake ilikuwa katika umbo zuri la mrembo yule! umbo namba nane,mwenye asili ya kiindi akika alikuwa na mvuto wa ajabu.
"mimi naita JOHN mwenzangu sijui unaitwa nani?" dada yule ndani ya gari alikaribishwa na swali
"MIMI NAITWA HUSNAT".....,.
Macho ya VERGAN yalikuwa katika mapaja mazuri yalokuwa muda wazi wakati huo,binti yule aliyejitambulisha kama HUSNAT alivaa kimini kidogo kilicho acha mapaja yake wazi! kutokana na msukumo wa pombe VERGAN alijikuta akishindwa kuzuia HISIA zake nzito kwa dada yule! akamtongoza! dada yule akuwa na kizuizi VERGAN akimchukulia kama changudoa akaelekea katika nyumba yake.akiwa na mwanamke yule ndani akipania kulala naye usiku mzima LAITI ANGEJUA?
-......-.....-.....-
Ilikuwa ni nyumba kubwa na ya kifahari gari aliyepanda VERGAN na msichana mrembo HUSNAT iliingia mpaka parking VERGAN akiwa kamshika mkono JINI yule wakatoka na kuelekea sebuleni ambapo awakukaa sana wakaelekea chumbani wakapanda kitandani kila mmoja akionekana kumuitaji mwenzake! VERGAN katu akuziona kwato zilizokuwa katika miguu ya bibie yule,macho yake ya kungaa katika giza pia kwa macho yake ya kawaida aliyaona kawaida! wakazama penzini! penzi ambalo katu VERGAN akuwai kulipata kwa binadamu wa kawaida,penzi liliyomlevya na kumpa usingizi mzito.baada ya VERGAN kulala jini HUSNAT akuwa na muda wa kupoteza akavaa nguo zake zote akanyoosha mkono wake juu barua ikatokea akaiweka pale kitandani na GHAFLA AKATOWEKA.
VERGAN alipapasa mbele yake apakuwa na mtu,akafumbua macho yake taratibu kajua cha asubuh kalitokeza kutarifu sasa kumepambazuka,VERGAN alishtuka na kucheki mlango
"UKUFUNGULIWA" Akakumbuka juu ya kukutana na HUSNA jana
"au nilikuwa naota?! hapana!" bado VERGAN alikuwa katika hali za sintofahamu akakurupuka kitandani pale akiita kwa nguvu kama mweu
"HUSNA! HUSNA! HUSNA!" Bado hakukuwa na jibu! akaingia chooni,bafuni ndani kwa ndani bado akukuwa na mtu!.vergan akiwa kama kachanganyikiwa akafungua mlango na kutoka nje alipomkuta kitatu
"umemuona msichana katoka humu ndani asubuhi hii?"
"msichana? msichana yupi bosi?"
"yule nlokuja naye jana usiku!"........
*****
JOHN VERGAN akazidi kuchanganyikiwa
!,akaenda sebuleni akajitupa somani!,mawazo yakaanza kupishana kama mishale ya saa "uyu binti atakuwa kaenda wapi yarabi?! mbona mlango ukufunguliwa? mlinzi naye anasema sikuingia na mtu jana usiku au nilikuwa naota? hapana hapana hapana nilimpa binti lifti HUSNA alinambia anaitwa HUSNA nikampenda! nkamchukua nkaja naye akanipa penzi tamu ambalo sijawai kulipata alafu! alafu ikawaje? HUSNA! HUSNA! hapana si ndoto kuna kitu" alijiuliza VERGAN na kujijibu mwenyewe akajinyanyua na kurudi tena chumbani macho yakadondokea kitandani kilikuwa shaghala baghala kuonesha kwamba usiku kucha kilitumika kikazidi kumpa picha sahihi kwa kile akiwazacho macho yake yakatua mezani akakuta barua imefungwa vizuri huku mkono ukiwa unatetemeka akaifata na kuishika ilinukia harufu nzuri,harufu ya manukato,alikum
buka manukato hayo ni ya HUSNA akaichukua ile barua na kuifungua na kuanza kuisoma naaam macho yalimtoka pima
"DEAR SAMAHANI! KWA KUONDOKA BILA KUKUTA HARIFU NILIHITAJIKA HARAKA NYUMBANI NA WAZAZI ASUBUHI NJEMA WAKO KIPENZI HUSNA NTARUDI"
VERGAN akashangaa,ilikuwa lazima ashangae
"aliitajika nyumbani!?,alipitia wapi?! aliondoka saa ngapi?!!" bado maswali mfululizo yalizidi kumuandama akairudia tena kuisoma ile barua yenye hati nzuri ila akupata majibu aloyaitaji akaikunja barua yake na kuirudisha pale mezani alitoka akaenda kuoga,kuswaki,kuvaa nguo za kazini dakika chache zilizofatia zilimkuta mezani akinywa chai aloandaliwa na mfanyakazi wake JASMINI alipomaliza alinyanyuka na kuliendea gari lake akapanda na kuelelea kazini.alimpita secretary wake MOURINE bila salamu na kuingia ofisini kwake MOURINE akaingia ili kumuuliza kama aliitaji amletee chai tofauti na matarajio yake VERGAN akaanza kushusha lawama
"hivi MOURINE kwa nini unantesa hivi? kwa nini jana ulindanganya na ukuja? kama ulikuwa utaki si ungenambia?.........
**
***
MOURINE huku akiwa anatetemeka akamwangalia bosi wake! "hapana bosi niliaribikiwa na gari"
"comon MOURINE kwa nini ukunambia kwa simu nikajua?"
"simu nayo iliisha chaji bosi...." wakati wakiendelea kuongea ghafla simu ya VERGAN ikaita alipoangalia kwenye scrini ilisomeka HUSNAT.Ubongo wake ukatingishika! akampa ishara MOURINE aondoke maswali yakaanza kutiririka katika kichwa chake!
"nani kampa namba zangu?" aliwaza alikuwa na uhakika akumpa wala akuserv namba zake.ili kupata jibu akaamua kuipokea
"alooo!" VERGAN alisema
"vipi sweet za kazi" sauti nyororo kama kinanda iliuliza VERGAN akaipuuza Na kwa hasira akamuuliza
"nani kakupa namba zangu?"
"si wewe sweet umenipa jana?"
"mimi sijakupa namba zangu"
"umenipa beby"
"sijakupa"
"umenipa!"
"ok ulikuwa unasemaje?" VERGAN aliuliza kwa hasira
"nilikuwa naitaji tuonane" HUSNA alisihi
"siwezi kuonana na wewe" VERGAN alijibu kwa jeuri akapokewa na kicheko kitamu kisha sauti laini ikafatia (basi my love ntakuja hapo kazini jioni tuondoke wote!) hapo hapo akakata simu ubongo wa VERGAN kwa mara nyingine ukatingishika idadi ya maswali yasiyo na majibu yakatiririka! (uyu ni binadamu au jini?,anapafahamu hapa kazini?) bila kujielewa akaanza kusarch namba ya HUSNA kusudi azipige NO AZIKWEPO!!! hakuweza kujizuia kutetemeka kwenye recevd azikwepo.wakati akiwa katika mawazo ya sintofahamu ghafla meseji ikaingia katika simu yake (usiwaze sana dear utaumwa na kichwa) namba zilikuwa ni jina tu JINA BILA NAMBA? akazipiga zikakataa! moyo ukaanza kumwenda mbio akaishika simu ya mezani na kumpigia secretary wake MOURINE naomba mwambie ZUBERI namwitaji ofisini kwangu dakika chache badae ZUBER aliingia akamwonesha ishara aketi.alikuwa ni kijana mrefu,alikuwa ndo meneja baada ya yeye ZUBER ndo alikuwa chini yake alimwamini kijana yule alikuwa ndo mshauri wake,siri zake ZUBERI alizijua,siri za ZUBER naye alizijua walikuwa kama ndugu waloshibana..
VERGAN alimweleza ZUBERI kila kitu!,"dah pole bosi huyo atakuwa ni jini tu! kubali ukatae! kwanza embu nioneshe hizo msg zake! mahana siamin" VERGAN akatii na kuchomoa simu yake mfukoni akaanza kutafuta zile meseji inbox HAZIKWEPO na anakumbuka akuzifuta kabisa! bumbuwazi likauvaa uso wake
"kah meseji azipo kak!"
"nini?" ZUBER akaoji kwa mshangao
"sijazifuta lakini nashangaa kutoziona!"
"basi BOSI jibu ndo ilo huyo atakuwa ni jini mahaba!"
"sasa nfanyeje rafiki yangu?"
"kuna mtaalamu namfahamu ntakupeleka"
"hapana best mim ni msomi siamini hao watu wengi wao matapeli....."
Katika vitu ambavyo JOHN VERGAN akuvipenda ni kuamini ushirikina "mganga wa kienyeji!" ZUBER alijaribu kumbembeleza lakin VERGAN akuwa tayari,mwisho akakata na tamaa!
"ina maana uyu ni mtu au jini?" bado maswali yasiyo na majibu yaliambaa katika kichwa chake.
"sura ya HUSNAT ikamjia kichwani mwake wakati walivyokuwa wakifanya mapenzi" miguno ya kimapenzi na hata sura yake alivyoikunja,utamu alokuwa nao,HISIA zikampanda,tabasamu likamponyoka.
"atakuwa ni binadamu anacheza na akili yangu tu!" akajifariji upendo moyon mwake ukafumuka kama mvua za masika ALIANZA KUMPENDA!. Akashangaa kumpenda ghafla kiasi icho! moyo wake aliujua vyema.aukuwa wa mtu aliyeyapendekeza mapenz akupenda kujiumiza kichwa kama kwa MOURINE aliyepanga kumuoa,lakini MOURINE anamzingua,alipobahatika kumuona HUSNA akajua jibu lake limepatikana lakini vitabia tabia vyake vinamshangaza naye ni jini? aoe jini?
"no siwezi kumpenda HUSNA!" akapingana kwa nguvu na HISIA zake
ilipofika jioni wakati anajiandaa kuondoka ghafla mlango ukafunguliwa na HUSNAT akaingia na tabasamu pana usoni uzuri wake ulikuwa mara mbili ya mwanzo bumbuwazi likauvaa uso wa VERGA akutegemea kama angekuja kweli mbona secretary wake ajampgia simu? alijawa na khofu ulochanganyikana na woga ilikuwa lazima aogope alikuwa kavaa gauni jekundu refu lililo mkaa vyema.akaenda kuketi kwenye viti vya wageni na kumpa mkono VERGA......
RIWAYA JINI HUSNAT
MTUNZI: ZUBERI MAVUGO
SEHEMU YA PILI
ilipofika jioni wakati anajiandaa kuondoka ghafla mlango ukafunguliwa na HUSNAT akaingia na tabasamu pana usoni uzuri wake ulikuwa mara mbili ya mwanzo bumbuwazi likauvaa uso wa VERGA akutegemea kama angekuja kweli mbona secretary wake ajampgia simu? alijawa na khofu ulochanganyikana na woga ilikuwa lazima aogope alikuwa kavaa gauni jekundu refu lililo mkaa vyema.akaenda kuketi kwenye viti vya wageni na kumpa mkono VERGA........
Mbona SECRETARY wake MOURENE ajampigia simu kumwambia juu ya mtu kumuitaji? au akumwona? au amemdhuru? au naye ameogopa? maswali hayo mfululizo yakakishambulia kichwa chake! akakiri kutoyajua majibu yake akagutuka baada ya kuuona mkono wa JINI yule
"vipi sweet?" sauti tamu imtoaye nyoka pangoni ilipenya katikati ya ngoma ya masikio yake ikawa burudani tosha ndani ya mfumo mzima wa masikio! lakin burudani hiyo katu aikuwepo katika ubongo wake ubongo wake ulikuwa katika tafakari zito tafakari lililomezwa na woga.JOHN VERGAN alitaitika! alikuwa akitetemeka na kusogea nyuma mara ghafla kiti kikadondoka!
"unaogopa nini sweet au aunipendi?" HUSNA kwa mara nyingine tena akauliza! VERGAN akujibu! akabaki kimya
"VERGA TAMBUA NA KUPENDA! NA UKIKUBALI KUWA NA MIMI NITAKUTAJIRISHA UTAMILIKI MALI NYINGI ZAIDI YA HIZI!,MAVIWANDA
,MAKAMPUNI,UTATEMBEA DUNIA NZIMA UNAVYOTAKA UTAPOKEA ZABUNI MPAKA MWENYEWE UTAZIRINGIA LAKINI UKINI KATAA NTAKUFILISI UTARUDI KIJIJINI MASIKINI MTAOMBA HADI VYAKULA NA UTAISHI MAISHA YA MATESO KATIKA DUNIA HII UTAKUWA UKIZARAULIWA NA KILA MTU CHAGUA MOJA.....KUMBUKA USINIKATAE KISA MIMI NI JINI! TAMBUA HATA SISI MAJINI TUNA MIOYO YA KUPENDA KWA DHATI ZAIDI YENU NYINYI BINADAMU HIVYO MOYO WANGU UPO KWAKO WEWE VERGA AU UJAVUTIWA NA MIMI?" aliuliza HUSNA huku akiwa anatembea tembea ofisini mule
"hapana! hapan...." ghafla kitasa cha mlangoni kikawa kina tingishika kuonesha mlango unafunguliwa kutoka nje "JINI HUSNAT AKATOWEKA apo apo"
"bosi unaongea na nani? bosi kuna nini? bosi mbona chini umefanya nini?" MOURINE alimuuliza maswali Mfululizo VERGA aliyekuwa kadondokea kwenye pembe ya nyumba
"ulivyo ingia ujamwona mtu?"
"mtu? mtu gani bosi mbona sikuelewi?"
"HUSNA! ujamwona HUSNAT?"
"Husna ndo nani bosi?"
kabla VERGAN ajajibu swali lile HUSNA akatokea na kumnyooshea VERGAN kidole mdomoni ishara ya kunyamaza.
"amna kitu MOURINE kaendelee na kazI"
"Amna kitu MOURINE kaendelee na kazi!"
alijibu VERGAN huku akinyanyuka na kujifuta futa vumbi HUSNAT ALISHATOWEKA!
"Bosi kuna wale watu wa idara ya mapato wanasema watakuja kesho ivyo uandae risiti zote"
"sa...w ni.meku..elewa" VERGAN alijibu kwa kubabaika secretary wake akaondoka VERGA akarud kwenye kiti chake na kukaa kitu "AKIKUKALIKA!" alinyanyuka na kuchukua koti! lake la suti lililokuwa nyuma ya kiti chake na kulivaa.akachukua simu na kumpigia MOURINE
"Namuitaji ZUBER"
"Sawa bosi"
baada ya muda ZUBER akaingia,
"sasa wewe kijana kaa hapa ofisini mimi naenda kupumzika kidogo"
"sawa bosi"
JOHN VERGAN akachukua brufcase yake na kuondoka!,aliitaji kupumzika aliisi kichwa kinamuuma,katu akujua balaa alilokuwa akilifata mbele yake
ZUBER alitafuta ma file na kuendelea kuyajaza taratibu! akujua kinachoendelea yeye alikuwa na yake kichwani katika kudhihirisha ule usemi umdhaniaye ndiye kumbe siye,au rafik yako ndiyo hadui yako,ZUBER alikuwa ni chui kwenye ngozi ya VERGAN ama kweli usilo lijua ni sawa na usiku wa kiza.
na kwa upande wa MOURINE secretary wa VERGAN kiti akikukalika! alijua bosi wake ana matatizo tu! japo hakuwai kumwambia kuwa anampenda ila moyoni mwake alikiri kumpenda sana bosi wake yule! hapa kuna kitu na lazima nifanye kitu kumsaidia bosi wangu wakati akiwa anawaza hayo ghafla arufu kali ya manukato ikaanza kusikika,upepo mkali ukaanza kuvuma! vumbi lililotengeneza kimbunga cha wastani kikaanza kuingia ndani na kupeperusha ma file yale pale mezani,makabati yakaanza kujifunga na kujifungua yenyewe na mara mtoto mzuri mrefu alovaa nguo ndefu akatokea! katikat ya chumba kile MOURINE akataka kukimbia akashindwa,akataka kupiga kelele pia akashindwa akabaki na butwaa "mimi naitwa "ZAIDATU BINT ROUJAT" ukoo wa kifalme wa kijini nimekuja kwa ajili ya msaada kwako.ila lazima ufe" kabla MOURINE ajafanya kitu JINI ZAIDATU akamvamia na kumnyonya damu yake.
******
JINI ZAIDATU baada ya kuakikisha amemuangamiza secretary yule MOURINE kwa kumfonza damu yake yote akaa chia ukelele mkubwa! kisha akatoweka! mara ghafla MOURINE akazinduka ilikuwa kama kazinduka toka usingizini! ila MOURINE huyu alikuwa tofauti na wa mwanzo! macho yake yalingaa! meno yalichongoka mawili! ila ghafla vyote vikatoweka akabaki MOURINE wa mwanzo! ZAIDATU alikuwa kaingia katika mwili wa MOURINE kwa kazi maalumu! ni kazi gani? aliijua moyoni mwake.aliendelea kufanya kazi zake kama kawaida.machoni alionekana ni MOURINE ila kumbe alikuwa ni jini hatari ilikuwa ni PATASHIKA.
Moyoni mwa ZUBER wazo lililotawala kichwa chake ni kuakikisha mali zote za VERGAN zinakuwa chini yake kwa namna gani? ilo alikumsumbua akakwa pua simu ilokuwa pale mezani na kupiga namba kadhaa akaweka mkonga wa simu yake maskioni "MOURINE nakwomba uniunganishe na PITER"
"sawa bosi" MOURINE aliitikia.na kuwaunganisha wakaongea machache.
dakika chache zilizofatia PITER au mwanasheria mkuu wa compuny ile alikuw mbele ya bosi wake yule. "nachotaka kuongea na wewe ni siri kukiwa na makubaliano au hata kama kusipokuwa na makubaliano!" ZUBERI alifungua kikao kile kwa onyo kali.
"na kama siri hii ikivuja sitokuwa na kingine zaidi ya kukuua!"
"what?" PITER aliamaki
"ndiyo! ni dili litakalo badilisha maisha yetu tutakuwa matajiri wakubwa kama bosi VERGA"
"SAWA nipo tayari weka kazi mezani!" PITER Alikubaliana na wazo la ZUBER na kuwa tayari kusikia dili lenyewe
"naitaji tutaifishe compuny hii iwe chini yetu! mimi na faida tugawane amsini kwa hamsini"
"unasema?"
"ndiyo naitaji compuny hii iwe chini yetu"
"sijakuelewa ZUBER ni vipi tutafanikisha ili?"
"swali zuri PITER wewe ni mwanasheria wa compuny una nyaraka hati zote muhimu ni kitendo cha kuzibadilisha tu"
"tatizo itakuwa nisahii yake"
"atatekwa na kulazimishwa kuweka sahii baada ya hapo tutamuua"
"sawa ZUBER nimekuelewa niachie nianze kazi..
*******
JOHN VERGAN alifika nyumbani kwake na mlinzi akafungua geti VERGAN akaingiza gari taratibu.mlinzi alimsalimia lakini VERGAN akuitikia.kichwa kilikuwa kikiwaka moto akaenda mpaka chumbani kwake na kujitupa mara ghafla akapitiwa na usingizi wakati akiwa yupo usingizini akaota yupo na JINI HUSNA akiwa pembezoni mwa jabali palipokuwa pameota majabali makubwa wakiwa wameegemeana kimapenzi HUSNA akasema:
"dear nna zawadi yako!"
"zawad gan sweet?" VERGAN akaoji akiwa kaushika mkono wa dada yule mrembo
"funga macho yako"
VERGAN akafumba HUSNA akatoa mkufu wa dhahabu na kumvalisha VERGA
"Fungua!"
VERGAN alipofumbua macho yake akuamini akamkumbatia kwa nguvu HUSNA mkufu ule ulikuwa ukimeremeta huku ukiandika jina la VERGAN ulikuwa na picha ya HUSNA na VERGAN wakiwa wamekumbatiana.Baada ya VERGAN kumkumbatia akamwachia ghafla akashangaa kumuona kabadilika kawa na sura mbaya ya kutisha meno yalochongoka pembe pembeni ya vichwa kucha ndefu VERGA akashindwa kuvumilia na kupiga kelele ghafla akazinduka.
"he! kumbe ilikuwa ni ndoto?"
VERGAN alitahayari alishindwa kuzuia mshangao dhahiri katika macho yake.wakati akiwa anashangaa wakati akiwa bado kakaa kitako kitandani.alipo
cheki pembeni ya kitanda AKAUONA ULE MKUFU! aliruka kitandani na kutaka kukimbia MLANGO UKAJIFUNGA kizaa zaa kikaanza.kelele za msichana akicheka zikasikika.
"VERGAN kwa nini unielewi? kwa nini utaki kunipenda? kwa nini utaki kunizoea? ama uitaji kuwa nami? niambie VERGAN nijue,hata mimi na moyo VERGAN!" ilisikika sauti ikisema na kimya kikafuata mlango ghafla ukafunguka.VERGAN kama mweu akatoka mbio alikimbia hadi getini mlinzi wake ndiye aliyefanikiwa kumzuia
"bosi wangu utaumia! una matatizo gani bosi tell me why?"
"niache! niache! niache KITALU niache!" (come down bosi come down punguza presha,relax,smile ,then tell me why ili niweze kukupa msaada) twende ukaone mkufu twende jini si ndoto ni kweli! VERGAN aliropoka.
***************
VERGAN na mlinzi wake KITALU waliongozana hadi ndani VERGA akiwa na lengo la kumuonesha ule mkufu wa ajabu! mkufu wa ndotoni walipofika AWAKUKUTA KITU!,MKUFU AUKUWEPO,VERGAN akakunguta mashuka lakini bado mkufu aukuonekana.ikabidi kwa maneno kuntu,maneno ya hisia VERGA amsimulie mgambo wake yule!
"bosi wangu! jambo doncho sana ili!,ili ni jini mahaba na kuna ustadh! swadakta maalim! sheghe ni shidaaaa! hana uwezo wa kumwita! kumpumbaza! kumkamata na kumfinyanga hadi aitwe marehemu anaitwa maalim sheghe RAJAB!"
"unaweza kunipeleka saivi kwa maalim?"
"bila shaka kabosi kangu! lakini pale kagetini katakaa kanani?"
"uc of pale ntamtafuta mtu mwingine"
"akah! na mimi si ntakosa ka kazi bos?!"
"hapana we ntakupandisha cheo utaenda katika compuny yang na ela itapanda."
"sawa bosi ngoja nkajiandae ili tukaka angamize ako kajini mahaba!"
ile saa KITALU anageuka tu nyuma akakumbana na mkono dhabiti! mkono imara wa HUSNA! lakin VERGAN akumwona KITALU alihisi kukabwa ghafla akaanza kukooa damu alikuwa akionesha kidole shingoni alipokabwa mara akadondoka chini na kufa hapo hapo.HUSNA akiwa na uso wa hasira akaiangalia kwa chuki maiti ile akairuka na kuweka mikono juu akatoweka.VERGA alichanganyikiwa! kitalu hakuwa mzima na sasa ni marehemu! kivipi? bado lilikuwa swali lisilo na jibu
polisi walikuja na kumchukua VERGA na house garl wake JASMIN na mwili wa marehemu ukapelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.alama za mikono shingoni zilionekana dhahiri! hivyo madaktari wakaanza kudili nazo.
cha ajabu alama za mikononi za JOHN VERGAN ndo zilizo onekana shingoni mwa MLINZI MACHACHARI KITALU.mshatakiwa namba moja akawa JOHN akawekwa chini ya ulinzi! moyo ulimuuma maswali ya siyo na majibu yakatiririka kichwani kwake.familia yake baba mama zote walikuja kumtembelea wakamtoa khofu kwa kuweka mawakili hatari pesa si ilikwepo.tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ikafika.baada ya kuamishwa katika mahaka
****************
SERIKALI ikapandisha shaidi namba moja! ambaye alitambulika kama afande MARWA.
MWENDESHA MASHTAKA@"taja majina yako matatu"
SHAIDI NO 1@ "MARWA JAFETY JOHN"
MW/MASHTAK@ "Unaweza kutuambia kilichotokea siku ya tukio?"
SHAID NO 1 "Yap nilikuwa kituoni siku hiyo mara simu ikaita kupokea ni msichana aliyekuwa akilia alidai bosi wake alikuwa akimnyonga mlinzi wake ndipo nilipochukua afande wengine mpaka eneo la tukio tulipofika tulimkuta mtuhumiwa kashafanya mauaji ndo tukawaweka yeye na house garl chin ya ulinzi"
maelezo haya ya AFANDE marwa yalimshtua kila mtu akiwepo JOHN VERGAN ambaye yeye ndiyo aliyepiga simu polisi iweje aambiwe ni mfanyakazi wake? pia mawakili wake walitazamana kwa kutoamini wakisikiacho kesi kwa upande wao ilizidi kuwa ngumu na kwa upande wa house gar yule alishangaa kuambiwa eti alipiga simu wakati bosi wake ndo alipiga ilikuwaje? kuna nin? ilikuwa ni mkanganyiko katika mioyo yao katu awakujua kuwa:
wakati JOHN VERGAN anapiga simu kituoni sauti yake iliishia mule ndani lakin katika masikio ya afande MARWA ilisikika sauti ya binti akiongea kwa jazba,woga,huyu si mwingine ni JINI HUSNAT aliyeyameza maneno ya VERGAN na kuongea kama JASMIN.ndivyo ilivyokuwa.
MW/MASHTAKA "mshtakiwa una swali lolote kwa shaidi no 1"
VERGAN "ndyo mh! afande marwa mimi ndo nlikupigia simu iweje useme ni JASMINI kwa nini lakin inakuwa hivi?"
baada ya kuuliza swali VERGAN akaanza kulaumu ikabidi akatishwe na nafas kurudi upande wa mawakili itaendelea
SEHEMU YA TATU
MOURINE huku akiwa anatetemeka akamwangalia bosi wake!
"hapana bosi niliaribikiwa na gari"
"comon MOURINE kwa nini ukunambia kwa simu nikajua?"
"simu nayo iliisha chaji bosi...."
Wakati wakiendelea kuongea ghafla simu ya VERGAN ikaita alipoangalia kwenye scrini ilisomeka HUSNAT.
Ubongo wake ukatingishika! akampa ishara MOURINE aondoke
Kabla ajaipokea maswali yakaanza kutiririka katika kichwa chake!
"nani kampa namba zangu?"
aliwaza alikuwa na uhakika akumpa wala akuserv namba zake, ili kupata jibu akaamua kuipokea simu ile....
"alooo!" VERGAN alisema
"vipi sweet za kazi" sauti nyororo kama kinanda iliuliza VERGAN akaipuuza Na kwa hasira akamuuliza
"nani kakupa namba zangu?"
"si wewe sweet umenipa jana?"
"mimi sijakupa namba zangu"
"umenipa beby"
"sijakupa"
"umenipa!"
"ok ulikuwa unasemaje?" VERGAN aliuliza kwa hasira
"nilikuwa naitaji tuonane" HUSNA alisihi
"siwezi kuonana na wewe" VERGAN alijibu kwa jeuri akapokewa na kicheko kitamu kisha sauti laini ikafatia
"basi my love ntakuja hapo kazini jioni tuondoke wote!"
hapo hapo akakata simu ubongo wa VERGAN kwa mara nyingine ukatingishika idadi ya maswali yasiyo na majibu yakatiririka!
"uyu ni binadamu au jini?,anapafahamu hapa kazini?"
bila kujielewa akaanza kusarch namba ya HUSNA kusudi azipige
NO AZIKWEPO!!!
hakuweza kujizuia kutetemeka akaziangalia kwenye recevid
kwenye recevd azikwepo!!!
wakati akiwa katika mawazo ya sintofahamu ghafla meseji ikaingia katika simu yake
"usiwaze sana dear utaumwa na kichwa"
namba zilikuwa na jina tu
JINA BILA NAMBA?
akazipiga zikakataa!
Azikutambulika na mtandao ule wa simu!
Lakini si ndo hizo zilizomtumia msg,?!
moyo ukaanza kumwenda mbio akaishika simu ya mezani na kumpigia secretary wake MOURINE
"naomba mwambie ZUBERI namwitaji ofisini kwangu" baada ya maneno Yale akakata simu
dakika chache badae ZUBER aliingia
Vergan akamwonesha ishara aketi
alikuwa ni kijana mrefu,alikuwa ndo meneja baada ya yeye ZUBER ndo alikuwa chini yake alimwamini kijana yule alikuwa ndo mshauri wake,siri zake ZUBERI alizijua,siri za ZUBER naye alizijua
Kwa kivipi walikuwa ni zaidi ya marafiki waloshibana,waloshauriana....
Zuberi akupata tabu kugundua bosi wake yule au rafiki yake yule yupo katika matatizo makubwa
Hiyo ni baada ya kuisoma simanzi ilotawaliwa na majonzi pamoja na woga katika uso wake ule
"Nimeitikia wito bosi"
Zuberi akatamka kwa sauti ya upole,akimwangalia kwa mashaka Vergan
VERGAN alimweleza ZUBERI kila kitu!,akimwacha kijana yule katika mshangao wa hali ya juu wa kutokuamini Yale aelezwayo....
Mwisho akatoa ushauri wake akitanguliza pole,
,"dah pole bosi huyo atakuwa ni jini tu! kubali ukatae! kwanza embu nioneshe hizo msg zake! maana siamin kabisa!"
VERGAN akatii na kuchomoa simu yake mfukoni akaanza kutafuta zile meseji inbox
'MESEJI HAZIKWEPO'
na anakumbuka akuzifuta kabisa! bumbuwazi likauvaa uso wake
"kah meseji azipo kak!"
"nini?" ZUBER akaoji kwa mshangao
"sijazifuta lakini nashangaa kutoziona!"
"basi BOSI jibu ndo ilo huyo atakuwa ni jini mahaba!"
"sasa nfanyeje rafiki yangu?"
"kuna mtaalamu namfahamu ntakupeleka"
"hapana best mim ni msomi siamini hao watu wengi wao matapeli....."
Katika vitu ambavyo JOHN VERGAN akuvipenda ni kuamini ushirikina
"mganga wa kienyeji!"
ZUBER alijaribu kumbembeleza lakin VERGAN akuwa tayari,mwisho akakata na tamaa!
Zuberi akaaga akihaidi kurejea baada ya kupata wazo lengine, akamwacha bosi wake katika mawazo Yale....
"ina maana uyu ni mtu au jini?" bado maswali yasiyo na majibu yaliambaa katika kichwa chake.
"sura ya HUSNAT ikamjia kichwani mwake wakati walivyokuwa wakifanya mapenzi"
miguno ya kimapenzi na hata sura yake alivyoikunja,utamu alokuwa nao,HISIA zikampanda,na ghafla tabasamu likamponyoka.
"atakuwa ni binadamu anacheza na akili yangu tu!"
akajifariji upendo moyon mwake ukafumuka kama mvua za masika
ALIANZA KUMPENDA!.
Akashangaa kumpenda ghafla kiasi icho! moyo wake aliujua vyema.
Aukuwa wa mtu aliyeyaendekeza mapenz akupenda kujiumiza kichwa kama kwa MOURINE aliyepanga kumuoa,lakini MOURINE anamzingua,
alipobahatika kumuona HUSNA akajua jibu lake limepatikana lakini vitabia tabia vyake vinamshangaza naye ni jini?
aoe jini?!!
"no siwezi kumpenda HUSNA!"
akapingana kwa nguvu na HISIA zake
ilipofika jioni wakati anajiandaa kuondoka ghafla mlango ukafunguliwa na HUSNAT akaingia na tabasamu pana usoni
Uzuri wake ulikuwa mara mbili ya mwanzo bumbuwazi likauvaa uso wa VERGA akutegemea kama angekuja kweli
mbona secretary wake ajampgia simu?
Na alikuwa kawaida mgeni kuingia bila 'secretary' wake kumpigia naye ndo amruhusu!
Lakini huyu!!!......
Verga alijawa na khofu ulochanganyikana na woga
ilikuwa lazima aogope alikuwa kavaa gauni jekundu refu lililo mkaa vyema, akaenda kuketi kwenye viti vya wageni na kumpa mkono Vergan aliyekuwa bado akitetemeka.....
nini kitaendelea hapo?!
ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: