Home → simulizi
→ 'CHOMBEZO YA MAPENZI'
'INAITWA'
'NANII TAMU!?.'
KUTOKA;BUKOBA TZ
EPISODE;02
Ilipoishia iliishia pale....
Wasimamizi wakiwa bado wanaendelea kukagua mara mwanafunzi mmoja wa kiume alitupa kitu fulani pembeni ya msimamizi, Msimamizi baada ya kuona kitu hicho alianza kuulizia kuwa ni nani aliyekitupa na alionekana kuchukizwa sana!!??..
Sasa endelea nayo..
Msimamizi aliendelea kuuliza pasipokujibiwa bali macho tu, ndo yalimtazama
'Hivi nyie wanafunzi mlishawai kusikia shule fulani imefungia kufanya mtihani au'. Msimamizi aliongea huku akiwa anaonekana wazi kuchukizwa na kitendo cha kuuliza pasipokujibiwa na mtu na wasimamizi wengine walidakia na kuanza kutuuliza kwa ukali sana.
Mkuu wa shule alikuja na baada ya kuja alielezewa na wale wasimamizi kuhusu kitu kilichokuwa kimetupwa pembeni ya msimamizi.
'Jamani wanafunzi haya ndo mnakuja kufanya tamati yaani ya kumrushia msimamizi kondomu eheee'. Mkuu wa shule aliongea huku akiwa ametutazama kwa ukali sana. Kila mwanafunzi alionekana wazi kuwa mgumu kutaja.
'Sikia wanafunzi ni nani ambaye amefanya hivi na mtu akijitokeza nitamsamehe'. Mkuu wa shule safari hii aliongea kwa ukarimu sana. Lakini hakuna mtu aliyejitoa kuwa ni yeye kuwa amerusha hiyo kondomu. Kwamaana kila mwanafunzi alimfahamu mwalimu mkuu jinsi ya kumpata mtu huwa anabadilika na kujifanya kuwa hakuna kilichotokea na hatimae baada ya kukiri kosa,mkuu wa shule hakuwa na huruma kwani alikuwa akifuza wanafunzi wanaokiri makosa yao, hivyo safari hii hakuna aliyejitokeza alisisitiza kipindi akiendelea kusisitiza mmoja wa maaskari aliwasogelea wasimamizi na kutuombea msamaha na kweli wasimamizi walilidhia japokuwa kama nusu saa ilikuwa imetuacha ya kufanya mtihani na unajua kuwa mtihani wa taifa ni lazima kwenda na wakati. Baada ya kuingia kwenye mtihani huo wa hisabati sikuwa najua kitu hivyo nilimshukuru sana Mungu kwa mkasa huo uliotokea na kuchukua muda.
Baada ya dakika kuisha msimamizi alisimama na kusema kuwa dakika zimeisha hivyo tulikusanya, kidaftari ambacho tulikuwa tumejibia. 'Vijana mnaona mlivyochezea muda mpaka wengine amjamaliza'!?. Msimamizi aliongea huku anatazama mitihani yetu kwa baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakileta mitihani yao huku wakionekana wazi kuwa na hawajamaliza kazi na wengine kama wakina sisi ambao hisabati ilikuwa mafuta na maji tulimshukuru sana Mungu kwa hilo.
Na hatimae mtihani wa kwanza tuliweza kumaliza,hivyo baada ya kutoka nje kila mwanafunzi alionekana kuwa bize na kusoma kipindi ambacho kilikuwa kinafuata,
kipindi ambacho kilikuwa kinafuata ni kiswahili somo ambalo nilikuwa nalipenda sana na pia katika mitihani ya kawaida ya shule nilikuwa nawabuluza darasa zima.
'David naomba unielekeze jinsi ya kupanga sentensi hizi na pia unipe pointi za wajerumani walivyokuja Tanganyika walikuja na dhana gani au sera gani'?. Nilimtazana nani aliyekuwa akiniuliza uso ulisinyaa na mwili ulijawa na msisiko baada ya kumuona Suzi akiwa mbele yangu huku akiwa ameshikilia daftari fulani.
'Ahaaaamna shida kaa basi nikuelekeze au huko tayari nikuelekeze umesimama au'?. Nilimjibu kwa taabu sana maana mapigo ya moyo yalienda kwa kasi sana kuzidi spidi yake ya mwanzo.
Nilimwelekeza na kumpa majibu yote na kisha Suzi baada ya kumuelekeza alinitazama na kisha alinishukuru na kwenda zake.
Nilibaki domo wazi baada ya kuona suzi akiondoka 'David we domo zege kila siku huyo demu anajileta harafu wewe unajifanya huoni'. Alikuwa ni rafiki yangu tulieshibana sana Frank.
'Frank sasa leo ndo unataka nimwambie au maana na mimi nimedata akyamungu nikimaliza lazima nionje hiyo nanii yake kama ni tamu'?. Niliongea huku nimemtazama Frank na huku nikitupia macho kwa kuibia alipo suzi.
Suzi alikuwa ni msichana ambaye kila mvulana wa pale shuleni alikuwa akitamani kuduu nae na pia hata walimu nao walitaka kutoka nae, kwamaana alikuwa ni msichana mwenye umbo zuri sana na pia sura yake ilivutia sana. Mpaka katika shule yetu tuliweza kumtunuku jina la 'Mrembo wa shule'. Mazoea ya mimi na Suzi yalianza kama masihala baada ya Mwalimu wa kiswahili kupanga makundi na kundi ambalo aliniweka ndo sehemu ambayo suzi alikuwa amewekwa, hivyo mwalimu wa kiswahili alivyokuwa akitupa kazi nilikuwa nikifanya hiyo kazi kwa kushirikiana na Suzi sana. Lakini niliweza kuzama kwenye mapenzi baada ya siku moja kugusana kwa bahati mbaya kwenye midomo yake baada ya dawati moja tulilokuwa tumekalia kusumizwa na mwanafunzi. Kitendo cha kugusana midomo Moyo ulinilipuka sana na pia ulidunda pasipo kawaida yake.
Nikiwa bado niko nawaza hayo mara kengele iligongwa nilitoka hapo kwa haraka na kwenda mpaka kwenye mstari, baada ya kufika mkuu wa shule alipiga makofi kuashilia kuwa tuache kelele
'Wanafunzi wangu leo mmenihudhi sana, na pia sasa ni muda wa kula hivyo nenda kwenye sehemu ya kulia na baada ya kula mtaingia kwenye hall ili muendelee na mtihani'. Mkuu wa shule baada ya kusema hivyo alirudi ofisini kwake.
Wanafunzj sote tulienda mpaka kwenye sehemu ambayo tulikuwa tunaitumia kulia, tulikula baada ya kula tulienda kwenye hall ili tuweze kuendelea na kufanya mtihani. Na kweli baada ya wasimamizi nao kula walikuja kwenye hall na kuanza kutugawia karatasi ya mtihani na kijidaftari cha kufanyia mtihani. Niliweza kubahatika kufanya mtihani vema huo na kuweza kujiesabia ushindi wa mtihani huo. Na kisha sote tulirusiwa kurudi nyumbani baada ya kumaliza mtihani huku tukisisitizwa kuwa tuwai, nikiwa njiani naelekea barabarani ili niweze kupanda pikipiki,
'Davi, davi,davi,'!?. Sikuweza kujua ni nani maana wanafunzi walikuwa wengi mbele yangu na nyuma yangu hivyo ilinibidi nimsubilie huyo aliyekuwa akiniita. Baada ya kumsubilia kitendo cha dakika kama dakika ishirini sikuweza kuona mtu bali niliona wanafunzi wakiisha katika safari hiyo. Nilianza safari ya kuondoka baada ya kuona mtu aliyekuwa akiniita simuoni
'Davi, mbona wewe si mvumilivu hivyo'?. Nilishutuka sana baada ya kusikia sauti ya kudeka ikiwa inaongea. Niligeuka mara macho kwa macho na Suzi na safari hii tulikuwa wawili njiani, Suzi alikuja kwa kasi sana na kunikumbatia.
'Hivi mtihani wa kiswahili umeuonaje na pia umeniona nilivyohotea'. Suzi alijinadi baada ya kuniuliza maswali na maswali kuletwa kwenye mtihani.
'Mtihani ulikuwa poa sana ila unaposibo maana ulivyoniuliza ndivyo vimekuja'?. Nilimjibu huku nikimtazama usoni kwa umakini sana.
'Kweli ninayo ila nimekuibia siri kwamaana Nakupenda nitakupa ila kuna karatasi fulani hiko kwenye peipa ambalo kesho tutafanya hivyo isome kabla ya kupitia hizo peipa'?. Suzi aliongea huku akibetubetua midomo kwa kuonekana wazi kuwa anadeko.
'Asante sana na mimi Nakupenda ila sasa wewe umeishaikopi au'?. Ilinibidi nimuulizie hivyo kwamaana alionekana kuwa na karatasi moja ya mtihani. 'Hapana usiwe na shaka nimeishatoa kopi hii ilikuwa kwa ajiri yako'?. Suzi aliongea huku akiwa ananikabidhi hizo karatasi na kisha baada ya kunikabidhi alipanda pikipiki na kuondoka.
Na mimi ilinibidi nisimamishe pikipiki baada ya kuisimamisha nilipanda pikipiki,mpaka iliponifikisha nyumbani baada ya kunifikisha nyumbani niliweka begi langu chini baada ya kuweka nilienda kuoga, baada ya kumaliza kuoga niliweza kumkuta mdogo wangu Filipo akiwa na kibarua fulani huku akicheka!!??...
JE:
Barua hiyo ilikuwa imeandikwaje na pia nini hatima ya mimi na suzi!!??...
Huu bado ni mwanzo wa chombezo yetu bado mambo hayajawai sawia..
Hivyo usikose kipande hata kimoja cha chombezo yetu ya NANII TAMU!?.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: