Home → simulizi
→ SHANGAZI ANATAKA
STORY NA 🅱
SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE :licha ya kupeana mashariti ya kwamba, akuna kuonjana mpaka wamalize shule na kufunga
ndoa, lakini wote walipendana sana, ungewakuta muda wote wakiwa pamoja, wakionekana wanafuraha sana, wakifurahia uhusiano
wao, Ulipita muda mrefu sana atimae, wakamaliza kidato cha nne, wakati wanasubiri matokeo ya mitihani wa taifa, baba yake
Stella yani Dr lazaro, aliamishwa tena nakurudishwa Dar es salaam, safari hii akipelkwa Hospital ya muhimbili, kwenye chuo
cha sayansi natiba, MUHAS, kiukweli ilikuwa nisiku ngumu sana kwao, ambayo ilipelekea kila mmoja wao asiisahau mpakaleo
wanaposimuliana mkasa huu, wote waliumia sana moyoni, kwani kila mmoja aliamini pengine mwenzie angetafuta mpenzi wingine na
kumsaau yeye, Asa Joseph ambae alijiona nimwenye bahati sana kuwa na mschana mrembo kama huyu, endelea.... "kweli sina
bahati" aliwaza Joseph ambae aliamini kutokana na uzuri wa Stellah asingeweza kukosa mtu wakuwa nae, lakini kwaupande wa
Stellah aliamini kuwa Joseph ata msubiri tu, kutokana na jinsi alivyo mwona kwa kipindi walicho kuwa pamoja, alimwona kuwa
ni mvulana mstaarabu sana tena mvumilivu, hivyo lazima angeweza kuvumilia na kumngojea, kwani kwa upande wake alikuwa
nauakika wa kuwa mwaminifu kwa mpenzi wake huyu, licha ya kupeana moyo wa kukutana tena lakini ukweli ni kwamba siku ilikuwa
Ngumu sana kwa wawili hawa, kila mmoja akiamini pengine mwenzie angeteleza na kutafuta mpenzi wingine nakumsaau yeye,
wakatafuta kitu ambacho kitawafanya watunze kumbukumbu ya penzi lao, na pasitokee mmoja kumsaliti mwenzake, waliamua kuweka
agano (kihapo) lakuishi pamoja, walichokifanya walikuchukua kisu nakujichanja kwenye kidole kidogo cha mwisho, kisha waka
viunganisha vidole vyao vikiwa vina churuzika damu, (kuwa kama mchezo wa kitoto wa pingana) yani kukubaliana, wakapeana
ahadi ya kuwa pamoja maisha yao yote,
Siku ilifika Stella na baba yake walianza kuelekea safari ya dar, wakiwa wame agana na familia ya kina Joseph pia
wakiwa wame waachia bahadhi ya vifaa vyandani ambavo waliona vitakuwa mzigo kwaa, aidha kwakuwa dar vipo au walikuwa na
uwezo wa kununua vingine wakifika dar, miezi mitatu baadae urafiki wa familia hizi mbili ulikuwa umepungua, baada ya baba
yake Stella kuamia Dar es salaam, ila ulibakia urafiki wa Joseph na Stellah tu, ambao kwa sasa walitumia mawasiliano ya njia
ya barua, Joseph akiwa na soma chuo cha ufundi, kinacho milikiwa na shirika moja la kidini, wakati Stellah alikuwa anasoma
kidato cha tano shule ya sekondali ya jangwani, kiukweli Stellah alikuwa msaada mkubwa kwa Joseph, kuhusu mambo ya ada na
matumizi pamoja namichango mbalimbali ya chuo, maana yeye ndie alie mshawishi Joseph kujiunga nachuo hicho, akiahidi
kumsaidia kwenye gharama za chuo, baada ya kupata matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne, Stellah alituma fedha kwa
Joseph, ambazo zilimsaidia sana katika matumaizi yake, nakumfanya aonekane kijana mtanashati, wanawake pia wakaanza
kujisogeza kwake, kwa kifupi Stellah akisaidiwa na baba yake Dr Lazaro na mama yake ambae alisha fahamu urafiki wa mwanae na
kijana huyu, Stellah alitumia fedha nyingi sana kumsaidia mpenzi wake huyo, ambae alitambua fika kwamba kwao awakuwa nauwezo
kifedha, napia alimsaidia kama mume wake mtarajiwa, siku zote Stella alikuwa akikwepa kujiingiza kwenye mapenzi, akitunza
ahadi aliyoiweka na Joseph, asa alipokuwa akiangalia jelaha dogo kwenye idole chake cha mwisho,
Joseph na Stella waliendelea kuwasiliana kwa barua wakitumiana picha na post card za mapenzi, wakipeana moyo kuwa
wakimaliza shule wangeanza rasmi kukutana kimwili, lakini mambo yalibadirika, baada ya Joseph kumaliza chuo cha ufundi na
kuajiriwa kwenye idara ya usalama, sekta ya ulinzi na usalama, kama fundi wa magari, kiukweli Joseph alipunguza mawasiliano
ya barua kwa Stellah, ata Stellah alipotuma barua zaidi ya tatu yeye alijibu moja, wakati huo Stella akiwa mwaka wa kwanza
chuo cha ma Doctor kule upanga, akisomea degree ya kwanza ya u’doctor chuo kikuu cha muhimbili, msimu walikizo yake ya pili,
akiwa chuoni alionelea aende songea kumtembelea mpenzi Joseph, na kutokana na mawasiliano kuwa magumu barua ambayo ilitumia
week mbili kufika songea kwa kipindi hicho, Stellah alijikuta akienda Songea bila taharifa kwa mpenzi wake huyo, kwakuwa
alikuwa anapajuwa nyumbani kwa kina Joseph, nawao wanamjuwa vyema, akaona hisinge kuwa shida kwake kufikia kwakina Joseph,
Week mbili baadae jioni moja, Stella alikuwa anaingia nyumbani kwakina Joseph, alipokelewa vizuri sana na ndugu zake
Joseph, wakimwita dada kama walivyozowea, nayeye akiwaita dada kama alivyo zowea toka zamani, lakini hakumwona Joseph wala
dalili ya uwepo wa Joseph pale nyumbani, lipo muulizia akaambiwa kuwa Joseph hivi sasa anaishi mjini, amepanga mtaa wa bomba
mbili, dada alie mwachia ziwa Joseph, ambae alikuwa anamchumba wake pale pale mtaa wa Mateka, akahaidi kumpeleka nyumbani
kwa Joseph kesho yake, sababu muda ulikuwa umeenda sana, maana aliingia songea mida ya saa mbili usiku, ilipo fika siku ya
pili, yule dada wa Joseph aliongozana na Stella mpaka nyumbani kwa Joseph, kiukweli Joseph hakuwepo, lakini walimkuta
mwanamke mmoja akiwa amebeba mtoto mwenye umri wa week mbili, akatambulishwa kuwa nimke wa Joseph, ni mwalimu washule ya
msingi sokoine iliyopo pale pale bombambili, na sasa yupo likizo ya uzazi, dada wa Joseph akiwa hajuwi lolote juu ya
uhusiano wa Stella na Joseph, akamtambulisha yule wifi yake mwenye mtoto, kuwa Stella ni ndugu yao, anasoma chuo kikuu huko
dar es salaam, basi waliongea kwa pamoja, huku Stella akiwa anajizuwia kuonyesha machungu aliyokuwa nayo moyoni, walikaa
mpaka jioni aliporudi Joseph, na kumkuta Stella akiwa amempakata mtoto wake wa kwanza wakiume, anayeitwa Jayden, Joseph
alistuka sana kumkuta Stella pale nyumbani, kiukweli alijiona msaliti mkbwa, japo hakujari sana maumivu ya Stella, alikuwa
amesaau misaada na upendo alio uonyesha kwake, Joseph alionelea bora, amtoe Stella pembeni kidogo na pale kwake, ili
wakaongee juu ya swala lile, Stellah hakiwa ameficha machungu ya moyoni mwake aliongozana na Joseph wakaenda kukaa ehemu
moja ya jirani, wakiwahacha dada yake Joseph na mama jayden nyumbani wakiwa hawaelewi kinacho endelea, Walienda kukaa maeneo
ya jirani katika bar moja nakukaa, wakitazamana, macho ya Stella yalishaanza kutokwa na machozi, ukweli sura yake nzuri
ilikuwa ikitia huruma, Joseph alishindwa kumtazama usoni Stella, “Joseph kanini umenifanyia hivi?” swalia la Stella ambalo
Joseph alishindwa kulijibu, akabaki ameinamia chini, “Joseph kwanini umeamua kuniumiza mpenzi wangu?, yani yote niliyo
kufanyia nikazi bure” aliongea Stella huku machozi yakizidi kumtoka na sauti yake ikianza kuambatana na kilio, “Stella
naomba unisamehe, kiukweli sikuwa na maana ya kukuumiza,” aliongea Joseph kwasauti ya kubembeleza, “sasa ulikuwa una maana
gani, Jose?, Hen! niambie ulikuwa namaana gani?” hapo Joseph hakuwa najibu “au kwasababu hatujawai kufanya mapenzi?,
si’ungepunguza hamu alafu ungenisubiri?” hapo Stella akatulia kidogo, akatoa kitambaa chake na kujifuta machozi, kusha aka
mtazama Joseph, “ok! Jose akuna, ubaya wewe nimwanamume, basi mimi naomba uniowe na mimi niwe mke wako wapili” aliongea
Stella hakionyesha akuwa na utani, kauli hiyo ilimstua sana Joseph, UNAZANI JOSEPH ALIJIBU NINI? ILIKUJUWA KISA NA MKASA HUU
ENDELEA KU LIKE NA KUCOMMENT KISHA TUWE PAMOJA, MPAKA MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: