KURUDI KWA MOZA: 10 Kwakweli taarifa hii iliraluwa moyo wa Rose, na kujikuta akichanganyikiwa sana, na alipouliza zaidi kuhusu gari iliyomgonga wale vijana walimtajia na hapo hapo akagundua kuwa ndio ile gari yake, Rose akaanguka na kuzimia. Ikabidi waanze kumpepea pale, yani mke wa babu alichanganyikiwa na taarifa ile ila akajua Rose imdmchanganya kutokana na mambo yanayomsibu. Rose alipepewa pale hadi akazinduka na aliona watu wanaanza kusogea nyumbani pale, kwakweli Rose alijiona kama yupo ndotoni kwani kila kitu kilitokea kwake bila ya matarajio, akamuita tena Yule kijana aliyeleta taarifa mwanzoni ili amuulize vizuri maana alihisi kama sio kweli vile, “Hebu niambie vizuri ilikuwaje?” “Yani mimi nilikuwepo kabisa eneo la tukio, babu alikuwa anavuka barabara mara ikatokea gari sijui mwenye gari alikuwa amelewa Yule yani alimgonga babu na kuondoka, tulijaribu kumpigia kelele ili asimamishe hakufanya hivyo. Pale tulipokuwepo ni mbali na hospitali, na msaada ulipatikana badae kabisa tena tulimpeleka babu na baskeli mpaka hospitali na kufika alikata roho hapo hapo, daktari akasema ni kwavile tumemchelewesha” Hapo ndio Rose akaelewa kabisa kuwa hiyo ajali ameisababisha yeye na kumfanya achanganyikiwe zaidi ila akaogopa kuropoka kuwa amesababisha ajali klwani alijua angezua mengine makubwa zaidi. Akawaza kimoyo moyo, “Sijui hata nifanyeje? Sina la kufanya kwakweli ngoja tu nisubirie pakuche halafu nitajua cha kufanya” Alikuwa na mawazo mengi sana. Kwakweli leo Sara ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala pamoja na mdogo wake Ana, kwahiyo siku zote huwa hajui kinachoendelea kwa Ana. Usingizi kwa upande wa Sara kwa siku ya leo ulikuwa ni wa mang’amung’amu sana kwani bado taswira ya makaburini ilimjia kichwani, akiwa kwenye usingizi wa kuvizia akamuona Ana akinyanyuka kitandani lakini alihisi kuwa Ana anaenda chooni kujisaidia. Ila Ana huyu alienda moja kwa moja dirishani na kutokea kwenye dirisha, kitendo hiko kilimshtua sana Sara na kumuogopesha, akajikuta akitazama pale ambapo Ana alilala mwanzoni. Kwakweli alistaajabu zaidi kwani alimuona Ana akiwa bado amelala hajitambui, jasho la uoga lilianza kumtoka Sara, ni kweli Ana ni mdogo wake ila matendo ya namna hii hajawahi kuyashuhudia kabisa. Sara alikuwa anaogopa hadi alianza kutetemeka kwa uoga, aliinuka haraka haraka na kukimbilia nje ya chumba huku akipiga kelele ambapo kaka zake walitoka na kumuuliza kuna nini, lakini bado alikuwa akilia kwa kelele nyingi, hadi kaka zake wakamshtua na kumuuliza kwa makini, “Sara, Sara una nini wewe?” Mara gafla akaja na Ana, kwakweli Sara ndio alizidi kuchanganyikiwa baada ya kumuona Ana na alikuwa akimnyooshea kidole, “Sasa mbona unamnyooshea kidole Ana kafanyaje?” “Ana ni……” Kabla hajamaliza sentensi yake, Ana alimuangalia kwa jicho kali sana dada yake na kumfanya dada yake azimie pale, wale mapacha wakamuangalia Ana na kumuuliza. “Kwani kapatwa na mimi?” “Jamani mi nitajuaje sasa!” “Utajuaje kivipi wakati ulilala nae!” “Nililala nae? Alilala na mimi muda gani?” “Mbona alikuja kulala na wewe” “Mi hata sijui kama alilala na mimi, kwanza ndio ustaarabu wa wapi unaenda kulala na mtu hata umwambii ili akukubalie au akukatalie. Hata sijui kilichompata kwani na mimi nilikuwa nimelala” Ilibidi wamuinue na kwenda nae sebleni ambapo waliendelea kumpepea ili azinduke huku wakitumaini kuwa akizinduka atawaeleza jambo. Mara Ana akawaambia, “Mnajisumbua tu kumpepea huyo, nendeni kamlazeni kitandani kwake halafu asubuhi akiamka ndio mtaongea nae” Walimpepea pale bila ya mafanikio ikabidi wachukue wazo la Ana, wakambeba Sara na kumpeleka chumbani kwake kumlaza kisha na wao wakarudi chumbani kwao. Kulipokucha asubuhi, hwa mapacha kabla hawajafanya lolote walienda kwanza kumuangalia dada yao ambapo walimuamsha ni kweli aliamka, ila walichomuuliza chochote hakuwajibu ndipo walipogundua kuwa dada yao amepoteza uwezo wa kuongea. “Sara, kuongea huwezi?” Alitingisha tu kichwa, kwa kifupi Sara hakuweza kusema chochote, walitoka na dada yao hadi sebleni wakijitahidi kumsaidi ya hapa na pale, Mr.Patrick alikuja na kushangaa huku akiuliza imekuwaje, “Inamaana baba hujasikia makelele ya usiku wakati dada Sara analia?” “Sijasikia chochote wanangu, yani leo nilijikuta nimelala hoi kabisa yani hoi sikujitambua mpaka kumekucha kwahiyo hakuna nilichosikia” Basi wakamueleza kinagaubaga kilichotokea hata yeye alibakia anastaajabu tu kwani bado ukweli alikuwa nao Sara pekee ila kusema tu ndio alikuwa hawezi kwani aliondolewa uwezo wa kusema. Ana alitoka na kuwaaga kuwa anaenda shule, Patrick akamuuliza Ana, “Kwahiyo huna hata mashaka na mama yako hajarudi hadi leo, na vipi dada yako aliyepatwa na ugonjwa wa gafla haongei. Hivi unapata wapi nguvu za kwenda shuleni Ana?” “Elimu ndio ufunguo wa maisha, kama nyie mlikimbia shule shauri zenu ila mimi acha nisome kwa raha zangu” “Laiti kama kusoma kungekuwa unavyosoma wewe basi walimu wote Tanzania wangeacha kazi” “Unanikosea heshima baba” “Naomba unisamehe, haya nenda shule mwanangu” Ana aliondoka zake ila inaonyesha alikuwa amekasirika vilivyo. Kulwa alimuangalia baba yao na kumuuliza, “Baba unafahamu nini kuhusu Ana?” “Ni mengi tu nayafahamu, huyu mtoto mbaya sana. Ndiye anafanyaga nilale kama mzigo” “Hebu tueleweshe baba” Mara Ana akarudi ndani, kisha akamuangalia baba yao na kusema, “Nimeghairi kwenda shule” Wote walimtazama Ana kwani ni maamuzi ya gafla ameyafanya, ila hawakumuuliza tena wala hawakuendelea kumuuliza baba yao mabaya ya Ana kwani ni wazi asingeweza kuwaeleza wakati Ana yuko pale. Kulikucha sasa nyumbani kwakina Salome pia ila leo Salome aligoma kwenda shule, “Kheee makubwa, mwanangu leo kwenda shule hutaki?” “Siendi mama, ila ungeenda kuniomnbea nipumzike kwa muda najiona siko sawa, kwakweli siwezi kwenda shule kwasasa” Ashura nae akaingilia kati, “Dada, kama hataki kwenda shule achana nae. Sio lazima shule, mwache azulule zulule akipata mimba ndio ataelewa” “Kheee Ashura ndio maneno gani hayo kwa mwanangu, badala umbembeleze na wewe ndio unamkandamiza” “Namkandamiza kitu gani, kwanza mtu mwenyewe vitu vingine anaongea hata haeleweki kama sio msomi na ndiomana jana sijampikia hizo nyanyachungu zake” “Kwanini?” “Atasemaje tumpikie ngoga eti ndio nyanyachungu wakati zinaitwa ngogwe” “Aaah kumbe ndio zinaitwa hivyo” “Wewe hukujua kama amekupiga changa la macho huyu tujue anajua Kiswahili kumbe hajui lolote, eti nipikieni ugali, samaki na ngoga. Katafute hiyo ngoga kama utaipata, hata sijui kaongea kilugha cha wapi” “Ila Ashura ni swala tu la kumuelekeza mtoto kuwa sio ngoga ni ngogwe, huyu bado mtoto anajifunza vitu. Ni kumuelekeza tu, mi mwenyewe mtu mzima sijui sembuse huyu mtoto jamani mmh!” “Kuwa makini na mtoto wako dada, kuwa naye makini sana” Ashura alitoka muda huo na kusema kuwa anawahi sokoni ili akanunue vitu, kwahiyo Neema alimuongeza na hela kidogo. Nyumbani akabaki Salome na mama yake, ila leo Salome alimuuliza mama yake swali ambalo mama yake hajawahi kutegemea kama angeulizwa na Salome. “Mama, hivi wewe na Ashura undugu wenu uko vipi?” “Halafu nishakwambia kuwa na adabu, Yule ni mamako mdogo ni mdogo wangu. Usimwitage Ashura” “Nisamehe kwa hilo mama, ila ningependa kujua huyu mamdogo na wewe ni mdogo wako kivipi? Na ndugu zako wengine wako wapi sijawahi kuwaona?” “Mmmh Salome jamani, si mwezi uliopita tu nilikupeleka kwa kaka yangu, tuseme ushasahau!” “Haya mama, tuachane na hayo ila huyu mamdogo ni ndugu yako kivipi kuna jambo nataka nikueleze niambie kwanza undugu wenu ndio nikueleze” “Sikia, mimi baba yangu na mama yangu walikuwa hawaishi pamoja na kwa upande wa mama na baba, mimi ni mtoto wao wa pekee sana ila kumbe baba alikuwa na mtoto mwingine ila sio mtoto aliyezaa na mkewe waliyokuwa wanaishi nae. Mimi kwa mama tumezaliwa wawili tu, yani mimi na kaka yangu niliyekupeleka kwake mwezi uliopita. Hatuna mazoea ya karibu sababu Yule kaka alikulia nyumbani kwa baba yake. Ila mama ndio alinitambulisha kama ni kaka yangu. Sasa kwa upande wa Ashura ni mtoto wa baba kumbe naye alikuwa analelewa na mama yake, yeye ndio alinitafuta mimi kwakweli alipojitambulisha nilifurahi sana kwani nilipata ndugu hadi leo niko nae.” “Mmmh kwahiyo ulimpeleka kwa baba yako akutambulishe?” “Baba alishakufa kitambo sana, na laiti kama angekuwa hai basi ningempeleka” “Na huyo mke wa babu si yupo, kwanini usimpeleke akutambulishe” “Sasa huyo atakuwa anajua vinini, kwanza wanitambulishe nini wakati mtu alishajitambulisha na tunaishia nae hadi leo” “Je shangazi zenu na baba zenu wakubwa au wadogo mnawatembeleaga” “Wapo kijijini, kwakweli hatujawahi kupanga safari ya kuwatembelea. Inatia uvivu ujue halafu hatujawazoea” “Mmmh na kaburi la baba yenu je mmewahi kwenda kulitembelea?” “Tunapangaga kufanya hivyo ila hata sijui inatokeaga nini, tunajikuta hatujaenda” “Mama, ngoja nikwambie kitu. Huyu unayemuita mdogo wako si ndugu yako” “Salome, si ndugu yangu kivipi?” “Wewe nielewe tu mama ila si ndugu yako na kama hujui shauri zako, atakapokufanyia kitu kibaya ndio utashtuka. Na angekuwa amekufanyia kitu kibaya mud asana, ila wewe unalindwa na mzimu wa baba yako. Huna kosa na wala hustahili kufanyiwa mambo mabaya, ila kwa kifupi huyu si ndugu yako, Tafakari, maswali niliyokuuliza na majibu uliyonipa halafu chukua hatua” Salome aliinuka na kwenda kuoga, muda huu Neema alibaki kwenye lindi la mawazo kwani hajawahi kufikiria hata mara moja kuwa Ashura anaweza akawa si ndugu yake, “Jamani huyu Salome mbona ananitisha, halafu yeye kajuaje kama huyu si ndugu yangu? Hivi inawezekana kweli nimeishi siku zote na mtu asiye ndugu yangu huku nikiamini ni ndugu yangu! Haiwezekani jamani” Neema aliwaza sana bila ya kupata jibu la aina yoyote ile, ingawa kuna mashaka aliyapata kwa jinsi alivyoambiwa na Salome. Akajikuta akimsubiria kwa hamu Ashura atakaporudi ili amuulize baadhi ya maswali, “Lakini hata hivyo, kama ni kweli si ndugu yangu ni kwanini amenidanganya? Hivi inawezekana kweli! Hapana nahisi Salome kachanganyikiwa tu” Muda kidogo Ashura nae alirudi, na Neema alijikuta akimuuliza, “Hivi Yule mke aliyekuwa anaishi na baba ulikuwa unamfahamu?” “Aah ndio, hapana hata sikumbuki” “Mbona sijakuelewa hapo, ulikuwa unamfahamu au la” “Nilikuwa mdogo sana, hata sikumbuki kama namfahamu au la” “Basi tupange siku tukamsalimie” “Mmmh umekumbuka kitu gani?” “Nimemkumbuka tu basi, najua atafurahi sana” “Sawa tutapanga” Ila Ashura alionekana kukosa furaha tangu Neema amuulize kuhusu mke wa baba yao. Rose alikuwa kwenye wakati mgumu sana na siku hii hakuweza kuendelea kuwepo tena pale msibani, aliamua kuwaaga kuwa anaenda kwanza nyumbani kwake halafu atarudi tena. Kiukweli alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa hivi, alijiona kama ameonewa kwa wakati huo. Mke wa babu alimfata Rose wakati anataka kuondoka, “Jamani, kweli unataka kutuacha wenyewe kweli kwenye wakati mgumu kama huu” “Hapana bibi, hujui tu jinsi msiba huu ulivyonichanganya hapa, nakosa hata uelekeo. Nina matatizo mzigo hata sijui naanzia wapi na kuishia wapi” “Naelewa kama una matatizo ila tafadhali usiondoke hadi tutakapozika” “Kwani mazishi ni lini?” “Ni leo, halafu kesho utaondoka. Tafadhali sana naomba usiondoke” Rose akajifikiria ila ikabidi apige simu nyumbani kwake kwani alijua ni wazi watakuwa na wasiwasi, na alimpigia simu Sara kwani anajuaga ndio kiherehere wa wasiwasi ila simu ya Sara iliita mara nyingi bila kupokelewa ikabidi ampigie simu mume wake, “Mbona Sara hapokei simu, au kaenda kazini leo?” “Hapana, Sara yupo ndani ila hawezi kuongea” “Hawezi kuongea kivipi?” “Sijui nikuelezeaje ila uwezo wa kuongea wa Sara umekatika gafla” “kheee jamani, mambo gani hayo? Ngoja nirudi le oleo” Rose akakata simu kisha akaenda tena kwa mke wa babu na kumpa taarifa za nyumbani kwake huku akimueleza kuwa anapaswa aende maana mwanae ni mgonjwa. Yule bibi hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumruhusu tu. Rose akapanda gari na kuondoka zake, alikuwa na mawazo mengi sana kushinda yale mawazo ya kwanza maana aliona kama matatizo yanamzidia ingawa kiuhalisia yeye ndiye chanzo cha matatizo yote. Wakati anaendesha gari akasikia sauti, “Rose, umenigonga nimekufa halafu kwenye maizshi yangu unakimbia!” Rose alishtuka na kusimamisha gari kwa haraka huku akiwa amejawa na hofu iliyomfanya ashindwe hata kutazama nyuma ya gari kuwa hiyo sauti inatoka wapi. Akiwa amejawa na hofu zaidi, ile sauti ikajirudia tena, na kumfanya Rose ashuke kabisa kwenye gari ile, alipokuwa chini akatazama kwenye kioo cha gari gafla alimuona kama Yule babu yupo ndani ya lile gari. Itaendelea kesho usiku…..!!!!! By, Atuganile Mwakalile Mapenzi na Maisha iko kwenye Facebook. Ili kuunganisha kwa Mapenzi na Maisha, jiunge kwenye Facebook leo. Jiunge au Ingia Mapenzi na Maisha KURUDI KWA MOZA: 10 Kwakweli taarifa hii iliraluwa moyo wa Rose, na kujikuta akichanganyikiwa sana, na alipouliza zaidi kuhusu gari iliyomgonga wale vijana walimtajia na hapo hapo akagundua kuwa ndio ile gari yake, Rose akaanguka na kuzimia. Ikabidi waanze kumpepea pale, yani mke wa babu alichanganyikiwa na taarifa ile ila akajua Rose imdmchanganya kutokana na mambo yanayomsibu. Rose alipepewa pale hadi akazinduka na aliona watu wanaanza kusogea nyumbani pale, kwakweli Rose alijiona kama yupo ndotoni kwani kila kitu kilitokea kwake bila ya matarajio, akamuita tena Yule kijana aliyeleta taarifa mwanzoni ili amuulize vizuri maana alihisi kama sio kweli vile, “Hebu niambie vizuri ilikuwaje?” “Yani mimi nilikuwepo kabisa eneo la tukio, babu alikuwa anavuka barabara mara ikatokea gari sijui mwenye gari alikuwa amelewa Yule yani alimgonga babu na kuondoka, tulijaribu kumpigia kelele ili asimamishe hakufanya hivyo. Pale tulipokuwepo ni mbali na hospitali, na msaada ulipatikana badae kabisa tena tulimpeleka babu na baskeli mpaka hospitali na kufika alikata roho hapo hapo, daktari akasema ni kwavile tumemchelewesha” Hapo ndio Rose akaelewa kabisa kuwa hiyo ajali ameisababisha yeye na kumfanya achanganyikiwe zaidi ila akaogopa kuropoka kuwa amesababisha ajali klwani alijua angezua mengine makubwa zaidi. Akawaza kimoyo moyo, “Sijui hata nifanyeje? Sina la kufanya kwakweli ngoja tu nisubirie pakuche halafu nitajua cha kufanya” Alikuwa na mawazo mengi sana. Kwakweli leo Sara ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala pamoja na mdogo wake Ana, kwahiyo siku zote huwa hajui kinachoendelea kwa Ana. Usingizi kwa upande wa Sara kwa siku ya leo ulikuwa ni wa mang’amung’amu sana kwani bado taswira ya makaburini ilimjia kichwani, akiwa kwenye usingizi wa kuvizia akamuona Ana akinyanyuka kitandani lakini alihisi kuwa Ana anaenda chooni kujisaidia. Ila Ana huyu alienda moja kwa moja dirishani na kutokea kwenye dirisha, kitendo hiko kilimshtua sana Sara na kumuogopesha, akajikuta akitazama pale ambapo Ana alilala mwanzoni. Kwakweli alistaajabu zaidi kwani alimuona Ana akiwa bado amelala hajitambui, jasho la uoga lilianza kumtoka Sara, ni kweli Ana ni mdogo wake ila matendo ya namna hii hajawahi kuyashuhudia kabisa. Sara alikuwa anaogopa hadi alianza kutetemeka kwa uoga, aliinuka haraka haraka na kukimbilia nje ya chumba huku akipiga kelele ambapo kaka zake walitoka na kumuuliza kuna nini, lakini bado alikuwa akilia kwa kelele nyingi, hadi kaka zake wakamshtua na kumuuliza kwa makini, “Sara, Sara una nini wewe?” Mara gafla akaja na Ana, kwakweli Sara ndio alizidi kuchanganyikiwa baada ya kumuona Ana na alikuwa akimnyooshea kidole, “Sasa mbona unamnyooshea kidole Ana kafanyaje?” “Ana ni……” Kabla hajamaliza sentensi yake, Ana alimuangalia kwa jicho kali sana dada yake na kumfanya dada yake azimie pale, wale mapacha wakamuangalia Ana na kumuuliza. “Kwani kapatwa na mimi?” “Jamani mi nitajuaje sasa!” “Utajuaje kivipi wakati ulilala nae!” “Nililala nae? Alilala na mimi muda gani?” “Mbona alikuja kulala na wewe” “Mi hata sijui kama alilala na mimi, kwanza ndio ustaarabu wa wapi unaenda kulala na mtu hata umwambii ili akukubalie au akukatalie. Hata sijui kilichompata kwani na mimi nilikuwa nimelala” Ilibidi wamuinue na kwenda nae sebleni ambapo waliendelea kumpepea ili azinduke huku wakitumaini kuwa akizinduka atawaeleza jambo. Mara Ana akawaambia, “Mnajisumbua tu kumpepea huyo, nendeni kamlazeni kitandani kwake halafu asubuhi akiamka ndio mtaongea nae” Walimpepea pale bila ya mafanikio ikabidi wachukue wazo la Ana, wakambeba Sara na kumpeleka chumbani kwake kumlaza kisha na wao wakarudi chumbani kwao. Kulipokucha asubuhi, hwa mapacha kabla hawajafanya lolote walienda kwanza kumuangalia dada yao ambapo walimuamsha ni kweli aliamka, ila walichomuuliza chochote hakuwajibu ndipo walipogundua kuwa dada yao amepoteza uwezo wa kuongea. “Sara, kuongea huwezi?” Alitingisha tu kichwa, kwa kifupi Sara hakuweza kusema chochote, walitoka na dada yao hadi sebleni wakijitahidi kumsaidi ya hapa na pale, Mr.Patrick alikuja na kushangaa huku akiuliza imekuwaje, “Inamaana baba hujasikia makelele ya usiku wakati dada Sara analia?” “Sijasikia chochote wanangu, yani leo nilijikuta nimelala hoi kabisa yani hoi sikujitambua mpaka kumekucha kwahiyo hakuna nilichosikia” Basi wakamueleza kinagaubaga kilichotokea hata yeye alibakia anastaajabu tu kwani bado ukweli alikuwa nao Sara pekee ila kusema tu ndio alikuwa hawezi kwani aliondolewa uwezo wa kusema. Ana alitoka na kuwaaga kuwa anaenda shule, Patrick akamuuliza Ana, “Kwahiyo huna hata mashaka na mama yako hajarudi hadi leo, na vipi dada yako aliyepatwa na ugonjwa wa gafla haongei. Hivi unapata wapi nguvu za kwenda shuleni Ana?” “Elimu ndio ufunguo wa maisha, kama nyie mlikimbia shule shauri zenu ila mimi acha nisome kwa raha zangu” “Laiti kama kusoma kungekuwa unavyosoma wewe basi walimu wote Tanzania wangeacha kazi” “Unanikosea heshima baba” “Naomba unisamehe, haya nenda shule mwanangu” Ana aliondoka zake ila inaonyesha alikuwa amekasirika vilivyo. Kulwa alimuangalia baba yao na kumuuliza, “Baba unafahamu nini kuhusu Ana?” “Ni mengi tu nayafahamu, huyu mtoto mbaya sana. Ndiye anafanyaga nilale kama mzigo” “Hebu tueleweshe baba” Mara Ana akarudi ndani, kisha akamuangalia baba yao na kusema, “Nimeghairi kwenda shule” Wote walimtazama Ana kwani ni maamuzi ya gafla ameyafanya, ila hawakumuuliza tena wala hawakuendelea kumuuliza baba yao mabaya ya Ana kwani ni wazi asingeweza kuwaeleza wakati Ana yuko pale. Kulikucha sasa nyumbani kwakina Salome pia ila leo Salome aligoma kwenda shule, “Kheee makubwa, mwanangu leo kwenda shule hutaki?” “Siendi mama, ila ungeenda kuniomnbea nipumzike kwa muda najiona siko sawa, kwakweli siwezi kwenda shule kwasasa” Ashura nae akaingilia kati, “Dada, kama hataki kwenda shule achana nae. Sio lazima shule, mwache azulule zulule akipata mimba ndio ataelewa” “Kheee Ashura ndio maneno gani hayo kwa mwanangu, badala umbembeleze na wewe ndio unamkandamiza” “Namkandamiza kitu gani, kwanza mtu mwenyewe vitu vingine anaongea hata haeleweki kama sio msomi na ndiomana jana sijampikia hizo nyanyachungu zake” “Kwanini?” “Atasemaje tumpikie ngoga eti ndio nyanyachungu wakati zinaitwa ngogwe” “Aaah kumbe ndio zinaitwa hivyo” “Wewe hukujua kama amekupiga changa la macho huyu tujue anajua Kiswahili kumbe hajui lolote, eti nipikieni ugali, samaki na ngoga. Katafute hiyo ngoga kama utaipata, hata sijui kaongea kilugha cha wapi” “Ila Ashura ni swala tu la kumuelekeza mtoto kuwa sio ngoga ni ngogwe, huyu bado mtoto anajifunza vitu. Ni kumuelekeza tu, mi mwenyewe mtu mzima sijui sembuse huyu mtoto jamani mmh!” “Kuwa makini na mtoto wako dada, kuwa naye makini sana” Ashura alitoka muda huo na kusema kuwa anawahi sokoni ili akanunue vitu, kwahiyo Neema alimuongeza na hela kidogo. Nyumbani akabaki Salome na mama yake, ila leo Salome alimuuliza mama yake swali ambalo mama yake hajawahi kutegemea kama angeulizwa na Salome. “Mama, hivi wewe na Ashura undugu wenu uko vipi?” “Halafu nishakwambia kuwa na adabu, Yule ni mamako mdogo ni mdogo wangu. Usimwitage Ashura” “Nisamehe kwa hilo mama, ila ningependa kujua huyu mamdogo na wewe ni mdogo wako kivipi? Na ndugu zako wengine wako wapi sijawahi kuwaona?” “Mmmh Salome jamani, si mwezi uliopita tu nilikupeleka kwa kaka yangu, tuseme ushasahau!” “Haya mama, tuachane na hayo ila huyu mamdogo ni ndugu yako kivipi kuna jambo nataka nikueleze niambie kwanza undugu wenu ndio nikueleze” “Sikia, mimi baba yangu na mama yangu walikuwa hawaishi pamoja na kwa upande wa mama na baba, mimi ni mtoto wao wa pekee sana ila kumbe baba alikuwa na mtoto mwingine ila sio mtoto aliyezaa na mkewe waliyokuwa wanaishi nae. Mimi kwa mama tumezaliwa wawili tu, yani mimi na kaka yangu niliyekupeleka kwake mwezi uliopita. Hatuna mazoea ya karibu sababu Yule kaka alikulia nyumbani kwa baba yake. Ila mama ndio alinitambulisha kama ni kaka yangu. Sasa kwa upande wa Ashura ni mtoto wa baba kumbe naye alikuwa analelewa na mama yake, yeye ndio alinitafuta mimi kwakweli alipojitambulisha nilifurahi sana kwani nilipata ndugu hadi leo niko nae.” “Mmmh kwahiyo ulimpeleka kwa baba yako akutambulishe?” “Baba alishakufa kitambo sana, na laiti kama angekuwa hai basi ningempeleka” “Na huyo mke wa babu si yupo, kwanini usimpeleke akutambulishe” “Sasa huyo atakuwa anajua vinini, kwanza wanitambulishe nini wakati mtu alishajitambulisha na tunaishia nae hadi leo” “Je shangazi zenu na baba zenu wakubwa au wadogo mnawatembeleaga” “Wapo kijijini, kwakweli hatujawahi kupanga safari ya kuwatembelea. Inatia uvivu ujue halafu hatujawazoea” “Mmmh na kaburi la baba yenu je mmewahi kwenda kulitembelea?” “Tunapangaga kufanya hivyo ila hata sijui inatokeaga nini, tunajikuta hatujaenda” “Mama, ngoja nikwambie kitu. Huyu unayemuita mdogo wako si ndugu yako” “Salome, si ndugu yangu kivipi?” “Wewe nielewe tu mama ila si ndugu yako na kama hujui shauri zako, atakapokufanyia kitu kibaya ndio utashtuka. Na angekuwa amekufanyia kitu kibaya mud asana, ila wewe unalindwa na mzimu wa baba yako. Huna kosa na wala hustahili kufanyiwa mambo mabaya, ila kwa kifupi huyu si ndugu yako, Tafakari, maswali niliyokuuliza na majibu uliyonipa halafu chukua hatua” Salome aliinuka na kwenda kuoga, muda huu Neema alibaki kwenye lindi la mawazo kwani hajawahi kufikiria hata mara moja kuwa Ashura anaweza akawa si ndugu yake, “Jamani huyu Salome mbona ananitisha, halafu yeye kajuaje kama huyu si ndugu yangu? Hivi inawezekana kweli nimeishi siku zote na mtu asiye ndugu yangu huku nikiamini ni ndugu yangu! Haiwezekani jamani” Neema aliwaza sana bila ya kupata jibu la aina yoyote ile, ingawa kuna mashaka aliyapata kwa jinsi alivyoambiwa na Salome. Akajikuta akimsubiria kwa hamu Ashura atakaporudi ili amuulize baadhi ya maswali, “Lakini hata hivyo, kama ni kweli si ndugu yangu ni kwanini amenidanganya? Hivi inawezekana kweli! Hapana nahisi Salome kachanganyikiwa tu” Muda kidogo Ashura nae alirudi, na Neema alijikuta akimuuliza, “Hivi Yule mke aliyekuwa anaishi na baba ulikuwa unamfahamu?” “Aah ndio, hapana hata sikumbuki” “Mbona sijakuelewa hapo, ulikuwa unamfahamu au la” “Nilikuwa mdogo sana, hata sikumbuki kama namfahamu au la” “Basi tupange siku tukamsalimie” “Mmmh umekumbuka kitu gani?” “Nimemkumbuka tu basi, najua atafurahi sana” “Sawa tutapanga” Ila Ashura alionekana kukosa furaha tangu Neema amuulize kuhusu mke wa baba yao. Rose alikuwa kwenye wakati mgumu sana na siku hii hakuweza kuendelea kuwepo tena pale msibani, aliamua kuwaaga kuwa anaenda kwanza nyumbani kwake halafu atarudi tena. Kiukweli alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa hivi, alijiona kama ameonewa kwa wakati huo. Mke wa babu alimfata Rose wakati anataka kuondoka, “Jamani, kweli unataka kutuacha wenyewe kweli kwenye wakati mgumu kama huu” “Hapana bibi, hujui tu jinsi msiba huu ulivyonichangan ya hapa, nakosa hata uelekeo. Nina matatizo mzigo hata sijui naanzia wapi na kuishia wapi” “Naelewa kama una matatizo ila tafadhali usiondoke hadi tutakapozika” “Kwani mazishi ni lini?” “Ni leo, halafu kesho utaondoka. Tafadhali sana naomba usiondoke” Rose akajifikiria ila ikabidi apige simu nyumbani kwake kwani alijua ni wazi watakuwa na wasiwasi, na alimpigia simu Sara kwani anajuaga ndio kiherehere wa wasiwasi ila simu ya Sara iliita mara nyingi bila kupokelewa ikabidi ampigie simu mume wake, “Mbona Sara hapokei simu, au kaenda kazini leo?” “Hapana, Sara yupo ndani ila hawezi kuongea” “Hawezi kuongea kivipi?” “Sijui nikuelezeaje ila uwezo wa kuongea wa Sara umekatika gafla” “kheee jamani, mambo gani hayo? Ngoja nirudi le oleo” Rose akakata simu kisha akaenda tena kwa mke wa babu na kumpa taarifa za nyumbani kwake huku akimueleza kuwa anapaswa aende maana mwanae ni mgonjwa. Yule bibi hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumruhusu tu. Rose akapanda gari na kuondoka zake, alikuwa na mawazo mengi sana kushinda yale mawazo ya kwanza maana aliona kama matatizo yanamzidia ingawa kiuhalisia yeye ndiye chanzo cha matatizo yote. Wakati anaendesha gari akasikia sauti, “Rose, umenigonga nimekufa halafu kwenye maizshi yangu unakimbia!” Rose alishtuka na kusimamisha gari kwa haraka huku akiwa amejawa na hofu iliyomfanya ashindwe hata kutazama nyuma ya gari kuwa hiyo sauti inatoka wapi. Akiwa amejawa na hofu zaidi, ile sauti ikajirudia tena, na kumfanya Rose ashuke kabisa kwenye gari ile, alipokuwa chini akatazama kwenye kioo cha gari gafla alimuona kama Yule babu yupo ndani ya lile gari. Itaendelea kesho usiku…..!!!!!

at 2:34 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top