Home → simulizi
→ RIWAYA: DAMU YA MWANANGU
SEHEMU YA TISA(09)
*****ILIPOISHIA******
alipoukaribia mlango wa kuingilia ndani ya nyumba,,ikasikika sauti ikiita jina lake!
sauti hiyo ilitokea nyuma yake,,akageuza shingo kutazama ni nani anayemuita!
akamuona muna,,akiwa kasimama kando,,, akinyoosha mkono wake ishara ya kumuita asogee karibu zaidi,,Punde si punde...zikasikika sauti za majibizano,,sauti hizo zilitokea ndani ya nyumba! Nyamwela alipogeuza shingo yake kutazama ule upande aliokuwa kasiamama Muna,,hakumuona tena,,ghafla ikasikika sauti nyingine ikiita jina lake,,,akageuza shingo yake haraka kutazama,,,akashtuka !!!macho yakamtoka,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi!!!!!! akazipiga hatua kurudi nyuma, akajikwaa na kudondoka chini! akaanza kupiga kelele huku kafunika uso wake kwa viganja vya mikono yake,,,mara ghafla!
****ENDELEA****
akasikia tena sauti ya mtu akiita jina lake! akaitambua sauti hiyo!!
akafunua uso wake kutazama,,akamuona rafiki yake kipenzi aitwae Mtiku.
macho yakamtoka! akabaki mdomo wazi huku kapigwa na bumbuwazi!
Matiku akauliza,,"mbona upo katika hali hiyo! umepatwa na nini?
Nyamwela hakujibu kitu!! uso wake ulionyesha kuwa na wasiwasi na hofu ya hali ya juu! macho yake yalitazama huku na kule,,,hasa ile sehemu aliyomuona Muna kasimama!
baada ya sekunde kadhaa ufahamu ukarudi...akajisemea moyoni,,"hivi haya niliyoyaona ni kweli au maruwe ruwe tu?
Nyamwela alijiuliza maswali mengi pasipokupata majibu!
Matiku akabaki kasimama huku akimtazama Nyamwela kwa mshangao,,,
Nyamwela akasema,,"naomba uniache tutaonana kesho,,sijisikii vyema.
Matiku akaondoka zake!
Nyamwela akanyanyuka kutoka pale chini alipodondoka,,akazipiga hatua kuingia ndani ya nyumba!
akaogopa kukisogelea kitanda,,akajisemea moyoni,,"nimepoteza mtoto wangu kwa ujinga wangu mwenyewe! na mke wangu pia...hasira gani hizi,,
Nyamwela aliwaza hayo,,huku machozi yakimtoka!
akajipa moyo ,,akakisogelea kitanda na kuketi juu yake,,,baada ya sekunde kadhaa kupita akaamua kujilaza,,,akapitiwa na usingizi,,akiwa ndotoni ,ghafla akasikia sauti ya mtoto mchanga akilia,,pumde si punde akamuona Muna,,katika ndoto,,akiwa kaweka mkono wake juu ya tumbo,,huku damu nyingi zikimtoka!
Nyamwela akashtuka kutoka usingizini! akaandaa mpango wa kuhama katika kijiji hicho.
Asubuhi palipokucha,,akadamka mapema,,na kuipiga nyumba yake mnada,akafanikiwa kupata mteja,,akauza nyumba hiyo kwa shilingi,,mitioni saba,,,
akachukua pesa hizo na kuziweka ndani ya begi!,,akaelekea kwenye kituo cha mabasi yanayokwenda jijini Dar es salaam,,
baada ya lisaa limoja akawa kafika mjini,,akakata tiketi,,,kisha akaingia ndani ya basi hilo! akalipakata begi lake...akisubiri safari ianze!
Baada ya dakika kadhaa kupita,,, akaangaza macho yake kutazama upande wa nje kupitia dirishani..
kwa mbali akamuona rafiki yake kipenzi ni yule Matiku...akaamua kuliweka begi lake lililokuwa na zile pesa zote pamoja na nguo zake....akazipiga hatua kutoka ndani ya gari. kumfuata Matiku,,angalau ampe taarifa kuwa ameamua kuhama na kwenda kuanzisha maisha mapya jijini Dar es salaam.
Nyamwela akaamua kutimua mbio amuwahi Matiku kabla hajafika mbali! akaamua kupaza sauti kumuita Matiku!
Matiku akaitambua sauti ya Nyamwela akageuza shingo yake na kusimama...
Nyamwela alipomkaribia Matiku,,,akasikia mngurumo wa gari likiondoka,,,alipogeuza shingo yake kutaza kule lilipokuwepo basi....akashtuka kuona basi hilo likitokomea kwenye barabara ya kuelekea Dar es salaam!
Macho yakamtoka!
ITAENDELEA..........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: