RIWAYA: DAMU YA MWANANGU SEHEMU YA NANE(08) *****ILIPOISHIA****** Muna akamtazama mumewe kwa macho ya mshangao! kisha akasema,,"ni siku kumi sasa sijafungua hiyo droo,ebu tazama kwa makini, Nyamwela akasema kwa ukali,,"pesa hizo sio za kwangu,,nilikopa kwa ajili ya kuandaa shamba,,nataka pesa zangu.. Muna akabaki kimya,, Nyamwela akaingiwa na hasira,,akafungua mlango na kutoka nje ya chumba,,akachukua kisu,,akarudi chumbani,,akamkuta muna kasimama kando ya droo akizitafuta pesa hizo.. alipogeuza shingo yake ,,,mara ghafla!!!!!!! ****ENDELEA**** Nyamwela akanyanyua mkono wake uliokuwa umeshikilia kisu, Muna akastaajabu akauliza kwa msangao! ,,"mbona wataka.kuniumiza pasipo kosa? kabla hajamaliza kuongea,, Nyamwela akamdunga kisu upande wa tumboni! macho yakamtoka Muna,,akashindwa hata kupiga kelele akabaki kshikilia tumbo lake,,kwenye ile sehemu aliyodungwa kisu! damu nyingi zikamtoka,,akadondoka chini na kupoteza maisha! akiwa na ujauzito wa kukaribia kujifungua! Nyamwela akatahamaki,,kuona mkewe kadondoka chini! akahisi kuchanganyikiwa akajiwemea moyoni,,"jamani nimeuwa! kwa nini nikefanya hivi! akatafakari nini cha kufanya,,,wazo likamjia,,"nisipofanya jambo la kupoteza ushahidi nitaozea gerezani.. akazipiga hatua za haraka haraka akatoka chumbani na kuelekea kwenye stoo,,akachukua jembe ,,sululu na koleo,,akarudi ndani ya nyumba,, akaanza kuchimba shimo ndani ya chumba chake cha kulala,,, alichimba shimo hilo kwa masaa kadhaa mfululizo,,alipohakikisha shimo hilo linafaa ,,akatumbukiza maiti ya Muna,,na kuanza kufukia shimo hilo,,,alipomaliza akaweka kitqnda juu ya shimo hilo! kiwha akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi! hakuweza kupata usingizi usiku kucha,,kutokana na mawazo aliyokuwanayo! Asubuhi palipokucha,,akadamka mapema,,na kuondoka zake,, Wakati huohuo,,alionekana mama yake Muna,,akijiandaa na safari ya kwenda kuwatembelea kwa lengo la kuwajulia hali,,, akatoka na kuzipiga hatua kuelekea nyumbani kwa Nyamwela... baada ya lisaa limoja akawa amefika Nyumbani kwa Nyamwela,,hapakuwa na umbali mrefu,,ni kijiji cha jirani. akastaajabu kuona mlango umefungwa! akalazimika kuketi kando ya nyumba hiyo katika mti uliokuwa na matawi mengi na kutengeneza kivuli tulivu. masaa yakazidi kusonga,,na hakuna dalili yoyote ya mtu kurudi nyumbani,,,akajiuliza,,"inamaana watakuwa wamekwenda wapi? mbona muda wa kujifungua umekaribia,,sasa kwa nini anazurura! mama Muna alijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu... akakata tamaa akaamua kurudi nyumbani kwake! ilipofika majira ya saa nne za usiku,,akaonekana Nyamwela akizipiga hatua kuusogelea mlango wa nyumba yake! akafungu mlango na kuingia ndani ya nyumba! lakini alikuwa na hofu,,kutokana na kitendo cha ukatiri alioufanya jana. akasukuma mlango wa chumbani na kuingia ndani,,,punde si punde akahisi kunamtu anatembea nje ya nyumba yake,,vishindo vya mtu huyo vilisikika jirani na dirisha la chumbani kwake! Nyamwela akaingiwa na wasiwasi,,akatoka nje ya nyumba kwenda kutazama ni nani anayetembea nje ya dirisha la nyumba yake! alipozipiga hatua kuzunguka nyuma ya nyumba,,,alipoangaza angaza macho hakuona kitu chochote akalisogelea dirisha la upande wa chumba chake,,,alipolikaribia,,akasikia sauti ya mwanamke akilia kwa uchungu ndani ya chumba! macho yakamtoka Nyamwela,,akazipiga hatua za kunyatia akachungulia uoande wa ndani kupitia matundu yaliyokuwa kwenye mbao za dirisha hilo,,punde si punde,, kikasikika kiwhindo cha mtu akitembe nyuma yake,,,akageuza shingo yake kutazama!!!!lakini hakuona kitu chochote.... akahisi kuchanganyikiwa,,hofu ikazidi kuongezeka....akaamua kuondoka eneoz hilo la nyuma ya nyumba huku macho yake yakitazama huku na kule! alipoukaribia mlango wa kuingilia ndani ya nyumba,,ikasikika sauti ikiita jina lake! sauti hiyo ilitokea nyuma yake,,akageuza shingo kutazama ni nani anayemuita! akamuona muna,,akiwa kasimama kando,,, akinyoosha mkono wake ishara ya kumuita asogee karibu zaidi,,Punde si punde...zikasikika sauti za majibizano,,sauti hizo zilitokea ndani ya nyumba! Nyamwela alipogeuza shingo yake kutazama ule upande aliokuwa kasiamama Muna,,hakumuona tena,,ghafla ikasikika sauti nyingine ikiita jina lake,,,akageuza shingo yake haraka kutazama,,,akashtuka !!!macho yakamtoka,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi!!!!!! akazipiga hatua kurudi nyuma, akajikwaa na kudondoka chini! akaanza kupiga kelele huku kafunika uso wake kwa viganja vya mikono yake,,,mara ghafla! ITAENDELEA..........

at 3:53 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top