Sitaki tena – 03
BAADA YA MIAKA 5
Vurugu zilizokuwa zinaendelea
katika Gereza la kufungwa watoto
watukutu lililopo mbeya,
Ndizo zilizosababisha watoto
wengi kupoteza maisha na
wengine kupata ulemavu wa
maisha kutokana na mgomo
waliokuwa wameuanzisha
kutokana nakupewa chakula
kidogo sana tena
kichafu,milipuko ya magonjwa
kama kipindupindu,msongamano
wa wafungwa kiasi cha wengine
kufariki kwa kukosa hewa wakati
wa kulala usiku..
Namba CG.016/007369, ndiyo
namba iliyokuwa inasomeka
katika sare yangu ya Gerezani .,
Tayari maisha nlikuwa
nimeshayazoea mule
gerezani,taarifa kutoka nyumbani
nilikuwa nikiletewa na afande
mmoja ambaye tayari nilimzoea
na hata kuanzia siku ile nilipo
hukumiwa pale mahakaman hali
ya baba yangu kiafya haikuwa
nzuri na hakukaa mda mrefu
akawa amepoteza maisha,
Mwenyezi mungu amlaze pahala
pema peponi..
Na sasa mama ndio mzazi wangu
pekee aliyebaki hata kama
nitatoka gerezani... ucheshi,
ufanyaji kazi kwa nguvu,bidii na
kujituma zaidi ndicho kitu
kilichokuwa kikiwavutia maaskari
wengi pale kiasi kwamba
nikapendwa sana na kuaminika..
"Levinaaa... Levinaaa..
...Wewe Levina Christian?..
Aliniita askari wa zamu lakini
sikuweza kumsikia vizuri kwa
sababu ya makelele ya wenzangu
waliokuwa wakipigana mule
ndani..
"Abeee afande..nilimuitikia"
"Embu fanya haraka kuna mgeni
wako kaja kukutembelea fanya
ukamuone.."
"Sawa afande..."
Mapigo ya moyo yalikuwa
yakinienda mbio,lakini
halmashauri ya kichwa changu
iliweza kupambanua haraka
haraka na kujua atakuwa ni
mama tu...
"Lakiiini...mbona afande
hakuniambia kama ni mama au
la!
Maana mama yangu anamjua
angeniambia tu?" ndio maswali
niliokuwa najiuliza nikiwa njiani
kuelekea chumba cha wageni..
Ghafla...
"Sasa mbona simuoni mgeni
wangu?.." nilijikuta namgeukia
yule afande aliyekuja kuniita na
kuniambia kuwa nina mgeni..
"Umeanza kisilani chako enhee..?
Au unataka ukalime heka tatu
peke yako sa hivi...?
" enhee..!
Nikabaki kimya huku nikiendelea
kumtolea macho ya ukali yule
askari ambaye alikuwa
anajulikana 'Jesca Tester'
kutokana na kuwa mkorofi kwa
wafungwa wabishi hata kipindi
kingine huwa anakorofishana na
maaskari wenzake..
"Si naongea na wewe
kinyamkera...?
Haya na huyu hapa ni mgeni wa
nani sasa..?"
Nikajinyamazia kimya huku
nikikaa katika kajidirisha cha
kuongea na wageni..nikimuacha
yule askari akiendelea
kubwabwaja pale..
"Na Nakupa dakika kumi tu uwe
umeshamalizana naye na upotee
hapa,sawa..?"
"Sawa mkuu nimekuelewa..!"
nilimjibu kwa heshima huku
nikianza mazungumzo na yule
mgeni wangu pale..
GERVAS; Sijui
umeshanikumbuka..?"
LEVINA; Hapana..
GERVAS; "Naitwa Gervas
Phota..Tumeishi wote kurasini na
kuchez..." kabla hajamalizia
kuongea tayari akili yangu
ilishaweza kuchambua fasta na
kumjua..
LEVINA; we si mtoto wa mzee
Phota pale jirani na nyumbani
kwetu.?
GERVAS; Haswaaa..! Ndiye mimi
kumbuka tulikuwa wadogo sana
lakini kwa bahati mbaya sikuweza
kuwepo kuanzia siku ya
tukio,kipindi cha kesi yako mpaka
leo kwa sababu nilipelekwa shule
mapema mno..
LEVINA; Usijali Gervas yote hayo
nimaisha namshukuru mwenyez
mungu mpaka nilipofikia hapa
kwani nimebakiza miaka sita tu
niwe huru..
"Mda umekwisha..haya we Levina
inuke uwafate wenzako
shambani..inuka" aliongea yule
askari Jesca ambaye mda wote
alikuwa akitusimamia..
Haraka haraka nilimuona Gervas
akitoa kijimfuko kilichoashiria kina
nguo.,kisha akatoa noti ya shilingi
elfu kumi akanipatia kisha yule
askari akampa shilingi elfu tatu
kisha akaniaga na kuniahidi kuwa
atakuwa akinitembelea mara kwa
mara...
Siku hiyo sikuweza kupata hata
lepe la usingizi kwani nilijihisi
tayari nipo nyumbani kwa zile
nguo nilizoletewa na Gervas
nilijikuta machozi yakinitoka
japokuwa yalikuwa ni machozi ya
furaha,
Ikawa haipiti mwezi lazima Gervas
aje kunitembelea na kuniachia
japo chochote, hivyo nikaamini
kuwa mtetezi wa maisha yangu ni
Gervas na mama yangu pekee
japo tangu nilipoletwa huku
gerezan hajawah kuniona,moyo
wa upendo taaratibu ulianza
kunijia kwani hakukuwa na mtu
aliyejionesha kunijali kama
Gervas..
BAADA YA MIAKA 2
Nakumbuka siku hiyo Gervas
alikuja kunitembelea lakini safari
hii alionekana kuwa tofauti na
siku nyingine kwani alikuja na
furaha ambayo sikuitegemea na
hakuweza kukaa sana ila
akachukuwa mkono wake wakati
ananiaga alipoachia nilihisi
itakuwa kama kawaida yake ya
kuniachia pesa lakini haikuwa
pesa ila ilikuwa ni kijikaratasi
kilichokuwa na ujumbe..
Niliagana na Gervas kisha
nikaenda kutafuta eneo lililokuwa
tulivu,taaratibu nikaanza
kufungua ile karatasi ghafla moyo
ukanilipuka,
"Mpendwa Levina,natumai u
mzima afya kwani mara nyingi
huwa tunaonana.,
Nashukuru mwenyezi mungu
mpaka hapa tulipofikia kwani
umenifanya nijue mengi
yanayotendeka humu ndani kwa
kifupi nimejuana na kuzooena na
maaskari wengi hapa,
Levina mim na wew tumetoka
mbali na sitapenda nikuache
uendelee kuteseka hapo gerezani,
Mwezi huu Rais atatoa msamaha
ikiwa ni pamoja na gereza lenu
lakini msamaha wenyewe
utalenga wale wenye ulemavu
nilichokifanya ni..
Kabla sijamalizia kusoma alitokea
afande Jesca Tester na kunifokea..
"Hivi wewe Levina mda wote
umekaa hapo umewakimbia
wenzako kule,unafanya nini?"
"Nika kaa kimya"..
aliendelea kuongea afande kwa
sauti ya ukali..
"Na kwanini umekuja kujitenga
peke yako huku?"
"Nisamehe afande sitarudia
tena..wakati namjibu ghafla kile
kikaratasi kikadondoka chini..
"Haya lete hicho
ulichoangusha..Letee..!
Inaendelea...
No comments:
Post a Comment