Sitaki tena –04
Nilijikuta nachukua kile kikaratasi
na kumpatia afande Jesca
nikiamini kuwa hajui kusoma
kwani huwa mara nyingi
akitumiwa ujumbe kwenye simu
yake huwa ananitafuta
nimsomee.. Alikichukuwa kile
kikaratasi akakigeuza geuza kisha
akanirudishia..
"Acha upuuzi wako nenda kwa
wenzako sawa?"
"Sawa" nilimuitikia lakini kishingo
upande huku akili yangu
ikinituma nielekee chooni
nikakimalizie kukisoma,taratibu
nikaongoza hadi chooni
nikakifungua kwenye gauni
kilipokuwa na kumalizia
kukisoma, enhe ikawaje vilee.,
"lakini msamaha wenyewe
utalenga wale wenye ulemavu
nilichokifanya ni kutoa ada yangu
yote niliyotumiwa shilingi laki mbili
na kuwaonga polisi kisha
wakalipitisha jina lako kwenye
orodha ya watakao kuwa huru"
Hapohapo nikakichukuwa
Kile kijikaratasi na kukichana
chana kisha nikakitupia katika
tundu la choo,nikitoka na furaha
ya hali ya juu huku nikijiona
mshindi,
BAADA YA WIKI MOJA
Ikiwa ni asubuhi na mapema
tukiwa tumejipanga mstari
halmashauri ya kichwa changu
kikawa kimeshafanya kazi
nakutambua ni kitu gani kilituleta
katika eneo lile.,
Kama kawaida ya afande kimbele
mbele afande Jesca alikuwa tayar
akiwanyosha watu mistari huku
akiwapiga na kuwafokea wale
waliojifanya ni wabishi,
Tayari maafande takribani nane
walikuwa mbele yetu huku mkuu
wa gereza akiwa kashikilia karatasi
bila kuchelewesha mda akaongea
kilichotuleta eneo lile na kuanza
kutuita majina naweza kusema
sikuamini kilichotokea kuwa kama
ndoto kwani ni kweli na mimi
nilikuwa katika ile orodha ya
walioachwa huru,
"nashndwa kujua nimfanyie nini
huyu kaka 'Gervas'..
Gervas...! Gervas...! Nakupenda na
Nitazidi kupenda daima"
nilijisemea kimoyomoyo huku
nikipiga ishara ya msalaba na
kukusanyika na wenzangu huku
tukitokea lango kuu,
****
Gari aina ya Land Rover yenye
namba T643 ABK iliyokuwa
imebeba magunia ya mpunga
kutoka Tunduma kuelekea Dar es
salaam huku ikiwa imepakiza
abiria wa nne tu,wawili wa kiume
na wawili wa kike.. nikiwamo
katika hilo gari kwa mwendo wa
taratibu huku nikiwa na mawazo
mengi yalionijaa akilini mwangu
ikiwa ni pamoja na hofu juu ya
safari kama tutafika salama, mda
huo ilikuwa imeshatimia saa 2
usiku,tulikuwa tunakaribia kufika
Iringa., mawazo gongana
yaliniandama ndani ya kichwa
changu hasa kwa kuzingatia kuwa
bado nilikuwa sijajiamini kwa kile
kilichonitokea kama kweli niko
huru ama la.!
Huku nikiendelea kuwa katika
dimbwi la mawazo usingizi
ukanipitia.
"Lete Jeki fasta...waambie na hao
wadada washuke huko..!"
sauti ya dereva wa ile gari
akiongea na mwenzake ndiyo
ilinishtua sana kwani gari lilikuwa
limeharibika kilomita chache
kabla hatujaingia Iringa..
Baridi lilikuwa kali sana,nilihisi
kama mwili umeganda sikuwa na
nguo yoyote ya kubadilisha,hivyo
sikuwa na jinsi zaidi ya kujilaza
pembeni ya lile gari huku
nikitetemeka mdomo na meno
yakiumana kama nimepigwa
ganzi..
Nikiwa pale chini natafuta tena
usingizi huku dereva akiendelea
kutengeneza lile gari., kwa
mbaaali niliona mwanga mkubwa
ukitumulika huku unasogea
taaratibu, akili yangu na wale
wenzangu haikuwa mbali kwani
lilikuwa ni gari lakini ilipofika
karibu yetu dereva wetu akawa
ameipungia mkono isimame kwa
ajili ya kuomba spana.. ilisimama
kisha wakashuka wanaume
watano waliokuwa wamevalia
makoti meusi huku mikononi
wameshika panga na bunduki
wakitufuata eneo tulilokuwa..
"Wote mikono juu"
Na ole wake mtu asimame au
aongee hata neno moja.."
aliongea mmoja wa wale
wanaume aliekuwa anasura ya
kikomavu iliyojikunja kunja mithili
ya mchekeshaji wanaomwita
'King'wendu', huku kavalia
miwani meusi na mdomoni
akivuta sigara na kutupulizia
moshi..tukiwa bado tupo pale
chini tukitetemeka na kuogopa
pia tulikuwa kama tumeshajitolea
kwa lolote litakalotupata..
Ghafla milio ya risasi ikaanza
kurindima kuelekea kwenye
matairi ya lile gari letu
yakapasuka yote manne kisha
wakamchukuwa dereva na
wenzake wakawachinja mbele ya
macho yangu kisha wakaondoka
na kuniacha na mwenzangu
niliyetokanaye gerezan, Roho ya
Ujasiri,ukatili na ukakamavu
niliokuwa nayo toka nipo
kifungoni ilinisaidia sana kwani
sikuogopa hata kidogo
kilichonitokea mda mfupi uliopita
nilimchukuwa mwenzangu na
kutokomea naye msituni..
Nikiwa nimemshika mkono
mwenzangu Pendo tulikuwa tayari
tumeingia msitu wa Ruaha ambao
kiukweli ulikuwa ni mkubwa sana
na uliojaa na miti
mirefu,hatukuweza kuogopa kitu
kwani maisha ya gerezani
yalikuwa tosha kwa mimi na
Pendo kuwa wajasiri,wakatili na
wakakamavu mda wote,
"Nimechoka.,nimechoka siwezi
kuendelea tena Pendo..tupumzike
hapa.." Nilimwambia pendo huku
nahema nikitokwa jasho usoni
kwa mwendo tuliokuwa
tunatembea haraka haraka
hakika ulikuwa ni mwendo mrefu
sana.,
"Sasa ukiendelea kudeka deka mi
nakuacha, au unapenda kubakia
hapa porini?" alisema Pendo kwa
ukali kudhihirisha kuwa alikua
amechoshwa na kitendo cha mimi
kupumzika.,Nilijikaza na kuinuka
tayari kwa kuendelea na safari
lakini..
"Pendo.! Pendo.! Mama yangu
wee mguu wangu..! Nilijikuta
namuita Pendo asiondoke kwani
mguu wangu kwa upande wa
nyuma ulikuwa umeshachanika
na damu nyingi zilikuwa
zikinitiririka., Pendo hakuwa na
jinsi kwani aliona kubaki na mimi
katika ule msitu
kungemchelewesha kufika kwao
kwani safari yake ilikuwa inaishia
Dodoma.,
"Pendo..! pendo..! Usiniache
pendo..! ntabaki na nani tena
Pendo..!"
aliniacha nikiwa katika hali mbaya
huku machozi yakinitoka,na
kukata tamaa,nakuona bora
ningemsubiri Gervas aje
kunichukuwa.,ulikuwa tayari ni
usiku sana nahisi ilikuwa imetimia
kwenye saa nane au tisa kwani
giza tororo ndilo lilitawala sana,
Nikiwa bado katika dimbwi la
mawazo na hasira nyingi pale
chini huku milio ya wanyama
wakali ikipaza huku na kule,
Ghafla nikaanza kusikia mshindo
wa kitu kama kinakuja tena kwa
kasi ya ajabu, kadri mlio
ulivyokuwa unazidi kuwa mkubwa
mapigo yangu ya moyo yalizidi
kunipelekesha.nilihema mpaka
nikajihisi nimeishiwa pumzi sikuwa
na lakufanya zaidi ya kujitoa kwa
lolote litakalonipata kutokana na
mguu kuumia vibaya kutokana na
kujiumiza na kipande cha bati
kwenye gari wakati tunakimbia
kujiepusha na yale majambazi
waliotuteka kulee..
Hatimaye nikaanza kutambua kitu
kilichokuwa kinakuja kwani
mwanzoni nilijua labda atakuwa
Pendo amerudi kuja kunichukuwa
lakini haikuwa hivyo kwani
alikuwa mnyama mkubwa mweusi
aliyefanania na nyati ila alikuwa
akija kwa mwendo wa taratibu
huku akinifuata katika eneo
nililokuwa nimekaa..mwili
ulinitetemeka sana hofu kubwa
ilitanda ndan ya kichwa
changu,nilitetemeka sana huku
mchozi ukiwa unanitoka
ukiambatana na mkojo kwa
kasi,maumivu ya ule mguu
yakatoweka kutokana na kile
kilichokuwa mbele yangu..
"jamani..! jamani..! jamani..!
Nisaidieni nakufaa..! nakufaa..!"
Nikiwa bado nalia pale ghafla..
INAENDELEA...
No comments:
Post a Comment