Sitaki Tena - 02
(season 1)
Usiku ule tangu nirudishwe tena
rumande kwangu haukuwa
mzuri,akili na viungo vya mwili
wangu
vilikuwa vimechoka sana, yote
hiyo ni kutokana
na kulia na kupigwa
pigwa,sikuweza kupata hata
chembe usingizi
kila nilipofikiria kilichonikuta.
.
"Hivi kweki nimeua..?
Mimi nimeua.?
Miiiimi..? Hilo ndo swali nililojikuta
najiuliza usiku kutwa bila kupata
majibu,nilitamani nishuhudie Jeni
akizikwa pengine labda ndo
ningeshawishika na kuamini kama
kweli
nimeua lakini
hiyo
haikuwezekana,
hakika usiku
ulikuwa mrefu sana
kwangu,mawazo mengi yalikuwa
tayari yameshatawala kichwa
changu pengine hata umri wangu
haukuniruhusu kufikiri sana lakini
tayar nikawa na fikra tena za
kikubwa zaidi kwa mda mfupi tu
tangu niwekwe rumande..
Sauti
za bundi,popo na mbwa ndizo
zilikuwa
zinapaa sana kuzunguka huku na
kule katika lile eneo
la kituoni, wenzangu walikuwa
wamelala fofo hawajielewi hiyo
yote ni kutokana na shuruba
shuruba za humu ndani,
Mpaka ilipotimia
saa 9 za usiku usingizi ukawa
Tayari umeshanipitia lakini kimoja
kilichokuja
kunishtua ni kaubaridi kalikokuwa
kakipenyeza ndani ya gauni
nililokuwa nimevaa, huku miköno
yangu miwili ndio ilikuwa
mto,mwili wote ulikuwa
ukinitetemeka mithili kifaranga
cha kuku kikinyeshewa na
mvua,kifupi palikuwa na baridi
sana nadhani ni kwasababu
sakafu ndo ilikuwa kitanda
changu..
Taaratibu nilianza kujihisi kama
kuna kitu
kinanipapasa kupitia mapajani
mwangu..lakini
sikuwa na wasiwasi kwani
nilijiamini sana kuwa tupo
wanawake tu na kama askari ndo
walikuwa mchanganyiko wakiume
kwa wakike..kila mda
ulivyokuwa unasogea ndivyo
hisia zikawa zinabadilika ndani ya
kichwa changu kwani niliweza
kulifungua jicho langu
La upande wa kushoto kuangaza
huku na huku kujua kitu gani
kinachonipapasa ghafla..
"Shhh... nyamaza...!
Na ole wako ufungua domo
lako.?" ilikuwa ni sauti ya askari
wa kike niliyekuwa nikimfahamu
kwa sura,alikuwa kanishika
mapaja yangu kwa nguvu huku
akiwaambia askar wenzake
ambao walikuwa wakiume
wafanye haraka haraka.,
Moyo ulinipasuka,nguvu
ziliniisha,hasira zilinikaa ghafla
huku nikikosa pumzi kutokana na
kuzibwa mdomo kwa mda
mrefu..
hatimaye wale askari
waliokuwa takribani watatu
walifanikiwa kuniingilia tena kwa
nguvu kwa takriban nusu saa pale
huku wakiniacha damu
nyingi zikinitiririka..
BAADA YA MWEZI
Hatimaye upelelezi ukawa
umeshakamilika na nilikuwa
tayari niko kizimbani..nywele
zilikuwa hazitamaniki,miguuni
sikuwa hata nandala,mavazi nayo
yakawa yameshachoka na
kuchafuka kwani toka mwezi ule
nibakwe Levina mimi ckuwa hata
na nguo nyingine ya
kubadilisha,nao mwili ulikuwa
tayari umeshadhohofika
kutokana na msosi mbaya
tuliokuwa tunapewa hakika
yalikuwa ni mateso makubwa na
si jambo dogo akilini kwangu..
Kama kawaida ya kesi nyingine
nadhani hii ni kutokana na
shauku iliowataka watu wajue ni
nini kitakachofuatia katika kesi
yangu kwani umati mkubwa sana
wa watu ulikuwepo ukishuhudia
kiasi cha kunifanya moyo wangu
ulipuke kwa huzuni..
Huku macho yangu yakiangaza
huku na kule ghafla nilifanikiwa
kumuona baba na safari hii
hakuwa na mawakili kama
ambavyo ningetegemea bali
alikuwa kakalia kibaiskeli cha
kupakia wagonjwa walemavu wa
miguu huku akikokotwa na dada
aliyekuwa amevalia mavazi
meupe wazo lilinijie paleple na
kugundua kuwa ni lazima
atakuwa ni nesi..
"lakini kwanini amekuwa vile..?
Au atakuwa amepooza nin?..."
nilijiuliza mengi kichwani bila
kupata majibu..
Mda wa kuanza kusoma kesi
yangu ulifika,pande zote mbili
zilikutana ikiwa ni pamoja na
mashahidi wa pande zote mbili..
"wewe ndio binti Levina..?
Ndio mimi..
Unakumbuka mnamo tarehe 1
mwezi wa 2 mwaka 2009
ulifanya kosa...
Nakumbuka..
Uliweza kuua tena kwa
kukusudia..?
Ndio.." hayo ndiyo maswali
niliokuwa naulizwa na kuyajibu..
Hatimaye yalikusanywa maswali
na majibu yote kuashiria kesi
imeeleweka na kuhukumiwa
kifungo cha miaka 10 gerezani..,
"Mwanangu...! mwanangu..!
Kweli unafungwa mwananguu..?"
hayo yalikuwa maneno ya
mwisho kwa mama yaliyofanya
na watu wengine waachie vilio
pale pale huku nikibakiwa na
roho ya kishujaa na kijasiri bila
hata kutoka mchozi..
BAADA YA MIAKA 5
Vurugu zilizokuwa zinaendelea
katika Gereza la kufungwa watoto
watukutu lililopo mbeya,
Ndizo zilizosababisha watoto
wengi kupoteza maisha na
wengine kupata ulemavu wa
maisha kutokana na mgomo
waliokuwa wameuanzisha
kutokana nakupewa chakula
kidogo sana tena
kichafu,milipuko ya magonjwa
kama kipindupindu,msongamano
wa wafungwa kiasi cha wengine
kufariki kwa kukosa hewa wakati
wa kulala usiku..
Namba CG.016/007369, ndiyo
namba iliyokuwa inasomeka
katika sare yangu ya Gerezani .,
Tayari maisha nlikuwa
nimeshayazoea mule
gerezani,taarifa kutoka nyumbani
nilikuwa nikiletewa na afande
mmoja ambaye tayari nilimzoea
na hata kuanzia siku ile nilipo
hukumiwa pale mahakaman hali
ya baba yangu kiafya haikuwa
nzuri na hakukaa mda mrefu
akawa amepoteza maisha,
Mwenyezi mungu amlaze pahala
pema peponi..
Na sasa mama ndio mzazi wangu
pekee aliyebaki hata kama
nitatoka gerezani... ucheshi,
ufanyaji kazi kwa nguvu,bidii na
kujituma zaidi ndicho kitu
kilichokuwa kikiwavutia maaskari
wengi pale kiasi kwamba
nikapendwa sana na kuaminika..
"Levinaaa... Levinaaa..
...Wewe Levina Christian?..
Aliniita askari wa zamu lakini
sikuweza kumsikia vizuri kwa
sababu ya makelele ya wenzangu
waliokuwa wakipigana mule
ndani..
"Abeee afande..nilimuitikia"
"Embu fanya haraka kuna mgeni
wako kaja kukutembelea fanya
ukamuone.."
"Sawa afande..."
Mapigo ya moyo yalikuwa
yakinienda mbio,lakini
halmashauri ya kichwa changu
iliweza kupambanua haraka
haraka na kujua atakuwa ni
mama tu...
"Lakiiini...mbona afande
hakuniambia kama ni mama au
la!
Maana mama yangu anamjua
angeniambia tu?" ndio maswali
niliokuwa najiuliza nikiwa njiani
kuelekea chumba cha wageni..
Ghafla...
INAENDELEA..
No comments:
Post a Comment