NIPE BHANA Sehemu ya 04 Mwandishi:mmaka Watsapp:0714435449 ...............ilipoishia............... Askari wanafika eneo la tukio na kuchukua miili ya jane pamoja na baba yake huku wakiondoka na baadhi ya mashuhuda wa tukoi lile kwa ajili ya msaada zaidi wakirushiwa video ya tukio zima kupitia mtandao wa Watsapp wakati huo nami nipo kwenye gari kurejea kijijini kwetu Manushi mkoani Arusha kujiokoa na kesi ya mauaji inayo nikabili baada ya kufanya mauaji tena ya kukusudia huku nikishuhudiwa na umati wa watu waliokuwa wakipiga picha na kuchukua video.. Gari nililopanda linazidi kuliacha jiji la Dar es salaam...... ......................endelea.................... Hatimaye polisi wana peleka miili ya marehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mwananyamala huku wengine wakiwafikisha kituoni mashuhuda wa tukio na kuwa hoji ambapo kila aliyeojiwa alithibitisha kuwa mimi ndiye niliyefanya mauaji yale ya baba na mwanaye huku wakiichunguza pia video nzima ya mauaji kila kitu kilidhibitisha mimi ndiye mhusika mkuu Hivyo picha zangu pamoja na video nzima ya mauaji zili sambazwa katika mitandao ya kijamii pamoja na picha kubandikwa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar msako wa kunitafuta unaanza Polisi wanaulizia maeneo ninayoishi na kuelekezwa katika nyumba niliyopanga kwa dada mwenye nyumba wanafika na kumkuta dada mwenye nyumba akifua nguo pamoja na baadhi ya kina mama wapengaji wenzangu ambao kazi yao naweza kusema kila siku ilikuwa kukaa kibarazani kujadili ya watu wakisubiri waume zao kuleta riziki nyumbani wakiwa bado wametia timu huku baadhi yao waki ondoka baada ya waume zao kurudi kutoka kazini Askari wanaingia na kuwafanya kina mama wale pamoja na dada mwenye nyumba kuacha walichlkuwa wanafanya na kunyanyuka kuwasikiliza askari wale "Habari zenu hapa"anatoa salamu mmoja wa wale askari "Salama karibuni na kulikoni" anajibu dada mwenye nyumba kwa kujiamini kwa niaba ya kina mama wale "asante,, jambo moja tu limetuleta hapa.. ...Anatoa picha yangu.. Nazani huyu kijana mnamfahamu na ni mmoja kati ya waliopanga eneo hili Tumekuja kumkama kwa kosa la mauaji ya kukusudia ya watu wawili tena akishuhudiwa na umati wa watu sasa tunataka kujua alipo sasa hivi kwani yupo chini ya ulinzi" anaongea mmoja wa askari wale aliye onekana mzee wa umri wa makamo Maneno ya askari yule yanastua waliokuwemo pale hasa dada mwenye nyumba wasiami kilicho tokea "eti unasemaje askari Sam huyu ninaye mjua ndio kafanya tukio la mauaji sidhani kama ni yeye labda mtakuwa mmekosea " anasema dada mwenye nyumba kwa fadhaa na hofu kuu "hatuna utani we dada tuna uhakika na tuna chokisema na tunachotaka kutoka kwenu ni kujua alipo mtuhumiwa na siyo kuulizwa maswali ya kipuuzi kama haya na mkitaka kuujua ukweli wa tukio ingieni kwenye mitandao ya kijamii" anasema kwa hasira askari mmoja mrefu na mweusi aliye jengeka mwili kwa mazoezi "masaa kama matatu yaliyo pita Sam alikuja hapa katika hali iliyo tushangaza kwa alikuwa amechafuka sana huku mwili wake umejaa michubuko na tulivyo muuliza kulikoni hakujibu chochote na baada ya muda alitoka akiwa amejisafisha na kubadili nguo akachukua bodaboda na kuondoka" anatoa ushahidi mmoja wa wanawake waliokuwa kibarazani wakati nilipoingia na kubadili nguo huku akisikilizwa kwa makini na askari wale.. "Asante kwa kutujuza na ni bodaboda gani huyo aliye kuja kumchukua " anaulizwa yule mwanamke aliyetoa ushahidi "kwa kweli sikumuona sura vizuri labda wenzangu walimuona" anajibu mama yule shuhuda "ni yule ibra kiduku wa kijiwe cha kwa tembo" anajibu mwanamke mwingine shuhuda "Asanteni kwa kutujuza sasa mko salama na mkizidi kupata taarifa kuhusu mtuhumiwa msiache kutujuza" anamaliza mmoja wa askari wale ambapo askari wate wanaondoka kuelekea kijiwe cha tembo alipo dereva bodaboda ibra kiduku Dada mwenye nyumba nguvu zinamuisha baada ya kufungua data kwenye simu yake ambapo zinaingia messege nyingi katika Watsapp yake ikiwemo video nzima ya mauaji "mungu wangu huyu Sam kafikia hatua ya kuuwa" anawaonyesha kina mama wale ambapo nao wanapigwa na butwaa kuona video ile wasiamini huku wengine wakiingia facebook na kukuta video na picha zangu zikipambwa kwa vichwa mbalimbali vya habari "Nilijua tu huyu kijana muuwaji maana alionekana mhuni mpaka kufikia hatua ya ku" anataka kumalizia mama yule lakini anafinywa na mwenzake aliekuwepo pembeni Maneno ambayo yanasikika vizuri kichwani mwa dada mwenye nyumba lakini hakuelewa kutokana na kukatishwa kwa maneno yale Upande mwingine askari wale wanafika katika kijiwe cha kwa tembo na kumuulizia dereva bodaboda alietambulika kwa jina la Ibra kiduku ambapo anajitokeza kijana mmoja mrefu ambaye kichwani mwake kama lilivyo jina lake alinyoa mtindo wa kiduku Wana mwamuru Ibra asogeze pikipiki pembeni kidogo mbali kuwa fuata na walipo wenzake "kijana tumekuita hapa kwa jambo moja tu huyu mtu nazani una mfahamu" anongea askari mmoja akiimuonyesha ibra picha yangu "ndiyo ni mteja wangu wa muda mfupi uliopita" "huyu mteja wako anakabiliwa na kesi ya mauaji sasa tunaomba utujuze ulipomfikisha mara ya mwisho" maneno yatamkwayo na askari yana mtia hofu kubwa Ibra lakini anajikaza kiume na kujibu "nilimfikisha kituo cha mabasi Ubungo alipopanda basi la hood akielekea Arusha"ana jibu Ibra kwa hofu akimuomba mungu amuepushe na mkasa ulio mbele yake "asante kwa kutujuza upo huru" "Nashukuru afande " anaondoka Ibra Taarifa za mimi kupanda gari aina ya hood nikielekea Arusha zilifikishwa haraka kituo cha polisi na amri kutolewa kwa askari wote wa babarani kwenye barabara ya moshi Dar kuzuia gari yoyote ya kampuni ya hood inayoelekea moshi huku baadhi ya askari wakichukua gari ya doria ya polisi na kuanza safari ya kulifuatilia gari nililo panda Upande mwingine nikiwa ndani ya basi la kampuni ya hood tukiwa tumefika maeneo ya muheza mkoani tanga nikimshukuru mungu kwa kuniepusha na hukumu ya kifungo cha maisha nikiwa nimekaa siti za katikati ya gari nilikaa na msichana fulani ambaye nilizoeana naye ndani ya muda mfupi tukawa marafiki tuliendelea kupiga stori mbalimbali huku mdada yule akiperuzi kwenye mtandao wa facebook lakini ghafla alinionyesha video ya mauaji niliyo yafanya ambapo mwishoni ilimaliziwa na maneno ya kamanda mkuu wa polisi akisema mtuhumiwa baada ya kufanya tukio alikimbia na inasadikika yupo ndani ya basi la kampuni ya hood akielekea Arusha na pia lilitangazwa dau nono kwa atakaye fanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa "yani huu ni mwisho wa dunia mtu anauwa mbele ya umati tena bila woga alafu naskia amepanda gari la kampuni ya hood akielekea Arusha usikute tumekaa na muuaji humu ndani" Anaongea dada yule maneno yanayozidi kunitisha hasa baada ya kuona video ile pamoja na maneno ya mkuu yule wa jeshi la piolisi yaliyoonyesha kuwa polisi walijua kila kitu kuhusu mimi kilicho baki ni kunikamata na mimi kufia gerezani tuu.. "mhh yani we acha tu dadangu wa siku hizi si binadamu ni wanyama" nilimjibu nikijidai kutazama simu yangu kuficha hofu niliyo kuwa nayo "ila sizani kama yupo kwenye gari hili tungesha mjua tu maana asinge tulia" naongeza huku dada yule akiwa bize mitandaoni huku masikioni akiweka ear phone hali iliyo nifanya kidogo nipate amani uzuri ni kwamba pamoja na kuangalia video ile pamoja na picha zangu kama muhalifu dada yule hakuweza kunitambua kutokana na kubadili mavazi na pia kofia niliyovaa iliweza kidogo kufunika makovu yangu ya usoni safari inaendelea hatimaye tuna fika sehemu ya kuchimba dawa yaani kujisaidia kukojoa au haja kubwa Basi waliohitaji kujisaidia wanashuka nikiwa mmoja wao na kuingia katika vichaka vilivyopo maeneo yale tukiwa bado ndani ya wilaya ya muheza mkoani Tanga Mimi nasogea ndani ya vichaka mbali kidogo na walipo wasafitri wengine waliokuwa wakihitaji kujisaidia Naanza kukojoa lakini ghafla natazama barabarani na kwa mbali naona difenda ya polisi ikija kwa kasi eneo tulipo huku askari watatu wakiwa nyuma ya gari huku wameinyoosha mitutu yao Kengele ya hatari inagonga kichwani kwangu ambapo akili inaniambia ndo hivyo usha kamatwa unaenda kufia jela Basi wazo lina nijia napiga kelele Nyokaaaa!!!!..... Nyokaaaaaaa!!!!!!!!...... Nakufaaa jamani .........nisaidieni............ Naanza kukimbia kwa kasi niki tokomea katikati ya vichaka vilivyo ndani ya pori lile nene ... Wakati uwo gari la polisi likikaribia lilipokuwa gari letu....... Je nini kitaendelea ?? Usikose sehemu ya (05)

at 11:05 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top