Home → simulizi
→ NIPE BHANA
Sehemu ya 03
Mwandishi:Mmaka
Watsapp:0714435449
.............ilipoishia..............
Pipiiiiiiiiiii!!!!!!!!!pipiiiiiiii!!!!!! inasikika sauti ya honi ya gari nje ya nyumba ya dada mwenye nyumba
"Sam tumekwisha !! Mume wangu huyo" anasema dada mwenye nyumba kwa hofu
Wote tuna kurupuka huku miili yetu ikitiririsha jasho la hofu pamoja na mechi fupi iliyokatishwa kabla ya filimbi ya mwisho nachukua nguo za navaa haraka haraka naye dada mwenye nyumba ana vaa chupi na dela lake ananifungulia natoka nduki nikielekea chumbani kwangu lakini sina bahati kwani napishana na mpangaji mmoja hivi mama wa makamo mama rehema aliye sifika kwa umbea mtaa mzima akielekea chooni ananiangalia ninavyotimua huku nimeshikilia suruali yangu na pia dada mwenye nyumba ambaye naye kwa hofu alikuwa ana lifungua geti
"Haloooo!!!! Mnalo mwenye nacho karudi sasa na kuambia mwaka huu mtanikoma"
Wakati huo nimeufikia mlango wangu naufungua kwa woga naingia ndani naelekea moja kwa moja mpaka kitandani najitupa
"Mungu wangu leo ningekufa mhhh na huyu mama kashajua basi mambo yashaharibika bora nihame huu mtaa kabisa maana kwa ninavyo mjua huyu mzee akigundua ataniuwa"
Najisemea kimoyo moyo huku tumbo likiunguruma kwa njaa natoka moja kwa moja mpaka kwenye kamgahawa kilicho jirani na eneo nililopanga naagiza ugali nyama na kula taratibu na baada ya kumaliza narudi geto kuutafuta usingizi japo inachukua mda lakini nakuja kustuka saa kumi na mbili na nusu
Natoka nje kujisaidia nakutana na dada mwenye nyumba akiwa na mume wake wanapiga mswaki nawasalimia wote wanaitikia lakini dada mwenye nyumba ananikonyeza akiachia tabasamu kwa mbali bila mumewe kugundua mimi namtazama tu na kuingia zangu chooni
Baada ya kumaliza shughuli za nyumbani najiandaa kwenda katika kibiashara changu kidogo kinachoniweka mjini lakini kichwani nikiwa na wazo la kuhama nilipokuwa nimepanga tena ikiwezekana jioni ya siku ile ile
Kabla ya kuingia kazini naenda moja kwa moja kwa mshikaji wangu Abdalla ambaye tulizoea kumuita kwa kifupi '
Dulla'
"oy mambo vp mwana"
"Fresh mishe nini"
"powa tu ndugu yangu"
"vp mbona leo mapema sana kwangu"
"Dah!!! Nahitaji chumba cha kupanga mwanangu kule nilipo nisha yaharibu"
"Duh umetembea na mama mwenye nyumba nini maana kuhama ghafla hivyo si kawaida"
Namweleza Dulla masaibu yote niliyo kutana nayo na kumuomba ahakikishe jioni nahamamia katika chumba hicho ambacho nahitaji kiwe na hadhi kama kilivyo chumba chake, naye ana nihakikishia chumba ntapata na kunitania kwamba na yeye ni mfanyie plan ambapo tayari najua huyu anahitaji pesa na mwambia pesa si tatizo cha muhimi chumba kwanza naondoka mpka kazini kwangu na fungua kibanda changu na weka mambo sawa natoka na kukaa nje kusubiri wateja
Mara anatokea Jeni "waohh mpenzi umeamkaje" anasema huku akinikumbatia.
"salama tu wewe umeshindaje "
"mi niko pw japo nili lala mchovu ila hakuna siku niliyo lala vizuri kama leo kweli wewe kiboko"
"Amna mbona kawaida hata wewe ulinikimbiza sana" tunaongea ilimradi kufurahishana Jane ana nichukua tunaenda kunywa chai lakini wakati wa kurudi tunafika dukani analisimamisha gari tuna shuka Jane ananisogelea na kunibusu shavuni
"baby bye tutaonana baadaye ila naomba tuendelee kuchati " ananiambia Jane lakini tunastushwa na sauti ya mzee wa makamo kama miaka sitini
"Ahhha!!! kumbe wewe Jane ndiyo mambo yako kutembea na vijana wachafu na wasio jielewa kama hawa ndo maana tunakutafutia mchumba unakataa kumbe ni huyu kikaragosi ndo anakuchanganya akili
Sasa wewe kijana nakuuwa na hamna mahali popote nitakapo pelekwa unaniaribia binti yangu niliyemsomesha nje ya nchi kwa gharama mpaka amefika alipo na anakataa kuolewa na vijana matajiri na wenye elimu kwa sababu yako wewe usiye na uwezo wa kumpa chochote maskini mlaaniwa mkubwa"
anaongea mzee yule akitoka dukani huku mkononi ameshikilia bastola na kuninyooshea hakika alionesha kudhamiria kufanya alicho kisema mimi kwa woga nikaanza kumuomba msamaha huku yeye akizidi kusogea karibu na mahali nilipo huku akiikoki kabisa bastola yake na kuninyooshea
"Mzee wangu naomba unisamehe sinta jaribu tena hata kumsogelea binti yako nilisema na wala yeye hakunieleza ukweli wa maisha yake" nilimwambia yule mzee kwa woga huku nikiamini siku yangu ya kufa ndo imefika
Mzee alizidi kunifuata ambapo tayari katika eneo lile tayari watu walisha kusanyika kushuhudia filamu iliyochezwa laivu huku kila mmoja akizungumza la kwake na kama unavyo jua tena Dar mtu unaweza kuibiwa watu wakabaki wakikushangaa na kumwangalia mwizi bila kuchukua hatua yeyote
Kuona vile Jane alikuja na kusimama mbele yangu "baba bora uniuwe mimi huyu kaka hana kosa lolote mimi ndiyo nilimlaghai kwa pesa ili anipende chonde baba naomba umuache kaka wa watu aende "
"Hivi wewe binti umelogwa nini yani umeniudhi na hujui pesa nilizo poteza ili usome leo hii unataka kunitia aibu na hasara uje kuzaa na hii takataka nakuambia sogea hapo nimmalize huyu ms***"
Anaongea mzee yule na kumvuta Jane atoke mbele yangu ili apate upunyo wa kunipiga risasi lakini anakuwa amefanya kosa kubwa kwani tayari niliona hapa ni kifo tu nikizembea cha muhimu nami nijitahidi kuuokoa uhai wangu
basi kwa haraka naushika mkono wa yule mzee aliokuwa kamshika nao mwanaye na mvuta kwanguvu nilipo na kumpiga kichwa cha nguvu kinachotua kwenye pua yake na kusababisha atoe ukelele wa maumivu huku akiiachia bastola inayoa nguka chini na kunipa chansi ya kuikokota ambapo yule mzee anaanguka chini kama gunia naichukua ile bastola na kumnyooshea japo siwahi kushika kifaa kile lakini ilinibidi niwe kama aliyezoea kukitumia
"Sasa nakuuwa kama ulivyotaka kunifanyia " niliongea nikionekana kumaanisha nilichosema
Kuona vile Jane alikuja mbio na kunisukuma ambapo niliangukia uso na kujiburuza kwenye vumbi nikijizuia nisiiachie bastola iliyo kuwa mkononi hakika nilichubuka uso mzima huku sura ikajaa mavumbi hapo ndo nikaamini kuwa mwanamke si mwenzako muda wowote anaweza akakubadilikia nilnyanyuka kwa hasira na kumfuata Jane aliyekuwa akimnyanyua mzee wake akimsaidia kusimama
"kweli nimeamini mwanamke si mwenzako yani wewe ndo umeniingiza kwenye matatizo yote haya alafu unanisaliti na kutaka kuniuwa sasa nimejua wewe na baba yako amna tofauti
Sasa nawauwa wote kwa kuwa mlitaka kuniuwa naongea maneno yale kwa ujasiri bila kujua nilipo utoa
Naachia risasi mbili mfululizo zinazotua katika kifua cha baba yake Jane anayeanguka chini akivuja damu na kufarika papo hapo
Kisha namgeukia aliyekuwa akiniangalia akitetemeka asiamini kilichotokea Jane wewe mwanamke nilikuona mwema na kukubali hisia zako kumbe lako lilikuwa lingine nashukuru kulitambua hilo mapema na kwaheri nafyatua risasi inayo kwenda moja kwa moja hadi kwenye paji la uso la Jane anayeanguka na kupoteza maisha pale pale
"Ameuwa" zinasikika sauti za waliokuwa wakishuhudia tukio lile huku wengine wakipiga picha na kurecord video tukio lile ambapo kama unavyojua wa bongo na mitandao ya kijamii lazima ile video inge sambaa
Kuona vile na weka bastola kiunoni na kulipangua kundi lile la watu na kukimbia katikati ya vichochoro nafika barabarani ambapo na chkua bodaboda anayeonesha kushangazwa na hali yangu
"vipi kaka mbna umeumia sana na unaonekana kuwa na haraka zote hizi"
"nipeleke tabata bonyokwa "
"Endesha haraka kuhusu malipo ntakupa elfu ishirini namwambia bodaboda yule ambaye naye japo kwa kusita anaondoa piki piki kwa kasi mpaka sehemu niliyo panga ambapo namwambia anisubiri naingia ndani ya geti na kuta kina mama wamekaa kibarazani akiwemo yule mama aliyeniona nikitoka kwa dada mwenye nyumba usiku ambapo baada ya kuniona wanacheka
"halooo!!!!! Mwaka huu utauama mji" wanaongea huku wakicheka lakini wanashangaa kuniona nilivyo chafuka mna mchubuko iliyojaa usoni japo wana jaribu kuniita lakini sikuwa na mda nao nafungua mlango wangu nachukua pesa yangu yote ya akiba niliyo hifadhi ikiwemo ile laki tano aliyonipa Jane ambaye kwa sasa ni marehemu nabadili nguo haraka na kunawa uso na kuvaa kofia yangu kubwa iliyoshonwa kwa nyuzi za sueta natoka bila kusahau bastola ambayo tayari nili jimilikisha na kufunga mlango wa chumba changu nikiondoka ila kuwasemesha wanawake wale ambao baada ya kuniona walibaki wananishangaa namkabithi bodaboda elfu hamsini na kumuambia anipeleke kituo cha mabasi ubungo ambaye anashangazwa na kiasi cha fedha nilichompa ila hasemi lolote anaondoa pikipiki namwambia aendeshebkwa mwendo ule ule tunaanza safari ya kuelekea ubungo stendi baada ya masaa kama mawili tunafika naagana na bodaboda ambaye anaondoka kurudi kwenye shughuli zake nami natafuta basi liendalo mkoani Arusha na kuanza safari ya kurudi kijijini kwetu ndani ya wilaya ya Arumeru
Taarifa za mauaji yale zinawafikia polisi wanaokuja na kuichukua miili pamoja na baadhi ya mashuhuda huku waki tumiwa video na picha tukio lote kuanzia mwanzo mpaka mwisho kwa njia ya mtandao wa Watsapp
Wanaondoka na msako unaanza wa kunitafuta wakati uwo nami gari linazidi kuliacha jiji la Dar es salaam...
Nimesha haribu mambo
Je nini kinafuata usiache kufuatilia sehemu ya (04)
Itaendelaa......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: