NJIA RAHISI 13 ZA KUWA NA FURAHA KILA SIKU  Mabadiliko yalio mepesi  kwenye tabia zako za kila siku yatakuweka kwenye mstari wa furaha unayoitaka Umejikuta uko kwenye siku tofauti,  story hizo hizo,  imekuwa ni kawaida yako?  Basi muda huu , sio kesho , sio wiki ijayo,  ni wakati wa kubadilisha historia yako. ni za haraka, rahisi  na hazina gharama unapofanya hivyo na matokeo yatakupa furaha unayoitaka. 1.Pata masaa 7 mpaka 8 ya kulala usiku. Kulala usingizi wa kutosha  unapata furaha, utaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi zako , na utakuwa na mahusiano mazuri. weka simu yako mbali unapoenda kulala,  usitumie chakula kingi wakati wa jioni. 2.Amka mapema , dakika 30 kabla . Kama wewe ni mfanya kazi wa kuajiriwa na una tabia ya kuchelewa kazini, jaribu kuamka mapema  dakika 15 au 30 kila siku kwa ajili ya kujiandaa vizuri na kukumbuka vitu vyote vya kufanya, kuchukua siku hio. utaona tofauti ya tabia yako. 3.Meditate. Hii ni kubwa. meditate kwa muda wa dakika 10 au 20, utapata faida nyingi zaidi ya furaha, pamoja na kuwa muwazi, kuwa na malengo  ya siku nzima. Anza siku yako na meditation. utajiepusha na tress na wasiwasi na  hutachanganyikiwa na kazi zako. 4.Jipe nafasi  wengi wetu huwa tunajaza vitu nyumbani, ofisini hata vile ambavyo havina kazi, hatuvitumii. inaharibu mfumo mzima wa akili yako, hisia zako,  na mwili wako. Ondoa vitu ambavyo huvitumii, tupa nje au gawia watu ambao wanahitaji kuwa navyo, hali yako ya furaha itaboreka. Na hutalemewa na kazi nyingi. 5.Jifunze kitu kipya Jitahidi kujifunza kitu kipya kila siku, kwa sababu hio ndio changamoto itakayokupa furaha, kujifunza kitu kipya inaboresha  afya yako ya mwili na akili, kujifunza utajenga ujasiri pia na utakuwa sharp. 6.Tembea mara kwa mara Kutembea kwa dakika 30 kwa siku  moyo wako utakuwa unafanya kazi vizuri, utapunguza hasira,  hutakuwa na chuki. Kama unaona ni ngumu kwako kutembea , hasa kama una gari , jifunze kupaki gari yako mahali mbali na ofisi , tembea . anza kutumia maji ya kutosha. utapata faida nyingi . 7.Usijihusishe na mambo ya mitandao. Ni rahisi kuingia instagram, facebook na zingine, lakini wachunguzi wanasema kwamba ukizidisha kujihusisha na mitandao unaweza kuharibu afya yako ya akili. badala ya kutumia nusu saa kwenye mitandao, unaweza kufanya kitu kingine unachokipenda, au kusoma kitabu, kujifunza mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiboresha mwenyewe kuwa mwenye afya. 8.Kuwa mwema. Ukarimu unakuongoza kwenye furaha yako mwenyewe na utakuwa mwenye afya bora. vitu ambavyo vinavyo chochea furaha ni kutoa , na kuwa mkweli , utapata faida , na utajisikia vizuri kuwa sehemu ya baraka kwa mtu fulani. kujitolea kufanya kitu, au kumwachia mtu kiti kwenye daladala. Sehemu ngumu? lakini nzuri. 9.Kaa na watu wenye furaha. Angalia watu unaoshinda nao, unaofanya nao kazi, ni watu wa aina gani. kwa sababu  kuna msemo unasema kuwa ukikaa na ua rose utanukia  hata kama ulikuwa hunukii. Fanya hivyo na utaweza kufungua mlango mpya kwa ajili yako maishani. utaiona furaha ikitiririka kama mto. 10.Don’t gossip. Kuseng’enya, umbeya, itakusababishia maradhi ya misongo na kukosa furaha. mtu mmbeya hawezi kusaidia kitu. wakati mwingine jitenge na watu kama hawa, au unapoona kuna kutoelewana na wafanya kazi wenzako, jaribu kutulia kwanza , badilisha negative to positive. Sema kitu kizuri kuhusu mtu. ni vizuri. kwa sababu utajiwekea alama nzuri kwako. 11.Tumia muda wako na watu unaowapenda Unapoongea na familia au marafiki kwenye simu , inatia moyo. mawasiliano hayo yanakupa afya na furaha.Fikiri ilivyo vizuri kama utaenda kula na rafiki yako mahali fulani, au kuamua kupika nyumbani , au kucheza na watoto wako kitu kama game, mpira, inafurahisha. 12.Journal Kuandika vitu vya kufanya kwa siku, au kuandika vitu unavyotaka kuvipata, Lengo hili dogo litaongeza IQ yako  na kuleta utulivu  wa kuboresha ujasiri  wako, ukiwa na tabia hii kila siku , furaha haitakosekana kwako na utapata faida ya akili na hisia zako zitakuwa bora. 13.Jizoeze kujijali. Unapojijali ,Utaona faida zake, pamoja na kuondoa stress na wasiwasi, utakuwa mtu wa kuwaza mazuri na utaboresha immunity.pata muda kila siku kufanya kitu kwa ajili ya furaha, kama vile mazoezi, kupika chakula kizuri, kusoma . utaanza kushangaa jinsi ilivyo rahisi kuwa na furaha  unapojijali  na utaboresha akili yako na mwili wako, na roho yako. Kama unavyojua , kuna njia nyingi  zinazotushambulia kwa siku, Ondoka mahali ambapo panaharibu ratiba yako. sasa, kama kitu kingine chochote,mafanikio ni kufanyia kazi. kwa hio pick one, and let the fun begin!

at 2:06 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top