Home → simulizi
→ NDOA YANGU.....HAPPY ENDING.
FINAL EPISODE .
ILIPOISHIA....
Mama mimi Nimekua muaminifu pale Vicky aliposhindwa kuwa muaminifu kwenye majukumu yake kwa ndoa, nimevumilia kipindi chote hicho mama sikuwahi kumsaliti hata siku moja......." Tony akawa akiongea kwa hasira huku akilengwa na machozi......
Sasa endelea......
"Tony tafadhali usitudanganye sisi kuhusu uaminifu. Kwahiyo unataka tukupe tuzo kwa kuwa sio msaliti? Nikadandia na kumkatisha aliyokua akiongea kwa kumwambia hayo!
"Funga mdomo wako Vicky, tena utulie kabisa, stupid woman" mama akanikaripia huku Tony akitingisha tu kichwa chake akionekana kusikitika. Nikajisikia aibu mama kunikaripia mbele ya Tony.
Nikawa kimya nikisikiliza mama na Tony wakiongea. Nikasikiliza mambo ya ukweli kabisa Tony aliyokua akimuelezea mama na nikayaona maumivu yake dhahiri kabisa alipokua akimsimulia mambo niliyokua ninamfanyia.
Nikaelewa uzito wa makosa niliyokuwa nikimfanyia Tony. Muda alipoanza kuzungumzia tu lile tukio la mimi kubakwa, nikaona machozi yakimtoka. Akakaa kimya, akainamisha kichwa chake chini...akachukua kitambaa chake na kujifuta machozi, kiukweli na mimi niliumia mno!
"Mama, nilimuonya Vicky. Nilimuonya asiondoke nyumbani. Mpaka leo hii sijaweza kuiondoa picha ya hilo tukio la mke wangu kubakwa kichwani kwangu. Ninaanzia wapi? Alikuwa akikataa kufanya tendo la ndoa na mimi kwa kisingizio cha mfungo na kwenda kumpa tendo la ndoa jambazi kirahis rahisi tu..aaah mama naumiaaa!!!"
"Tony, tafadhali usiseme alimpa jambazi kirahisi. Ule ulikuwa uvamizi na walikuwa na silaha. Wote bado tunayo maumivu juu ya lile tukio hasa mke wako.
Maumivu aliyonayo juu ya lile tukio ni makubwa mno. Anahitaji muda mwingi sana mpaka asahau na kuwa sawa tena. Na tushukuru Mungu kwani ameshapima mara sita sasa hajaambukizwa ugonjwa wa zinaa wala hakupata ujauzito." Mama akaongea.
"Nilimuonya mama, nilimuonya lakini." Tony akaendelea kusisitiza.
"Ni kweli mwanangu Tony, majaribu hayana budi kuja, ni vile tu kuwa na moyo imara wa kusamehe"
Mama akaanza kuongea na Tony kuhusu sisi kuwa na mawasiliano mazuri, kuelewana na kuwa wepesi kusameheana. Akaongea mengi mno ambayo yalinigusa moyo wangu moja kwa moja na nikajawa na huruma nyingi na majuto kila nilipokuwa nikimuangalia Tony usoni.
Nafsini nikajiambia huyu ni mume wangu, kati ya wanawake wote amenichagua mimi peke yangu, kwa kweli sikustahili kumfanyia yale niliyokuwa nikimfanyia, naijutia nafsi yangu!!
Baada ya ushauri na maneno mengi ya busara kutoka kwa mama, Tony akaanza kuelewa na kupunguza hasira juu yangu.
"Wote wewe na mmeo mnatakiwa mfanye maombi, muwe wavumilivu na mjifunze kuwasiliana na kukubaliana jambo."
"Mama, kusema ukweli, mimi sina uhakika kama hii ndoa bado ipo. Kwa sababu mimi sijui hata nitaanzia wapi na Vicky."
"Tony mwanangu, msimpe shetani ushindi wa mezani kiwepesi hivyo, wote mnatakiwa muanze kwa kusameheana kwanza na baada ya hapo mambo mengine ni hatua kwa hatua. Mnaanza na maongezi, yale maongezi ya karibu sana yatakayounganisha mioyo yenu, mshirikiane maumivu na hofu na baada ya muda fulani wote mtajikuta mkiwa vizuri tena."
"Sawa mama, asante sana."
Kwa kuwa mama alikuwa na tiketi ya kwenda na kurudi, Saa moja baadae mama akaondoka na kuelekea Airport kurudi Mwanza. Akagoma kabisa kubaki hata kwa siku moja tu akidai amemkumbuka mume wake na anahofu kumuacha peke yake na wala hakutaka tusimsindikize bali akataka tumkodie tax tu.
Na kwa hilo nikajifunza jambo jingine kubwa tu, kuwa karibu na mume wako kadiri unavyoweza!
Baada ya mama kuondoka tu, nikamfuata Tony na kumkumbatia kwa nguvu.
"Baby, I am sorry, nisamehe kwa yote niliyokufanyia nakiri kwako na mbele za Mungu sitarudia tena, kuanzia sasa nitakua nikikusikiliza wewe tu, na zaidi wazazi wako na wangu basi...i love you my Tony!"
"Vicky, i am sorry too, nisamehe kwa kuwa sikuwa na wewe katika kipindi kigumu cha maumivu ya kutendewa unyama na wale mafedhuli.
"Ukweli ni kwamba nilichanganyikiwa baada ya baba kunieleza lile tukio na mpaka sasa hivi sijui nitawezaje kuliondoa lile tukio kichwani mwangu" Tony akanieleza hayo huku nae akiwa amenikumbatia.
”We will babe”, nikamwambia Tony kwa kujiamini ”we will, one day at a time”.
LEO HII.
Tupo likizo Nchini China, mimi na mume wangu Tony na mwanetu Jayden akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu. Siku zote namshukuru sana Mungu kwa kunipa Tony wangu! He is such a darling...i love him to death!!!
T H E E N D !
Asante sana wote mliosoma simulizi hii na kushare mawazo yenu kuhusiana na kisa hiki. Maneno yenu siku zote yamenifanya niwe na moyo wa kuandika. Maombi yangu ni mkono wa Mwenyezi Mungu utaponya kila ndoa iliyopo katika matatzo na utawaongoza wote ambao bado wako single kufanya maamuzi sahihi.
THANK YOU SO MUCH, I
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: