Home → simulizi
→ ®HADITHI PICHA®
👙👙👙 DADA VUA👙👙👙
PICHA NO:_1
MWENDELEZO 2500 TU
TUNAANZA RASMI KIGONGO CHETU KINACHOKWENDA KWA JINA LA DADA VUA CHUPI👙👙👙
Simulizi yetu inaanzia katika jumba moja la familia ya mzee maarufu sana hapa mjini
Kama unavyojua katika familia nyingi wazazi hufikia mahali kuwagawia watoto wao baadhi ya mali ili waanze kujitegemea katika maisha yao.Basi leo katika familia ya Mzee Nassor ilikuwa ni siku rasmi kwa ajili ya mgao wa baadhi ya mali kwa watoto wao.Kiukweli mzee Nassor alikuwa na mali nyingi sana.Basi siku ya leo Mzee aliwaita wanae woote kisha akawaketisha chini na kuwaambia"WANANGU LEO NIMEWAITA HAPA ILI NIWEZE KUONGEA NANYI MANENO MACHACHE KABLA YA KUFANYA TUKIO KUBWA NA LA KIHISTORIA KWENU.KWANZA KABISA MIMI PAMOJA NA MAMA YENU TUNAWAPENDA SANA NA FURAHA YETU INAKAMILISHWA NANYI WANETU,KILA WAKATI NIMEKUWA NIKIWAFAHAMISHA JUU YA MALI NINAZOMILIKI MIMI BABA YENU.SASA LEO NATAKA KUWAMEGEA ANGALAU ROBO YA MALI ZANGU ILI NANYI MUANZISHE FAMILIA ZENU"Kabla hajaanza kugawa zile mali mzee alimuita mkewe na kumnong'oneza"Mke wangu najua unatamani sana nifanye hicho unachofikiria lakini kumbuka masharti tuliyopewa na mtaalamu".......Mkewe alijibu"Mume wangu mimi kuhusu hili wala sina hofu moyoni mwangu kinachoniumiza ni suala la kuwapoteza wanangu wote wa kike bora tungewatoa wa kiume tuu lakini tuachane na hayo kikubwa tuna hizi mali basi hakuna kinachoshindikana tufanye vile tulivyoagizwa"
Basi walikubaliana pale kisha mzee na mama wakarudi pale walipo watoto wao wanne ambao ni Shukuru,Sudi,Wedi na Sule.Mzee alianza kwa kusema"Sasa nianze na wewe Wedi chukua hii hati ya umiliki wa (Senshen supermarket na Kadi 2 za gari)Hivo vinakutosha kwa kuanzia maisha wakati mkisubiri ujenzi wa nyumba zenu uanze.Wedi alifurahi sana kitendo cha yeye kupewa zile mali amiliki yeye.Mzee alimgeukia mwanae wa pili (Sudi) na kumwambia"Naona unagugumia mate kwa kutamani kusikia nini unapewa haya shika hizi(Sudi alizitoa zile karatasi ndani ya bahasha ambapo ilikuwa ni Kadi za mabasi mawili yanayofanya safari za Arusha to Mwanza pamoja na hati ya umiliki wa hoteli moja maarufu iliyoko Mombo).Basi ilikuwa ni furaha sana kwa watoto wale Baba aliitoa bahasha ya tatu kisha akamfungulia mwanae(Shukuru) kisha akamwambia "Shukuru wewe utasimamia na kumiliki hii kampuni ya (Senshen tours).
Watoto wote walipatiwa kile kilichowastahili kasoro sule pekee.Baba alimtazama Sule kisha akamwambia" Sule wewe tunakuandalia nyaraka zako tutakupa mwezi ujao"Sule alidakia"Baba wala hata usihangaike na mimi kwani sio mara ya kwanza kufanya hichi ulichonifanyia leo"Sule aliongea huku macho yake yakionesha machozi na uso ukiwa na huzuni tele sule aliongea tena"Siumii kwa kuwa hujanipa mali bali naumia sana kuwaza mi ni nani kwenye hii familia na pengine sina wa kunipa ukweli juu ya hilo nitaishi kama mfungwa angali nikohuru".Mama alidakia "Mwanangu Sule mbona unaongea maneno machafu kiasi hiko Ina maana humuheshimu baba yako,kwani si umefahamishwa kuwa mwezi ujao utapata haki yako!!?"........"Mamaaa eeeeh nimesha sema sitaki hata mia yenu nachotaka kujua mi ni nani kwenu maana moyo wangu umechoka kuvumilia haya mnayonifanyia".
Sule aliongea maneno mazito sana ndipo Wedi aliposimama na kutaka kuweka mambo sawa" Jamani eeeh!! tusigombane sisi ni familia moja"Wedi alimgeukia baba yao kisha akamwambia"Sasa baba fanya hivi,Kwenye hizi mali ulizotugawia fanya kurudia upya ugawaji ili Kaka yetu Sule naye apate maana hata mimi sijapenda hichi ulichokifanya kwa kaka yetu"......."Wedi mimi ndio Baba yenu na ninajua kile ninachokifanya msinione mpumbavu sawa!? sidhani kama mnaweza kunipangia nini cha kufanya".,......Sudi alidakia"Lakini Baba si kuna sheli nne si ungempa hata moja ile iliyoko Mwanza?"........"Sijashindwa kumpa hata hii iliyoko hapa Arusha lakini kila jambo linaenda na mipangilio ok!!".
Sule alinyanyuka kimya kimya na kuwaacha wote wakimshangaa wasijue ni kwanini anaondoka pale.Wakati huo Mama wa watoto hao hakuwa na nguvu ya kubadili maamuzi yaliyotolewa na kichwa cha familia (Baba).Sule alitoka mpaka nje huku akitafakari nini cha kufanya,Alirudi akapita mpaka chumbani kwake kisha akaanza kupanga nguo zake kwenye kirasket kidogo dogo tuu.Katika kupanga panga nguo aliona picha ya dada zake walipiga wakiwa pamoja,Aliitazama picha ikamrudisha nyuma kimawazo kwani walikuwa bado wadogo sana kipindi hicho.Basi sule aliikumbatia picha ile kwa mapenzi mazito kwani dada zake walikuwa wamesha tangulia mbele za haki(Walifariki miaka 14 iliyopita).Sule alinyanyua kibegi chake akawa anatoka nje huku akifikiria aende wapi kwani hawezi tena kuendelea kuishi ndani ya ile nyumba"Sasa sijui niende wapi kwani kwa vyovyote lazima niondoke leo"...Sule aliwaza akakumbuka kipindi cha nyuma alishawahi kuishi katika kijiji fulani kinaitwa Ngare kule aliwahi kufanya shughuli za kilimo cha nyanya na alikuwa na hali nzuri tuu kimaisha japo nizamani sana kama miaka 16 ishapita.
Wakati anajiandaa kutoka alikuja mama yake akaingia mpaka chumbani kwake...."We sule unataka kufanya nini!!?"...."Kiukweli mama nikikaa hapa nitazidi kuumia tuu kwani sitaweza kuvumilia hiki kinachoendelea"......"Sasa unakwenda wapi mwanangu sule!!!?"......"Mama mimi ninakwenda lakini nitarejea mungu akipenda lakini kama nitakufa bila kuonana nawewe basi ni mapenzi yake mungu".Sule aliongea maneno yaliyojaa ghadhabu na kumuacha mama yake katika hali ya mshangao.Sule alifika pale walipokuwa wameketi baba na wadogo zake kisha akawaambia"Sina sababu ya kuendelea kulazimisha kuishi na wazazi wasionijali,Simaanishi kuwa nataka mali zenu laa!! bali nalihitaji mapenzi ya wazazi wangu lakini nashangaa mimi nabaguliwa mpaka wadogo zangu wananidharau kisa ni nyie wazazi hamkunipa heshima ya kuwa kaka wa wadogo zangu.Sasa leo nawaacha huru acha nikayatafute maisha yangu mwenyewe"Sule alionge kisha akatoka nje akiwa na hasira mpaka machozi yanamdondoka.Wakati anaondoka Baba alionyanyua simu kisha akasogea pembeni na haikufahamika anampigia nani.
Sule alinyanyua kibegi chake vizuri kisha akakiweka mgongoni na kuelekea Ngare.Kweli aliondoka akipitia barabara ya msitu wa Momela/Arusha National Park.Akiwa anaanza kuingia katika pori la msitu alihisi kitu kinatokea mbele yake maana alisikia mchakacho,Basi Sule aliamua kujibanza kwenye shina la mti ili kama ni kitu cha hatari aweze kukabiliana nacho.
Je nini kitaendelea usikose sehemu ya pili ya simulizi yetu.usisahau kudondosha like na coment ili nipate mzuka wa kuleta vitu vikali zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: