RIWAYA: HIGH SCHOOL SEHEMU YA TATU. Niliyazoea mazingira ya shule mpya, ilikuwa ni shule ya kifahari ambayo haikuwa rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kumsomesha mtoto wake. Ufaulu wangu pia ulikuwa juu. Mwalimu Maloya ambaye alikuwa ni mwalimu wa mazingira alikuwa akifatilia maendeleo yangu kwa ukaribu zaidi, mara zote nilipokosea aliniita ofisini kwake na kunionya. Na wakati nilipofanya vizuri hakusita kunisifia mbele ya watu, nilimpenda kwakuwa alijali maendeleo yangu. Candy aliendelea na tabia yake ya kulala kila mara, mara nyingi nilimkuta amelala wakati wa vipindi, nilijua ndio aina yake ya maisha aliyokuwa akiishi tangu alipofika shuleni kwani pamoja na tabia yake ya kulala kupitiliza Candy alikuwa vizuri kimasomo, kitaaluma alikuwa juu na alikuwa akiwaongoza wenzie darasani. Dharau za Candy zilizidi maradufu sikujali kabisa. Urafiki wangu na Martin ulizidi kadri siku zilivyozidi kwenda, alikuwa ni mvulana mwenye kujali, mpole na mwenye haiba nzuri. Mwanzoni sikupenda kampani ya wavulana, lakini kutokana na haiba yake niliweza kumzoea na tulishirikiana kwenye masomo na kuweka ushindani baina yetu. Nilikuja kugundua martin ni raisi (kiranja mkuu wa shule) na pia alikuwa ni kiongozi wa kwaya kwenye jumuiya yetu kanisani. Alipenda kuimba na alikuwa na sauti nzuri sana. Pia nilikuja kujua kuwa Candy alikuwa ni kiongozi wa mazingira. Candy alianza tabia ya kujiandaa alfajiri mapema kabla sijaamka kila nilipoamka nilikuta tayari ameshamaliza na wakati mwingine alishaondoka. Hakuwa na nafasi katika akili yangu hivyo nilimpotezea. Ilikuwa ni siku ya ijumaa siku niliyowahi kuamka tofauti na kawaida nilimshuhudia candy akivaa mkanda wa kupunguza tumbo nilijiuliza maswali bila majibu mkanda wa nini na hakuwa na tumbo. Huku nikijifanya nimelala niliendelea kumtazama wakati akivaa. “Ili tumbo mwishowe litaniumbua, looh!” alijiongelesha mwenyewe. “Leo lazima huyu kidudu mtu anipe mustakabali wangu kabla mambo hayajawa mabaya”, aliongea. Nilichelewa kugundua kuwa candy ni mjamzito. aliendelea kujiandaa na kisha alijongea kabatini kwake. Alipofika kwenye meza ya kujisomea mahali nilipoweka daftari zangu na vitu vyangu alisita, alichomoa kitambaa ambacho hata kwangu kilionekana kipya sikuwa nimewahi kuwa na kitambaa cha namna hiyo nilijiuliza kimetoka wapi na cha nani na kimefikaje kwangu, bila majibu. Candy alikitazama, akasonya na kisha akakirudisha kilipokuwa na kisha akaliendea kabati lake. “Candy” sauti ilipenya kwenye masikio yangu, alikuwa ni msichana mwingine ambaye nilizoea kumwona pale shuleni ambaye alikuwa akiitwa Naima alipenda kujiita Nana. “Niambie best yangu” Candy alijibu, “meseji yako nimeiona leo asubuhi nikaona nije sasa hivi kabla ya kuingia darasani” alisema Naima. “Ndio hivyo shoga yangu” Candy alijibu. “sasa itakuwaje?” Naima aliuliza, “Nataka nimfate maloya anipeleke nikaitoe kwa maana imeshafikisha miezi miwili, mwisho wake tumbo litakuwa kubwa itajulikana hali itakuwa mbaya zaidi.” Kijasho chembamba kilinitiririka kumbe Candy ana uhusiano na Maloya uhusiano uliozaa mimba na sasa wanampango wa kuitoa hiyo mimba, duuh! Nilichoka. Waliendele na maongezi yao hadi walipofikia muafaka kuwa candy aende kwa Maloya ampeleke kuitoa hiyo mimba. “Huyu kiazi ajasikia kweli?” aliongea Naima kwa dharau “mmmh, linalala kama ling’ombe” Candy alijibu kwa nyodo wakacheka na kisha wakatoka. Niliendelea kuwaza pale kitandani candy kwanini umefanya hivyo jamani we ni msichana mzuri kwanini unajiaribia uzuri wako niliwaza. Ni kweli Maloya alikuwa kijana tena mzuri alikuwa ni mwalimu mzuri sana na zaidi ya yote alikuwa na haiba nzuri, lakini Candy ni kwanini ukaingilia mambo haya wakati sio wako. Ona sasa umepata ujauzito na sasa unataka kuhatarisha maisha yako kwa kutoa huo ujauzito. Niliendelea kuwaza pasipokuwa na majibu. Nilikuja kushituka wakati umeshaenda na nilikuwa nimeshachelewa sana niliamka na kujiandaa kwa haraka na kukimbilia darasani muda wote nilionekana mtu mwenye mawazo sana, Martha aliligundua hilo na Martin pia, kila mmoja aliniuliza kwa wakati wake. Nilimjibu Martha sina tatizo. “Martin ninaomba mda niongee na wewe” nilimwambia Martin “aaanh sawa tutaongea wakati wa mapumziko” alinijibu kwa sauti yake nzuri. Kiukweli nilishindwa kuvumilia kuyabeba mambo ambayo niliyasikia asubuhi ya siku hiyo niliona ni vema kumshirikisha Martin kwa sababu nilikuwa nikimuamini na alikuwa rafiki yangu wa karibu sana. Wakati wa mapumziko hatukwenda kula tulibakia darasani. “Martin” “nakusikiliza bibie” Martin alijibu. “Unafahamu kwamba naishi na Candy chumba kimoja?” “ndiyo najua” alisema. “Kiukweli nimejua kitu ambacho binafsi kimenichanganya sana na nimeshindwa kuvumilia kukaa nacho nimeona bora nikushirikishe” “niambie kitu gani hiko?” alisema Martin. “Candy ni mjamzito” Martin alishituka isivyo kawaida tofauti na nilivyo tegemea. “Say whaaat!?” alisema kwa ghadhabu “Martin candy ni mjamzito.” “Huweza kuwa serious Catherine, kwanini unaongea utani?” aliniuliza. “Hapana sio utani nina uhakika na hilo.” Alishindwa kuendelea alibakia akitweta huku jasho jembamba likimtiririka. “Na ana mpango wa kuitoa” niliendelea, hakujibu aliendelea kujiinamia pale chini. “Kibaya zaidi” niliendelea, “ujauzito huo ni wa mwalimu maloya.” Martin aligeuka na kunitazama kwa jicho kali “unaongea nini wewe?” “Martin huamini ninachokuambia?” niliongeza. “Katika siku ambayo umewahi kunichanganya leo ni siku ya kwanza sitaki kukwamini Catherine sitaki kabisa” alisema Martin kwa sauti ya kukata tamaa. “Martin nina uhakika na ninacho kiongea.” “Kumbe ndo mana candy amebadilika sana siku hizi aonekani darasani hataki tena kuja kuniona naa…..” Ni kama alishitushwa na akaishia hapo, “ok sawa nitalifanyia kazi kwaheri Catherine.” Aliondoka Martin mbele yangu, nilitamani kumwita lakini nilishindwa nilijua kutokana na yeye kuwa ni raisi wa shule lazima ingemchanganya lakini sio kwa kiwango kama hicho. Ana nini huyu Candy anamhusu vipi? Nilijiuliza maswali bila majibu. Mwisho wa yote niliendelea kukaa darasani kwa ajili ya vipindi Martin hakurudi tena, vipindi vilipoisha nilirejea bwenini kwetu. Nilipoingia chumbani kwangu nilimkuta Naima na Candy wamesimama kana kwamba wanamsubiri mtu kisharishari nilisita nikaingia na kisha nikawasalimia mambo zenu, hawakunijibu. Nilishangaa kwani kuna tatizo lolote niliuliza hawakunijibu baada ya kukosa majibu niliamua kuendelea na mambo yangu, nikasogea mezani kwangu kwa ajili ya kuweka madaftari yangu, candy alinisukuma. <<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA >>>>>>>>>>>>>>>>

at 10:27 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top