Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA NNE.
“Wewe ndiyo unaejifanya mzuuuuri kuliko wote hapa shuleni kiasi cha kuchukua wanaume za watu unajiamini nini na kwa uzuri gani unanitafta nini wewe kidudu mtu, eeenh” aliongea Candy kwa hasira zenye mchanganyiko wa jazba, nilishindwa kumwelewa nilibaki nimetoa macho huku nimeachama mdomo.
“Candy sielewi unaongea nini?” nilisema.
“Uelewi naongea nini?” Candy aliongea huku amenibania pua.
“Mpumbavu sana we msichana umefika hapa shuleni unaanza kujiona wewe ni mzuri umeshazoea shule kiasi unaingia anga za watu nataka nikwambia kwamba hapa umekalia kuti kavu.”
“Candy unanichanganya sijui unaongea kuhusu nini mbona sikuelewi kwani nimekufanya nini mimi?”
“hujui ee hujui unajifanya hujui” alidakia Naima.
“Usione tumekunyamazia kimya tunakuogopa tunakuchora tu maana umekuja hapa unataka kujifanya wewe staaa eee” walizidi kunichanganya nilishindwa kuwaelewa.
“Candy kama hutaki kunielezea ni nini kimetokea mimi sikuelewi na siwezi kuendelea kukusikiliza nina mambo mengi ya kufaya nielezee tatizo ni lipi ili mi nijue tatizo likowapo sasa unaniambia tu unaniongeleshaongelesha mi vitu sivielewi nashindwa kukuelewa” niliongea kwa kupaniki,
“unashindwa kunielewa?”
Alichukua leso ambayo ilikuwa katika madaftari yangu pale juu.
“hii leso umeipata wapi unajua imetoka wapi hii wewe eee?”
haaa! Nilishangaa.
“Hiyo leso hata sijui kwangu imefikaje” niliongea huku nikionesha kutojiamini
“hiyo leso hata sijui kwangu imefikaje” Aliongea huku amebana pua zake, nilibaki tu nimeshangaa.
“sikia nikwambie kaa mbali na wanaume za watu”
nilijiuliza maswali yaliyokosa majibu, maloya ameweka wapi leso yake kwenye madaftari yangu na ni lini?, nikabaki najiuliza.
Waliendelea kunipasha na kunipashua. Sikutamani kuendelea kuwasikiliza, nilijawa na mawazo mengi sana, waliongea, walinisema na matusi makali ya nguoni walinitukana waliporidhika walicheka kwa dharau na kisha wakatoka.
Nilipanda kitandani kwangu nikiwa mnyonge na mwenye mawazo mengi, nililia sana, nililia mno nimekosa nini mimi, toka nimefika hapa shuleni sina hata miezi miwili tayari nimeshaanza kukutana na mambo ya ajabu kama haya nitaweza kweli, Maloya kwanini umenisababishia matatizo hivi uliweka vipi leso yako katika madaftari yangu ona sasa jinsi nilivyotukanwa, mungu nisaidie, nililia kwa uchungu.
Nililia hadi nilipopitiwa na usingizi nilikuja kuamka tayari ilishakuwa jioni, nilihisi njaa lakini sikuwa na hamu ya kula kabisa. Nilioga na kisha nikatoka kwenda darasani sikutamani hata kuhudhuria kwenye kipindi cha dini cha siku hiyo nilikuwa na mawazo mengi sana, nilipoingia darasani nilishindwa kujisomea, nilikuwa mnyonge sana niliendelea kuwaza na kuwazua pasipo majibu.
“Cathe” Martin aliniita niligeuka na kunitazama kisha nikaendelea nikarudisha macho yangu chini alivuta kiti na kukaa pembeni yangu,
“Cathe unaonekana mnyonge sana leo, unaumwa?” aliniuliza kwa upole
“hapana siumwi niko salama” niliongea kana kwamba nimelazimishwa,
“unaonekana hauko sawa any way kama huoni umuhimu wa kuniambia sawa.”
Niliinama pasipo kumjibu lolote
“Cathe nataka nikwambie kitu” aliongea.
“Nilipofika hapa shuleni nilikuwa nikisumbuliwa sana na wasichana, wengi walikuwa wakinitaka kimapenzi lakini nilikataa kwa vile sikutaka kuwa nao yote kwa yote nilishindwa kwa mtu mmoja tu sio kwa sababu ya kwamba yeye ni mzuri au kwa sababu alikuwa na kila kitu ambacho nilikuwa na kihitaji au kwasababu alikuwa na pesa ila kwasababu alitumia nguvu kuniforce. Muda mchache wa mapenzi yetu nilijikuta nampenda sana aliongea kwa hisia kali zenye kugusa moyo niligeuza macho yangu na kumtazama
“eeeehe” nilimwambia huku nikionesha utayari wa kuendelea kumsikiliza.
“Alitumia nguvu sana kuniforce sikuwa na jinsi kwa maana alitumia hadi vitisho kwa vile mimi nayeye hatutokei mkoa mmoja niliona atakuwa akinisumbua sijui ni nini kilinifanya najikuta nampenda hivi, vituko vyake vilinichosha. Maisha yaliendelea lakini alikuwa akionekana akibadilika sana kitabia nilichoka kumvumilia,, nikampa uhuru afanye kile anachokitaka, niliendelea na maisha yangu. Siku akinimisi alikuwa akija kwa mbwembwe nyingi, vizawadi na ahadi kemukemu, alikuwa anajishaua mbele yangu, nilikuwa nikimwonesha ushirikiano kwasababu yeye ni mtoto wa kigogo mkubwa sana baba yake ndiye anamiliki hii shule alikuwa akinitishia kunifukuzisha shule mara kwa mara wazazi wangu walikuwa wakinihusia sana kuhusu kusoma, kwasababu wanatoa hela nyingi sana kunilipia ada hapa shuleni hivyo walikuwa hawapendi nifanye ujinga hapa shuleni nilitii amri, kiukweli taarifa yako imeniumiza sana sitaki kuamini kwamba candy wangu alikuwa anatembea na maloya kiasi cha kubeba mimba”
Nilishituka, nikajikuta nimetoa macho, nilishtuka pasipo na kifani. Nilishituka pasipo kawaida pasipo na kifani,
“Martin unaongea nini?” nilimuliza kwa sauti darasa zima waligeuka na kutuangalia
“aaanh sorry class mnaweza mkaendelea kusoma” niliongea kwa woga
Martin alitikisa kichwa pasi na hakuniangalia
“ndivyo ilivyokuwa Cathe” nilishusha pumzi za uwoga,
“inamaana wewe ndiyo uliweka leso yako kwenye madaftari yangu”
aligeuka kwa haraka na kuniangalia
“sijaiyona leso yangu leo nina siku ya pili, ni leso ambayo alinipatia candy”
“ooh my god kumbe” nilionge
“nimetukanwa sana na Candy kisa hiyo leso nilijua ni leso toka kwa Maloya sikujua kama una mahusiano na Candy samahani kwa kukuletea taarifa mbaya” niliongea nilinyanyuka na kusimama, alinivuta mkono,
“martin sikuwahi kujua kama uhusiano wangu na wewe utaleta shida nimekuja hapa kwa ajili ya kusoma sio vitu vingine tazama nimeanza kugombana na watu kisa ni wewe endelea na candy wako na mimi niache nisome” nilisema kwa hasira lakini kwa upole wa ajabu chozi likinitoka.
“Candy yupi sasa?” ailiniuliza kwa kutojiamini,
“Candy mwenye ujauzito wa mwalimu na bado unasema Candy wangu” nilishindwa kuongea nilimwonea huruma sana
“pole kwa kilichokukuta Cathe”
“asante” nilisema kwa upole
“yaliyotokea yamesha tokea la muhimu ni kujua nini kinachofuata nashukuru mungu sihusiki na ujauzito wa Candy” aliongea lakini kwa sauti iliyoonesha kukata tamaa,
“martin kuna tatizo zaidi ya hili?”
“ndio tatizo lipo….., nilijua ni kwa nini Candy alinitakaa mimi na hakupenda uhusiano wetu uwe wazi”
“kwa nini?” niliuliza
“anataka kunitumia mimi kama chambo endapo tatizo litakuwa kubwa” “unamaanisha nini?”
“ninamaanisha huo ujauzito utakapogundulika Candy atanitaja mimi na sio Maloya”
“huuu” nilishusha pumzi ndefu
“pole Martin”
“sijapoa na sitapoa mbele yangu naona giza kubwa sana.”
Nilijutia kiherehere changu cha kwenda kumwambia Martin kuhusu Candy. nilishindwa nimwambie nini mtoto wa watu aliyekuwa mbele yangu amekata tamaa.
“Martin nitakuwa bega kwa bega na wewe nitahakikisha kwamba hakuna kitu kibaya kinatokea kwako, nitakupigania kadri ya uwezo wangu naomba usikate tamaa wala usijifikirie vibaya kuhusu Candy nitasimama upande wako” niliongea kwa kujiamini zaidi, aliniangalia, akaachia tabasamu la uchungu
“aaahh sawa” alisema.
“ok”
“tuendelee kusoma” nilisema.
“sina mood wa kusoma kabisa” alisema,
“mimi pia”
“basi tupige story nyingine.”
Tuliendelea kupiga story nyingine mpaka mda wa prepo ulipoisha aliomba kwenda kupumzika na mimi nilielekea chumbani kwajili ya kupumzika.
Kila siku ugumu ulizidi, nilikuwa nikitukanwa kila sehemi niliyokuwa napita na marafiki zake Candy nilichekwa bila sababu, huku nikiendelea kupata adhabu.
Siku moja niliitwa na mwalimu Maloya ofisini kwake niliogopa hata kwenda ingawa na jinsi, nilipofika alinikaribisha kwa tabasamu pana lililofanya uzuri wake uzidi kuonekana zaidi.
“karibu Cathe, karibu ukae.” Nilikaa kwenye kiti.
“Cathe unajua wewe ni msichana mzuri sana sijaona msichana mzuri kama wewe hapa shuleni, naomba unisaidie kitu kimoja” aliongea, nilishikwa na bumbuwazi lisilo na kifani.
“nikusaidie nini tena mwalimu, mimi nina uwezo wa kukusaidia kitu gani?”
“aaaaa usiwe na haraka Cathe nisikilize kwa umakini” aliongea.
Alisimama kutoka kwenye kiti chake akazunguka meza iliyokuwa katikati yetu hadi alipofikia kwenye kiti ambacho nilikuwa nimeketi akanishika begani,
“Cathe nakuhitaji” alisema
“aaaaaa hapana mwalimu” niliongea nikiutoa mkono wake.
“sitaki”,
“Cathe embu nionee huruma mwenzio nakuhitaji sana”
Alinichefua nilitamani kumwambia kuhusu yeye na Candy lakini nilisita nikaamua kunyamaza kimya.
“hapana mwalimu ninakuheshimu sana naomba heshima hii iendelee kati yangu mimi na wewe, siwezi naomba uniache ” niliongea kwa kujiamni na kisha kutoka nje.
Nikarejea bwenini, sikuweza kuendelea na vipindi vya siku hiyo, nikajifungia mlango nikaanza kulia.
Nikajuta kujua kwangu mahusiano kati ya Candy na Martin na kati Candy na Maloya.
Nilijiona nimejisababishia matatizo makubwa sana kitu ambacho sikujua ni kwamba kuna matatizo makubwa mbele yangu zaidi ya hayo yaliyokuwa yakinikabili, katika maisha yangu yote niliilaumu high school imenibadilisha maisha yangu sana na kunifanya kuwa kiumbe mwenye roho ya utofauti.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
>>>>>>>>>>>>>>>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: