Home → ushauri
→ *Njia ya kuondoa michirizi*
Stretch Marks (michirizi) hutokea sehemu mbali mbali za mwili, mikononi, miguuni, mapajani, tumboni nk, wengi hutokewa kutokana na kuongezeka kwa mwili (kunenepa) au Ujauzito hii hutokana na ngozi kutanuka. Wengi hawaipendi na wana tafuta namna ya kuziondoa unaweza kuondoa stretch marks naturally (kwa njia za asili) bila kwenda kununua madawa ya bei ghali.
1) MAFUTA YA MNYONYO
Mafuta ya mnyonyo husaidia sana kwenye ngozi kama mikunjo ya ngozi husoni, chunusi, mabaka meusi kwenye ngozi lakini pia husaidia katika kuondoa michirizi.
paka mafuta ya mnyonyo mahala palipo kuwa na michirizi
funga eneo hilo kwa mfuko wa plastic kama uonavyo pichani
kisha weka kitu chenye joto juu ya mfuko huo kama heating pad au chupa ya maji ya moto kwa dakika ishirini (20) kila siku mpaka utakapo ona mabadiliko.
2)ALOE VERA husifika kwa kutibu magonjwa mbali mbali ya ngozi hivyo pia husaidia kuondoa michirizi hii ya ngozi kwa njia mbili zifuatazo,
kwanza unaweza kupaka Aloe Vera tu na kuiacha ikae kwenye sehemu iliyo kuwa na michirizi kwa dakika 15 kisha uoshe kwa maji ya vuguvugu au,
njia ya pili, ni kuchanganya majimaji ya Vitamin A, Vitamin E na Aloe Vera yenyewe kisha paka kwenye eneo lililo athirika na michirizi kila siku. Paka kama mafuta ya kupakaa mwilini.
3)SUKARI
Chukua sukari mbichi kijiko kimoja, mafuta ya Almond na Maji maji ya ndimu, changanya kwa pamoja halafu paka pale palipo athirika
Fanya hivi kila siku kabla ya kwenda kuoga, fanya kwa mwezi mzima na utaona matokeo yake.
4) JUISI YA VIAZI vina vitamini na madini ambayo kukuza ukuaji wa seli za ngozi.
kata kata kiazi chako katika vipande vyembamba
chukua kipande cha kiazi na ukisugue pale kwenye michirizi yako hakikisha yale maji ya viazi yame ingia kwenye michirizi ako.
kaa nayo kwa muda na kisha uondoe kwa maji ya uvugu vugu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: