Mzunguko Wa Hedhi  Mwnamke yeyote mwenye afya mwilini na aliye na umri wa miaka kumi na miwili kuendelea, huwa na nyakati ambapo hutokwa na damu sehemu za unzazi, hali ambayo hujukana kama hedhi. Hali hii ni ya kawaida na huonyesha ya kuwa youle mwanamke ni amefikia kiwango cha kutunga mimba. Hali ya maisha ya siku hizi imebadilisha umri wa kuanzia kutokwa na hedhi ikawa hata watoto wa umri wa miaka tisa wanajipata wakati mwingine wakiwa na hali hii. Mzunguko huu wa hedhi huendelea ukirudiwa kila baada ya siku kama ishirini na nane isipokuwa wakati wa uja uzito na miezi kadhaa baada ya kujifungua. Wakati mwingine wa kutopata hedhi ni  mwanamke anapokoma uzazi kwa sababu ya umri, hali ambayo huanzi aumri wa miaka 45 na kuendelea hadi 49 au 50. Hedhi au kutokwa na damu, huwa ni hali ya nyumba ya uzazi inapoachia yai amabalo limefikia wakati wa kurutubishwa kwa mbegu yakiume lakini halijapata. Yai hilo hutoka nje likianadamana na ngozi ya ndani ya nyumba ya uzazi amabayo huwa imeandaliwa kwa ajili ya kufunga mimba.  Ngozi ile hutoka ikiwa kama damu, na kuacha nyumba ya uzazi ikiwa tayari tena kwa mbegu nyingine. Hedhi ni kipindi maalumu katika mzunguko wa mwanamke mwenye umri wa kuzaa. Wakati huu kwa kawaida unarudi kila baada ya mwezimmoja hivi, yeye hutokwa na damu kwenye sehemu ya uke. Wasichana wengi hupata siku zao za kwanza kati ya umri wa miaka kumi na moja na kumi na nne. Lakini baadhi ya wasichana wanaweza kuanza mapema wakiwa na umri wa miaka nane na wengine wakachelewa hadi miaka kumi na saba. Msichana anapopata hedhi ina maana kuwa mwili wa mwanamke unakuwa umepevuka na ni maandalizi kwa ajili ya baadaye kupata mtoto. Wakati wa hedhi, mifuko ya tumbo la uzazi (mji wa mimba) hutumika kumwaga damu kwa njia ya uke. Kutokwa na damu kwa kawaida huchukua muda wa siku nne hadi saba (lakini inaweza kujichukua muda mrefu kidogo zaidi ya hapo ) na kwa kawaida hutokea kila mwezi. Wakati binti anapokuwa kwenye siku zake anapaswa kujisafisha mara kwa mara. Anaweza kutumia vitambaa safi kwa ajili ya kuzuia damu. Jinsi ya kuhesabu mizunguko tofauti Mzunguko wa siku kumi na sita Huu si mzunguko wa kawaida ila kuna wanawake ambao hua na aina hii ya mzunguko. Kama umemeanza kutoa damu leo tarehe 12 / 7/2016 chukua daftari na uandike alafu uhesabu kuanzia hapo mpaka utakapo fika tarehe kumi na sita na ujua siku ya kumi na sita itaangukia tarehe ngapi? utakuja kuona siku ya kumi na sita itakua  tarehe 27/7/2016 hivyo hedhi yako inafaa kuanza 28/7/2016. Hivyo utaanza kuhesabu kutoka tarehe 28/7/2016 mpaka kumi na sita na utakuja kungundua kuwa siku ya kumi na sita itakuwa ni tarehe 12/8/2016. hivyo inatakiwa uanze hedhi tarehe 13/8/2016. Kila mwezi unafaa kuendelea kuhesabu hivyo. Wanawake wanaopatwa na hedhi siku kumi na nane kurudi chini huwa wana matatizo hivyo wanatakiwa waende kumuona daktari kwani kitaalamu sio sahihi. Mzunguko wa siku ishirini na nane Kama umeanza hedhi tarehe kumi na mbili mwezi wa saba unafaa kuhesabu kuanzia siku hio. Ili kujua siku utakayo pata hedhi unaeza ongeza siku ishirini na nane. Hivyo basi utapatwa na hedhi tena tarehe nane mwezi wa nane. Ikifika siku ya nane yai huwa liko yatari na huanza kushuka. Kipindi hiki msichana hutokwa na ute mzito wa kunata ambao huwa ni dawa kwa ajili ya kulinda na kutengeneza mji wa mimba kuwa tayari kupokea mbegu za kiume kwa ajili ya urutubisho. Hivyo mbegu za mwanaume huweza kusafiri kwa urahisi zaidi katika maji maji haya. Mzunguko wa siku thelathini Kama umeanza hedhi tarehe kumi na mbili mwezi wa saba. Unafaa kuhesabu siku thelathini ili kujua utakayoipata tena. Ukifanya hivyo utaona kuwa siku utakayopata hedhi ni ya nane tarehe kumi na mbili nmwezi wanane lakini utaanza kuhesabu tena tarehe kumi na moja. Siku za hatari Ikiwa mwanmke anataka kutofunga mimba au youko katika hali ya kupanga uzazi anapawa kuwa mwangalifu kuhakikisha ya kwamba hashiriki ngono mara baaddha ya mwezi wake kuanza na pia pale mwhishoni. Nyakati hizo huwa hatari maana kuna uwezekano zaidi wa kuwa na mbegu za unzazi zilizoko tayari kwa kutunga mimba. Njia mwafaka ni kuwa na nukuu ya matukio katika mzunguko wa hedhi ili kubaini nyakati barabara. Watu wa mzunguko wa siku ishirini na nane wanafaa kuchukua ishirini na nane watoe kumi na nne hivi basi watapata kumi na nne kumaanisha kuwa siku yao ya hatari ni ya kumi na nne. Kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa ishirini na nne ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya kumi na nne ni hatari. Mwanamke wa mzunguko wa siku thelathini  anafaa kuondoa kumi na nne kutoka kwa thelathini ili apate kumi na sita. Hivi basi siku ya kumi na mbili, kumi na tatu , kumi na nne, kumi na tano, kumi na sita na kumi na sita ni hatari kwani anaweza kupata mimba haraka. Dalili kuwa uko katika siku hatari ni kuongezeka kwa joto , tumbo kuuma , na ute unaotoka sehemu za siri kuwa mzito kushinda siku za kawaida, ute hua huwa na rangi kwa mbali kama vile kutu, matiti ya upande wa kulia chini ya tumbo huuma kwa mbali. Kugeuka kwa mzunguko wa hedhi Wakati mwingine mzunguko wa hedhi hubadilika. Sababu  zinazofanya mzunguko wa hedhi wa mwanamke ubadilike ni kama zifuatazo: Kubadili njia ya Mpango wa uzaziUjauzito au kunyonyeshaMatatizo ya mazoezi mazitoOvari kuacha kufanya kazi mapemaMatatizo ya tezi ya thyroid – Uvimbe katika nyumba ya uzazi husababisha damu kutoka kwa wingi wakati wa hedhi na kutokwa damu katikati ya hedhi.Kubadili chakula unachokula au kupungua kwa mwili.

at 2:15 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top