Home → simulizi
→ HYUNG NIM
TRUE STORY
Aliniomba urafiki katika mtandao wa kijamii wa facebook ilikuwa ni wakati niko likizo ya mwisho kabla sijamaliza elimu yangu ya sekondari kidato cha sita katika shule ya wasichana ya Ruvu iliyoko mkoani Pwani.
Nilikubali ombi lake kama nilivyokuwa nikikubali maombi ya watu wengine nilijua ni moja kati ya marafiki wengi niliokuwa nao.
Alikuja sehemu ya ujumbe mfupi akanisalimia.
“mambo Jenny”
“poa” nilimjibu kiuchangamfu tu.
“mzima?”
“Mzima, sijui wewe” nilijibu.
“pande za wapi?” aliuliza
“nipo Kilwa, uwanja wa taifa” nilimjibu
“aaah, nipo Dar karibu”
“ahsante” nilijibu.
“Mishe zipi?” aliuliza.
“nasoma”
“unasoma wapi?”
“Ruvu, Pwani, HGE” nilimjibu kwa mkato.
Nilianza kutopendezwa na maswali yake mengi yasiyo na maana,
“anataka nini huyu?!” niliwaza.
“Sawa karibu Dar, mimi niko pale chuo kikuu cha Dar es salaam nasomea Accounting”
“Wooow! Hongera ni ndoto yangu pia.”
Hatimaye kati ya mambo yote ambayo ambayo alikua akiniongelesha hilo la kwanza alinifurahisha.
“Nilikuwa na ndoto ya kufika chuo kikuu cha Dar es salaam na kusomea mambo ya Accounting”
Kwa hilo nilimpenda.
“Naomba basi namba yako ya simu” alisema.
Nilipoisoma hiyo meseji nilikasirika,
“Fyuuu” nikasonya.
“Kumbe walewale tu” alikuwa ni moja wapo kati ya wanaume wengi ambao walikuwa hawaishi kuniomba namba ya simu katika mtandao wa Facebook.
Nikamwambia hivi karibuni nitarejea shuleni kwahiyo haitakuwa na maana.
“We nipe tu nikae nayo ukirudi shuleni nitakutafuta” aliongea kiunyonge.
Nikaamua tu kumpa kwani nilijua mpaka nitakaporudi shuleni angekuwa amekwisha ipoteza.
“Ahsante” alishukuru.
Na kisha akanitumia meseji kwenye namba yangu
“ni mimi Gibson”
nikamjibu kiufupi “poa”
Siku iliyofuata nilienda shuleni.
MIEZI MITANO BAAADAE.
Nilirejea shuleni baada ya kuhitimu elimu yangu ya sekondari, nilikaa nyumbani nikisubiria matokeo yangu ya kidato cha sita kwa ajili ya kujiunga na chuo.
Nilipofika mama yangu alinikabithi simu nzuri kabisa aina ya huawei. Nilifungua simu yangu na kisha nikajiunga na mtandao wa whatsapp.
Nilikuta namba nyingi za marafiki zangu, nikaanza kuchati nao. Mara ghafla iliingia meseji katika namba ambayo sikuijua.
“Hello Jenny mambo?” aliandika.
“Poa, nani mwenzangu?” niliuliza.
“Mara hii ushanisahau au namba yangu umefuta?” alinitumia text hiyo.
“Sikujui wewe ni nani naomba uniambie wewe ni nani” nilimjibu kwa dharau.
“Aaah bwana! Mimi Gib” aliniandikia.
“Gib! Mbona sikujui”
“Gibson, Gibson Jude”
“Aaah! Gibson niambie za siku” nilijibu kiunyonge wala sikupendezwa kuwa na mawasiliano nae.
“Poa tu, naona ukafuta namba yangu”
“Aanh, hamna sikufuta” nilimjibu.
“Sawa niambie” alionekana kuchukulia kawaida tu.
“Poa, hongera kwa kumaliza shule” aliniambia.
“Aaaah ahsante”
“mtihani ulikuaje?”
“Kawaida tu”
“kwahiyo utafaulu si ndio”
“yaah kufaulu lazima” nilijibu.
“hongera bwana, una ndoto za kwenda kusomea wapi?”
Sikutaka kumwambia nia yangu ya kwenda kusoma chuo kikuu cha Dar es salaam.
“nataka niende kusoma chuo kikuu cha Dodoma”
“kwanini umechagua chuo kikuu cha Dodoma”
“Nimepapenda tu Dodoma sitaki kuishi sehemu nyingine zaidi ya Dodoma” nilimwambia.
“Sawa kama unapendelea iwe hivyo”
Tuliendelea na urafiki wa karibu.
Hatimaye siku moja aliniambia kitu cha kunikera.
“Jenny nakupenda naomba uwe mpenzi wangu”
Nilishangaa huyu mkaka vipi hanijui hata hajawahi kuniona anaanza kuleta mambo yake ya ajabu ajabu. Kanikuta tu facebook
“fyuuu” nilisonya.
“Sorry nina boyfriend wangu” nilimwambia
“Jenny unaniumiza, nakupenda sana nimekusubiri kwa muda wote huo.”
“Am sorry nampenda sana Tony siwezi kumwacha nampenda sana na siwezi kumsaliti naomba tu tuwe marafiki” nilimwambia.
Alikubali kwa shingo upande.
Tuliendelea kuwasiliana kama marafiki wa kawaida.
Niliwaonyesha marafiki zangu Maria, Angel na Lily picha zake na hata dada yangu Jackline. Kila nilipowaonesha picha zake hawakutaka kuongea kitu chochote, nilijua wamempuuzia kwa sababu ni wakawaida sana hata mimi nikaanza kumchukulia wa kawaida. Hakuchoka kuendelea kuwasiliana na mimi mara kwa mara tuliendelea kuwasiliana.
Siku moja nilimuazima dada yangu simu yake.
“Dada naomba simu yako mara moja”
“unataka ya nini bwana?” aliniambia.
“Aaah we nipe tu mara moja”
“halafu simu yangu mbovu unajua whatsapp yangu haidownload picha wala audio yani haidownload kitu chochote vile naomba nitengenezee.”
Dada yangu hakuwa mtundu kama nilivyokuwa mimi, niliweza kuchezea simu na kuzitengeneza.
Hivyo alinikabidhi simu yake nimtengenezee.
Nilipofungua upande wa jumbe fupi nilikuta namba niliyoifahamu ilikuwa ni ya Gibson.
“Gibson anawasiliana na dada yangu!” nilishangaa
“amemjuaje?” nilibaki najiuliza.
“aaah! Kumbe ndiyo tabia yake huyu Gibson kaniomba mimi namba Facebook akamwomba namba na dada yangu na usikute anatutaka wote.”
“fyuuu” nilisonya,
“pumbavu na kuanzia saa hizi sitawasiliana na yeye tena” nilisema.
Mara kwa mara Gibsona alijaribu kunipigia simu sikupokea alituma jumbe zake nilisoma na kisha kuzifuta.
“Kaa mbali na mimi Gibson” niliwaza.
Muda mrefu ulipita bila kuwasiliana na Gibson.
Siku moja nilipokea ujume katika namba nisiyoifahamu
”mambo”
“poa” nilijibu.
“nani?” niliuliza.
“Gib”
“Gibson!” nilishaanza kumsahahu.
“Gib ndiyo nani?” niliuliza kwa ukali.
“aaah Gibson, umenisahau Gibson Jude.”
“aaah Gibson Oooh sory” nilisema ingawa sikuwa namaanisha wala sikutaka kumwomba msamaha sikutaka kuwasiliana naye kabisa.
“Usijali vipi?”
“poa”
“Tokeo limeshatoka umepata ngapi?” aliniuliza.
Sikupenda “nimepata One”
“Aaah Hongera, hongera sana”
“One ya ngapi?”
“Nimepata One ya tisa”
“Aaaah! hongera sana aisee kumbe una akili” nilicheka tu.
“Aaah! Jenny bado una mpango wa kwenda kusoma chuo Dodoma?” aliniambia.
Katika maisha yangu hakuna kitu ambacho siwezi kama kumdanganya mtu, nilishindwa kumdanganya.
“hapana sitaki kwenda kusoma chuo cha vilaza?”
Akacheka.
“chuo kikuu cha Dodoma siyo chuo cha vilaza Bwana”
“Just joke” nilimwambia.
“Kwahiyo unataka kwenda chuo gani?”
“Nataka kusoma chuo chochote kilichopo Dar es salaam sitaki kutoka nje ya Dar”
“Wooow! Karibu sana chuo kikuu cha Dar es salaam”
“Ahsante ila sijui kozi za kuchagua”
“Usijali”
“Mimi sifahamu kozi nyingi sana lakini nitakuunganisha na dada yangu atakusaidia kuchagua kozi.”
“Wooow! nitafurahi sana Gibson” nilimwambia.
Hakika alikuwa mtu mzuri sana Gibson nilipenda ukarimu wake.
Nilikaa nikisubiria anitumie namba ya simu ya dada yake lakini ghafla nilitumiwa ujumbe mfupi wa maandishi.
“Mambo Jenny, mimi naitwa Grace ni dada yake na Gibson ameniambia nije nikupe maelekezo kuhusu kozi za kuchagua katika chuo kikuu cha Dar es salaam.”
Nilifurahi sana.
“yaah ahsante.”
Aliniorodheshea kozi akinipa na maelezo ya kozi nzuri za kuchagua, nilifurahi sana hakika alinisaidia sana kuchagua kozi nzuri. Niliweza kuchagua kozi na kumaliza maombi ya vyuo vikuu.
“Karibu sana chuo kikuu cha Dar es salaam” aliniambia
“Aaah tuombe Mungu tu nichaguliwe hapo.”
Siku zilienda na marafiki zake waliweza kunifahamu, alinitambulisha kwa marafiki zake watatu Wilson, Jose na Albert. Walikuwa wakinipenda sana hao marafiki zake ingawa hatukuwahi kukutana nao hata siku moja.
Tuliwasiliana katika mitandao mbalimbali, mara nyingi tulipigiana kwa video Call na tulitumia muda mwingi sana kuongea nao.
Familia yangu zima walijikuta wakimfahamu kwa maana kila mara wakinikuta naongea na simu kwa video Call nilikuwa naongea na yeye.
Mama aliniuliza siku moja “huyu mtu ni nani?”
“Ni rafiki yangu mama anaitwa Gibson”
Mama alicheka “ni rafiki yako kweli?” mama aliuliza.
“Ndiyo mama ni rafiki yangu”
“Sawa kama ni rafiki yako.”
Mama alitilia shaka urafiki wetu,
Nilicheka tu.
Nilichaguliwa chuo kikuu cha Dar es salaam katika kozi ile ile ambayo niliitaka Accounting.
Mama yangu alifurahi sana na familia yetu nzima kwa ujumla,
“hatimaye ndoto zako zinatimia mwanangu” mama aliniambia.
“Lakini utaendaje Dar na siyo mwenyeji wa kule itabidi nikupeleke” mama aliniambia.
“Aahah hapana mama kwa bahati nzuri tumechaguliwa na marafiki zangu chuo kimoja Maria, Angel na Lily wote tunaenda chuo kimoja kwahiyo tutaondoka wote”
“aaah, mkiwa nyie wanne wala hata sipatwi na hofu” mama alisema.
“Mtafikia wapi mwanangu”
“Lily amesema tutafikia kwa mama yake mkubwa wote ametuombea”
Kwa kuwa familia zetu zilikuwa marafiki haikutia shaka.
Mama akanikabidhi kwa rafiki yangu kipenzi Lily na kisha tukaondoka kuelekea chuoni.
Gibson alikuwa ubungo akitusubiria nilifurahi sana kumwona Gibson. Tofauti na alivyokuwa akionekana kwenye picha alikuwa ni mzuri zaidi ya picha zake, hakika Gibson alikuwa ni Handsome. Alikuwa ni mrefu hakuwa mnene wala mwembamba alikuwa na sura nzuri ya kuvutia.
Ngozi yake laini macho mazuri na zaidi ya yote alikuwa na vishimo katika mashavu, alikuwa na dimples.
Nilifurahi sana kumwona nilimkumbatia kwa nguvu.
“Karibu sana Dar” aliongea kwa sauti yake tamu.
Nilihisi kusisimkwa kwa mwili kuwa karibu naye.
Alinipeleka chuoni pamoja na marafiki zangu akatuonesha baadhi ya maeneo ya chuo huku akitusaidia kufanya mambo mbalimbali yaliyokuwa yakihusiana na usajili nilifurahi sana kuwa karibu yake, siwezi kuielezea furaha niliyokuwa nikihisi.
“Gibson you are going to be my man” nilisema.
Nilipangiwa kukaa hostel za chuoni katika ukumbi namba tatu jengo B chumba namba 718.
Kwa Gibson alikuwa mwaka wa pili yeye hakupangiwa chumba hivyo alifanikiwa kununua katika ukumbi namba 3 jengo D chumba namba 1115.
Rafiki yake Jose alikuwa akiishi ukumbi namba 1wilson na albert walikuwa wakikaa ukumbi namba tatu Block A chumba namba 115.
Nilifurahi sana aliponitambulisha kwa marafiki zake niliweza kukutana nao walionesha upendo mkubwa kwangu. Nilikuwa ni kana kwamba wananisubiria kwa hamu na walikuwa wamefurahi sana kukutana na mimi. Nilijisihisi wa upekee na wa tofauti sana alinionesha mazingira ya chuo alinifundisha vitu vingi.
Moyo wangu ulikuwa na uhakika kwamba nilikuwa nikimpenda Gibson kila mara nilihisi moyo ukienda mbio na mapigo ya moyo yakiongezeka nilipokuwa karibu naye.
Kila nilipomtazama nilihisi akili ikipaa.
Nilijiona kama malkia kuwa karibu naye.
“Your mine” kila mara nilikuwa nikiwaza.
Siku moja Jose aliniuliza
“Jenny Gibson ana wivu sana juu yako” nilicheka
“hasa anionee wivu mimi kama nani?”
“Si mpenzi wake” alisema.
“Hamna mimi siyo mpenzi wake mimi ni rafiki yake” nilisema.
Ni kitu ambacho nakijutia siku zote za maisha yangu.
“Acha utani kila mtu anajua wewe ni mpenzi wake, hasa huo urafiki umetoka wapi?”
“hahaha….” nilicheka
“kama mimi ni mpenzi wake muite mwambie aje anitambulishe”.
Niliongea kwa pozi.
“aaah kwahiyo unataka kuniambia kwamba hamko katika mahusiano si ndio.”
“yaah” nilijibu.
“sawa kama umeamua kunidanganya”
“hamna siwezi kukudanganya sina sababu ya kukudanganya Jose” nilimwambia.
“Poa basi kama vipi”
“Sawa”.
Wilson na Albert waliniuliza pia.
“Wanataka nini hawa” niliwaza,
“potelea mbali” nikawapotezea.
Mara zote nilipokutana faragha na Gib nilimpenda na kumpenda alikuwa so romantic alinipa wakati mzuri sana wa kuwa pamoja naye.
Sikumtamani tena wala kuwa na mpenzi wangu Tonny niliazimia kumwacha Tonny ili kuendelea kuwa na Gibson ingawa iliniwia vigumu sana kumwambia Tonny.
Mara nyingi Gibson alikuwa akiniuliza huyu ni nani kila alipoona picha ya Tonny, ni rafiki yangu nilimwambia alicheka tu.
“Hasa kucheka kwake inamaanisha kanielewa au kanidharau” niliwaza,
“aaah shauri yake.”
Nilijuwa Gibson amevutiwa na mimi kwa kila hali na nilijua Gibson ananipenda sana ingawa sikutaka kuonesha watu kuwa nampenda sana Gibson ukizingatia tayari walikuwa wanamfahamu Tonny hata wao pia walimpenda Tonny isingekuwa rahisi kwao kukubaliana na mahusiano yangu mapya niliyotaka kuyaanzisha kati yangu na Gibson.
Lily aliniita “Jenny” siku moja
“unajua kuwa Gibson anakupenda sana” nilicheka,
“muache anipende.” Niliongea.
“anakupenda sana.”
“Shauri yake”
“Sawa.”
Aliamua kuishia hapo.
Ni kama kuna vitu alitaka kuniambia lakini aliamua kusitisha kutokana na jinsi nilivyomjibu.
Gibson alianza kunibadilikia.
Hanipigii tena simu kama ilivyokuwa mwanzo, hanitumii meseji hadi nimuanze, wakati mwingine nikimpigia simu ananifokea.
“Gibson kwanini umekuwa hivi?”
“nimekuwaje?”
“Nimebadilika nimekuwa wa kijani? Eee?.”
“Mbona umekuwa too harsh to me jamani” niliongea kwa sauti ya kubembeleza.
“Aaah, niko kawaida halafu nina mambo mengi usiniletee drama zako za ajabu ajabu”
“Gibson kwanini umekuwa hivi” niliwaza.
“Whats wrong?” nilijiuliza maswali bila majibu.
Kadri siku zilivyozidi kuendelea ndivyo Gibson alivyozidi kubadilika nilikosa amani kabisa nilihisi kupungua uzito.
“Gibson mimi nakupenda kwa nini unanifanyia hivi” niliwaza kwa nafsi yangu.
Hakika Gibson alikuwa amenichanganya kabisa.
Nilishindwa kujiongoza mimi mwenyewe.
Lily aliniita.
“Jenny una nini?”
“Lily nampenda sana Gibson lakini nashangaa kwanini siku hizi anakuwa hivi kwanini ananifokea haoneshi tena kunipenda.”
“Jenny, Gibson anakupenda” lily aliniambia.
“hapana siyo kweli Gibson hanipendi kama angekuwa ananipenda asingekuwa ananifanyia hivi.”
“Jenny Gibson alishawahi kukwambia kwamba anakupenda” aliniuliza.
Lilikuwa ni swali la ghafla sikutengemea.
“Ndiyo alishawahi kuniambia”
“Ulimwambiaje?”
“Nilimwambia tu tuwe marafiki”
“Hamna mtu ambaye anayeweza kuvumilia hivo, Jenny yani anakupenda halafu umwambie kwamba mtakuwa marafiki, hapana hamna mtu anayeweza kuvumilia.
Na hiki ndiko kilichotokea kwa Gibson amejitahidi sana kufanya urafiki na wewe lakini yeye anaumia moyoni kwa sababu anakupenda anachokifanya ni kuwa mkali kwa sababu anajua hawezi tena kuwa na wewe kwahiyo anataka kuwa mbali na wewe.”
“Jamani!!” nilishituka sana kwa taarifa hiyo.
“Mungu wangu nifanye nini sasa?” nilijiuliza.
“Mimi naenda kumwambia”
Nilimwita ingawa mara kwa mara alikuwa kila nikimwita alikataa kuja siku hiyo alikuja.
Tulikaa sehemu tulivu tukiongea.
“eeeh niambie” aliongea
Mara nyingi tunapokuwa sehemu kama hizo huwa hawi mkali kwangu ananionesha mapenzi yote.
“Nakusikia bibie”
“Gibson nakupenda” nilimwambia.
“Nakupenda pia” alijibu.
Nilifurahi sana moyoni mwangu kusikia hivyo nilijua hayo yote yameisha.
“nakupenda sana Jenny” aliniambia huku akinivutia kwake alinikumbatia na kisha ndimi zetu zikakutana. Ilikuwa ni busu zito na refu ambalo liliniacha na faraja kubwa ndani ya moyo wangu.
“sasa wewe ni wangu.”
Tuliendelea kubaki hivyo kwa muda mrefu hadi usiku mwingi ulipoingia.
“Ni mda wa kurudi sasa” aliniambia.
“Sawa”
Nilikuwa na furaha sana wala sikutaka kumficha.
Alinisindikiza hadi karibu na kwangu.
Akanivuta akanikumbatia na kisha akanibusu kwenye paji la uso
“uwe na usiku mwema” aliniambia.
Hakika nilifurahi sana.
Niliondoka na kurudi chumbani kwangu nikiwa na furaha, Lily aligundua kwamba nina furaha sana.
“Jenny mbona umefurahi hivyo”
“amna kawaida tu” nilimjibu huku nikichekacheka kwa aibu.
“sawa bwana kama siku hizi tunafichana”
Ni kweli hatukuwa na tabia ya kufichana lakini sikuona umuhimu wa kumwambia.
Mara nyingi Lily hakuonesha kuvutiwa na Gibson ni kitu ambacho nilikuwa sikipendi sana,
“kwanini anamchukia Gibson wangu? Hata afanyeje hawezi kunifanya niache kumpenda Gibson nampenda sana” niliwaza.
Asubuhi ya siku iliyofuata niliamka mapema sana na kumpigia simu Gibson ili kumtakia siku njema, nilipiga simu haikupokelewa.
“Au hajaamka.” niliwaza
“au ameenda kuoga?” nilijiuliza maswali yasiyo na majibu
“ngoja nijaribu tena asipopokea nitampigia baadaye.”
“Haloo” ilikuwa ni sauti kavu na ya ukali.
Nilitetemeka.
“Mambo” niliongea kwa sauti ya upole.
“Poa ongea shida yako”
“Enhee! Gibson una nini?”
“Sina kitu ongea haraka.”
Nilibaki kimya nilishindwa kujua nini cha kuongea.
“ana nini huyu?! inamaanisha yale yote tuliyofanya jana hayana maana yoyote, kwanini tena awe hivyo”
“kama huongei nakata simu”
“noo Gibson subiri” nilikuwa nimeshachelewa simu ilikuwa imeshakatwa.
Nilibaki tu na maumivu moyoni mwangu.
Nilishindwa kuingia darasani siku hiyo.
Lily aliniuliza
“una nini?”
“Naumwa” nilimwambia.
“Twende hospitali”
“Hapana siendi” nilinyong’onyea sana.
Ilipofika jioni hali yangu haikuwa nzuri mara nyingi nilikuwa nikisumbuliwa na vidonda vya tumbo. Nilipelekwa hospitali nikalazwa.
“Jenny una nini wewe?” Lily aliniuliza.
“sina kitu kuumwa ni kawaida tu” nilimwambia.
“daktari aliniambia kwamba kutokana na kwamba una vidonda vya tumbo hupaswi kuwa na mawazo”.
“Kwanini una mawazo?”
“Jenny hujui tuko shuleni hapa eee?”
“Hapana Lily ni hali ya kawaida tu shukuru Mungu naendelea vizuri”
“aaah” nilivuta pumzi.
“Gibson hajaja kuniona?” niliuliza
“hajaja”
“ulimpa taarifa kwamba naumwa”
“ndiyo nilimpa taarifa kabla hutujakufikisha hapa”
“alijibu?”
“Alisema tu mpe pole.”
Niliangalia chini kwa huzuni.
“saa hizi hajapiga simu kuulizia hali yangu”
“hajapiga”
“ok sawa”
Moyoni mwangu niliumia sana.
“kwanini Gibson unanitreat hivi? Nimekufanyia nini lakini au kwa sababu umejua nakupenda”
Nilikaa hospitalini takribani wiki nzima na kisha nikaruhusiwa kurudi hostel.
Gibson hakuja kuniona hata baada ya kupewa taarifa kuwa nimerudi niliamua kunyamaza kimya na mimi, siku ya tatu yake nilishindwa nilimtumia ujumbe
“Mambo”
“poa unaendeleaje”
“vizuri” alinijibu.
“naumwa hata kuja kuniona Gibson kwanini unakuwa hivyo?”
“nilikuwa sijui kuwa umeruhusiwa, halafu nina mambo mengi sana yamenibana”
wala hakuhisi kuwa amefanya kosa aliona ni kitu cha kawaida tu. Niliamua kuyaacha yapite.
“Sawa tu.”
“Kuna siku utajua thamani yangu” nilimwambia.
Mara kwa mara nilikuwa nikimsisitizia nakupenda alijibu tu nakupenda pia.
Rafiki zake walikuwa wakinipenda sana hasa Jose.
Siku moja Jose aliniita chumbani kwake nilienda nilipofika nilimkuta Gib.
Nilikaa kitandani.
Jose aliniambia “Jenny natoka mara moja narudi sasa hivi”
Nilijua alitaka kutupa muda wa kuwa pamoja na kuongea mawili matatu.
Gibson akasema
“tunaondoka wote.”
Jose akamwambia
“si ubaki na Jenny”
“twende bwana si atabaki mwenyewe” wakaondoka.
Nikabaki tu mwenyewe nimekaa.
Pembeni yangu ilikuwepo simu ya Gibson kwa sababu alinifundisha jinsi ya kuifungua niliichukua na kuifungua nikaanza kuangalia picha sikuamini nilipokuta picha yake na msichana fulani hivi mzuri sana.
Niliumia sana kugundua kwamba Gibson ana msichana mwingine.
Nikaamua kufuatilia ili nijue huyo msichana ni nani, nilikuja kujua kwamba anaitwa Elizabeth na walianza mahusiano yao muda mrefu.
Kumbe wakati wote ulikuwa ukinilaghai tu.
“Potelea mbali”
Nilirudi chumbani kwangu nikiwa mnyonge sana
“Gibson kwanini umeniumiza?”
Nilifika chumbani kwangu Lily aligundua kwamba nimebadilika.
“una nini Jenny?”
“Nothing, naomba tu nilale” alinipisha nikalala.
Ni kweli nilikuwa natembea na maumivu makubwa sana sikuwahi kuhisi kama kuna siku ningekuja kugundua ukweli wenye kuumiza kama huo.
“Gibson ana msichana mwingine! Na ndiyo maana siku hizi amekuwa mkali kwangu.”
Nilitamani sana kuwa na mahusiano na Gibson lakini nilikuwa nimechelewa.
Marafiki zake hawakuacha kunisumbua, hasa jose.
“Utamng’ang’aniaje Gibson wakati unajua kuwa ana mpenzi wake?”
“niache nampenda hivyohivyo” niliwambia.
Jose, Wilson na Albert wote walikuwa wakinitaka lakini kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana Gibson sikutaka kuwa nao.
“Aaah sina jinsi wacha nikubali tu, nitamwomba niwe mwanamke wake wa pembeni.”
Ilikuwa tofauti na matarajio yangu Gibson hakuwa na hisia tena juu yangu.
Niliumia sana katika ukweli huo.
“Sawa kama ameamua kufanya hivi mimi siwezi kumlazimisha acha afanye anachokitaka” nilisema.
Katika urafiki wetu nilikuwa karibu sana na Angel wakati Lily alikuwa karibu sana na Maria tulikuwa tunapenda sana kuchati kwenye kikundi cha whatsapp na zaidi ya hapo kila mtu alikuwa anachati na mtu yoyote binafsi, nilikuja kugundua jumbe zisizofaa kati ya Lily na Maria.
Moyo uliniuma siwezi kuelezea.
“Maria ana mahusiano na Gibson!! Lily anajua. Na wakati wote walikuwa wakinitia moyo na amekuwa akinishauri kwamba Gibson siyo mtu mzuri.”
Najua kuwa Lily anampenda sana Maria kuliko mimi lakini sikutengemea angeruhusu kitendo cha kinyama kama hichi kifanyike kwangu.
Nililia sana.
Lakini yote nimeyataka mwenyewe.
Najuta sana kitu ambacho nimekifanya kwasababu ni kweli sana nilimpenda Gibson lakini nilijiona kwamba mimi ni wa thamani sana kuliko hisia zilizokuwa ndani ya moyo wangu, najua nimempoteza Gibson milele hawezi kuwa wangu tena.
!
Ni mtu ambaye nilikuwa nampenda sana.
Lakini kwa sababu ya dharau nilizokuwa nazo, kwasababu ya jinsi ambavyo nilikuwa nikijichukulia.
Nilijiona mimi ni wa thamani sana.
Lakini sasa hivi nalia na maumivu yangu.
HYUNG NIM
(nimekupa jina hili kwa kuwa wewe ni nyota yangu kipenzi kwa kuwa siwezi kukushika ila naweza kukuona tokea mbali popote niwapo sitaacha kukutazama)
Mwanaume niliyekupenda uende kwa amani.
*🅱 professional love*
>>>>>>>>>>>>>>>> MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: