Home → simulizi
→ HOT POINT.
SEHEMU YA 1.
Haikuwa mara yangu ya kwanza kuambiwa napendwa, lakini upendo wa mwanamke huyu niliyemuheshimu kama rafiki tu wa karibu ulininyima amani.
Niliona hata aibu kumtazama, si kwamba alikuwa mbaya la hasha, bali ni muonekano wake wa kuvutia ndio ulionifanya nione aibu kumtazama, sikufikiri kama naweza kuwa karibu naye na kuzoena naye kiasi hicho, labda kutokana na kazi yangu ya ususi na upakaji rangi kucha.
Shughuli yangu niliridhika nayo kwakuwa ilikuaa inaniingizia kipato, japo ni kidogo lakini kilinitosha sikuwa na tamaa, kazi yangu ilinifanya kufahamiana na wasichana wengi wa kila aina, ila sikutaka kuvunja maadili ya kazi yangu niliyojiwekea.
Nilipenda sana kuzunguka maeneo ya vyuoni hapa jijini hasa chuo cha UDSM na IFM, huko nilikuwa na wateja wengi maana ndipo warembo wengi wamjini wanapopatikana. Hivyo haikunipa shida katika soko langu.
Ila leo ni huyu msichana, Melisa ananinyima raha kabisa, nahisi mapigo yangu ya moyo yamebadili uelekeo wake, yanaenda kasi sana.
Ilikuwa ni siku ya Tamasha kubwa chuo kikuu cha Dar, kila mwanamke alitaka kumzidi mwenzie kwa urembo, kutokana na umahiri wangu wa upambaji na usukaji, nilijikuta kuwa na foleni kubwa waliniomba niwasuke na kuwapa rangi kucha, kabla ya siku hiyo kuwadia,
Kila mmoja alisisitiza hilo, kwangu ilikuwa neema maana mfuko niliamini utajaa, hakika usilo lijua ni sawa na usiku wa giza nikiwa gheto natafakari nkupanga hesabu zangu mida ile ya jioni, ghafla nilisikia honi ya gari nje, mara ya kwanza nilipuuzia nikijua yatakuwa ni nje ya barabara,ninapokaa ni ubungo maji, hivyo vurugu ni kawaida.
Ila zilipozidi sikuwa na budi kutoka, aaaahhhh sikuamini nilichokiona, ulikuwa ni mguu mmoja wa shampeni uliovaa kiatu chenye kamba ndefu alizozufunga mpaka magotini, sikuweza kumuona sura kwa haraka, maana mlango wake wa gari aliufungua nusu kisha kushusha mguu nje.
Nikiwa nimeduaa kutafakari, niliona ishara ya mkono ukiniita, nilijivisha vazi la kujiamini, bila woga wa dhahiri nilisogea, harufu ya marashi niliyoyasikia, thamani yake ni mtaji wa biashara yangu, yalikuwa ghari mno.
Hatimaye macho yangu yalimuona msichana niliyehisi atakuwa mzuri, kutokana uzuri wa mguu wake,
"hi am Melisa"
Kwa pozi alinyoosha mkono kunisalimia, alizungumza lugha tamu, japo biashara ninayoifanya wengi huzani niko nyuma kwenye utambuzi wa mambo, hasa ujuzi wa kiingereza, lakini kwangu nakimudu vyema mno, hasa ninapokutana na watoto wakali na mabrother men wenye mashauzi.
"am Chuba, nice to meet you Melisa, you are welcome"
"wooh, i cant believe this, amazing its real you?"
"yeah its me, whats happen?"
"for sure, sikudhani kama unaweza kuzungumza kiingereza kiasi hiki tena kwa kujiamini"
"so ulivyoanza kunisalimia kiingereza ulitaka kunihadhiri?"
"Ooh comeiin, am sorry i dont mean dat, by the way, hapa kwako nimeelekezwa, nashida nahitaji ukanisuke nyumbani,
Alizungumza kwa pozi huku akilizungusha jicho lake, na kutupia kifuani kwangu, mwanzo sikugundua hilo, ila nilipoona umakini umemtoka nilijitazama anatazama nini,
"ooh sorry, ndani kuna joto ndio maana nikavua shati"
"ooh worry out, so tunaondoka au?"
"Aah Melisa nahis kutingwa sana, maana foleni ni kubwa ya wanaotaka kusuka, nitakuwa pale kijiweni, kesho kwaajili ya kuwasuka, mida hii kuna mtu naahadi naye kwaajili ya rangi ya kucha"
"Please dont do that to me, pleasee, i will pay you double"
Dah sauti ya Melisa inaweza kukufanya uhonge hata mtaji, anajua kuitumia na kulaghai, kama mwanaume rijali huwezi kutoka, nilibaki nikisema kwa sauti ya chini,
"sawa, hakuna neno, we shall go, ngoja nikachukue vifaa, ila dah, muda umeenda now, si unajua na foleni za kwenye daladala zetu huku. Hasa nyakati kama hizi"
"worry out, kajiandae nakusubiri"
Sikutaka kupoteza muda hasa kwenye swala la pesa, nilijikusanya na vifaa vyangu, nikamkuta Melisa yuko ndani ya gari akinisubiri, nlitaka kukaa siti za nyuma lakini aliomba nikae mbele, sikuwa na hiyana, bila kuchelewa safari ikawa imeanza kuelekea nisipo pajua.
Nilibaki nikishangaa tu jinsi Melisa alivyokuwa akizungusha usukani na kuingiza gia, tukiwa tumeikamata baba ya kuelekea mabibo, nilijikuta nimekuwa bubu nikimtazama mpaka alipo nisemesha,
"Hey men, why you are so cool"
"ooh nothing to say"
Jibu langu lilimfanya Melisa atabasamu tu, sikujua kilichokuwa kinamfanya atabasamu lakini nilihisi huenda bado hakuamini kama naweza kubwabwaja kimomdo, japo sina kitu lakini huwa sipendi kijiweka nyuma.
Yote hayo yakiendelea ghafla nilisikia honi, pipiii, nilishtuka, nikagundua kwamba tumeshafika tayari, mbele yangu nilikuwa naona geti kubwa jeusi, na nyumba yenye paa rangi ya kijani, mazingira ya nje tu yalionesha mjengo wa ndani sio wa kitoto, kidogo niliingiwa na hofu, na sikujua Melisa alijiamini nini mpaka kunipeleka kwao mida ile mibovu, jua likiwa linaelekea kutua.
"You are.welcome, feel at home"
Alinikaribisha huku akiwa amefungua mlango wa kuingia sebleni baada ya mlinzi kufungua geti na kuingia ndani,
"Thank you"
Nilijikuta mgeni wa mazingira nilipokaribishwa kwenye makochi, kisha melisa kuikamata korido, sikujua alipo elekea, punde alirejea akiwa amevaa Taulo jeupe, alililojifunga mpaka kwenye matiti yake, huku sehemu kubwa ya mapaja yake yakiwa nje, nilijikuta namsahili mpaka miguuni, alikuwa amevaa kikuu mguu wa kushoto,
Mkononi alishika chupa moja ya wine, na grass mbili,
"sorry kwa kukuacha mwenyewe kwa dakika kadhaa, karibu kinywaji"
"asante"
"can you wait for me? Naenda kuoga mara moja, újue nilitoka chuo ndio nikakupitia. Na bongo yetu si unajua tena"
"aah sawa sawa"
Melisa alizidi alizidi kubadilisha akili yangu kwa muda mfupi, hasa alipoinama wakati ananimiminia kinywaji, nilishindwa hata kumsemesha kwamba asiweke kinywaji maana mimi sio mnywaji wa vilevi.
Tulijikuta tukitazama kwa sekunde, pumzi aliyokuwa akiitoa, ilifika barbara kwenye moyo wangu,.
Ghafla Melisa alijikuta akiniangukia pale kwenye kochi nilipokuwa nimekaa, alishtushwa na mdudu aliyemtekenya kwenye unyayo.
Kifua chake kilikuwa juu ya Kifua changu kwa wakati huo, mikono yake juu ya mabega yangu,
Nilihisi msisimko wa ajabu, kana kwamba sikuwahi kukumbatiwa, taratibu nijikuta napeleka mikono yangu kwenye mgongo wake, pua zetu zikagusana, midomo ikashikana, nilisikia sauti yake sikioni mwangu,
"ashiiiii you kill meee!!!!!!" ITAENDELEA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: