SIMULIZI YA KUSISIMUA... Ndoa Yangu Inanitesa part 3 Kesho yake ilikuwa siku ya mimi kupimwa afya ikiwemo na kupimwa virusi vya Ukimwi, sikuwa na wasiwasi nilisubiri waje kunipima kwani nilijiamini sikuwa na virusi, japo nilifanya mapenzi na Jennifer kule Thailand bila kutumia kinga yoyote.Na hata mapenzi niliyofanya yenyewe yalimfurahisha na kumridhisha Jennifer na kukiri mimi ni miongoni mwa wanaume wanaojua mapenzi. Sikupenda Jennifer anidharau kwa upande wa kutomridhisha kimapenzi. Waliingia Daktari waliovaa magwanda meupe wakiwa na vipimo vyao. Waliongozana moja kwa moja ofisini kwangu, cha ajabu baada ya kusalimiana nao walitaka nivue nguo nibaki na kaptula, jambo hilo nilipinga. “Kama kunipima damu ninatolewa damu kwenye mkono sio karibu na uume wangu. Nyie ni daktari kweli?” “Ndio sisi ni daktari unataka vitambulisho?”. “Sina shida na vitambulisho vyenu. Nyie chukueni damu mkaipime, mkileta majibu mabaya nitarudia hospitali nyingine niliwaeleza waziwazi bila kuwaficha kitu.”Nikiwa nimeketi kitini,wao walikuwa wamesimama. Haraka haraka daktari mmoja alitoa sindano iliyokuwa na kitu kama maji, sijui ilikuwa sumu au ilikuwa nini!. Maji hiyo ilikuwa ndani ya bomba la sindano. Kama cc 200. Sikuweza kuona nilikuwa nimegeuka kwa upande mwingine ili nisione sindano inavyopenya na kuingia kwenye nyama za mwili wangu. Kwa kifupi nilikuwa muoga wa sindano japo nilikuwa mtu mzima. Wakati sindano ipo kwenye mshipa wa damu nilisikia kitu kama maji yenye uchungu wa dawa, nilipata maumivu makali nilipogeuka ndipo niliona akigandamiza bomba la sindano kwa haraka ili nisione kitu, lakini niliona kitu kilichoingizwa kwenye mshipa wa damu. Nilishindwa kujua kilikuwa ni kitu cha kuniletea matatizo ama kunijenga ndani ya mwili wangu. “Dakitari wewe unanipiga sindano au umekuja kunitoa damu ili upime Virusi vya Ukimwi?. Iweje unipige sindano?”. Nilimuuliza daktari kwa hasira baada ya kusikia ile sindano mwili mzima, nilihisi kizunguzungu mwili ukakosa nguvu. Tofauti na kabla ya kuingiza sindano yao, halafu walikuwa bado hawajatoa damu. “Usijali Sweedy sijakupiga sindano, nataka kutoa damu” alisema huku akivuta damu kwenye bomba la sindano. Na muda mfupi waliniaga, alionekana nesi mmoja kati ya wale waliokuja kunitoa damu mwenye majonzi. Alinitazama kama mtu aliyenionea huruma sana, machozi yalimlenga lenga lakini hakutaka niyaone aligeuka upande wa pili na kujifuta na kitambaa alichokuwa nacho mkononi. Nahisi alikuwa anajua kila kitu kilichotendeka kwa muda ule na sura yake ilikuwa sio ngeni machoni mwangu, lakini nilishindwa kumkumbuka vizuri. Alijua mipango yangu yote hasa ile ya kufunga pingu za maisha. Alijaribu kuwa wa mwisho kuniaga. Nilisikia akiniambia “Pole sana Sweedy, moyo unaniuma Mungu akubariki maishani. Nenda kanywe maziwa mengi yatakusaidia”. Nesi huyo aliondoka taratibu, huku akigeuka nyuma na kunitazama kwa macho ya huruma. Nilishindwa kumjibu, nilibaki nikiyaganga maumivu ya sindano niliyochomwa mara ya kwanza, ambayo sikuweza kuielewa ilikuwa ya nini mwilini mwangu. Robo saa baada ya wale daktari kuondoka mkono niliopigwa sindano na kutolewa damu nilihisi unakufa ganzi, kila nilipotafakari yale maneno ya yule nesi na kilio chake nilishindwa kumuelewa zaidi ya kujilaumu kwa nini nimekubali kupimwa pengine wamenipiga sindano yenye sumu ambayo itanidhuru. Kwa upande mwingine sikuamini niliona yule nesi alinipenda bure, na Mzee Jophu asingeweza kuwatuma watu wanipige sindano yenye sumu . Nilimuamini sana tajiri yangu. **************** Wiki tatu zilitimia na siku ile ya harusi iliwadia. Kila mtu aliisubiri kwa hamu sana siku hiyo hasa wazazi wangu kwani walijisikia furaha kwa mtoto wao wa kiume pekee kufunga pingu za maisha. Nadhani moyoni mwao walijisemea, sasa ule wakati wa kuwaona wajukuu toka kwa mtoto wetu Sweedy umewadia. Mzee Jophu ndiye alikuwa mtu wa kwanza kwa watu walionichangia mchango mkubwa katika kuifanikisha harusi yangu. Sherehe ilipendeza sana, watu walikula na kunywa hadi wakasaza. Namshukuru Mungu sikupata lawama yoyote ya kuhusu sherehe yangu. Getruda ambaye ndiye ubavu wangu sasa aligubikwa na furaha isiyo kifani. Sherehe iliyopendeza kwa shamrashamra na vifijo, DJ alitumbuiza kwa muziki wa taratibu wa wapendanao hasa kibao kilichopigwa na mwanamuziki Bob rudala nadhani msomaji unaupatapata ule wimbo vilivyo . Utajisikia vipi ukipigwa siku ya harusi yako? “NIMEKUCHAGUA WEWE” nakumbuka baadhi ya maneno yake, “Nimekuchagua wewe uwe wangu, wangu wa maisha wa kufa na kuzikana”msomaji sitaki nikumalizie uhondo tafuta wako na wewe awe wa maisha ili ujiepushe na mengi hasa janga la Ukimwi. MC au Msema chochote watu wa mjini wanavyoita alikuwa anaitwa MR.Kicheche ni kicheche kweli si mchezo ukumbi haukuruhusiwa kukaa kimya siku hiyo watu wote walikuwa wakicheka na kutabasamu kwa wale wasio na bandama. Kwa ufupi sherehe ilipendaza mno, hatukuwa matajiri lakini watu wailiridhika na kila idara ya sherehe. Sherehe ilipoisha, tulichukuliwa na gari maalumu siku hiyo kwa bwana na bibi harusi na tukaelekea kwenye hotel moja iliyoitwa NGORONGORO HOTEL kujipumzisha. Tulipofika tulikwisha andaliwa kila kitu, chumba kilinukia harufu nzuri za manukato, choo na bafu ndani kwa ndani ilipendeza kwa kweli. Washenga waliondoka tukabaki mimi na mke wangu Getruda Kimario. Nilikuwa na shauku kubwa ya kukabiliana na binti ambaye alikuwa kigoli, ambaye hakuwahi kuguswa, nilitamani kupata ukweli wa maneno ya baba aliyenieleza kuwa mke niliyeoa alikuwa bikira, na mimi nilitamani kumtoa mwenyewe yaani kama ni gari lilikuwa jipya ‘New model’ na sio mtumba. Tuliongozana bibi mbele bwana nyuma, wote tukiwa tumefunga taulo tuliingia bafuni na kuanza kuoga. Kweli uzuri wa mke wangu niliufananisha na lulu au tunda Apple. Alikuwa na umbo dogo lenye figa, ambalo lilinifanya nimtamani zaidi na zaidi. Si kifuani, usoni na umbo lote lilinivutia sana. Nilimuogesha nae aliniogesha, tulipomaliza tulijifuta na taulo na kuelekea chumbani. Tulijitupa kitandani, “Samahani mpenzi nikumbatie, nahisi baridi…nahitaji…..” Ilikuwa sauti ya Getruda iliyojaa mahaba na iliyonisisimua mwili na kuhisi joto . “Usihofu kila kitu kitakuwa shwari, nitakupa kila kitu unachokitaka” nilimjibu kwa sauti nzito iliyomuingiza kwenye ulimwengu wa mahaba. “Lakini mpenzi unajua nakupenda sana” Getruda aliongea macho ya udadisi yakiwa yametuwa usoni mwangu. “Naamini unanipenda mke wangu ndio maana ukaamua tuoane, lakini nahisi mimi ndiye nimezimika kwako zaidi” nilimweleza na hapo hapo tulikumbatiana na mabusu motomoto yalishamiri, si mashavuni, mdomoni na kwenye paji la uso kote tulipeana mabusu ya upendo. Niliyasikia mapigo ya moyo wake yakienda kwa kasi jasho jepesi lilimchuruzika taratibu nilishindwa kuelewa kwani AC au ‘kipupwe’Kiyoyozi kwa jina letu la kiswahili kilikuwa kinafanya kazi yake kama kawaida. Kila nilipomshika kwenye kona za mapenzi nilimsikia akizizima kwa sauti za mahaba, si kwikwi wala kuweweseka zote zilimburudisha. Niliamua kutulia kidogo baada ya kuona mambo yote nilikuwa namfanyia uume wangu hausisimka hata kidogo, tofauti na siku za nyuma busu moja kila kitu kimesisimka, leo mambo yote sikuona hata dalili. “Oooh.!!! Sweedy unajua mimi sijawahi kuguswa kabisa!” “Eti!, samahani sijakuelewa mke wangu” “ Sijawahi kufanya mapenzi toka kuzaliwa. Naomba unifundishe” sauti nyororo na ya simanzi ya Getruda ilinifanya nilie mwenyewe, sikuwa na nguvu za kiume, bali nilitamana kumkabili mke wangu nilishindwa kujua Ugonjwa wa kupooza kwa uume wangu ulitoka wapi na nitamuambia nini mke wangu, na je atanielewa na wakati nishamchezea kila sehemu, nilizidi kulia sikuwa na la kufanya. “Unalia nini tena mume wangu?” Getruda aliniuliza akiwa kalala chali, kama mgonjwa aliye mahututi . Mweupe mwili wake ulipendeza na kuzidi kung’ara kila nilipomtazama usiku ule, kwa ufupi alikamilika kila idara,nilitamani nimrukie lakini jogoo wangu hakutaka kuwika kabisa. Nilidanganya “Mke wangu nimeshikwa na kichomi cha tumbo sijui ni hiyo AC “kipupwe” niliongea kidhaifu nikiwa nimeshika tumbo, machozi yakiendelea kuchuruzika taratibu, niliamini kwa maneno ya kusema “Naumwa” Getruda angeridhika na kunionea huruma, aliniangalia kwa huruma na kusema “Basi mume wangu tuzime usije ukapata matatizo zaidi”. Nikaona duh! Acha nizidi kujitetea “Labda upunguze kidogo”Nilisema nikiwa nimekunja sura na kushika maeneo ya tumbo. “Pole mpenzi” mke wangu alisema kwa sauti ya utulivu. “Usiku huu tutapata wapi dawa?. Jikaze usilie”Mke wangu alinionea huruma. “Usijali mama watoto.Huwa natokewa na tatizo la kichomi ninapofikia hatua ya kufanya tendo la ndoa” “Kwa hiyo utafanya je?” “Daktari aliniambia tatizo hili litaisha baada ya kuzoea mwanamke” “Mwanamke gani, mbona sikuelewi?” “Wewe, Usijali tatizo hili litaisha”Nilizidi kumpa motisha mke wangu.Lakini moyoni bado wasiwasi ulitanda kuhusu jambo hili geni kabisa mwilini mwangu. Maneno hayo ndio yaliyomfanya Getruda, mke wangu ainamishe kichwa magotini mwangu kama mtu aliyekuwa akisujudu. Sikujua aliwaza nini akilini mwake, lakini nikahisi yote yalikuwa juu ya matatizo niliyonayo.Muda wa dakika takribani tano nilihisi kitu kama maji maji angali yenye uvuguvu yakidondoka gotini kwa tone moja na moja.Matone hayo nilihisi ni machozi ,nikaamua kuinua uso wake kutizama kwamba ni nini hasa.Kila nilipojaribu kumuinua alikaza shingo.Wazo ambalo nilihisi kwamba alikuwa akilia likajidhatiti akilini na kuhisi sikukosea.Pia nilijaribu kwa mara nyingine kumuinua uso wake, safari hii akanisemesha akionekana kukasirika. “Mume wangu umeamua kunitesa angali unajua unamatatizo. Kwanini usingenieleza kabla, umenitesa naunaendelea kunitesa. Utafanya nini ilikunisaidia, najisikia vibaya sana mwenzio” aliongea kwa sauti ya chini akiwa anadondosha machozi, mwili wake ulikuwa umelegea, macho mekundu na ya kurembua, hakuweza kuvumilia zaidi ya kulia kwa kwikwi, alitamani niondoe hali ya ubikira na kumpeleka kwenye utu uzima. Maneno ya Getruda yaliniumiza moyo wangu, nilimuonea huruma alivyokuwa akijigaragaza kitandani. Machozi yalichuruzika kwa kasi nilizidi kuwaza. “Au ni kwa vile ndio mara ya kwanza kukutana naye nini?. Lakini hapana sijapaniki” labda ni uzuri wake unanichanganya nini? . Au ni chango la tumbo limesababisha nini?.Sasa tatizo hili litaniumbua” Nilijiuliza bila kupata muafaka wala sikuweza kuhisi kitu chochote zaidi ya ugonjwa wa kawaida. Tuliupitisha usiku huo usio na ladha ya mapenzi, si mimi wala Getruda wote tulihuzunika. By brayton starpoz

at 9:08 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top