UWE FARAJA KWA MUMEO Uzito wa mzigo wa maisha huchukuliwa na wanaume kwa sababu wao wanao wajibu wa kutunza na kusaidia familia zao. Katika kutimiza wajibu huu, mwamaume wa familia lazima akabiliane na matatizo mengi na vikwazo vingi nje ya familia yake. Baadhi ya matatizo haya yanaweza kuwa ukubwa wa kazi, mizozo kwenye msongamano, foleni za magari na usumbufu wa kungoja na kupanda mabasi kutoka nyumbani kwenda ofisini na kurudi nyumbani, wasiwasi kuhusiana na masuala ya marafiki na wafanyakazi wenzake na wasiwasi wa kiuchumi na kisiasa kwa siku hiyo, wasi wasi wa marafiki na wafanya kazi wenzake, na wasiwasi wa kujaribu kuboresha hali ya maisha ya familia yake. Kiasi cha mishughuliko na wasiwasi wa mtu mwenye kuwajibika ni mkubwa na wenye sehemu nyingi. Usishangae kuona kwamba wastani wa umri wa mwanaume ni mdogo zaidi ya ule wa mwanamke. Ili mwanadamu aweze kwenda sambamba na mizigo ya maisha ni muhimu kuwa na mtu ambaye atakusikiliza na kukuhurumia. Mumeo ni mmoja wapo wa watu hao. Anaweza akahisi yu mpweke na akahitaji kupata kimbilio na faraja akiwa katikati ya misukumo hii. Ni kawaida kwamba mwanaume hutarajia kupata faraja na utulivu kutoka kwa mke wake na familia yake. Kwa hiyo, yatambue matarajio na mahitaji yake. Uwe mkunjufu na mchangamfu wakati ambapo kwanza ndio anarudi nyumbani kutoka katika kazi zake, na apate viburudisho au umfanye ahisi kwamba wewe upo tayari kusikiliza mahitaji yake. Jaribu kutokumwingiza kwenye shari kwa kuanza kumlaumu mara tu umuonapo. Ngoja apumzike na apate nguvu upya kabla ya kumweleza mambo binafsi ya familia. Mumeo anapokuja nyumbani, jaribu kutabasamu na kumsalimia kwa uchangamfu. Mpokee, msindikize mpaka anapotaka kubadilisha nguo, msaidie katika hilo, na mtimizie mahitaji yake ya kimwili ya uchovu, njaa na kiu. Halafu muulize kuhusu matatizo yake. Kama hayupo tayari kusema uwe msikilizaji mzuri na umhurumie. Jaribu kuonesha kuwa unaguswa na kila jambo lake kwa dhati na halafu umsaidie kutambua kwamba matatizo si kwamba hayawezekani, na si makubwa kama anavyodhani. Mpe moyo wa kumuunga mkono na kumsaidia aweze kukabiliana na masuala ipasavyo. Unaweza kumwambia kuwa: “Matatizo haya yanawapata watu wengi. Kwa utashi na uvumilivu, inawezekana kuyatatua matatizo almuradi mtu asiruhusu yamshinde. Matatizo haya, kwa kweli ni mitihani na pia hujenga tabia ya kweli ya mtu. Usikate tamaa. Unaweza kuyatatua kwa kuazimia na ustahamilivu. Kama unayo mawazo fulani kuhusu jinsi ya kuyashughulikia, mwaambie mumeo. Kama huna, labda unaweza kumshauri amuone rafiki mzuri ambaye anao ujuzi na sifa zaidi. Dada yangu mpendwa! Wakati wa matatizo, mumeo anahitaji sana umjali na mapenzi yako. Unatakiwa umsaidie na umtunze kama mtaalamu wa maradhi ya akili na mke mwenye huruma. Kiwango gani cha matunzo ambacho mtaalamu wa maradhi ya akili angempa ambacho na wewe ungempa? Usikadirie uwezo wako wa kumtuliza na kumpa nguvu. Hakuna mtu muaminifu na mwenye kuhusika zaidi kuhusu ustawi wa mumeo isipokuwa wewe. Ataweza kupata nguvu kutokana na mapenzi yako kwake na aweze kukabiliana na matatizo yake kwa hali ambayo itapunguza mhemuko wake na wasiwasi wa akili. Hatimaye, mapatano ya kuheshimiana na upendo utakuwa mkubwa zaidi. Kumbuka kuwa, hakuna kitu bora zaidi duniani kuliko kuwa na mke mwema. Na mke mwema ndiye huyo ambaye mume wake hufurahi pindi amuonapo. Na usisahau kuwa, lipo kundi la wanawake ambalo huzaa watoto wengi. Ni wanawake wema na wana huruma. Huwasaidia waume zao wakati wa matatizo na katika mambo ya dunia hii na ile ijayo. Wanawake hawa hawafanyi matendo yoyote ambayo yangewapa hasara waume zao kuongeza matatizo yao.

at 1:58 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top