Home → ushauri
→ #UREMBO NI KAMA #MAUA HUNYAUKA NA KUKAUKA
Maua hata yawe ya kupendeza kiasi gani ila ikifika wakati au hali isiyo rafiki hunyauka na kukauka huo unakua ndio mwisho wao hakuna ataevutiwa nayo, hakuna ataetaka kupiga picha nayo, hakuna atakayeyanunua wala kuyapeleka nyumbani kwake. Kuharibika kwa maua kwaeza tokana na umri, juakali, ukame, magonjwa au wadudu waharibifu vivyo hivyo urembo na uzuri wa mwanamke waeza potea kutokana na umri au vitu vingine vinavyoeza kuingilia maisha yake ikiwemo ajali, magonjwa n. k
Wapo mabinti wanaotumia uzuri na urembo wao kama silaha kuu ya kumteka mwanaume kiakili wanasahau kuwa mwanaume akili zake nae ni kama mtoto na siku zote mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Kwa hiyo ukitaka uzuri na urembo wako viwe ndio vivutio vyake vukuu kwako siku ukianza kuzeeka itakuaje, ukizaa watoto wawili au watatu una uhakika gani kuwa utabaki katika standard hiyo hiyo?
Uzuri hupotea unapozeeka ila pia waeza pata ajali ikapelekea kuharibu mwonekano na sura yako sasa je utafanyaje ikiwa mmeo ulikua umemtekea uzuri na urembo wako????
Namaanisha binti ni lazima uwe na vigezo vya ziada kumteka mwanaume kiakili, ambavyo vigezo hivyo hata kama uzuri na urembo wako ukiisha vyenyewe vitabaki kama silaha kuu ya kumzuia kukuchoka au kukusaliti na hata kukubwaga.
Jitahidi pamoja na uzuri na urembo wako ila pia mwanaume avutike kwako kutokana na tabia hizi
1) ucha Mungu
2) upole
3)ujasiriamali
4)ukarimu
5) usikivu
6)uvumilivu
7)uaminifu
8)heshima
9)kuridhika
10)usafi
11)ucheshi
12)umakini
13)utii
Tabia hizo zitakua kama mtaji wako na kumdhibiti kisawasawa mmeo maana atakua kazimika kwako na vingi mno ukiachilia mbali uzuri na urembo wako, hata ukizeeka bado atakuona wa thamani kubwa, hata ikitokea ajali au ugonjwa ukaharibu uzuri na urembo wako bado atakujali na kukupenda kama awali maana wewe kwake ndio kila kitu, hajakupendea urembo na uzuri wako pekee.
Poleni sana pia mabinti mnaoringia uzuri na urembo wenu kiasi kwamba kila wanaume waoaji wanaojitokeza mnawakataa na kuwasonya eti hawana hadhi, kumbukeni umri unaenda uzuri na urembo unafifia taratibu shauri zenu nyie endeleeni kuchezewa na hao matozi na mapedeshee mnaohisi wana hadhi kumbe sio waoaji.Itafika wakati rekodi zako zitamtisha kila anaekuzunguka mwili wako utachakaa kama brush ya kuoshea masufuria, utaonekana USED MNO watakukimbia hawatojali uzuri na urembo wako.
Binti jitahidi, sali na muombe sana Mungu akujalie upate mwanaume atakaekupendea vingi na sio yule ataejali tu uzuri na urembo wako pekee, huyo atakua kavutika kwa tamaa zake juu ya uzuri na urembo wako ila sio upendo wa kweli
Kama umeipenda WEKA COMMENT YAKO HAPO CHINI kisha SHARE post hii na marafiki zako wapate funzo hili
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Usisahau ku LIKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: