Home → simulizi
→ SHORT STORY:-Maumivu ni sehemu ya kufanya kitu kuwa bora.
STORY BY:-TRUE STORY
“Kwanza sina budi kusema mimi na John sina ugomvi naye wala chuki katika kipande cha moyo wangu sina.Nanena hivi kwa uhakika na sina hata chembe ya uhoga.”Sina ugomvi na John nampenda sana na kumtakia kila la heri.Nakupenda John we ni mwanaume mwenzangu,sipendi uumie kama mie”.Nimeanza kwa nena hivyo kwa sababu ya msingi kabisa ili mbele unielewe nataka kuzungumza nini.
Kama ningeweza jua kama John na Mariana ni wapenzi,sidhani kama ning’ethubutu kuvua nguo na kuogelea maji yenye ulinzi mklai,hakika sikujua.Nilipomfuata alisema ananipenda na mie nilimpenda sana tena zaidi ya sna ,hakika nilimpenda.Mapenzi matamu ndugu zangu pale mtu anapokuonesha upendo,basi lazima usikie raha.Kwani nilijipanga kama mwanaume na kuhakikisha ndoto yangu inakuja kutimia siku moja kwa uwezo wa allah.
Lakini nyuma ya panzioa nikaja kugundua kuna mwanaume mwenye jinsia kama yangu,mwenye upendo wa dhati kama wangu na mwenye malengo kama yangu ila nina uhakika yake yamenizidi mimi ndio maana Mariana ameamua kunisaliti.John aliweza kufika nyumbani na kujitambulisha na kuweka wazi lengo na nia yake ya msingi ni ipi katika maisha yake na Mariana.Niliumia sana tena niliumia siwezi kusema maumivu moyo niliyoweza kupata Kivuli mimi.
Kwa nini alinidanganya?Kwa nini alinitumia kwa muda?Kwa nini alinisaliti?Ndio kitu kinaniumiza usiku na mchana japo hakuwahi kuniambia na nilikujua kugundua kwa uwezo wangu.Kipindi chochote hicho hata yeye aliweza kutambulika kwa ndugu wa mume nay eye alimtambulisha mumewe mtarajiwa katika familia yake.Jambo la furaha sana kusikia hivyo,ni dhairi huyo ndio mwanaume mwenye malengo ya kweli.”Nisubili nijitengeneze kimaisha nitakuoa!Nivumilie nakupenda sana” Ndio kauli niliyopenda kumwambia kila siku,lakini hakutaka kuifanyia kazi na kuamua kumpa moyo wake mtu mwingine na kuniacha naumia.
Kwa hayo machache nadhani umenielewa nilitaka kunena nini.Cha muhimu nasema sina ugomvi na Mriana na wala rafiki yangu John.Na wapenda sana ten asana,kwa sababu sote binadamu ni ndugu kabisa.Naomba kwa mungu wafikie malengo yao ya kufunga ndoa kwa moyo mmoja tena bila kuongea vibaya.Japo niliwaomba kwa sasa kutohitaji mawasiliano nao,mpaka pale moyo utapokuwa umepoa basi nitawatfuta mie mwenyewe na kuongea nao.
Japo sitaki tena kuwa na mwanamke kwa sasa,sihitaji kuanzisha mahusiano na wanawake mpaka pale nitakapokamilisha maisha yangu na kupata mwanamke na kumuoa ndani ya muda mfupi tu.Mungu nisimamie kwa hili wala usiniache mwenyewe.Upendo wangu sina budi kuweka na kuujaza kwa wadogo zangu wapenzi kila siku.Nitawapenda sana wadogo zangu na sihitaji wajue chochote kuhusu ili.Na pia upendo wangu nitaimrisha zaidi kwa wanafunzi wangu shuleni maradufu na wao sihitaji walijue ili.
Mwanzo wa story ndio mwisho wa story,japo nipo katika maumivu makali ila ipo siku ya takwisha.Nashukuru kwa kusoma storu yangu fupi na tumai umeweza kujua nini kilichonipata.Ni boara kwa sasa nipate Furaha na sio mpenzi,Mapenzi ya naumiza ndugu yangu.
MM brayton
MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: