Mfumanie panya anakula chakula utakimwaga upike kingine ila sio Umfumanie Mume wako akiwa na mwanamke mwingine INAUMA ASIKWAMBIE MTU! Niliolewa na Fred yapata miaka mitatu sasa na tangu naolewa sikuwahi kuijuwa tabia halisi ya mume wangu maana ni mtu wa safari nyingi pamoja na kazi nyingi na hilo lilipelekea kuishi na Mume wangu muda mchache sana, Fred alionyesha upendo mkubwa sana kwangu, Nilikuwa mfanyakazi lakini mume wangu alinihudumia kila kitu akitekeleza majukumu yake kwangu, Siku moja nilikuwa ofisini na wakati nikiendelea na kazi zangu ghafla nikaingiwa hamu kali ya kumuona Mume wangu japo nim-kiss tu, sina tabia ya kumfuata mume wangu kazini japo hajawahi nikataza ama kuniwekea masharti, Nikaaga stuff wenzangu na kuelekea tunakoegesha magari nikaingia na kuwasha gari langu kuelekea ofisini kwa mume wangu... Ofisini kwa Fred wala si mbali na ninapofanyia kazi Mimi nikapaki gari katika maegesho yao na kutelemka kuelekea ofisini kwa mume wangu, Niligonga Mlango bila kuitikiwa ndipo nikazungusha kitasa na Mlango ulifunguka nikaingia ndani, Ni kama macho yangu yamepatwa ukungu kama sio maluweluwe kwa picha niloikuta ofisini kwa Fred, Alikuwa msaidizi wa mume wangu aliyeitwa Fiona ndiye aliyekumbatiana na Mume wangu, Fiona aliniona japo hakushituka hata kumsababisha Fred ajue Kwani Fred ndo kwanza alilegea mtoto wa kiume nami kama naangalia Thamthilia wala sikujitingisha wala kusema lolote, Moyo wangu ukaanza kuingiwa sumu kali, Wivu ukanipanda, Hasira zikaelekea kichwani nikaanza kutetemeka tu, Fiona alibaini hali yangu na akawa anajinasua kifuani kwa Fred, Fred aliyekuwa amenipa mgongo akamuuliza Fiona "NINI TENA BABY? Hapo sasa ndipo alipoharibu maana ndilo jina hupenda kuniita Mimi, Fred ni wewe ama naota? Fred alikurupuka akageuka nyuma na kuniona kwakweli FUMANIZI NI MBAYA! Fred alionekana kupaniki sana hasa akikumbuka ahadi zake kwangu, Fred aliishi nami kwa kunipa hakika kuwa SINA MPINZANI MOYONI MWAKE nami nilitembea kifua mbele nikiamini hivyo, Fiona naomba uondoke niongee na mke wangu... Aondoke aende wapi au Kuna jipya gani unataka kusema kwa siri ikiwa tayari mliishatenda dhambi ya usaliti kwangu? Fiona ni wewe ambaye kila mara huwa unaniambia nimepata mume mstaarabu na pia mpole na kumbe ustaarabu na upole wake ndo huu? Nilisikia hasira sana nikawa Natamani kama nifanye fujo lakini kila nikikumbuka stuff wenzie na Fred jinsi wanavyoniheshimu nilibaki nalia tu, Dada Rebecca naomba nisamehe Mimi Kwani kama bin adam nilimpenda sana mume wako hasa nilipogunduwa kuwa anajiheshimu na anaipenda familia yake nami nilitamani japo nimjue kwa njia hii, Rebecca sisi wanawake ndo chanzo cha kuzivuruga akili za wanaume, Nimefanya mitego mingi sana kwa Fred na sikukumbuka kama ana mke ila nimuombee msamaha na nikuhakikishie kuwa HILI HALITAJIRUDIA TENA... Unajuwa ni kama nimewekewa kaa la moto moyoni, Nasikia hasira kiasi machozi yananichuruzika kama vile maji, Hivi Fiona unanionaje kwa mfano kunidhihirishia kuwa umeshiriki nami katika kumjuwa mume wangu? Mke wangu naomba Fiona aondoke ili tuzungumze Kwani alosema yanatosha tuzungumze kama familia sasa, Niliitikia OK! Na Fiona aliondoka mahala pale, Nilimsikiliza Fred jinsi alivyokuwa akitaka ninuelewe lakini kila nikifumba macho niliiona movie ile wakiwa wamekumbatiana kwakweli sikujuwa kama ningemsamehe mume wangu, Hasa nilipoutafakari ufundi wake kitandani hapo ndipo nipagawa, Nilimpiga Fred makofi mawili akainuka kama anataka kukimbia nikamshika na kumlilia sana kufuani kwake, Nyamaza mke wangu ukweli nimekukosea sana nashindwa hata kujieleza ila naomba shusha hasira zako tupo ofisi za watu, Mlango wa ofisini kwa Fred ukagongwa nikamuachia mume wangu na kufuta machozi yangu ili atakayeingia asijue kilichokuwa kinaendelea, Aliingia Mzungu ambaye alikuwa mteja wa ofisi ya akina Fred, Ujue yule jamaa alisalimia na kuuliza Kuna tatizo? Mimi nilikataa na kusema hakuna tatizo na nikam-kiss mume wangu na kumuaga nirudi ofisini kwangu, Fred hakujizuia akaniambia REBECCA WEWE NI KILA KITU KWANGU akili yangu itatulia ikiwa wewe una amani mke wangu, Naomba ulifute akilini tukio hilo ili tuendelee na maisha yetu Kwani Shetani hana nafasi tena juu ya maisha yetu na ukumbuke KUTELEZA SIO KUANGUKA... Nilitabasamu na kumwambia mume wangu uwahi kurudi ili twende mahali tukapumzike, Nikafunga mlango na kuelekea nilikopaki gari, Nilipoingia kwenye gari yangu nikajikuta nacheka peke yangu, Sababu ya kucheka eti nami leo nimekuwa BOUNCER nimempiga mume wangu wala hakujibu na akataka kunikimbia, Nikawasha gari na kurudi ofisini, Nilivyokuwa nampenda Fred wala ile movie siikumbuki tena nawaza tu muda wa kufunga ofisi ufike niwahi home nijiandae nitoke na Mume wangu, Nilisikia honi getini nikachomoka kwenda kufungua mlango alikuwa Fred, Karibu mume wangu Leo bwana nimezidisha MAHABA kumbe nisipokuwa makini nitaibiwa mume hivyo NIMEJIPANGAAA... Niliona tabasamu la Mume wangu likichanua na nilimwambia yalopita si ndwele sasa tugange yajayo, Fred asiye amini ananitazama kwa huruma, nikamwambia NAKUPENDA SANA MUME WANGU sipo tayari nikupoteze kisa hasira wakati hata huko nitakwenda siwezi kuwa na hakika kama sintoumizwa, Nisamehe mke wangu KAMWE SINTORUDIA! Fred nimekusikia na futa kesi hii kichwani mwako twende ukaoge Mume wangu tutoke, Asante sana Mke wangu kwa hakika nimeliona pendo lako kwangu na sasa niseme hii ni zaidi ya DHAMANA YA PENDO.

at 2:34 AM

Bagikan ke

1 comments:

avatar

Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma

Kwaheri Gerd Ulrich

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top