Jukumu la malezi kwa mtoto si la mama tu! Mwanamke alipewa kibali kuilinda FAMILIA yake lakini pia baba analo jukumu la kuitunza FAMILIA hiyo... Imezoeleka kwa wenzetu weupe MWANUME KUMHUDUMIA MTOTO KAMA KUMLISHA, KUMUOGESHA NA HATA KUMPELEKA HOSPITALI kwao ni kawaida ila kwetu ngozi nyeusi ni nadra sana, Mwanaume wa kiafrica huwaogopa watu kuliko kusimamia furaha ya ndoa yake, Mwanaume mwenye kujitambuwa HAFIKILII NANI ATAMUONA AMA ATAMSHANGAA maana mtoto ni wake, Mapenzi ya baba kwa mtoto ni jambo ambalo huusababisha moyo wa mkewe kusitawi na siku zote huishi kwa amani akijisemea NINAE MUME BORA... Usiishi kwa kuwatazama watu watasema nini bali UYAISHI MAISHA YALETAYO FURAHA KATIKA NDOA YAKO.

at 8:19 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top