Home → ushauri
→ π·JAMBO FORUMπΉ
``` MAISHA YA NDOA NI WIVU ```
W. I. V. U. .
πππππππ
Wivu ni yake asili,
Mapenzini kujivisha,
Aliye wivu mkweli,
Penzi hajabahatisha,
Asiyewivu tapeli,
Penzini anakuchosha.
πππππππ
Wivu waleta mapenzi,
Mapenzi yaleta wivu,
Mwenye wivu anaenzi,
Hatokuacha mkavu,
Mwenye wivu mjenzi,
Penzi litaota shavu.
πππππππ
Ila wivu na karaha,
Daima havipatani,
Wivu mwenzie furaha,
Karaha sio penzini,
Utanawiri wajiha,
Asowivu limbukeni.
πππππππ
Uonyeshe wivu wako,
Na katu usiogope,
Onyesha mpenzi wako,
Mapenzi sio mapepe,
Wakisema watu wako,
Maneno yao yatupe.
πππππππ
Mwenye wivu nahodha,
Kwa jahazi ya mapenzi,
Wivu si kufanya adha,
Mwenye wivu si mshenzi,
Mwenye wivu analadha,
πππππππ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: